Elimu ya Watu Wazima

Egypt's Dar Al-Ifta

Elimu ya Watu Wazima

Question

Kuna uhalali gani wa elimu ya Watu Wazima na kuwafuta ujinga 

Answer

Elimu ya Watu Wazima na kufuta ujinga wa kutojua kusoma na kuandika ni jambo linalohitajika Kisharia, kutokana na Aya pamoja na Hadithi zinazoonesha umuhimu wa elimu na kujifunza pamoja na heshima ya watu wake, na kuitafuta elimu hakuishii kwenye kiwango fulani au umri fulani, kwani hakuna tofauti katika kuitafuta elimu kati ya mdogo na mkubwa, wala kati ya mwanaume na mwanamke, kwani wote katika kuitafuta elimu jukumu lao lipo sawa. Imepokewa kuwa Wanachuoni wengi na Wasomi wakubwa wa Umma hawakutafuta elimu isipokuwa wakiwa katika umri mkubwa, hakuna hata mmoja wao aliyeona aibu kwa utu uzima wake au nafasi yake.

Share this:

Related Fatwas