Utafiti Kuhusu Mufti wa Lazima

Egypt's Dar Al-Ifta

Utafiti Kuhusu Mufti wa Lazima

Question

Utafiti Kuhusu Mufti wa Lazima

Answer

Umeandaliwa Na:

Ahmad Mahmoud Ally.

Mtafiti wa kitengo cha tafiti za Kisharia Ofisi ya Mufti wa Misri.

Utangulizi…

Shukrani zote anastahiki Mwenyezi Mungu, rehma na amani zimuendee Mtume wa Mwenyezi Mungu pamoja na watu wa nyumbani kwake Maswahaba wake na wale wenye kumfuata.

Baada ya Utangulizi:

Utaratibu wa Mwenyezi Mungu kwa mwanadamu umefanyika kwa kuifanya asili ya maumbile yake kuelekea kwenye utashi wa kupenda furaha, na Mwenyezi Mungu amemjengea njia kuelekea kwenye hilo, hivyo akawapeleka Mitume akateremsha Vitabu na kuweka Sharia ili kukidhi mahitaji ya kimaumbile ya mwanadamu na kufungua njia mbele yake kwa lengo la kuifikia kwenye furaha ya muda mrefu.

Ujumbe wa Uislamu ndio ujumbe wa mwisho wa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu Mtukufu akampitisha Mja wake wa kubeba Ujumbe huu mkubwa ambaye ni kiumbe wake bora na ampendaye zaidi, ambaye ndiye mwisho wa Mitume na Manabii naye ni Mtume wetu Muhammad S.A.W. Ujumbe huu umekuja na kila kinachohitajiwa na maumbile ya mwanadamu, umekuja ukiwa unasema ukweli wenye kuongoza kwenye ukamilifu na kufikisha kwenye furaha.

Ukweli wa dini na akida zake pamoja na miongozo yake, ni kwenye misingi na hukumu zake, na furaha ya kweli duniani na Akhera ni kwa mwenye kuamini imani ya Uislamu, na kuyafanyia kazi mafundisho yake miongoni mwa maadili na hukumu…

{Enyi watu! Yamekujieni mawaidha kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na ponyo la kuponyesha yaliyomo vifuani, na uwongofu, na rehema kwa Waumini * Sema: Kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na rehema yake! Basi nawafurahi kwa hayo. Haya ni bora kuliko hayo wanayo yakusanya} Yuunus: 57, 58.

Msingi wa maarifa kwa Waislamu ni: Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Sunna za Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W kutokana na misingi hiyo hufahamika akida na mambo ya dhahania, na hutolewa kanuni na hukumu, pamoja na kupatikana maadili mema…

Mwenyezi Mungu Mtukufu Amemuamrisha Mtume wake wa mwisho kufikisha Ujumbe na kuwalezea watu, ikiwa ni huruma yake Mola Mtukufu na ukarimu, wala amri haikuhusisha ufikishaji tu bali ufikishaji na ufafanuzi…

{Nasi tumekuteremshia wewe Ukumbusho ili uwabainishie watu yaliyo teremshwa kwao, wapate kufikiri} An-Nahl: 44.

{Na hapana juu ya Mtume ila kufikisha Ujumbe wazi wazi} An-Nuur: 54.

Katika Aya hizi kuna dalili kuwa Kitabu Kitukufu cha Mwenyezi Mungu kimekusanya ukweli hekima na maana isiyoweza kufahamika kwa yeyote kwa kusoma tu maneno na misemo, bali siku zote inakuwa nyuma ya misemo kuna ishara na siri za kina, kwani Kitabu cha Mwenyezi Mungu ni hazina ya siri zisizoisha, na msaada wa uwongofu usiokwisha…

{Sema: Lau kuwa bahari ndio wino wa maneno ya Mola wangu Mlezi, basi bahari ingeli malizika kabla ya kumalizika maneno ya Mola wangu Mlezi, hata tungeli ileta mfano wa hiyo kuongezea} Al-Kahfi: 109.

Hivyo ubainifu ndio jambo ambalo Mwenyezi Mungu alimsimamisha Mtume wake Mtukufu kuongoa watu na kuwaongoza kwenye njia iliyosahihi.

Kutokana na mahitaji ya mwanadamu, ubainifu ni jambo endelevu kizazi baada ya kizazi, na maisha ya Mtume S.A.W katikati ya watu yalikuwa na mipaka na mwisho, Mwenyezi Mungu ametuongoza turithi kazi ya kufikisha na kubainisha, tukiwa waaminifu juu ya Ujumbe wake baada ya Manabii, Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema:

{Na pale Mwenyezi Mungu alipo fungamana na waliopewa Kitabu kuwa: Lazima mtawabainishia watu, wala hamtakificha} Aal-Imran: 187. Akasema tena:

{Basi waulizeni wenye elimu ikiwa nyinyi hamjui} Al-Anbiyaai: 7.

Na Mtume S.A.W amesema:

“Hakika Wanachuoni ni warithi wa Manabii, na Manabii hawakuwarithisha Dirham wala Dinar bali wamerithi elimu, basi mwenye kuichukuwa atakuwa amepata kwa bahati kubwa” ([1]).

Hivyo tunafahamu kuwa akida ya Uislamu na ukweli wake hukumu zake na makusudio yake ni maalumu kwa ubainishaji na ufafanuzi wake kwa Wanachuoni, na hii ni katika huruma ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja, si  jambo jepesi kwa kila mtu kujitenga ili kujikita zaidi katika utafiti wa elimu na vyombo ambavyo vitamuwezesha kwenye kufanya Ijitihadi na ufahamu sahihi wa ukweli wa Qur`ani Tukufu hukumu zake na maana zake, lau Mwenyezi Mungu angelazimisha hilo kwa watu basi lingekuwa gumu kwao na kukinzana na kauli ya Mola Mtukufu:

{Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini} Al-Hajji: 78. Lakini Mwenyezi Mungu ameulazimisha Umma kuwepo baadhi yao Wanachuoni wenye weledi wanaobeba ubainifu na ufafanuzi wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume wake S.A.W na akalazimisha watu wengine katika Umma warejee kwao kwa kujifunza kuuliza na kutaka Fatwa.

{Wala haikuwa kwa Waumini kutoka wote. Lakini kwanini hawatoki baadhi katika kila kundi miongoni mwao, wakajifunze vyema Dini, na kisha waje kuwaonya wenzao watakapo warejea, ili wapate kujihadharisha} At-Tawbah: 122.

Kwa maelezo haya yanaonesha wazi kiwango cha mahitaji ya Umma kuhitaji Wanachuoni Wanaojitihada na sehemu ya kupata Fatwa za dini, ili watu kufundishwa yale yaliyoletwa na Sharia Tukufu miongoni mwa ukweli wa hukumu na maadili yanayosimamia maisha yao kwa mfumo wa Mungu, na kuyafikia masilahi katika dunia yao na Akhera yao, na kwa hilo kufikia furaha ya kweli ambayo wanaihitaji kwa maumbile ambayo Mwenyezi Mungu amewafanyia na kuwatukuza kwayo…

{Na hakika tumewatukuza wanadamu, na tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tulio waumba} Al-Israa: 70.

Imamu wa Al-Haramain Abul Maaly Al-Juwainy anasema:

“Wabeba Sharia na kuwa nayo ni Mamufti walio na vigezo vya elimu za kufanya Jitihada, na wenye ucha-Mungu na kufuata njia iliyo sawa” ([2]).

Dibaji:

Katika maelezo yaliyotangulia ni wazi kuwa utoaji Fatwa una nafasi kubwa, na umuhimu wake katika Uislamu haujifichi, nao ni kwamba Sharia imetoa jukumu la utekelezaji wake kufanywa na Wanachuoni, na wala si kila Msomi wa elimu mbalimbali za Kiislamu anafaa kubeba jukumu hili, hivyo kumekuwa na vigezo maalumu kwa mtoa Fatwa miongoni mwa Wanachuoni, muhimu zaidi ni uwezo wa kufanya Jiitihada. Wanachuoni wametenganisha kati ya aina mbili za Jitihada na wakaziita Jitihada ya moja kwa moja, na Jitihada funganishi.

Matukio yamelazimisha Waislamu wachache wa kufanya Ijitihada au kukosekana kabisa kwa mtazamo wa baadhi, jambo linalofanya kigezo cha Ijitihada kuwa ni kigumu kinachowaingiza Waislamu kwenye uzito, mahitaji ya Waislamu katika kila nchi kuwa na Mamufti ambao watawaelezea watu ukweli wa Uislamu hukumu na Sharia zake ni mahitaji makubwa na muhimu sana, ili maisha yao yapate kusimama na kufuata mfumo wa Mungu ambao unajenga maisha yao na Akhera yao.

Uislamu umekuja kuwa ni uongofu na rehma kwa walimwengu, rehma hii imeenea maadili mema katika Sharia za Uislamu hukumu zake na katika yale yanayolinganiwa, miongoni mwa hayo ni pamoja na Sharia kufanya wepesi na kuondoa uzito kwa wapewa jukumu, na kwa asili hii zimetengenezwa kanuni nyingi za Fiqhi ya Kiislamu, kama kanuni:

(Uzito unaleta wepesi) (Madhara huondoshwa) (Madhara hayaondoki kwa madhara mengine) (Pindi yanapogongana maovu mawili huangaliwa lenye madhara makubwa zaidi na kufanywa lilo jepesi) (Jambo la dharura uhalalisha lilo haramu) na (Lilo jepesi haliondoki kwa lilo zito).

Kutokana na kanuni hizi na zinginezo ambazo zimeletwa na Wanachuoni kutoka kwenye Sharia na mantiki ya Uislamu, Jamhuri ya Wanachuoni imekubaliana usahihi kwa asiye Mwanajitihada kushika nafasi ya utoaji Fatwa kwa masharti tutakayoyaleza, na hilo ili kuurahisishia Umma na kulinda dini, na kufanyia kazi ucha-Mungu inavyowezekana kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{Basi mcheni Mwenyezi Mungu kama mwezavyo} At-Taghabun: 16. Na kauli ya Mtume S.A.W:

“Pindi ninapowakataza jambo basi jitengeni nalo, na ninapowaamrisha jambo basi litekelezeni kadiri muwezavyo” ([3]).

Pembezoni mwa haya baadhi yao wamesema haifai kushika nafasi ya Fatwa kwa asiyekuwa Mwanajitihada tofauti na mtazamo wa Wanachuoni wakubwa.

Na katika uchambuzi huu tutazungumzia mielekeo ya Wanachuoni katika masuala haya muhimu, ili tupate kuona dalili zilizotolewa na kila kundi pamoja na kujadili hilo ili kuweza kuona kauli zenye nguvu… lakini kwa kuwa hukumu ya kitu ni sehemu ya mtazamo wake basi imekuwa ni lazima kwetu kuleta tafiti mbalimbali zinazoweka wazi makusudio ya (Umuhimu wa Mufti) kabla ya kuhukumu kati ya kauli za rai, hivyo chambuzi hizi zinagawanyika sehemu kuu nne kama ifuatavyo:

Uchambuzi wa Kwanza: Maana ya utoaji Fatwa.

Uchambuzi wa Pili: Maana ya Mufti.

Uchambuzi wa Tatu: Maana ya Mufti wa lazima.

Uchambuzi wa Nne: Hukumu ya Mufti wa lazima kushika nafasi ya utoaji Fatwa.

Uchambuzi wa Kwanza: Maana ya Uoajifat’wa.

