Kusoma Msahafu katika Swala

Egypt's Dar Al-Ifta

Kusoma Msahafu katika Swala

Question

Je. Inajuzu kusoma Msahafu katika Swala?

Answer

Sifa zote njema anastahiki Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote, na swala na salamu zimshukie Bwana wetu Muhammad, Muaminifu, na jamaa zake na Maswahaba zake wote, na baada ya hayo:

Mwenyezi Mungu Mtukufu amekiteremsha Kitabu chake Kitukufu kama nuru na taa iwaangaziao Wenye kuikusudia na kuwaongoza waliojisahau, na akatilia mkazo wa kuifanyia kazi na kuambatana nayo na kuisoma

Basi Mtume wake S.A.W. amesema: "Mfano wa Muumini aisomaye Qur``ani ni kama vile mti unaofafanana na mchungwa, harufu yake ni nzuri na ladha yake ni tamu, na mfano wa Muumini asiyeisoma Qur`ani ni kama vile tende, haina harufu lakini ladha yake ni tamu."[1]

Na Mtume S.A.W. amesema: "Anayesoma herufi moja kutoka Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu basi ana thawabu, na thawabu ni kiasi cha thawabu kumi, mimi sisemi Alf lam Mim ni herufi moja, lakini Alf ni herufi, lam ni herufi na mim ni herufi".[2] Na nyingine kutoka matini za kisuna.

Na Wema waliotangulia walikuwa wao R.A, ni wenye pupa kuliko mtu yeyote mwingine katika kulinda usomaji wa Qur`ani Tukufu kwa wingi na pamenukuliwa kutoka kwao desturi nyingi tofauti tofauti, na miongoni mwao wamo waliokuwa wanahitimisha kila baada ya miezi miwili. Na kwa baadhi yao wanaihitimu kila mwezi, na kwa baadhi yao wanahitimisha kila usiku kumi, na kwa baadhi yao wanahitimisha kila usiku nane, na wengi wao wanahitimisha kila siku saba, na imenukuliwa tofauti na haya. [3]

Na katika mambo bora zaidi ya kuyafanya kwa ajili ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na Sunna mbalimbali za kufanya mema ni mja kukusanya mambo mawili: Swala na Kusoma Qur`ani Tukufu, na kupupia kuihitimisha Qur`ani Tukufu katika Swala zake, na kwa kuwa jambo hili sio jepesi sana kwa kila mtu kufanya hivyo akiwa ameihifadhi moyoni, ndipo lilipojitokeza swali la uwezekano wa kuutumia msahafu katika kuisoma Qur`ani wakati wa Swala, na hiyo ni kwa njia ya kuubeba Msahafu mkononi, au kuuweka juu ya kitu ambapo anayeswali anaweza kusoma.

Na iliyokubaliwa ni kujuzu kwa kusoma Msahafu katika Swala, kwa Imamu na anayeswali peke yake, hakuna tofauti baina ya Faradhi na Sunna, au baina ya mwenyekuhifadhi na wengineo.

Na imethibiti kutoka kwa Aisha R.A., kwamba alikuwa  akiswali nyuma ya Mtumwa wake Dhakraan na alikuwa akisoma kwenye Msahafu.[4]

Na Adhuhriy aliulizwa kuhusu mwanamume anasoma Msahafu katika mwezi wa Ramadhani, basi akasema: "Wema wetu walikuwa wakisoma katika Msahafu"[5]

Na kusoma Qur'ani kama ni ibada basi pia kuutazama Msahafu ni ibada. Na kuunga ibada na ibada nyingine haiwajibishi kuzuia, bali inawajibisha ziada katika thawabu, kwani ina ziada katika kazi kama kutazama Msahafu na nyinginezo.

Imamu Al Ghazali alisema: "Na imesemwa kwamba kuhitimu Msahafu ni kiasi cha siku saba, na kwamba kuutizama Msahafu pia ni ibada" [6]

Na vilevile kilichojuzu kukisoma waziwazi kinajuzu pia kinyume chake,[7] na lengo ni kupatikana usomaji, na pindi lengo hili linapofokiwa kwa njia ya kuangalia kilichoandikwa basi njia hiyo inajuzu, na msingi wake ni kwamba njia huchukua hukumu ya malengo.

