Tukio la unyanyasaji mwanamke

Egypt's Dar Al-Ifta

Tukio la unyanyasaji mwanamke

Question

Nini hukumu ya unyanyasaji mwanamke au kumfanyia maudhi ya kimaneno au kimaana.

Answer

Mwanamke ni nusu ya jamii, naye ni mwenza wa mwanaume katika ubinadamu wake, na nafasi yake umuhimu wake haupishani na nafasi ya mwanaume, naye ni nusu ya jamii na mama wa nusu ya pili, Mtume S.A.W amefanya kipimo cha ubora wa wanaume kinapatikana katika kumfanyia wema mwanamke, anasema:

 “Waumini waliokamilika Imani ni wale wenye maadili mema, na wabora wenu ni wale wabora kwa wake zao”. Imepokewa na Tirmidhy ndani ya kitabu cha Al-Jaamii. Kutokana na hivyo Uislamu umehimiza uharamu wa unyanyasaji au kumfanyia maudhui, kutoka kwa Maakal Ibn Yasaar R.A amesema: Mtume S.A.W amesema:

 “Kuchomwa sindano ya chuma kichwani kwa mmoja wenu ni bora zaidi kuliko kumgusa mwanamke si halali kwake”. Imepokewa na Twabrany.

Share this:

Related Fatwas