Kilugha na Kimsamiati:

Neno kutoa Fat’wa na Fat’wa yenyewe kwa upande wa lugha: Ni maneno mawili maana zake zipo karibu sana, kwani maana ya neno Fat’wa upande wa lugha: Ni jina la kisoukomo cha maana ya neno utoaji Fat’wa, na uwingi ni: Fat’wa, husemwa: Nimetoa Fat’wa pindi ninapojibu maswali, na husemwa pia: Nimetoa Fat’wa kwa ndoto aliyoiona, ni pale ninapomueleza, na katika kauli yake Mola Mtukufu akielezea:

{Enyi waheshimiwa! Nambieni maana ya ndoto zangu, ikiwa nyinyi mnaweza kuagua ndoto} Yusuf: 43.

Na maana ya kutaka Fat’wa kwa upande wa lugha:  Ni kutaka jibu la jambo lililotengenezwa, na katika kauli ya Mwenyezi Mungu:

{Wala usiulize habari zao kwa yeyote yule} Al-Kahfi: 22. Inaweza kuwa kwa maana ya swali tu, nayo ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{Hebu waulize: Je! Wao ni wenye umbo gumu zaidi au hao wengine tulio waumba. Hakika Sisi tuliwaumba wao kwa udongo unao nata} As-Swafatat: 11.

Na katika maana ya Kimsamiati: Hubainisha hukumu ya Kisharia kwa dalili kwa mwenye kuuliza kuhusu matukio yaliyotokea, au kuhusu hukumu ya Kisharia iliyotengenezwa ([4]).

Fat’wa ni ubainifu wa hukumu ya Sharia katika tukio linalohusiana na Sharia, na ubainifu huu lazima uwe umetokana na dalili inayozingatiwa Kisharia, hivyo Fat’wa kabla ya kutolewa hupitia hatua mbalimbali tutazizungumzia hapo baadaye:

Hatua za Fat’wa:

Fat’wa hupita katika ufahamu wa Mufti kwenye hatua nne kuu, baada ya hapo hutoka katika sura yake ambayo anaisikia au kuiona mwenye kutaka Fat’wa, na hatua hizi nne ni: Hatua ya kufikiri, hatua ya kuendana na Fat’wa, hatua ya kutohoa hukumu na hatua ya kutoa Fat’wa.

Hatua ya Kwanza: (Kufikiri).

Ndani ya hatua hii hufikiriwa  masuala ambayo yameletwa na muulizaji, na kufikiri sahihi kunakoendana na hali halisi ni msingi mkuu wa kutolewa Fat’wa sahihi inayoendana na hali halisi, na kasoro za kufikiri kimsingi hutokea kwa muulizaji, lakini Mufti anapaswa kuchunguza kupitia swali lenyewe pande nne ambazo hutofautiana hukumu kwa kutofautiana pande hizo, nazo ni upande wa wakati sehemu mtu na hali, kama vile Mufti anapaswa kuwa na uhakiki kufungamana na swali kwa mtu mmoja mmoja au Umma, kwa sababu Fat’wa hutofautiana kwa kutofautiana mambo haya mawili.

Kufikiri kunaweza kuwa kwenye kitendo kilichotokea au kwa jambo linalokadiriwa bado halijatokea, wakati huo ni lazima kuchunga matokeo na mahusiano, kwa kiwango cha uwezo wa Mufti kufikiri ndipo Fat’wa huwa karibu zaidi na kufikia makusudio ya Kisharia na kufikia masilahi pamoja na kuondoa uovu.

Hatua ya Pili: (Kuendana).

Nayo ni kukubaliana sura husika na milango ya Fiqhi na masuala yake, kwa mfano kuendana kwa masuala ni mlango wa mashirikiano na wala si mlango wa ibada, na hatua hii huandaliwa ili kuelezea hukumu ya masuala ya Kisharia, na kuendana na fat’wa ni katika kazi za Mufti, na kunahitaji mtazamo wa kina.

Wanachuoni wametofautiana hatua hii, na tofauti hii ni moja ya sababu za kutofautiana Fat’wa, kauli yenye nguvu wakati huo kati ya wenye kutafautiana inarejea kwenye nguvu ya dalili yeyote miongoni mwao, na inarejea kwenye kina cha ufahamu wa uhalisia, na inarejea kwenye kufikia makusudio na masilahi pamoja na kuondoa matatizo, nayo ndio malengo makuu ya Sharia.

Hatua ya Tatu: (Kutohoa hukumu).

Mufti baada ya hatua ya kufikiri tukio, na kuweza kuainisha katika ufahamu wake vipengele vye taathira na kuainisha eneo la kifiqhi ambalo anatafiti vipengele hivi, kinachobakia kwake ni kuleta hukumu ya Kisharia kwa vipengele hivyo kutokana na dalili za kina, na hii ni hatua ya tatu na muhimu ya Fat’wa.

Na hukumu ya Kisharia huchukuwa dalili za hukumu iliyopitishwa katika misingi ya Fiqhi kama Qur`ani, Hadithi, Ijmai, Qiyas, na misingi mengine, na inapaswa kwa Mufti kuwa mwenye kufahamu dalili hizi na taratibu zake, na maana ya maneno ya Kiarabu njia za kuleta hukumu, pamoja na kutambua matukio kwa ufahamu sahihi.

Hatua hii inakuja kwa kupata elimu ya makusudio, kama vile elimu ya misingi, fiqhi, lugha, Hadithi na mifano yake, kujifunza kutoa Fat’wa ambayo anaianza kwa kuwa na umiliki na uwezo, vile vile kujipamba na ucha-Mungu pamoja na matendo yanayonufaisha watu, hivyo hakuna shaka kuwa watu wacha-Mugu macho yao huangaziwa na nuru za Sharia na kushikamana na ukweli wake zaidi kuliko watu wengine.

Hatua ya Nne: (Kutoa Fat’wa).

Nayo ni hatua ya kuleta hukumu ambayo imefikiwa na Mufti katika tukio ambalo amelifahamu, kisha kumfahamisha hukumu mwenye kutaka Fat’wa, hapo ni lazima kuhakikisha kuwa kinachotolewa fat’wa hakipingani na makusudio ya Sharia kwa kubatilisha, wala kwenda kinyume na Andiko wala makubaliano ya Wanachuoni kwenye hilo wala kanuni ya kifiqhi, ikiwa kutapatikana kitu chochote katika hivi basi ni jukumu lake kurejea fat’wa yake, ili isipingane na mambo yaliyothibiti Kisharia.

Tofauti kati ya utoaji Fat’wa, Fiqhi, hukumu na Jitihada:

Ili kuweka wazi zaidi maana ya Fat’wa tunahitaji kutenganisha kati ya maana yake na maana zingine zinazoingiliana nazo wakati mwingine, na maana hizi zinaweza kuwa maana ya Fiqhi, hukumu au Jitihada...

Fiqhi: Ni elimu ya hukumu za Kisharia kivitendo itokanayo na dalili.

Fat’wa: Ni ubainifu wa hukumu ya Kisharia yenye dalili kwa mwenye kuuliza.

Hukumu: Ni wajibu wa mtu aliye na usimamizi wa kutoa Maamuzi ya Kisharia baada ya kupelekwa kwake.

Msomi wa Fiqhi: Anatoa hukumu za Mwenyezi Mungu Mtukufu kutokana na dalili, na hukumu hizo hufikia makusudio jumla ya Sharia, muelekeo wake wa kwanza unakuwa kwenye Andiko ili kutoa kanuni na hukumu za Kifiqhi ambazo zinapatikana, na wala sio nafasi ya Mwanachuoni wa Fiqhi kufanya tafiti ya hali iliyopo, lakini pindi anapoelekea kufanya utafiti wake basi hufanya hivyo ili kuona kiwango gani kitamuwezesha kufanyia kazi kanuni na hukumu ambazo amezitoa kwenye tamko kwa sura tofauti, ili kufahamu kupitia utekelezaji kanuni zengine mpya, yote haya lengo lake ni kuweka kanuni ili kumuwezesha Mufti kuzitumia pale anapoangalia masuala mapya yasiyo na Maandiko.

Ama Mufti: Kwanza huwa anaelekea kwenye tukio ili kutafiti, kisha hugeukia kwenye Fiqhi ili kuchukuwa hukumu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwenye hali kama hii ili kufikia makusudio ya Sharia.

Ama Kadhi: Yeye huingilia kati ili kubalidilisha tukio na kulazimisha pande zenye kuvutana kwenye hukumu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ambayo imewekwa na Mwanafiqhi na kutolewa Fat’wa na Mufti, wakati mwingine huingiliana nyazifa hizo zenyewe kwa zenyewe hivyo Kadhi hufanya kazi ya Mwanachuoni wa fiqhi au Mufti, na Mwanachuoni wa fiqhi hufanya kazi ya Mufti, isipokuwa bado kutaendelea kuwepo tofauti kati ya maana hizo na nyadhifa zinazoendeshwa, na kwa kiwango gani cha wajibu kwa wengine.

Inawezekana kuyaweka wazi tuliyoyataja kwa mifano ifuatayo:

Kwa mfano Mwanachuoni wa fiqhi anasema: Pombe ni haramu kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: 

{Bila ya shaka ulevi, kamari, kuabudu masanamu na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shetani. Basi jiepusheni navyo} Al-Maidah: 90.

Mufti anasema kwa mwenye kutenzwa nguvu baada ya kufahamu hali yake na kutekeleza kanuni ya Kisharia ya wajibu wa kufanya ovu lenye madhara madogo kati ya maovu mawili na kuondoa baya zaidi kati ya mabaya mawili: Kunywa pombe pamoja na uharamu wake ili usife.

Na Kadhi anatekeleza adhabu kwa mwenye kunywa pombe, wala hatekelezi adhabu kwa mtenzwa nguvu, na anatoa hukumu ya kumwagwa pombe.

Maelezo yaliyotangulia yanaweka wazi kuwa Mwanachuoni wa Fiqhi anazifahamu hukumu, Mufti anazielezea hukumu, na kadhi ni mtekelezaji wa hukumu hizo, hivyo ana haki ya kutoa adhabu ya kifungo na ile aionayo yeye, kama vile kutekeleza adhabu na kutekeleza kisasi.

Ama Jitihada: Yenyewe ni Mwanafiqhi kufanya juhudi katika kupata hukumu ya Kisharia.

Tofauti kati yake na Utoaji Fat’wa: Ni kuwa utoaji Fat’wa unakuwa kwa kile kilichofahamika moja kwa moja au kidhahania, ama Jitihada haiwi katika hukumu za moja kwa moja au kilichofahamika katika dini kuwa ni jambo muhimu, hilo ni katika lisilo na Jitihada ndani yake, lakini yafaa kutoa Fat’wa kwa maana kufikisha hukumu yake kwa asiyejua.

Pia miongoni mwa tofauti: Ni kuwa jitihada inakamilika kwa Mwanafiqhi kufikia hukumu yeye mwenyewe, wakati fat’wa haikamiliki isipokuwa kwa kufikisha hukumu kwa muulizaji.

****

Uchambuzi wa Pili: Maana ya Mufti.

Tumefahamu katika uchambuzi uliopita maana ya Fat’wa, nayo ni jukumu la lazima kufanywa na mtu haliwezi kusimama lenyewe, ni juu yetu kufahamu ni nani mtu huyo ambaye anafaa kutakiwa Fat’wa na watu, na inafaa kwake kuwatolea Fat’wa, na inafaa kwa kiongozi wa nchi kumteua katika majukumu ya utoaji Fat’wa?

Haya tutayazungumzia kwa utashi wake Mwenyezi Mungu Mtukufu kwenye uchambuzi huu:

Tumefahamu katika maelezo yaliyotangulia kuwa utoaji Fat’wa ni kubainisha kwa dalili hukumu ya Kisharia kwa aliyeuliza, hivyo tunafahamu kuwa Mufti ni mtu ambaye anafanya kazi hii ya kubainisha yaliyotajwa, na nafasi hiyo haimfai kila mtu kutekeleza jukumu hili, hivyo ni lazima kuongezea kifungu katika maana ya Mufti, na tunasema:

Mufti: Ni Mtu mwenye vigezo maalum vinavyomuwezesha kubainisha - kwa dalili - hukumu ya Kisharia kwa mwenye kuuliza.