Hayo ni Madhehebu ya Kishafi, na hutolewa Fatwa katika Madhehebu ya Kihanbali, na imenukuliwa na Atwaa na Yahya Al-Answariy miongoni mwa Wanachuoni wa Fiqhi wa Salaf.[8]

Imamu An Nawawiy miongoni mwa Wanazuoni wa kishafi amesema: "Na ikiwa atasoma Qu`rani Tukufu katika Msahafu Swala yake haitabatilika, awe mtu huyo amehifadhi Qur`ani au hajaihifadhi, bali anawajibika kufanya hivyo kama hajahifadhi Suratul Fatha (Alhamdu Lillah), hata kama atageuza geuza kurasa za Msahafu baadhi ya nyakati Swala yake haitabatilika."[9]

Na imesemwa katika kitabu cha: "Kashafu Al Qinaa'" miongoni mwa vitabu vya wanazuoni wa kihanbaliy: "Na mtu huyu anaweza kusoma Qur`ani katika Msahafu hata kama amehifadhi… na Swala za Faradhi na za Sunna zote ni sawa katika usomaji huu, Ibn Hamid aliyasema hayo.[10]

Na Imamu Abu Hanifa - Mwenyezi Mungu Amrehemu- anaona kwamba kusoma Msahafu katika Swala inabatilisha, na hayo ni Madhehebu ya Ibn Hazm miongoni mwa Ad Dhahiriyah, na akato dalili miongoni mwayo:

Ya Kwanza: Kauli ya Mtume S.A.W., "Hakika katika Swala kuna kazi”[11] Swala yenyewe inamshughulisha mja na kumuepusha na kila ambacho hakuna andiko lolote la kukihalalisha, na kuangalia Msahafu ni jambo ambalo hakuna matini yoyote iliyohalalisha katika Swala".

Ya Pili: Hakika mambo yalivyo, mtu ambaye hajaihifadhi Qur`ani Mwenyezi Mungu Mtukufu hakumkalifisha kuisoma kama hajaihifadhi kwani hilo liko nje ya uwezo wake. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyo} [AL BAQARAH 286]. Na iwapo atakuwa si mwenye kukalifishwa kufanya hivyo, basi huko kumkalifisha kwa kitu asichokiweza ni jambo batili.[12]

Ama kuhusu dalili ya kwanza: Na kama tutakubali ya kwamba kuisoma Qur`ani katika Swala kwa kuiangalia kwenye Msahafu hakuna dalili zozote zilizokuja kuhalalisha kwa umaalumu wake huo, lakini sio kila kile ambacho hakuna dalili yoyote iliyokuja kuhalalisha kwake kwa umaalumu wake, kuifanya kwake kunabatilisha Swala. Na imepokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W. Hadithi zinazouzungumzia uhalalishaji wa vitu vichache katika Swala katika vile visivyokuwa sehemu ya Swala na havihukumiwa kubatilika kwake. Miongoni mwao yaliyotajwa kwamba Mtume S.A.W. alikuwa anaswali na yeye amembeba Umamah Bint Aby Al Aasw Ibn Ar Rabii' basi akisujudu humweka na akiinua kichwa chake humbeba.[13]

Na miongoni mwa hayo Hadithi ya Ibn Abbas kwamba alisimama kuswali upande wa kushoto wa Mtume S.A.W., basi Mtume S.A.W., alimchukua na kumuweka upande wa kulia. [14]

Na miongoni mwa hayo ni kwamba Waanswari walikuwa wakiingia kwa Mtume S.A.W. na yeye akiswali, na wakamsalimia na yeye akijibu salamu kwa ishara ya mkono wake,[15] Na miongoni mwa hayo kuamuru kwake kwa kuua katika Swala; nyoka na nge.[16] Na aliamuru kumzuia anayepita mbele ya  mwenye kuswali,[17] na nyinginezo.

Ikiwa Matini hizi zimepokelewa katika matendo mabaya kuliko kuangalia tu, na Swala haikubatilika kwayo , basi hakika Swala kutobatilika kwa kuangalia Msahafu ni bora zaidi, na kama ikiwa kuangalia huko kwa masilahi ya kuswali, ni kama vile kuangalia Msahafu kwa lengo la kusoma, basi ni bora kabisa.

