Dhikiri / kumtaja Allah kwa kila h...

Egypt's Dar Al-Ifta

Dhikiri / kumtaja Allah kwa kila hali

Question

Je, inajuzu kwa  mtu mwenye  janaba kusoma tasbihi na kumdhukuru Allah?

Answer

Kumdhukuru Allah ni ibada ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu ameipanua katika wakati wake, hali yake, na masharti yake. Ibada hii inapendekezwa katika kila hali na wakati kwa ujumla, katika hali ya usafi kamili au vinginevyo. Kwa hivyo amri ya kumdhukuru Allah ilikuja pasipo na kifungu, kwa hivyo hii inaashiria kuruhusiwa kwa kumdhukuru Allah katika hali yoyote; Mwenyezi Mungu amesema: {Enyi mlio amini! Mdhukuruni Mwenyezi Mungu kwa wingi wa kumdhukuru. (41) Na mtakaseni asubuhi na jioni.} [Al-Ahzab: 41-42]. Mwenyezi Mungu anasema pia:{Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi na kukhitalifiana usiku na mchana ziko Ishara kwa wenye akili. (190) Ambao humkumbuka Mwenyezi Mungu wakiwa wima na wakikaa kitako na wakilala, na hufikiri kuumbwa mbingu na ardhi, wakisema: Mola wetu Mlezi! Hukuviumba hivi bure. Subhanaka, Umetakasika! Basi tukinge na adhabu ya Moto} [Aali Imraan: 190-191].

Mtume (S.A.W), alikuwa akimdhukuru Allah, katika hali zake zote. Imepokelewa kutoka kwa Bibi Aisha, Mama wa Waumini, (R.A), amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W), alikuwa akimdhukuru Mwenyezi Mungu katika kila wakati wake.” Imesimuliwa na Imam Muslim.

Imamu An-Nawawiy alitaja kwamba makubaliano ya wanachuoni juu ya kuruhusiwa kumdhukuru Allah kwa moyo na ulimi kwa yule ambaye hana udhu, mwenye janaba, mwenye hedhi, na wanawake baada ya kuzaa. Amesema katika kitabu chake “Al-Adhkaar” (uk. 11): [Wanachuoni wamekubaliana kwa kauli moja katika kujuzu kwa kumdhukuru Allah kwa moyo na ulimi kwa yule ambaye hana udhu, mwenye janaba, mwenye hedhi, na wanawake wa baada ya kuzaa, na hiyo ni katika kumtakasa Allah, kumsifu, kumhimidi, kupiga takbir, na kumswalia Mtume wa Mwenyezi Mungu, (S.A.W), dua na kadhalika.].

Na Mwenyezi Mungu pekee ndiye Anayejua Zaidi.

Share this:

Related Fatwas