Na vigezo hivi maalumu vinagawanyika kwenye vigezo vilivyokubalika kati ya Wanachuoni na vyengine wametofautiana…

Vigezo walivyokubaliana:

Uislamu: Haifai kwa kafiri.

Kubaleghe: Haifai kwa mtoto mdogo.

Kuwa na akili: Haifai kwa mwendawazimu au mjinga, na huingia kwenye kigezo hiki kuwa na sifa ya utambuzi na ufahamu wa kina.

Vigezo walivyotofautiana…

Uadilifu: Jamhuri ya Wanachuoni wamesema kutofaa Fat’wa ya mtu fasiki bali baadhi yao wamenukuu hivyo kwa makubaliano ya Wanachuoni ([5]), kwa sababu fat’wa ni kuelezea hukumu ya Kisharia, na mtu fasiki kuelezea kwake hakukubaliki, baadhi yao wakaondoa Fat’wa ya fasiki mwenyewe, kwa sababu anafahamu ukweli wa nafsi yake ([6]), na baadhi ya Maimamu wa madhehebu ya Imamu Abu Hanifa wakapitisha kufaa kwa fat’wa ya fasiki, kwa sababu anajitahidi ili asinasibishwe na makosa ([7]).

Utambuzi: Wala haifai kwa mtu aliyezidiwa na hali ya ujinga na kujisahau, Imamu An-Nawawi anasema: “Kimewekwa pia kigezo kwa Mufti kuwa mwenye muamko na nguvu ya udhibiti, hivyo haikubaliki kwa mtu aliyezidiwa na ujinga na kujisahau” ([8]), na Ibn Aabidiin anasema: “Hiki ni kigezo cha lazima ndani ya zama zetu, kwani kawaida ya leo ni kuwa mwenye kuwa mikononi mwake na fat’wa ya Mufti hujikweza kwa mpinzani wake kwa kule kusema kwake tu nimepewa fat’wa na Mufti, kwamba haki ninayo na mpinzani mjinga hafahamu kilichokuwa kwenye fat’wa, hivyo ni lazima Mufti awe mwenye uelewa anafahamu hila za watu na fitina zao” kisha anasema: Ufupisho wa hayo ni kuwa ujinga wa Mufti unapelekea madhara makubwa katika zama hizi” ([9]).

Jitihada: Hakuna shaka kuwa asili ya utoaji Fat’wa ni mtu kufanya Jitihada hata kama tutasema inafaa fat’wa ya mwenye kuiga, kwa sababu ukweli wa mambo haiwezekani kuwa na fat’wa huru bila ya kuegemeza kwenye Jitihada.

Lakini je ina maana kuwa Jitiahada ndio asili au asiyekuwa na uwezo wa kufanya Jitihada hafai kuitwa Mufti?

Dr. Wahba Az-Zuhaily anasema:

“Wanachuoni wa elimu ya misingi wa Fiqhi wamezungumza kuhusu maana ya Mufti, na tumekuta kuwa wao walikuwa wanatumia msamiati wa Mufti Msomi Mwanajitihada na Mwanafiqhi kuwa maneno yote hayo ni visawe, kutokana na maelezo hayo imebainika kwetu kuwa neno Mufti kwa upande wa Wanachuoni wa misingi ya Fiqhi lilikuwa linatumika kwa Mwanajitihada tu, kwa maana ambaye amefikia cheo cha kufanya jitihada, kisha baada ya hapo wakamuita Mwanachuoni wa madhehebu, ambapo walihusisha kazi zao katika kunukuu maandiko ya vitabu vya Fiqhi” ([10]).

Mwanachuoni Al-Kamal Ibn Al-Himam amesema katika wasifu wa Fat’wa ya asiyekuwa Mwanajitihada:

“Fahamu kuwa yaliyotajwa kwa Kadhi yametajwa pia kwa Mufti hakuna awezaye kutoa Fat’wa isipokuwa atakuwa ni Mwanajitihada, mtazamo wa watu wa misingi wamekubaliana kuwa Mufti ndio Mwanajitihada, ama asiyekuwa Mwanajitihada miongoni mwa wale wenye kuhifadhi kauli za Mwanajitihada huyo sio Mufti, wajibu wake pindi anapotakiwa kutaja kauli ya Mwanajitihada kama vile Imamu Abi Hanifa, anafahamu kuwa Fat’wa zinazofanyika ndani ya zama zetu si Fat’wa bali ni kunukuu maneno ya Mufti ili kuchukuliwa na mwenye kutaka fat’wa” ([11]).

Pamoja na kuwa Jitihada ni sharti la msingi kwa Mufti ispokuwa watu wa madhehebu ya Abu Hanifa wamefanya sharti la kipaombele na wala si sharti la kufaa kutoa fat’wa, kwa maana inafaa kupewa nafasi ya Mufti mwenye kuiga kauli za wengine, lakini anapopatikana mtu wa Jitihada inakuwa ni bora zaidi kupewa nafasi ya Mufti ([12]). Kwa upande wa Wanachuoni wa sasa wamepitisha Jitihada kutokuwa sharti katika kazi za utoaji fat’wa kama ilivyonukuliwa na Wanachuoni wengi.

Mwanachuoni Taqiyyudiin Ibn Daqiq Al-Eid anasema:

“Kuihusisha Fat’wa na mtu wa Jitihada kunapelekea uzito mkubwa, hivyo kilichopitishwa ni kuwa mpokezi kutoka kwa Maimamu pindi akiwa mtu adilifu mwenye uwezo wa kufahamu maneno ya Imamu, kisha akamuelezea mwenye kuiga kauli yake kuwa anatosha, kwa sababu katika hilo hudhaniwa na wengi kuwa ni hukumu itokayo kwa Mwenyezi Mungu, na Wanachuoni wa zama zetu wamekubaliana juu ya aina hii ya Fat’wa” ([13]).

Sharti la Jitihada katika utafiti wetu huu linazingatiwa ni jambo la msingi.

Hivyo tutaleta ufafanuzi zaidi na umuhimu kama ifuatavyo:

Viwango vya Jitihada:

Jitihada kwa maana ya Lugha: Ni kufanya juhudi zaidi katika jambo lenye ugumu.

Na katika maana ya Kimsamiati: Mwanachuoni kujikita zaidi ili kupata maana ya hukumu ya Kisharia ([14]).

Katika elimu anayohitaji Mufti kumuwezesha kwenye jitihada Imamu Al-Haramain anasema:

“Mufti: Ni mwenye kuweza kufahamu hukumu za matukio kwa wepesi pasi ya uzito wa elimu, sifa hii inapelekea aina tatu za elimu:

Aina ya kwanza: Lugha ya Kiarabu: Si sharti kuwa mbobezi wa lugha na kufikia kiwango cha kuwa alama ya Waarabu, wala hajitoshelezi kwa kutegemea kauli za pembeni, bali udhibiti wa kauli katika hilo kuwa na lugha ya Kiarabu inayomuinua zaidi ya nafasi ya waigaji katika ufahamu wa Kitabu na Sunna, na hii inahitaji nafasi ya kati katika elimu ya lugha ya Kiarabu.

Aina ya Pili: Ujuzi wa kufasiri Fiqhi, lazima kubobea kwenye hilo na kufahamu kanuni zake na maana zake, kisha ujuzi huu unajumuisha haja ya kunukuu madhehebu zilizopita, na kutaja aina za dalili kwa maandiko na maana za wazi za Kitabu, na kukusanya habari zinazohusu hukumu pamoja na kutaja wapokezi na sifa zinazozingatiwa katika elimu ya Hadithi, ikiwa hali itahitaji mtazamo zaidi katika habari basi vitabu vinavyotaja mambo sahihi na yasiyo sahihi ni vingi, na marejeo yake kwa lugha ya Kiarabu ni mepesi wala si mazito, na mahitaji muhimu katika fiqhi kujifunza kuchukuwa mambo ya dhahania katika masuala ya hukumu, na hili ndio linaitwa “Utambuzi nafsi” nayo ni katika sifa bora zaidi za Wasomi wa Sharia.

Aina ya tatu ya elimu: Elimu inayofahamika kama “Misingi ya Fiqhi” kutokana na elimu hiyo hubainika viwango vya dalili, zile zinazotangulizwa na zinazocheleweshwa, wala mtu hafikii cheo cha uhuru wa elimu bila ya ujuzi tosha wa taalama hii, basi mwenye kukusanya taaluma hizi atakuwa amepanda cheo cha juu cha watoa Fat’wa” ([15]).

Wanachuoni wamegawa Ijitahada kwenye nafasi mbalimbali ambazo hutofautiana kwa mujibu wa viwango vya watoa fat’wa, hivyo Jitihada hugawanyika kwenye Jitihada moja kwa moja na Jitihada funganishi… ([16])

Ama Jitihada moja kwa moja inagawanyika:

Jitihada Huru.

Jitihada Shiriki.

Ama Jitihada funganishi inagawanyika:

Jitihada katika Madhehebu.

Jitihada katika Fat’wa.

Na viwango vya utoaji fat’wa hugawanyika sehemu tano tofauti kwa mujibu wa madaraja ya Jitihada.

Daraja la Kwanza: Mwanajitihadi Huru.

Imamu An-Nawawi anasema: “Kigezo sha Mufti ni kuwa mwenye jukumu, Muislamu, kuaminika, kuepukana na sababu za ufasiki, kukosekana murua, mtambuzi, mwenye akili salama, uimara wa kufikiri, mtambuzi wa hukumu, kuwa makini ni sawa kwa mtu huru, mtumwa, mwanamke, kipofu au bubu pindi anapoandika au kufahamika ishara zake”..

Kisha anasema akinukuu kutoka kwa Ibn Swalaha: “Aliyehuru sharti lake pamoja na tuliyotaja ni kuwa mwenye kufahamu dalili za hukumu za Kisharia kutoka kwenye Kitabu Sunna Ijimai na Qiyas, awe mwenye kujua masharti yaliyopo katika dalili, na aina za dalili, na namna ya kuambatanisha na hukumu zake, haya yanaelezwa zaidi kwenye somo la misingi ya fiqhi, awe mwenye kufahamu elimu za Qur`ani, Hadithi, Aya zinazofuta na zilizofutwa, somo la sarufi lugha na matumizi ya lugha, tofauti za Wanachuoni na makubaliano yao kwa kiwango ambacho kinamuwezesha kutekeleza masharti ya dalili, mwenye ujuzi wa Fiqhi, hivyo mwenye kukusanya sifa hizi basi huyo ni Mufti huru, ambaye anapelekea ulazima wa kutosheleza, naye ni Mwanajitihada huru, kwa sababu ana uhuru wa dalili pasi ya kuiga na kujifungia kwenye madhehebu moja” ([17]).

Na Dahlawi anasema: “Ni wazi kwenye maelezo yao kuwa mwenye uhuru anakuwa na sifa zaidi ya mwengine kwa mambo matatu…

Jambo la Kwanza: Matumizi katika misingi ambayo hujengea Jitihada zake.

Jambo la Pili: Kufuatilia Aya Hadithi na Athari ili kufahamu hukumu ambazo majibu yake yametangulia, na kuteua baadhi ya dalili zenye kukinzana na kubainisha hukumu yenye nguvu kutokana na makisio yake na kuelezea vyanzo vya hukumu za hizo dalili, ambalo tunaloliona na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua zaidi ni kuwa hayo ni sehemu ya elimu ya Imamu Shafi Mwenyezi Mungu amrehemu.