Imamu An Nawawiy –Mwenyezi Mungu Amrehemu- amesema kufikiri na kuangalia hakubatilishi Swala kwa makubaliano ya Wanachuoni, kama ikiwa katika usiokuwa Msahafu, basi katika Mshafu ni bora zaidi.[18]

Vilevile mtu halazimishwi kufumba macho yake katika Swala, jambo ambalo linamlazimu kutozuiliwa kuangalia kuangalia kitu chochote ambacho sharia tukufu haikizuii, kwani Sharia inamzuia mtu anayeswali kuangalia mbinguni. Mtume S.A.W. amesema: "Inakuwaje kwa watu wanaonyanyua macho yao mbinguni katika Swala zao.. waache mara moja jambo hilo au wapokonywe macho yao,[19] na akazingatia ya kwamba kuyatumia macho katika kuangalia vitu vinavyozingatiwa kuwa ni vya kipuuzi kwa mtu anayeswali pamoja na mapambo mbali mbali ni jambo linalochukiza; kwa sababu ya kwenda kwake kinyume na unyenyekevu unaohitajika katika Swala".

Na Mtume S.A.W, aliposwali kwa nguo yenye michoro akaiangalia michoro hiyo mara moja na alipomaliza akasema: "Nendeni na nguo yangu hii kwa Abu Jahmi na mniletee nguo ya kianbaji iliyotengenezwa kwa sufi na haina michoro kwani nguo hiyo ilinishughulisha hapo kabla katika Swala yangu.[20] Ama kuangalia msahafuni hakuna chochote kinachokuzuia kisharia na kwa ajili hiyo asili yake inaendelea kuwa inajuzu kufanya hivyo.

Ama Dalili ya pili: Inazungumzwa ya kwamba kisomo cha mtu anayeswali kwa upande unavyotakiwa kisharia, kisomo hicho kinaweza kuwa katika upande wa wajibu kama vile kuisoma Suratul Fatha katika kila rakaa, au ikawa kwa upande wa Sunna kama vile kusoma kiasi kidogo cha Qur'ani Tukufu baada ya Suratul Fatha katika sehemu ambazo ndani yake panahitajika kusoma Qur'ani. Na kilichoamuliwa na Wanachuoni ni kwamba mambo ya wajibu na mambo ya Sunna yako ya aina mbili: Moja yake ni Makusudio, na ya pili yake ni njia, na njia zina hukumu za makusudio, na sharia inapelekea malipo kupitia Njia kuelekea katika Utiifu kama ambavyo Sharia inapelekea malipo katika Makusudio.[21]

Na kwa ajili hiyo, kuangalia msahafuni kunakuwa na hukumu ya kutakiwa kufanya hivyo kwa mwenye kutaka kwani hiyo ni njia inayopelekea kitu kingine kinachotakiwa na kinachokusudiwa nacho ni kisomo, na huko sio kumkalifisha mtu kwa yale asiyoyaweza, na wala haisemwi pia kwamba kusoma  msahafuni wakati wa kuswali kunamlazimu mtu yale ambayo sio ya lazima, kwani usomaji huu wa Qur'ani katika uchache wa hali zake unakuwa Sunna, na Sunna ni katika Hukumu za Kimajukumu kwa maana ya kutakiwa kutekeleza na sio kwa njia ya kuwajibisha na kulazimisha, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

Na kwa Abi Hanifa kubatilika kuna hali mbili:

Ya kwanza: Kwamba kuubeba Msahafu na kuutazama na kuzigeuza kurasa zake ni kazi nyingi.

Ya Pili: Ni kwamba kusoma kwenye msahafu, inakuwa kama kusomewa na mtu mwingine, na kwa njia hii ya pili hakuna kwake tofauti baina ya Msahafu uliowekwa sehemu na Msahafu uliobebwa, na kwa njia ya kwanza wanagawanyika.