Jambo la Tatu: Kuzungumzia masuala ambayo hayakuwa na majibu yaliyochukuliwa kwenye dalili hizo” ([18]).

Daraja la Pili: Mwanajitihada Mshiriki.

Imamu An-Nawawi anasema: Mufti mshiriki ana hali Nne:

Hali ya Kwanza: Kutomuiga kiongozi wake, si katika madhehebu wala katika dalili, kwa sifa huru aliyonayo, bali hunasibishwa kwa kiongozi wake kwa kufuata njia yake katika Jitihada, Abu Ishaqa ameelezea sifa hii, akawaelezea wafuasi wa Imamu Maliki na Ahmad na Daud pamoja na wafuasi wa Abu Hanifa kuwa walikuwa kwenye madhehebu ya Maimamu wao wakiwaiga, kisha akasema: Kilicho sahihi ambacho kimeelezewa na wahakiki ni kile kilichoelezewa na watu wetu, nacho ni wao walikuwa wafuasi wa madhehebu ya Imamu Shafi na wala si kumuiga, bali walipopata njia zake katika Jitihada na Qiyas walifunga njia zengine wala hawakuwa na ulazima katika Jitihada kufuata njia yake, hivyo walitaka kufahamu hukumu kwa njia ya Imamu Shaafi. Na Abu Ally As-Sinji alisema mfano wa haya: Tulimfuata Imamu Shafi pasi ya wengine, kwa sababu sisi tuliikuta kauli yake ina nguvu zaidi, wala hatukumuiga.

Nikasema: Haya ambayo ameyataja yanakubaliana pindi walipoamrishwa na Imamu Shaafi kisha Al-Muzini mwanzoni mwa ufupisho wake kwa kusema:

“Kwa ufahamu wake amekataza kumuiga na kumuiga mwengine” Abu Amru amesema: Madai ya kujitosheleza na kuiga hayasimami, wala kuendana na hali yao inayofahamika au hali za wengi wao, akaelezea baadhi ya watu wa misingi ya fiqhi miongoni mwetu kuwa hakujapatikana baada ya zama za Imamu Shaafi Mwanajitihada huru ([19]).

Addahlawi anasema: “Mshikiri ni katika mtiririko wa msingi wa Sheikh wake na kutumia maneno yake mengi katika kufuata dalili na kuelezea vyanzo, nalo pamolja na hayo ni mwenye uhakika wa hukumu kwa upande wa dalili zake mwenye uwezo wa kupata hukumu ya masuala yawe machache au mengi” ([20]).

Daraja la Tatu: Mwanajitihada wa Madhehebu.

Hali ya Pili: Imamu An-Nawawi anasema: Mwanajitihada awe ni mwenye kujifungamanisha na madhehebu ya Imamu wake, akiwa huru katika maelezo ya misingi yake kwa dalili, isipokuwa katika uletaji wake wa dalili asipindukie misingi ya Imamu wake na kanuni zake, na sharti lake awe ni Msomi wa fiqhi na misingi yake, pamoja na dalili za kina za hukumu, mwenye muono wa mwenendo wa ulinganishi na maana, mkamilifu wa utoaji wa hukumu, mwenye kutambua yasiyoongelewa na Imamu wake, wala kumumbua kuhusu kumuiga kwa kasoro za baadhi ya vitu vya kujitegemea kifat’wa, kama vile kuwa na kasoro katika Hadithi au lugha ya Kiarabu, mara nyingi kasoro hizo mbili huwa kwa wenye kuigwa, kisha kuchukuwa maelezo ya Imamu wake kuwa msingi wa kutolea hukumu kama kitendo huru cha tamko la Sharia, huenda akatosheka kwenye hukumu kwa dalili ya Imamu wake, wala haangalii pingamizi kama kitendo huru katika matamko, sifa hii watu wetu ni watu wenye mitazamo tofauti, na kwa mitazamo hiyo walikuwa nayo Maimamu wa watu wetu au zaidi yao, na mwenye kufanyia kazi Fat’wa hii ni mwenye kumuiga kiongozi wake na wala si fat’wa yake, kisha maelezo ya wazi ni kuwa mwenye kuwa na hali hii haipelekei faradhi ya kutosheleza, Abu Amru amesema: Ni wazi kunapelekea ulazima katika Fat’wa, hata kama hakupelekei kukuza elimu ambazo ni kuendelea kwa Fat’wa, kwa sababu amechukuwa nafasi ya kiongozi wake huru ikiwa ni tawi la usahihi, nao ni kufaa kumuiga mtu aliyefariki.

Kisha muigaji anaweza kuwa huru katika masuala au mlango maalum kama ilivyoelezwa, na anaweza kutoa fat’wa katika masuala yasiyoelezwa na kiongozi wake, huu ndio usahihi ambao unafanyiwa kazi, kisha pindi anapotoa Fat’wa basi mtoa Fat’wa ni mwenye kumuiga kiongozi wake na wala si Fat’wa yake, haya ndio yameelezwa na Imamu Al-Haramaini katika kitabu chake cha Al-Ghiyathi na faida zake nyingi” ([21]).

Dahlawi anasema kuhusu Mwanajitihada wa Madhehebu:

“Ni muigaji wa kiongozi wake katika yale yaliyoelezewa, lakini anafahamu kanuni za kiongozi wake na anayoyajengea madhehebu yake, ikiwa kutatokea tukio hakufahamu maelezo ya Imamu wake katika hilo hujitahidi kwenye madhehebu yake, na kulielezea kwa kauli zake na mtindo wake” ([22]).

Imamu Al-Haramaini anasema katika wasifu wa Mwanajitihada wa Madhehebu:

“Ama atakayekuwa Mwanachuoni mwenye muono wa mifumo ya kidhana mwenye ujuzi kwa njia za maana katika taaluma hizi, lakini hajafikia viwango vya Wanajitihada kwa kutokufikia kiwango kinachokusudiwa katika adabu, au kutobobea kwake katika taaluma ya ufasiri misingi ya Fiqhi, kwa kuwa kwake haepukani na kanuni za misingi ya fiqhi, ni Mwanachuoni mkubwa na muelewa katika Fiqhi hata kama si huru kwenye mifumo ya milango yake na kufafanua sababu zake… mfano wa Mwanachuoni huyu pindi anapofuata madhehebu ya Imamu katika Maimamu waliotangulia, na huyo Imamu ndio ambaye huonekana katika dhana za watoa fat’wa kuwa ndio mbora wa watafiti pale wanapokuta jambo limeelezewa kwenye madhehebu yake, hulimalizia na kutumia maelezo kwa maana yake kama ilivyoelezwa, tukio likiwa gumu lazima kufanyia kazi ulinganishi, na Mwanachuoni huru wa madhehebu ya Imamu wake huelezea mapito ya kipimo chake na hatua zake katika kukutanisha kisichoelezwa na Sharia na kile kilichoelezwa basi hatopata ugumu, anapaswa kuelezea kila tukio kipimo cha madhehebu ya Imamu wake…

Kisha anachofikia humueleza mtaka fat’wa kufuata jitihada za Mwanachuoni kama huyu katika kufikia kwake njia za uoanisho ambazo amezitengeneza na kuelezea yasiyo na maandiko ya mwenye madhehebu kwa kanuni za madhehebu” ([23]). 

Daraja la Nne: Mwanajitihada wa Fat’wa.

Hali ya Tatu: Imamu An-Nawawi anasema: Kutofikia cheo cha watu wa rai, lakini ni mtambuzi, mwenye kulinda madhehebu ya Imamu wake, mwenye kufahamu dalili zake, hufikiri, huchukuwa maamuzi, huandaa, huipa nguvu kauli, lakini yupo chini ya hao kwa kasoro yoke katika kulinda madhehebu au uwezo wa uchambuzi wa hukumu, au kufahamu misingi na mfano wake katika vyombo vyao, na sifa hii ipo kwa Wanachuoni wengi waliopo sasa ambao wameyagawa madhehebu ugawaji ambao watu wengi wanatambulishwa nayo hii leo, na wala hawajakutana na wale wa kabla yao katika utoaji hukumu, ama fat’wa zao walikuwa wakirahisisha kwa urahisishaji kama wa hao waliowatangulia au karibu na wao, na wanapima yale yasiozungumziwa, pasi ya kujikita zaidi na kipimo cha wazi, miongoni mwao wapo waliokusanya Fat’wa zao na wala hazijafikia katika kuzikutanisha kwake na madhehebu kiwango cha fat’wa za watu wa rai” ([24]).

Dahlawi anasema kuhusu Mwanajitihada wa Fat’wa:

“Ni mbobezi katika madhehebu yake, mwenye uwezo wa kuipa nguvu kauli moja zaidi ya nyengine na rai katika rai za watu zaidi ya wengine” ([25]).

Daraja la Tano: Si Mwanajitihada mtetezi wa madhehebu.

Katika maelezo ya Imamu An-Nawawi kwenye hali ya nne ya Mufti mshiriki, ni kuwa Mufti si anayetokana na nafasi yeyote katika nafasi za Jitihada…

Hali ya Nne: Imamu anasema, anatakiwa kulinda madhehebu, kunukuu na kuyafahamu katika mambo yaliyowazi na yasiyowai, lakini ana udhaifu katika kupitisha dalili zake na vipimo vyake, hii inategemea nukuu yake na fat’wa zake katika yale anayoyaelezea miongoni mwa maelezo ya madhehebu yake katika maandishi ya Imamu wake, na kuwagawa wanajitihada katika madhehebu yake,  na anayokuta hayajanukuliwa ikiwa atakuta maana yake kiasi ambacho anafahamu bila ya fikra kubwa kuwa hakuna tofauti kati yake basi inafaa kutolea fat’wa, vile vile anayofahamu kuunganishwa kwake chini ya udhibiti ulioandaliwa katika madhehebu, na yale yasiokuwa hayo basi anapaswa kujizuia na kuyatolea Fat’wa, mfano wa haya hutokea mara chache sana kwa upande uliotajwa” ([26]).

Imamu Al-Haramaini anasema katika wasifu wa mnukuu wa madhehebu:

“Hawi huru kunukuu masuala ya Kisharia mwenye kutegemea kutetea wala harejei kwenye uelewa na asili ya Sharia, kwani kufikiria masuala ni jambo la kwanza, na kuleta fikra yake kwa sura yake ni jambo la pili, hawezi kulifanya hilo isipokuwa ni mtu wa Sharia.

Kisha kunukuu madhehebu baada ya kukamilisha kufikiri hakuji isipokuwa kwa mtu mwenye nafasi ya juu na mzoefu katika Sharia, wala hateremki katika kunukuu masuala ya Sharia nafasi ya kunukuu habari visa na athari mbalimbali, ikiwa atalazimika kunukuu mambo ya wazi kwa mwenye kumuamini utetezi wake na kukubalika katika uaminifu wake, basi haiwezekani kulazimika kunukuu yaliyofichikana pasi ya kuwa na maarifa huru” ([27]).

Hakika kufanya jitihada ikiwa kutafanyika basi hugeuka na kuwa jitihada moja kwa moja ni sawa sawa ikiwa jitihada huru au shiriki, wala jitihada katika madhehebu au Fat’wa haibebi isipokuwa pindi inapokuja ikiwa imefunganishwa.

Tunakamilisha utafiti huu kwa kauli ya Imamu An-Nawawi:

“Hizi ni aina za watoa Fat’wa nazo ni tano, na kila aina imewekewa sharti la kulinda madhehebu na uelewa, basi mwenye kutoa Fat’wa pasi ya kuwa na sifa hii atakuwa amefanya ubaya mkubwa” ([28]).

*****

Uchambuzi wa Tatu: Maana ya Mufti wa lazima

Katika chambuzi mbili zilizopita tumemaliza kufahamu maana ya utoaji Fat’wa na maana ya Mufti…na tumefahamu kuwa miongoni mwa vigezo vya Mufti walivyotofautiana ni pamoja na kuwa mtu wa Jitihada, na zimeelezwa hatua nne za Jitihada, na kuwa watoa Fat’wa wanatofautiana kwa tofauti za hatua hizi nne, na mwisho wa uchambuzi tutaelezea aina tano za Mufti kama Imamu An-Nawawi alivyotaja, nao ni hawa:

 Mufti Mwanajitihada Huru.

Mufti Mwanajitihada Mshiriki.

Mufti Mwanajitihada katika Madhehebu.

Mufti Mwanajitihada katika Fat’wa.

Mufti si Mwanajitihada mtetezi wa Madhehebu.

Swali ambalo linajitokeza lenyewe hivi sasa ni: Mufti wa lazima anakuwa wapi katika aina hizi tano?

Jibu: Mufti wa lazima ameitwa hivyo, kwa kuwa kwake lazima ndio sababu ambayo kwa ajili hiyo amepitishwa atoe Fat’wa pamoja na kutokamilika masharti ya maana ya Mufti, hapa kuongezwa msababishaji kwenye sababu ni kama kauli ya Wanachuoni inayosema: Sijida ya kusahamu, kwa maana sijida ambayo sababu yake ni kusahau.

Mufti wa lazima ni yule asiye na kigezo mojawapo muhimu katika vigezo vya wataoa Fat’wa, nacho ni kigezo cha Jitihadi…Wanachuoni wamezungumzia hilo katika tafiti zao chini ya anuwani “Mufti wa Kuiga” na “Mufti asiye na Jitihada” … na hilo ni kwa sababu Jitihada ndio tofauti kubwa kati maana ya Mufti na Mufti wa lazima.

Hapa kusudio la Jitihada ni Jitihada ya moja kwa moja na wala si Jitihada tu… jitihada tu inakusanya kila kinachoitwa jitihada na kuna aina nne zilizotajwa.

Ama Jitihada ya moja kwa moja inakusanya aina mbili tu:

Jitihada Huru.

Jitihada Shirikishi.

Na kwa msingi huu Mufti wa lazima anakubaliwa na kila: Mwanajitihada wa Madhehebu, Mwanajitihada wa Fat’wa, na mtetezi wa madhehebu si Mwanajitihada.

Hilo ni kwa vile nafasi ya Mufti ni kuunganisha tukio na hukumu ya Kisharia kupitia kufahamu kwake tukio na kufahamu kwake hukumu ya Kisharia kupitia ushiriki wa moja kwa moja na dalili… ama mwenye kuiga mwengine katika ufahamu wa hukumu au katika njia ya uzalishaji wa hukumu pamoja na dalili, basi huko hakuitwi kwa ufahamu wake huu Jitihada bali ni kuiga, hivyo hawezi kuwa Mufti kweli.

Mwanajitihada Shiriki ni hufuata msingi wa kiongozi wake baada ya kuangalia na kuleta dalili, kwa maana rai yake imekubaliana na rai ya kiongozi wake pasi ya kumuiga, hivyo tunaona anaweza kutofautiana naye katika kanuni za kifiqhi kwa uhuru wake wa kuangalia na kwa kujihusisha moja kwa moja na dalili, huyu Mwanajitihada shiriki anafahamu hukumu ya Kisharia kwa dalili yake kwa uhuru, huyo ni Mufti kweli.

Ama Mwanajitihada wa Madhehebu na Mwanajitihada wa Fat’wa na Mtetezi wa madhehebu ya Mwanajitihada, hao wote wamefuata msingi wa kiongozi wao na matawi yake kwa kuiga, kwa sababu hawajafikia cheo chake katika rai na utoaji dalili, hao wote si Mamufti, na lau watatoa Fat’wa wanatoa fat’wa kwa umuhimu.

Lakini Sheikh Al-Islamu Zakaria Al-Answari amesema kumwambia Taji Deen As-Sabaki kuwa hakuna tofauti kwa Mwanajitihada wa madhehebu kutoa fat’wa, bali tofauti ni kwa Mwanajitihada wa fat’wa mwenye uwezo wa kuipa nguvu kauli pasi ya kutoa hukumu, vile vile mnukuu ambaye hawezi kupitisha kauli yenye nguvu ([29]).

Haya yakiwa sahihi Mwanajitihada wa madhehebu anakuwa nje ya maana ya Mufti wa lazima, na anabakia ndani ya mzunguko wake wa Mwanajitihada wa Fat’wa na mwenye kunukuu, lakini hili ni tatizo, kwa sababu Mwanajitihada wa madhehebu hategemewi kuwa muigaji wa kiongozi wake katika misingi matawi na kanuni, tofauti ipo kwenye kumuiga mtu aliyefariki, hulazimika kwa Mwanajitihada wa madhehebu ikiwa kiongozi wake amefariki, jambo ambalo linaonekana na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua uwepo wa tofauti pia.

Kutokana na hayo ni wazi kuwa marejeo ya Mufti yanakuwa vyanzo moja kwa moja vya Sharia, na marejeo ya Mufti wa lazima yanakuwa ni maandiko ya Mwanajitihada au kanuni za madhehebu yake na misingi yake katika ufahamu na utoaji wa hukumu kutoka kwenye vyanzo, au tunaweza kusema kwa maelezo ya kina kuwa hurejea kwenye vyanzo vya Sharia lakini kupitia uelewa wa Imamu Mwanajitihada na ufahamu wake.

Ikiwa patasemwa: Ni ipi sura ya Mufti wa lazima ambapo kwa sura hiyo imepitishwa kutoa fat’wa kwa asiye Mwanajitihada?

Ninajibu: Kuwa kulinda dini ni moja ya makusudio matano ya lazima ambayo yameletwa na Uislamu, na ambayo Wanachuoni wa Sharia wametumia msamiati wa kuyaita kama “Mambo ya lazima” nayo ni kulinda (Nafsi, akili, dini, heshima na mali).

Na kulinda dini kunakuwa kwa kuwabainishia watu dini mpaka wajifunze na kuifanyia kazi, jukumu la Mamufti na walinganiaji dini ni hii kazi ya kubainisha, ambapo sifa inayotofautisha kati ya ubainishaji wa Mufti na ubainishaji wa mlinganiaji, ni kuwa nafasi kuu ya mlinganiaji ni kuwabainishia watu mazuri ya dini, thawabu za utiifu na adhabu za kuasi, ili kuwalingania hayo watu washikamane na dini na kufanyia kazi hukumu zake. Ama Mufti jukumu lake kuu ni kuwabainishia watu ukweli wa dini ili wawajibike nayo, hana nafasi ya kuwapa mawaidha au kuwaathiri kwa njia za hotuba mbalimbali tofauti na mlinganiaji.

Kunapelekea kuepukana kwa nafasi ya Mufti na jukumu la kubainisha na kuelezea dini, jambo linalopelekea kuepuka utekelezaji wake kwa utekelezaji sahihi unaokubaliana na maudhui yake na ukweli wake, au kunapelekea watu kuwaondoa kwenye kufanyia kazi, kwa kukosa kwao marejeo ya kidini pamoja na kuhitaji kwao mtu wa kuwabainishia hukumu za Sharia kwa mambo yanayotokea kwao na mambo mapya ya maisha.

Kukosekana kwa nafasi ya Mufti, watoa fat’wa – hata kama watakuwa waigaji – ni madhara makubwa yanayoondoa ulinzi wa dini, na madhara lazima yaondolewe, kwa kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W: “Hakuna kudhuru wala kujidhuru” ([30]).

Kutokana na hayo, wakati wa kukosekana nafasi ya Mufti aliye na vigezo vya Umufti anapaswa mtu kugombea nafasi hii ili asimamie haki ya dini na wajibu wa kubainisha dini, ikiwa kutakuwa na ugumu wa kuwepo vigezo vyote basi ataomba yule mwenye vigezo zaidi, hivyo huchaguliwa aliye karibu zaidi, wala haviwekwi vigezo vigumu na kuachwa nafasi wazi, kwa sababu kilicho chepesi hakiondolewi na kizito. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: 

{Basi mcheni Mwenyezi Mungu muwezavyo} Attaghabun: 16. na Mtume S.A.W amesema: “Pindi ninapowakataza jambo basi jiepusheni nalo, na pindi ninapowaamrisheni jambo basi lifanyeni muwezavyo” ([31]).

Ikiwa itasemwa: Maneno yenu haya ni kutokana na kutokea mfano wa madhara haya zama kukosa Mwanajitihada moja kwa moja, lakini ikiwa itathibiti haiwezekani zama kumkosa, hubatilika madai yenu ya umuhimu wa Mufti wa lazima kuchukuliwa na muigaji… je inafaa zama kukosa Mwanajitihada moja kwa moja?

Ninajibu: Kufikiwa masuala haya kunakuja katika uchambuzi ujao kwa utashi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

 Uchambuzi: Zama za kukosekana Mwanajitihada.

Wanachuoni wametofautiana katika swala hili, kuna Wanachuoni wengi kama vile Imamu Arrazi, Imamu Al-Aamady, Imamu Ghazaly na wengine wamesema inawezekana kiakili na Kisharia ([32]), na wengine kama wafuasi wa Imamu Hambali wao wamesema Kisharia kutowezekana hilo ([33]).

Wanaosema linawezekana hilo wametumia dalili zifuatazo:

Dalili ya Kwanza: Kiakili haipelekei kutokea kwake kutowezekana, kwani hali yenyewe inawezekana, na asili kukosekana kwake mpaka pawe na dalili, na wala hakuna dalili sahihi ya uwezekano wa hilo na kupinga uwezekano, hivyo sisi tunashikamana na asili.

Dalili ya Pili:  Katika Sharia imekuja kuwa kuna zama itakuja hakutakuwa na Mwanachuoni, hali hii inamaanisha kupinga uwepo wa Mwanajitihada ndani ya zama fulani, kwa sababu Mwanajitihada ni katika Wanachuoni, na limekuja hili ndani ya Hadithi nyingi miongoni mwa Hadithi hizo:

“Hakika Mwenyezi Mungu haichukui elimu kwa waja kwa mara moja, lakini huichukuwa elimu kwa kuwachukuwa Wanachuoni, mpaka hatobakia Mwanachuoni watu wakamfanya kiongozi isipokuwa ni mjinga, watu watamuuliza na kuwatolea fat’wa pasi ya kuwa na elimu hivyo watu watapotea na kupotezwa” ([34]).

Hadithi hii imepingwa kwa sababu inaelezea hali za zama za mwisho kwa kauli nyengine ya Mtume S.A.W:

“Karibu na wakati wa kiyama kuna masiku elimu itaondolewa na kubakia ujinga pamoja na kuenea kwa ghasia” ([35]).

Dalili hili inajibiwa kuwa: Zama zozote zilizopo zinafaa kuwa ni zama za mwisho, pamoja na kuwepo mfano wa uwezekano huu haiwezekani kabisa zama zikakosa Mwanajitihada si wa kiakili wala wa Kisharia, wala haisemwi kuwa: Maelezo ya zama iliyopita na wala si zama iliyopo, kwa sababu sisi tunasema: Haiwezekani kutenganishwa kuwa (zama za mwisho) jina linaloaminika na wote likifuatana na zama zilizotangulia na wakati wa hivi sasa, ambapo kunasibishwa kwa kundi hili kunakuwa na umri wote wa dunia, kama vile kunasibishwa sehemu ya mwisho ya kitu kwenye kitu kizima.

Dalili ya Tatu: Kukubalika kukosekana kwa Mwanajitihada katika baadhi ya zama zilizopita, Imamu Arrazy anasema: “Wametofautiana mtu asiye wa jitihada je inafaa kwake kutoa fat’wa kwa yanayozungumzwa na wengine…ndani ya zama zetu hizi wamekubaliana kufaa Fat’wa ya aina hii kufanya kazi, kwa sababu ndani ya zama hizi hakuna Mwanajitihada na makubaliano ya Wanachuoni ni hoja” ([36]).