Labda inatoa dalili kwa Ibi Hanifa kwa iliyotolewa na Ibn Ibi Dawud katika kitabu cha: [Al Maswahef] kutoka kwa Ibn Abbas amesema: "Amiri wa Waumini ametuzuia sisi kuwaswalisha watu tukiwa kama Maimamu kwa kusoma Msahafu", basi hakika katazo hapo linahukumiwa Ufisadi.[22] 

Na akabagua hilo na kwamba inapokuwa mtu amehifadhi Qur'ani anayoisoma, na akausoma Msahafu bila ya kuubeba basi hakika kwa hali hiyo, haibatilishi Swala yake; kwani usomaji huo unaongezwa katika kile alichokihifadhi sio katika kusomewa kutoka katika Msahafu hiyo na kwa kuuangalia tu Msahafu bila ya kuubeba hakuharibu Swala kwa kutokuwa na mielekeo ya kuharibu Swala.[23]

Na inajadiliwa sura ya  kwanza kwa kuzuia kwamba kuwa kubeba Msahafu na kugeuza kurasa zake ni kazi nyingi inabatilisha Swala, ama kubeba basi Mtume S.A.W. ameswali akimbeba Umamah Bint Abi Al Aasw, akisujudu alimtua ardhini na akisimama akimbeba.

Ama kuzigeuza kurasa zake, basi tumetaja baadhi ya Hadithi zinathibitisha kwamba kazi sahili katika Swala kuwa ni halali, kugeuza kurasa ni aina ya kazi sahili inayoisamehewa.

Na wanavyuoni wa kihanafi wenyewe wametofautiana katika uchache na wingi katika kauli tatu:

Ya Kwanza; Hakika yanayofanywa kwa mikono ni mengi sana kwa kawaida, na kwamba kitendo chake kwa mkono mmoja ni kama kujifunga kilemba na sio kuvaa Kanzu, na yanayofanywa na mkono mmoja ni machache sana na ikiwa atafanya kwa mikono yake miwili kama vile kuvaa kofia na kuivua. Na kila kifanywacho na mkono mmoja ni kichache kama hakikukaririwa.

Ya Pili: Ni kuipa nguvu rai ya Mwenye kuswali na ikiwa atazidisha basi itakuwa zaidi na ikiwa atapunguza itakuwa kidogo.

Ya Tatu: Hakika mambo yalivyo ikiwa mwangaliaji ataangalia Msahafu kwa mbali, ikiwa hajishuku kwamba yeye hayuko katika Swala basi hiyo itakuwa inaharibu kwa kiwango kikubwa na ikiwa atashuku basi yeye sio mharibifu wa Swala.[24] 

Na Kauli yeyote kati ya Kauli hizi tatu, hakika mambo yalivyo Usomaji wa Msahafu hauwajibishi kuwafikia wengi, kwani kugeuza geuza kurasa za Msahafu kunakuwa katika uchache wake, na inawezekana ikasaidia zaidi kwa kuweka Msahafu wenye maandishi makubwa zaidi juu ya kitu kilicho juu mbele ya Sehemu ya mtu anayeswali ili ausome Msahafu huo, ukurasa mmoja au kurasa mbili, na wala hahitaji kugeuza geuza mara nyingi kurasa zake.

Ama kubainisha sura ya pili katika sababu ya uharibifu: "Ni kwamba kusomewa kunakoharibu Swala kwa mujibu wa Madhehebu ya Imamu Abu Hanifa ni kwa yule asiyemfuata Imamu wake; Alkasaaniy  amesema: “Kwani kufanya hivyo ni kusomesha na kujifunza, kwani msomaji anapomfungulia mwingine inakuwa kama vile anasema: baada ya nachokisoma, nikumbushe, na mfunguaji kwa kufungua Msahafu ni kama vile anasema: baada ya kusoma hivi na vile basi chukua kutoka kwangu".[25]

Ama kwa upande wa anayemfuata Imamu akimfungulia  Imamu wake, basi kitendo hicho hakiharubu Swala yake; kwani yeye ndiye anayelazimika kuifanya  Swala yake kuwa sahihi na hicho kilikuwa ni miongoni mwa vitendo vya Swala yake. [26]

Na anayesoma msahafuni akiwa katika Swala yake basi yeye ni kama mtu anayetamkishwa na inakuwa kama kujifunza kutoka katika msahafu huo, na amesema Alkasaani: "Huoni kwamba anayesoma msahafuni anaitwa mwanafunzi, na hali hiyo imekuwa kama mtu anayefundishwa na mwalimu wake kusoma.[27]