Dalili hii imepingwa kwa madai si sahihi kukubaliana kufaa kwake, kwa sababu makubaliano yenye kuzingatiwa ni makubaliano ya Wanajitihada, na zama kuzingatiwa haina Mwanajitihada basi kukosekana kwao kunakosekana makubaliano ya Wanachuoni” ([37]).

Maelezo haya yanajibiwa kama ifuatavyo:

Makubaliano yanagawanyika sehemu mbili, makubaliano maalum ya Wanajitihada, na makubaliano jumla ya Umma mzima, na kusudio hapa ni makubaliano ya jumla, nayo ndio ambayo yanapelekea uyakini kwa mujibu wa maelezo ya Imamu Al-Aamady ([38]).

Umma kwa ujumla wake ni wenye kuzuiliwa kukubaliana jambo lenye makosa, kwani kukubaliana kwao zama kukosa Mwanajitihada ni makubaliano yaliyozuiliwa na kukosewa hata kama yatatolewa kutoka kwa asiye Mwanajitihada, ni kwa kuwa kwake kwa wakati huo ni  kauli ya Umma wote.

Makubaliano yao ya Mufti wa lazima kufaa kutoa Fat’wa ni kutokana na walichofundisha ni katika dharura ya dini kuwa Sharia ni yenye kubaki na wala haifai kukwamishwa, ni sawa sawa Mwanajitihada amepatikana au hajapatikana, imebainika kwao kuwa Mwanajitihada mwenye kuiga inawezekana kukaimu nafasi ya Mwanajitihada kamili kwa upande kuelezea hukumu na kulinda Sharia, na hilo ni kupitia uwezo wake wa kuendeleza fat’wa kutoka kwenye madhehebu ya Wanajitihada na mifumo yao.

Umma kwa ujumla Wanajitihada waliokuwa katika masuala haya basi huzoelekea makubaliano hayo, na hilo ni kwa kauli yenye nguvu ya kugawanyika kwa Jitihada, nayo kauli sahihi kwa Watu wa misingi ya Sharia ([39]).

Dalili ya Nne: Ni kuwa haioneshi kitu kufaa kwa kutokea kwake, imethibiti kutokea hilo katika baadhi ya zama zilizopita kama inavyofahamika katika historia ya Sharia.

Imamu Al-Haramaini amesema, baada ya kutaja sifa za Mamufti Wanajitihada: “Kwa hakika nimetaja sehemu ya sifa za Mamufti na hukumu zao ili kubainika kwa mtazamo zama kukosa Mamufti” ([40]).

Hoja ya Uislamu Abu Hamid Al-Ghazaly amesema: “Pia kuna zama ilikosa Mwanajitahada huru” ([41]).

Imamu An-Nawawi amesema: “Kwa muda mrefu alikosekana Mufti huru na Fat’wa zikawa kwa wanaonasibishwa na Maimamu wa madhehebu wanaofuatwa” ([42]).

Imamu Zarkashy amesema: “Ukweli ni kuwa kuna zama alikosekana Mwanajitihada, hata Mwanajitihada katika madhehebu ya mmoja wa Maimamu wanne” ([43]).

Waliosema inazuiliwa wameleta dalili zifuatazo:

Dalili ya Kwanza: Ni kauli ya Mtume S.A.W:

“Bado kuna kundi katika Umma wangu wanapigania haki hawadhuriki na anayewadhalilisha mpaka pale amri ya Mwenyezi Mungu itakapokuja na wao wakiwa hivyo” ([44]).

Hii inaonesha kuwa hakuna zama zilizokosa uwepo wa Mwanajitihada mpaka pale Mwenyezi Mungu atakapoleta amri yake kwa maana ya ndani ya zama za mwisho, kwa sababu zama kukosa Mwanajitihada kunazuia sifa ya kundi hilo kuwa ni la haki, kwa sababu Mwanajitihada ndiye anayefikisha haki katika matukio yanayoibuka kisha huwatolea watu fat’wa.

Dalili hii inajibiwa:

Hakuna ulazima kuwa kwao kwenye haki na kuwa Wanajitihada au kuwa na Mwanajitihada hai, kwani kuwa kwao kwenye haki kunaweza kuwa na maana ya wenye kushikamana na haki ambayo wameifahamu kwa Wanajitihada, na wenye kushikamana na mifumo ya Wanajitihada na madhehebu yao kwa kutoa hukumu za masuala yanayojitokeza kwenye misingi na kanuni za Wanajitihada waliotangulia.

Mapokezi ya Hadithi ni mengi vile vile na maneno yake ni mengi, mapokezi haya yanajifasiri yenyewe kwa yenyewe, na kupitia mfululizo wa mapokezi ya Hadithi inabainika kuwa kundi hilo la Waislamu linafanya kazi ya kulinda Uislamu, kwani maadui wa Uislamu kila wanapojaribu kuupiga vita na kuushambulia ili kuumaliza wanapambana na kundi hilo la Waislamu wakiwashambulia na kujibu uadui wao, Mwenyezi Mungu husimama upande wao na kuwatetea kwa sababu wao wanapigana kulinda haki kwani wao wapo kwenye haki ambayo ni Uislamu Akida na Sharia, wala hawadhuriki na watu kuchelewa kuwatetea kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtuukufu Ndiye ambaye anasimama nao dhidi ya maadui wao hivyo wanakuwa washindi…

“Bado kundi katika Umma wangu linaendelea kupigania haki mpaka siku ya Kiyama – akasema – Atakuja Nabii Isa A.S na kiongozi wao atasema: Njoo utuswalishe, atasema: Hapana, kwani nyinyi kwa nyinyi kuna viongozi. Kutokana na ukarimu wa Mwenyezi Mungu kwa Umma huu” ([45]).

“Bado kundi katika Umma wangu linaendelea kupigania haki wakiwashinda wapinzani wao mpaka wa mwisho wao atashambuliwa na Masihi Dajjal” ([46]).

Hivyo kusudio hapa la haki sio kufahamu hukumu za matukio yanayojitokeza, bali kusudio ni Uislamu kwa Akida yake Maudhui yake na Misingi yake sahihi, wala hakuna sharti la kuwepo kwa Mwanajitihada hai katika kila zama ili maudhui ya Uislamu na Akida yake vibakie, bali inatosha kuwepo Wanajitihada ndani ya zama iliyopita na Jitihada zao zikafanya kazi ndani ya zama zijazo.

Wala si sharti katika kundi hilo ili kuwa kwenye haki watu wake wote au baadhi yao kuwa ni Wanajitihada, bali inatosha wote kushikamana na haki ambayo itawafikisha kwenye Jitihada kupitia Wanajitihada.

Dalili ya Pili:  Jitihada ni jambo la lazima inayotosheleza, kwa sababu matukio si yenye kwisha, zama ikiwa itakosa Mwanajitihada basi sifa ya Uislamu kufaa na kufanya kazi zama zote itakatika, na Umma utakusanyika kwenye batili kwa kuacha ulazima wa Jitihada, na kiwango cha Sharia kushindwa kutoa hukumu kwenye mambo yatakayopatikana, kubatilika yote hayo yanayofahamika katika dini kama mambo dharura, hivyo wakati huo zama haitawezekana kukosa Mwanajitihada.

Dalili hii inajibiwa:

Zama kukosa Mwanajitihada hailazimu mliyotaja, kwani Mwanafiqhi mwenye kuiga katika matukio anaweza kutoa hukumu kwa madhehebu ya Wanajitihada waliotangulia, hivyo dini itaenea na itafaa kwa zama zote na sehemu zote.

Imamu Al-Haramain anasema: “Ambalo limezungukwa na kanuni za madhehebu ya Imamu Shafi kwa mfano, na kupata mafunzo katika vipimo vyake na kunyosha pande za mitazamo yake na njia ya matendo yake, hushuka katika kukutana na maelezo ya Imamu Shafi nafasi ya Mwanajitihada ambaye kwa njia za dhahania anaweza kukutana na maelezo yasiyoelezewa katika Sharia kwa yale yaliyoelezewa”.

Na anasema: “Ambayo ninayapitisha ni kuwa hulazimishwa mwenye kutaka Fat’wa kufuata Jitihada mfano wa Mwanafiqhi kama huyu katika kufuata kwake njia za kulinganisha ambazo ameziweka na kuelezea katika yale yasiyo kuwa na maandiko kwa mwana madhehebu kwa kanuni za kimadhehebu” ([47]).

Kisha Jitihada hata kama itakuwa ni jambo la lazima ya kutosheleza isipokuwa yenyewe itapokuwa ngumu kwa Waislamu basi hawana dhambi, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu hailazimishi nafsi isipokuwa kwa uwezo wake:

{Mwenyezi Mungu hamlazimishi mtu ila kwa kadiri ya alicho mpa. Mwenyezi Mungu atafanya baada ya dhiki faraja} Attwalaaq: 7.

Wala hailazimiki mwenye kushindwa kufanya Jitihada ni kuwakusanya watu kwenye upotevu, na ikiwa watashindwa basi watafanya wanachoweza kwa kutoa hukumu kwa madhehebu ya Wanajitihada, hivyo wanakuwa hawana dhambi au wamekusanyika kwenye batili, kwa kauli ya Mola Mtukufu:

{Basi mcheni Mwenyezi Mungu kama mwezavyo} Attaghabun: 16.

Na kauli ya Mtume S.A.W: “Pindi ninapowamrisha jambo basi litekelezeni muwezavyo” ([48]).

Haya ni mambo ya lazima ya Mwenyezi Mungu ambayo amewawekea waja wake mara nyingi yanakuwa na mbadala katika hali ya kushindwa kuyatekeleza, kama vile Mola Mtukufu amewalazimisha waja wake kutayamamu wakati wa kushindwa kutawadha kwa kutumia maji, vile vile haitokuwa mbali kulazimishwa wakati wa kushindwa kupata fat’wa kwa Mufti Mwanajitihada, wapate fat’wa kwa Mufti wa lazima, ambapo mwisho wa yote, marejeo ya fat’wa yake hayatatoka nje ya madhehebu za Wanajitihada.

Katika kuelezea mitazamo iliyopita na kuijibu, rai iliyo na nguvu kwa upande wetu – Mwenyezi Mungu Anajua zaidi – ni ile ya kwanza inayosema, inafaa katika zama kukosa Mwanajitihada, kwa kuwezekana kwake kiakili na kutozuilika Kisharia…

Ikichukuliwa kwa mfano zama za kutofaa kukosa Mwanajitihada, basi hitajio ambalo linachukuwa nafasi ya lazima linatosha kufaa nafasi ya Mufti wa lazima, pamoja na kuwepo Mufti wa Jitihada, kwa sababu haitakuwa wepesi kwa kila mtu kufikia nafasi hiyo ya kutoa fat’wa, ni ugumu kwake kuwa na muda kamili wakati wote wa kutakiwa fat’wa na kila Muislamu duniani, hivyo katika kuondoa uzito kwake na kwa Umma, inalazimika nafasi ya Mufti wa lazima kuwepo nchi zote akikaimu nafasi ya Mufti kamili – ikiwa atapatikana – na kutegemewa katika fat’wa zake.

Kwa sura hii unathibiti uhalali wa nafasi ya Mufti wa lazima (Ili kuondoa madhara) kwa mtazamo wa wanaosema yafaa kufanya hivyo zama kukosa Mwanajitihada, au (Kukidhi hitajio) ambalo linachukuwa nafasi ya lazima kwa mtazamo wa wanaosema haifai zama kukosa Mwanajitihada.

Swafiyyul-Hindi anasema katika kuzungumzia masuala haya:

“La kwanza katika hilo ni ulazima na kuhitajika, kwani sisi lau hatutapitisha mfano wa haya basi hilo litapelekea kuwa Sharia haitoshelezi kuelezea zaidi matukio yanayoibuka, na inafahamika kuwa hilo linapelekea kwenye kuharibu hali za watu” ([49]).

Linabakia swali lengine:  Je kila muigaji anafaa kuwa Mufti wa lazima au lazima awe na vigezo maalum?

Jibu la swali hili litakuja kupitia rai za Wanachuoni na mitazamo yao katika uchambuzi ujao.

Uchambuzi wa Nne: Hukumu ya Muigaji (Mufti wa Lazima) Kuchukuwa Nafasi ya Mufti

Asili ya Mufti kama ilivyoelezewa ni mtu wa Jitihada, na tumefahamu kuwa kukosekana Wanajitihada au uchache wao na uwingi ni hitajio la watu la kutaka Fat’wa, na huonekana umuhimu na haja kubwa kwa wale wanaokaimu nafasi za Mamufti Wanajitihada na wanaendesha majukumu yao kwa njia ya kuiga kwao na kupata maelezo kwenye madhehebu yao na kufikia hukumu za matukio kwa misingi yao na kanuni zao…

Lakini Wanachuoni hawajakubaliana juu ya kufaa kutoa fat’wa muigaji au anayeitwa kwa jina la (Mufti wa lazima) bali wametofautiana kwa rai mbalimbali:

Rai ya Kwanza: Haifai kabisa.

Rai ya Pili: Inafaa anapokosekana Mwanajitihada.

Rai ya Tatu: Inafaa kwa sharti ya Jitihada ya madhehebu.

Rai ya Nne: Inafaa kwa sharti la kujua dalili za Mwanajitihada.

Rai ya Tano: Inafaa kwa sharti la udhibiti na uadilifu.

Rai ya Sita: Inafaa kwa sharti la udhibiti, uadilifu na kumuiga Mwanajitihada hai.

Tusimame kwenye ufafanuzi wa rai hizi na kinachoweza kujibiwa ili mwisho wa yote tufikie kauli yenye nguvu na kukubalika.

Rai ya Kwanza: Haifai kabisa.

Wanachuoni wengi wa madhehebu ya Imamu Hambali, Imamu Al-Halimi, Imamu Arrawyani ([50]), Imamu Al-Maawardi ([51]) katika watu wa madhehebu ya Imamu Shafi, Imamu Abul-Hussein Al-Baswary katika watu wa Muutazila ([52]), wamesema muigaji hafai kabisa kuwa Mufti, na Umufti hauwi isipokuwa kwa Mwanajitihada.

Katika rai hii wametumia dalili zifuatazo:

Dalili ya Kwanza: Mufti wa kuiga si mwenye kufikiri kabisa, kwa sababu mwenye kuiga ni mwelezeaji wa fat’wa na wala sio muanzilishi wa fat’wa, hivyo anamuhitaji Mwanajitihada, kwa sababu fat’wa hutoka kwake na hunukuliwa na muigaji, kazi mfano wa aina hii inakuwa ni kuelezea wala sio upande wa fat’wa ([53]).

Dalili hii inajibiwa kuwa, matamshi hayana athari na uhalisia, ikiwa mtaita ni kazi ya kutoa habari au kazi ya Fat’wa uwazi wake ni jambo moja, kwa sababu maelezo ya kumfaa muulizaji huelekeza kwa huyu Mufti muigaji kisha hufanyia kazi alichokisikia kutoka kwake iwe ni habari au Fat’wa iliyoanzishwa na yeye… (Ifahamike hapa kuwa kuanzisha kunakokusudiwa ni kuanzisha Fat’wa na wala sio kuanzisha hukumu ya Kisharia).

Dalili ya Pili: Mufti muigaji hutoa Fat’wa kwa kile kinachoelezewa na wengine na hali hii haifai, kwa sababu huulizwa maswali anayoyafanyia Jitihada na wala haulizwi Jitihada za wengine ([54]).

Dalili hii inajibiwa kuwa, muulizaji anahitaji hukumu ya Kisharia, na hukumu nyingi za Kisharia ni za kidhana, na Mufti muigaji anayo dhana ya hukumu ya Kisharia kupitia kumuiga kwake Mwanajitihada, na muulizaji anakuwa na dhana pia wakati wa fat’wa yake na madhehebu ya Mwanajitihada, ikiwa muulizaji anahitaji Jitihada ya Mufti, basi huwa anahitaji Jitihada zinazokubalika iwe jitihada hizo ni za kwake au za mwengine.

Dalili ya Tatu: Mufti wa kuiga anapofanya Jitihada na kutoa kauli katika masuala, hapaswi kurudia Jitihada wakati wa kujirudia swali akiwa mwenye kukumbuka kauli yake katika masuala na njia ya Jitihada yake, lakini akiwa hakumbuki basi kilichowajibu wakati huo kwake ni kurudia Jitihada, kwa sababu hajui kabisa njia ya Jitihada katika masuala, kisha hawezi kurudia Jitihada wakati wa kujirudia kwa swali ([55]).

Dalili hii inajibiwa kuwa, ujinga wa njia ya Jitihada katika masuala kwa Mufti wa kuiga hauna madhara, kwa sababu muigaji ni sehemu ya mtu mjinga, na inafaa kwa mtu mjinga kumuiga Mwanajitihada bila ya kusimama kwenye njia ya Jitihada yake katika kila masuala.

Kisha Mufti wa kuiga hapaswi kurudi kwa Mwanajitihada wakati wa kujirudia kwa swali kwa kuwa tu yeye anakumbuka madhehebu yake, na haya ni kama mlivyosema kutolazimika kurudia Jitihada madamu Mwanajitihada anakumbuka kauli yake na njia ya Jitihada zake katika tukio, vile vile mtu mjinga pindi tukio linapojirudia hapaswi kurudia swali kwa kuwa  anakumbuka hukumu yake, kama si hivyo lau Umma utaingia kwenye tatizo kubwa ikiwa tukio hujirudia kila siku, basi vile vile Mufti muigaji hapaswi kurudia.

Imamu Raziy amesema kuwa Mwanajitihada ikiwa tukio litajirudia na akawa anakumbuka hukumu ambayo aliwahi kuifikia hapo mwanzo lakini amesahau njia ya Jitihada yake katika masuala na wala hajafanya tena Jitihada mpya, basi inafaa kwake kutoa fat’wa kwa hukumu ya nyuma…

Imamu Razy anasema: “Kwa kuwa dhana kubwa aliyonayo ni kuwa njia ambayo ameifuata mwanzo ni njia yenye nguvu, hivi sasa akafahamu kuwa hiyo njia yenye nguvu ni njia sahihi, basi inafaa kwake kutoa Fat’wa kwa sababu kuifanyia kazi dhana hiyo ni jambo la lazima” ([56]).

Mwisho wa mjadala tunasema: Kwa nini mumesema Mufti wa kuiga hajui njia ya Jitihada katika masuala? Kwani muigaji huwenda akajua chanzo cha Mwanajitihada na njia ya kuleta hukumu katika masuala, wala hawi tu kwa maarifa haya ni Mwanajitihada, kwa kushindwa kwake kwenda kinyume na kiongozi wake katika chanzo hicho.

Dalili ya Nne: Muigaji amehalalishwa katika matawi ya Kisharia kwa umuhimu wake, wala hakuna umuhimu hata mmoja kwa waigaji kushika nafasi ya Mufti, kwa sababu hakuna zama inayokosa Mwanajitihada.

Dalili hii inajibiwa kuwa, kujengewa kutokana na kauli ya zama kutofaa kukosa Mwanajitihada, si kauli yenye kufuatwa na Jopo la Wanachuoni kama ilivyoelezwa ([57]), na tuchukulie imefuatwa na Wanachuoni basi haja ambayo inachukuwa nafasi ya lazima inajuzisha Mufti muigaji kushika nafasi ya Mufti, kutokana na uchache wa Wanajitihada na uwingi wa wataka fat’wa.

Rai ya Pili: Kufaa wakati wa kukosekana Mwanajitihada.

Walioitaja rai hii ni baadhi ya Wanachuoni ([58]) kama vile Ibn Burhan na Elkiya katika wafuasi wa madhehebu ya Imamu Shafi ([59]), na Ibn Hamdan katika wafuasi wa madhehebu ya Imamu Hambali katika yale Al-Mardawi mwenye kitabu cha Attahbiir ([60]) aliyoyanasibisha kwake, vile vile Imamu Al-Haramain Abul Muali Al-Juwainy.

 Ikiwa Imamu Al-Juwainy anaipa nguvu kauli ya kuchukuwa fat’wa ya Mwanajitihada aliye hai na sio aliyefariki, hii inaonesha jinsi gani anaipa nguvu na ni kizuizi cha kuchukuwa fat’wa ya muigaji wa Mwanajitihada aliyefariki ikiwa anapatikana Mwanajitihada aliye hai.

Anasema: “Mwenye kuwaangalia watoa rai atakubaliana naye kama ilivyoelezewa hapo mwanzo, na mtazamo wake ukapelekea kumuiga Imamu wa Waislamu Imamu Shafi R.A lakini katika zama zake kukawa na Mufti aliyekidhi vigezo na Fat’wa zake zikatofautiana na madhehebu ya Imamu Shafi katika baadhi ya matukio, basi mtoa Fat’wa ambaye ni mfuasi wa Imamu Shafi atamuiga Mufti wa zama zake au atafuata madhehebu ya Imamu Shafi na atayashika kwa mujibu wa ukubwa wa kuhitajiwa na muigaji wake?”.

Kisha swali hili linajibiwa na anasema: “Mtazamo wangu mimi ni kwamba mtoa Fat’wa atamuiga Mufti wa wakati wake” ([61]), kwa maana ya Mwanajitihada aliye hai.

Wafuasi wa Rai hii wametumia dalili ifuatayo:

Dalili ya Kwanza: Asili ya Mufti ni kuwa Mwanajitihada, ama mwenye kuiga ni badala ya Mufti, wala hawi mbadala isipokuwa panapokosekana wa asili, na kukosekana kwa asili ni kutokuwepo kwake.

Maelezo haya yanakusanya kauli yao: “Fat’wa ya mwenye kuiga inafaa kwa dharura wakati wa kukosekana Mwanajitihada, wala hakuna dharura wakati wa kuwepo kwake, hivyo haifai” ([62]).

Dalili hii inajibiwa kuwa, maana ya udhuru au dharura katika kukosekana kwa Mwanajitihada inazuiliwa, kwa sababu udhuru kama unavyokuwa ni jambo la kihisia kwa kukosekana asili, na unakuwa ni jambo la dhihinia pale asili isipotosheleza kukidhi mahitaji, hii ndio maana katika masuala, kutokana na uwingi wa wahitaji fat’wa, umbali wa miji yao na ugumu wa kuwafikia, ndio njia za kisasa za mawasiliano zimefanya ulimwengu wote kuwa kama kijiji kimoja, isipokuwa bado kuna udhuru kwa Mufti Mwanajitihada kujibu idadi kubwa ya fat’wa za kila siku zinazokuja kutoka maeneo mbalimbali ya ulimwengu, na mara nyingi ni fat’wa zinazojirudia, hivyo umuhimu au kuhitajika Mamufti waigaji haupunguzwi na kuhitajika kwa Mufti Mwanajitihada.