Na sisi tunazuia kuharibika kwa Swala kwa kutamkishwa Qur'ani na mtu mwingie kiasili, iwe mtamkaji huyo ni mwenye kumfuata Imamu au awe nje ya Swala. Basi kutoka kwa Al Mussawar Bin Yazid R.A. amesema: Nilimtazama Mtume S.A.W., anasoma katika Swala zote na akaacha kitu ambacho hajakisoma na mtu mmoja akamwambia: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hakika mambo yalivyo ni hivi na hivi, na Mtume S.A.W, akasema: Kwanini usinikumbushe nilichokiacha?[28]

Na Kutoka kwa Anas Bin Malek R.A., amesema: Maswahaba wa Mtume S.A.W., walikuwa someana katika Swala. Na kutoka kwake ni kwamba yeye alikuwa anaposimama kwa ajili ya kuswali basi nyuma yake husimama kijana mwenye Msahafu na anapoponyokwa na kitu basi yule kijana humfungulia.

Na kutoka kwa Amer Bin Saad alisema: "Nilikuwa nimeketi Makkah na punde nikamwona mtu wa makamo mwenye harufu nzuri anaswali, na huku nyuma yake kuna mtu amekaa anamtamkisha, na huyo alikuwa Othmani R.A,[29] pia utamkishaji si chochote isipokuwa ni kumzindua Imamu kile kilichosahihi katika Swala, na kwa ajili hiyo imefananishwa na Tasbihi yaani kusema Subhaana Llaahu. [30]

Na kwamba maelezo ya kitaalamu ya Kihanafi ni kutoharibika kwa Swala kama anayefungua ni Maamuma kwani yeye wakati huo anakuwa amelazimika kurekebisha Swala yake kwa maneno machache kwani yeye hahitaji kufanya hivyo katika Swala ya Sunna, na kiwango kidogo kabisa kinachotosha katika usomaji kwenye Swala kwa mujibu wa Abu Hanifa ni Aya moja tu, na kwa mujibu wa wenzi wake ni aya tatu fupi fupi au aya moja ndefu.[31]

Na kilicho zaidi ya hapo hakisemwi: kwani hakika yeye analazimika ndani yake kuirekebisha Swala yake, na ikiwa tutakubali kwamba yeye anahitaji kuirekebisha Swala yake basi inawezekana kusemwa hayo pia katika haki ya Maamuma kwa ujumla , iwe kwa kutamkishwa na yule aliyeaminiwa au yoyote yule, na hicho ndicho wasichokisema Wafuasi wa Madhehebu ya Abu Hanifa.

Na imebainika wazi kwa njia hiyo ya kwamba hakuna tofauti ya kumfungulia Imamu ndani ya Swala au nje ya Swala, na pia hakuna tofauti baina ya kusoma kwa moyo au kusoma msahafuni wakati wa Swala.

Ama Athari ya Ibn Abbas basi iliyotolewa na  Ibn Abi Dawud katika kitabu Al Maswahif, kwa kitamko: "Amiri wa Waumini ametukataza sisi kuwasalisha watu tukiwa kama Maimamu kwa kusoma Msahafu, na hatuswalishi isipokuwa mtu Baleghe" Nayo haithibiti; na katika Isnadi yake Nahshal bin Saidi Nisaburiy, naye ni mwongo aliyepuuzwa, Imamu Bukhari anamzungumzia akisema: Hadithi zake ni katika Hadithi zenye hukumu ya Munkar, na amesema Annasaaii: Huyo sio katika waaminifu, na wala yeye haziandiki Hadithi za mtu huyo.[32]

Na kwa kukisia kukubali kuwa imethibiti, kunakuwa na uwezekano wa kuzuia kupitia mlango wa Sera za Kisheria na wala sio kupitia Hukumu za Kisharia; ili watu wasizembee katika kukihifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu kwa mfano, na kilichoamuliwa na Wanachuoni ni kwamba Kiongozi ana madaraka ya kuzuia yale yanayokuja kuleta madhara kwa anaowaongoza, na ana yeye nafasi ya kufungamanisha Halali kwa ajili ya masilahi yanayozingatiwa.

Na upeo wa jambo hili uwe ndio mwenendo wa Omar R.A, na kwa hiyo ukawa unakinzana na yaliyonukuliwa kutoka kwa Bi Aisha R.A, na Amswahaba pindi wanapohitalifiana haitumiki hiyo kama ni hoja baina yao, na hii ikiwa kunukulu huko ni Sahihi kutoka kwao wote, inakuwaje na haijasihi?

Ama kuhusu yale ambayo baadhi wanaweza kuyapokea ya kwamba usomaji wa Qur'ani Msahafuni unapingana na Unyenyekevu; kwa sababu huo usomaji unaiondoa, kutokana na kuambatana na kuangalia kwa muda mrefu na kufikiri pia. Tunasema sisi kwamba hatukubali ya kuwa kuisoma Qur'ani Msahafuni kunaondosha Unyenyekevu kwa njia yoyote ile.

Masuala haya yanatofautiana kwa kutofautiana watu, bali na mazingira yao pia, kisha hili jambo letu ni athari ya huko kusihi Swala na kutokusihi kwake, na kukosekana unyenyekevu hakuathiri kusihi kwa Swala; kwani hiyo sio katika nguzo au masharti ya kusihi kwa Swala. Basi Mtume S.A.W., ameswalia katika nguo ya kianbaji iliyotengenezwa kwa sufi na akasema: "Nguo hiyo ilinishughulisha hapo kabla katika Swala yangu"[33] na ingawa ya hayo hakuikataza Swala yake, na hakutaja kwamba hiyo inabatlisha Swala. Na haikutajwa kwamba alirudia Swala. Na hata kama tutakubali ya kwamba Usomaji wa Msahafu katika Swala unaondosha unyenyekevu haiwezekani kuitumia hiyo kama dalili ya kuivuruga Swala.

Na wafuasi wa Madhehebu ya Maliki wametofautisha baina ya Swala ya Faradhi na Swala ya Sunna, na wakaona ya kwamba inachukiza kwa mwenye kuswali kusoma Msahafu katika Swala ya Faradhi iwe mwanzo wa Swala, katikati ya Swala, na inachukiza pia katika Sunna iwapo ataanza wakati anaiswali, kutokana na kujishughulisha kwake kwa kiwango kikubwa, na inajuzu kufanya hivyo katika Swala ya Sunna ikiwa ataaanza kusoma Msahafu kuanzia mwanzo wa Swala yake na hili halichukizi; kwani ya kwenye Swala ya Sunna yanasameheka ndani yake yale yasiyosameheka katika Swala ya Faradhi.[34]

Na imetajwa katika kitabu cha: [Al Modawanah] Ibn Al Qasim amesema: Nilisema kwa Maliki kwa mwanamume anayeswali Swala ya Sunna na anashuku katika herufi, na ana Msahafu ulio wazi, je atazame Msahafuni kujua herufi? Basi akasema: hapana asitazame katika herufi hiyo lakini lazima atimizie Swala yake kisha atizame Msahafu. Akasema: Na Maliki akasema: Hakuna ubaya wowote kwa Imamu kuwasalisha watu Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kusoma Msahafu, nikamwambia Ibnul Qaasim: kwanini Maliki amelipanua sana jambo hili na akaona kwamba inachukiza kwa yule mwenye kuangalia herufu moja? Akajibu kwamba: kwa sababu huyu alichokianza tangu mwanzo ni kuangalia.

Akasema: Na Maliki akasema: Hakuna ubaya wowote kwa Imamu kuwaswalisha watu Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kusoma Msahafu, na katika Swala ya Sunna. Ibn Al Qasem akasema: akachukiza hayo katika Sala ya Faradhi"[35]

Na chaguo hili la Imamu Maliki la kukarahisha linakuja pale kazi inayofanywa inapokuwa ya Kipuuzi, ambayo ni mchezo na ni kazi isiyo na faida yoyote, na kwa ajili hiyo huwa inachukiza kwa mwenye Kuswali kufanya jambo kama hilo; kwa jinsi jambo hili kinachokwenda kinyume na unyenyekevu. Ama kusoma Msahafuni kwa haja inayokusudiwa. Na kila kilicho katika mlango huu hakuna ubaya wowote wa mtu kukifanya na asili yake ni yale yaliyopokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W, kwamba yeye alivua ndala zake wakati wa Swala, pindi aliposhushiwa wahyi kwamba ndala hizo zina uchafu.[36] 

Na Maswahaba mawili kutoka madhehebu ya Kihanafi Abu Yusuf Al Qadhiy na Mohammad Bin Al Hassan As Shaibaniy walikwenda kwamba Hakika usomaji wa Qur'ani Tukufu katika Msahafu ni jambo linalochukiza kwa vyovyote vile, iwe katika Swala ya Faradhi au ya Sunna, lakini hakuharibu Swala; kwani kufanya hivyo ni ibada inayopelekea ibada nyingine, na uchukizaji wake unafanana na wafanyavyo Watu wa Kitabu.[37]

Na anajadili hayo kwa kusema kwamba kupatikana kwa yanayofanana na yale wayatendayo Watu wa Kitabu yanakatazwa kama mtendaji atakuwa amekusudia kupatikana mfanano huo; kwani mfanano huo ni mwingiliano, na Mada hii inaonesha mfungamano wa nia na mwelekeo wa  kuelekea kwenye lengo la kitendo hicho na mahangaiko yake, na katika Misingi ya Kisharia ni kuzingati kusudio la Mbeba majukumu.

Na inaashiria kwa hayo pia yaliyopokelewa na Jaber R.A. akasema: Mtume S.A.W, alilalamika tukaswali nyuma yake hali ya kuwa ameketi na akatugeukia na akatuona tukiwa tumesimama na akatuashiria tukae na tukakaa kisha akatoa Salamu na kusema: mmekaribia hapo  kabla mnaweza kufanya vitendo vya Wafursi na Warumi ambao wanawasimamia wafalme wao na hali ya kuwa wafalme hao wameketi, msifanye hivyo, wafuateni Maimamu wenu, wakiswali wamesimama basi nanyi Swalini mkiwa mmesimama, na wakiswali wamekaa basi nanyi Swalini hali ya kuwa mmekaa.[38]

Na inakaribia kumaanisha kuthibitisha juu ya kutoweka kwa Hadithi yake pamoja na kujongelea kutuka kwake, na kitendo cha Wafursi na Warumi ni kitendo kilichotokea kiuhalisia lakini Maswahaba hawakukusudia kufananisha, na wasifu huo umetoweka kwao kisharia, kwa hivyo, Mtu anayeswali ambaye anasoma Msahafu hawazii kujifananisha nao mbali hata na nia yake.[39]

Ibn Najiim alisema: Tambua kwamba kujifananisha na watu wa Kitabu hakuchukizi katika kila kitu, na sisi tunakula na kunywa kama wafanyavyo wao, bali hakika mambo yalivyo, jambo lililo haramu ni kujifananisha nao katika yale yaliyokatazwa na yale yanayolengwa kuwa ndio hasa mambo ya kujifananisha nao, na kwa sababu hiyo, kama isingekusudiwa kujifananisha isingelichukiza kwao.[40]

Na kwa mujibu wa yote yaliyotangulia, yanathibitika yale tuliyoyasema ya kwamba Kusoma Msahafu katika Swala kunaweza kukawa ni Faradhi, au Sunna, ni sahihi na kunajuzu kisheria na wala hakuna chukizo lolote ndani yake, sembuse iwe ni katika kuiharibu Swala.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi

Imeandikwa na: Ahmad Mamduh na Mustafa Abdulkariim. Katika: Tarehe 29, mwezi wa Ramadhan, ,waka wa 1427, iliyoafikiana na tarehe ya 22, mwazi wa Oktoba, mwaka wa 2006.

 

[1] - Inawafikiana nayo, imesimulia na Al Bokhariy (5111) na Muslim (797)

[2] - Imesimuliwa na At Termeziy (2910), na akasema kwamba hadithi hiyo ni sahihi na ngeni.

[3] - kwa ajili ya hayo tazama kitabu cha: "At Tibian katika Adabu ya  wenye Qura'ni" kwa Imamu An Nawawiy.

[4] - Ilihangaika na Al Bokhariy katika sahihi yake, kwa kauli ya kukaza kutoka kwa Aisha R.A. katika Malngo uiamau wa mtumwa kwa bwana wake- na iliwasiliana na Al Baihaqiy katika Sunnan zake 253/2, na Ibn Abi Shaibah katika Muswanaf yake 235/2. Al Hafedh Ibn Hajar akasema katika kitabu chake: Taghliq Ataliq 291/2, " hiyo ni athari sahihi"

[5] - Kitabu cha: "Al Mudawanah Al Kubra" 288-289/1, na Al Mughniy 335.

[6]  - Kitabu cha: "Ihiyaa Aulum Ad Deen", 229/1

[7] - Kitabu cha:: "Al Mughniy" 336/1

[8]  - Kitabu cha:: "Al Mughniy" 336/1

[9]  - Kitabu cha: Al Majmu' 27/4

[10] - Kitabu cha: "Kashaafu Al Qinaa' toka Matni ya Al Iqnaa" kwa Al Bahutiy, 384/1

[11] - Iliafikiana nayo, Imesimulizwa na Ak Bokhariy (1140), Na Muslim (837)

[12]  - Al Hemaliy 365/2, 141/3

[13]  - Imeafikiana nayo, imepokelewa na Al Bokhariy (494), na Muslim (543)

[14]  - Imeafikiana nayo, imepokelewa na Al Bokhariy (135), na Muslim (763)

[15] - Inapokelewa na Abu Dawud (792) na At Tirmiziy (336)

[16] - Imepokelewa na wanne; Abdu Dawud (786), At Tirmiziy (355), na alisema kwamba ni sahihi na Hasan, na An Nasaiy (1187) na Ibn Magah (1235).

[17] - Imeafikiana nayo, imepokelewa na Al Bokhariy (479), na Muslim (782)

[18] - Kitabu cha: Al Majmuu' 28/4

[19]  - Imepokelewa na Al Bokhariy (717)

[20] - Imeafikiana nayo, imepokelewa na Al Bokhariy (366), na Muslim (556)

[21] -  Kitabu cha: Qawaed Al Ahkaam 54/1

[22] - Kitabu cha: "Al Bahr Ar Ra'eq Sharhu Kanz Ad Daqa'eq" kwa Ibn Najiim, 11/2. Na Al Athar imepokelewa na Ibn Ani Dawud katika kitabu cha: [Al Maswahef] Uk. 655

[23] - Kitabu cha: [Tabeienu Al Haqa'q Sharhu Kanz Ad Daqa'q] kwa Az Zulai'iy 159/1.

[24] - Kitabu cha: [Bada'e As Swana'e] 241/1, na Kitabu cha: [Al Fatawa Al Hindiyah] 101-102/1.

[25] - Kitabu cha: [Bada'e Aswana'e] 236/1.

[26] - Rejea kitabu cha: Al Mabswutw 194-195/1,  na kitabu cha: Al Enayah, 399-400/1

[27] - Kitabu cha: [Bada'e As Swana'e] 236/1.

[28] - Imepokelewa na Abu Dawud (907), na Al Baihaqiy katika Sunan zake 211/3.

[29] - Athari hizo za mwisho zimepokelewa na Al Baihaqiy katika Sunan zake 212/2

[30] - Kitabu cha; [Al Mughniy] 298/1

[31] - Kitabu cha: [Al Enaya Sharhu Al Hedayah] 331- 332/1.

[32] - Kitabu cha: At Tareekhu Al Kabiir 115/8, kitabu cha Tahzeebu At Tahzeeb 427/10

[33] - Inaafikiana nayo, impokelewa na Al Bukhariy (366) na Muslim (556).

[34] - Kitabu cha: [Manhi Aj Jalili katika Sharhu ya Mukhtswar Khlili], 345/1. Na Kitabu cha: [Sharhu Al Kharashiy Ala Al Mukhtswar] 11/2.

[35] - Kitabu cha: [Al Modawanah] 288/1

[36] - Imepokelewa na Abu Dawud (650), Na Ahmad katika Musnadi yake 92/3, kutoka kwa Abi Saidi Al Khudriy R.A.

[37] - Kitabu cha: [Al Bahr Ar Raai'q]11/2.

[38] - Imepokelewa na Muslim (624)

[39] - Rejea yaliyoandikwa na As Sayed Abdulhay Bin As Swdeq katika kitafiti kamili katika kitabu chake cha: [Hukumu ya Moshi na Kuuomba] Ku. 39-49,  juu ya hukumu ya kufananishia Watu wa Kitabu.

[40] - Kitabu cha: [Al Bahr Ar Raai'q]11/2.

Share this:

Related Fatwas