Inawezekana kuelezea dalili nyengine ya rai hii kwa sura ifuatayo…

Dalili ya Pili: Mufti muigaji ima akubaliane na Mwanajitihada aliyehai au atofautiane naye, ikiwa atakubaliana naye basi hakuna haja ya Fat’wa zake kwa kujitosheleza na Fat’wa za Mwanajitihada ambayo ndiyo asili, na ikiwa atatofautiana naye bado dhana yenye nguvu ni wajibu wa kuchukuwa Fat’wa za Mwanajitihada aliyehai kwa kupitia kwake mazingira ya wakati na mambo mengine ambayo Fat’wa hubadilika kwa kubadilika kwake.

Dalili hii inajibiwa kuwa, kwa mfano kumekuwa na makubaliano, maelezo yamesema uwepo wa kuhitajika kwake na kutotosheleza kwa Mufti Mwanajitihada, na ikiwa kuna hali ya kutokubaliana basi Jitihada haivunjwi, vile vile kauli sahihi kwa idadi kubwa ya Wanachuoni wa Umma ni kufaa kumuiga Mwanajitihada aliyefariki ([63]).

Kisha miongoni mwa Mamufti waigaji wapo wanaoweza kuleta hukumu ya mambo mapya ya kila zama kwa mujibu wa kanuni za Mwanajitihada aliyefariki, kwani misingi ya kubadilika fat’wa inawezekana kwa muigaji kuifahamu pia na kuifanyia kazi kwa utashi wa madhehebu ya Imamu wake.

Imamu Al-Haramaini ana neno tunaomba ruhusa kulitumia katika sehemu hii, ambapo anasema: “Huenda Mwanachuoni huru wa madhehebu ya Imamu akawa na uwezo zaidi wa kufahamu misingi ya madhehebu ambayo yanatokana na Mwanajitihada katika jaribio lake la kufahamu misingi ya Sharia, kwani Imamu muigaji amefanya juhudi zake kubwa katika kupangilia na kitabu kukiwekea milango na kuandaa sura za uwiano na sababu za kitabu cha madhehebu ambayo yanatokana na Mwanajitihada ambaye anapaswa kurejesha jambo kwenye asili ya Sharia bila ya kukabiliana na maandalizi anayokutana nayo mnukuu wa madhehebu katika asili ya madhehebu yaliyopangiliwa vizuri” ([64]).

Rai ya Tatu: Kufaa kwa sharti la Jitihada ndani ya madhehebu.

Wafuasi wa Abu Hanifa pamoja na Al-Aamidiy na Ibn Al-Hajib pia Al-Swafy Al-Hindi na wengineo wamesema kuwa Haifai muigaji kutoa Fat’wa, isipokuwa kama atakuwa Mwanajitihada katika madhehebu ya kiongozi wake, mwenye uwezo wa kutoa hukumu, kukusanya na kutenganisha kati ya yanayofanana na kutofautiana, mwenye uwezo wa kuamua na kuleta dalili na kuzungumza ili kutetea madhehebu ([65]).

Al-Mardawi ametaja kuwa madhehebu ya Wanachuoni wengi yamepitisha fat’wa ya asiye mwanajitihada ikiwa ameangalia vizuri chanzo na kuwa mtu wa mtazamo ([66]), makusudio yake ni Mwanajitihada wa madhehebu.

Wakatoa dalili ya rai hii kwa maelezo yafuatayo:

Dalili ya Kwanza: Kutokea mfano wa fat’wa hii ndani ya wakati wa Wanajitihada bila yeyote kati yao kupinga hivyo inakuwa ni makubaliano ya wote juu ya kufaa kwake, watu wa madhehebu ya Abu Hanifa walikuwa wanatoa fat’wa kwa madhehebu ya Abu Hanifa ndani ya zama za Imamu Shafi pamoja na Imamu Ahmad na wengine kama vile Ibn Muinu na Ibn Ayiina na Atwaa bila yeyote kati yao kupinga ([67]).

Dalili ya Pili: Makubaliano ya watu wa kila zama ya kukubali fat’wa za Mwanajitihada wa madhehebu, na kutokubalika kwake kama hatokuwa hivyo ([68]).

Dalili hii inajibiwa kwa kutofuata madai ya makubaliano ya kutokubalika hilo katika kulinda madhehebu na Wanajitihada wa fat’wa.

Dalili ya Tatu: Mwanajitihada amejiimarisha uwepo wake, na muigaji haifai hukumu yake, Mwanajitihada anabakia katika madhehebu ya Imamu, na dharura imepelekea kujitosheleza nayo ([69]).

Maana ya hii ni kuwa dharura yenye kuhitajika zaidi kwa asiye Mwanajitihada, lakini kutokana na dharura kuwa inaweza kuondolewa na Mwanajitihada wa madhehebu kutopitisha fat’wa ya asiyefikia kiwango chake miongoni mwa waigaji, kwa sababu dharura hukadiriwa, na kwa kuwa kwake mbali zaidi na makosa kuliko vitu vyengine.

Dalili hii inajibiwa kuwa, dharura kama inavyohitajika kwa Mwanajitihada wa madhehebu pia inahitajika kwa mwanajitihada wa fat’wa na mtetezi wa madhehebu.

Dalili ya Nne: Ni lazima kutenganisha Mufti akiwa muigaji na asiyejua lolote, kama si hivyo basi itafaa kila mjinga kutoa fat’wa kwa watu wengine kwa kule kupitia kwake kitabu, ikiwa Mufti na wengine wapo sawa katika uwezo wa kupitia, basi kutofautisha Mufti na mjinga kunabakia kwa Mwanajitihada katika madhehebu ya Imamu wake, mwenye uwezo wa kuangalia na kuzungumza.

Dalili hii inajibiwa kwa kutenganishwa mtetezi wa Madhehebu Mwanajitihada wa Fat’wa na mtu mjinga wa kujifunza kwa Wanachuoni na kuangalia Madhehebu ya Wanajitihada, na kushughulishwa zaidi na kuhifadhi na kujifunza.

Rai ya Nne: Kufaa kwa sharti la kujua dalili za Mwanajitihada.

Al-Marudy ameelezea baadhi ya maelezo ya Imamu Shafi kuwa, mtu mjinga pindi anapojua hukumu ya tukio na dalili zake inafaa kwake kutoa Fat’wa, na baadhi yao wakatenganisha wakasema: Inafaa dalili ikiwa ni andiko kutoka kwenye Qurani na Sunna na wala sio kwa mtazamo wa uchimbuaji hukumu ([70]).

Rai hii ni tofauti na rai iliyopita ambayo imeweka sharti la muigaji kufikia daraja la Jitihada katika Madhehebu, kwa sababu jitihada katika madhehebu maana yake ni uwezo wa kutoa hukumu kuipa nguvu kukusanya kutofautisha kuangalia na kujadili, ama watu wa rai hii hawakuweka sharti zaidi ya kufahamu hukumu ya tukio kwa kuitolea dalili, wala si sharti kwao kufanya tafiti katika kujadili pingamizi au dalili za walio kinyume.

Wakachukuwa dalili kuwa ujinga wakati huo unakuwa umefikia kwenye ujuzi wa hukumu kwa dalili hiyo hiyo ambayo imemfikisha Mwanajitihada hivyo wanakuwa sawa katika kupitisha fat’wa kwa hukumu.

Rai hii inajibiwa kuwa, mtu mjinga hata kama atajua dalili ya Mwanajitihada lakini hajawa na nafasi pana katika kufahamu hukumu kama Mwanajitihada, kwa kutoangalia kwake dalili za ukinzani, na kutokuwa na uwezo wa kukusanya au kuipa nguvu kati ya dalili.

Na Imamu An-Nawawi anasema akiwa anapinga rai hii: “Akiwa si mbobezi huenda akadhani kisichokuwa kwenye madhehebu yake kwa upungufu wa ufahamu wake na uchache wa kupitia kwake dhana za masuala na tofauti za maandiko ya huyo Mwanajitihada na kauli yenye nguvu na mengine hasa madhehebuya Imamu Shafi R.A ambayo anafahamu yaliyotolewa fat’wa isipokuwa wachache kutokana na uwingi wa kuenea kwake na kutofautiana mnukuu wake katika kunukuu na kuipa nguvu” ([71]).

Wakachukuwa dalili ya rai ya mwenye kuweka sharti katika dalili kuwa ni andiko katika Qur`ani au Sunna, kuwa hivyo viwili ndio asili, makubaliano ya Wanachuoni ni lazima yawe na kiegemeo ndani ya Qur`ani na Sunna, ulinganisho haukubaliki ikiwa andiko litakuwa kinyume na hivyo, na kutegemea shina kuna nguvu zaidi ya kutegemea tawi, hivyo Mwanajitihada pindi anapotegemea andiko anakuwa karibu zaidi na usahihi kuliko akitegemea kauli za Wanachuoni au uwiano, kwani inawezekana kutoangalia kwake waliotafautiana katika kauli za Wanachuoni, au kutoangalia kwake andiko hubaditilisha pia Qiyasi au kuoanisha, na mfano wa uwezekano huu upo mbali kwa upande wa Maandiko ya Qur`ani na Sunna.

Lakini rai hii inajibiwa kuwa, kukubali mbali na mfano wa uwezekano huu wa maandiko, lakini kuna uwezekano mwengine hauko mbali, unaweza pelekea dalili ya Mwanajitihada ya andiko kuweza kuwa na makosa, na tofauti nyingi kati ya Wanajitihada zinatokana na uwezekano uliopo kwenye maandiko, kuanzia kufuta kuhusisha kufungamanisha, kushirikisha, kufumbanisha, na mengineyo, na kufahamu mfano wa uwezekano huu na kutafuta dalili katika wigo wake, ni miongoni mwa kazi za Mwanajitihada na wala sio kazi ya muigaji, hivyo hakuna tofauti kati ya muigaji kupitia dalili ya Qur`ani na Sunna au dalili zingine, kwa kushindwa kwake kufanya utafiti katika yote kwa kuwa kwake muigaji.

Rai ya Tano: Kufaa kwa sharti la udhibiti na uadilifu.

Madhehebu ya Imamu Abu Hanifa na baadhi ya wafuasi wa madhehebu ya Imamu Hambali na baadhi ya wafuasi wa madhehebu ya Imamu Shafi ([72]) wamesema inafaa fat’wa ya muigaji kwa njia ya kuelezea madhehebu ya Mwanajitihada ikiwa vigezo na masharti ya upokeaji yatakamilika ikiwa ni udhibiti na uadilifu.

Wafuasi wa rai hii wametumia dalili ifuatayo:

Dalili ya Kwanza: Fat’wa ya muigaji wakati huo inakuwa ni kwa upande wa kunukuu habari, ikiwa mwenye kunukuu ni mwenye udhibiti na muadilifu basi kwa makubaliano ya Wanachuoni inafaa kufanyiwa kazi habari yake, na hilo ni kutokana na kumuiga Mwanajitihada aliyenukuliwa na wala sio kwa kunukuu kwa muigaji ([73]).

Dalili ya Pili: Makubaliano ya Umma kufanyia kazi mfano wa aina hii ya fat’wa pale penye uchache wa uwepo wa Wanajitihada ([74]).

Dalili ya Tatu: Mufti mwenye kuiga akiwa ni mwenye udhibiti na muadilifu, kwa mtu asiyejua hudhani ni ukweli wake yale anayoelezea, ikiwa atazungumzia kauli ya Mwanajitihada anayeaminika atakuwa na dhana nyengine ya ukweli wa Mwanajitihada katika yale aliyoyatolea fat’wa, kwa kukutana dhana mbili huchukuwa nafasi zaidi dhana ya mtu asiyejua kuwa katika masuala hukumu ya Mwenyezi Mungu ni iliyoelezewa na Mufti muigaji, na kufanyia kazi dhana yenye nafasi kubwa ni jambo la wajibu ([75]).

Rai hii inajibiwa kuwa, ikiwa hakujawekwa sharti la uwezo wa kutoa hukumu za matukio, Sharia itakwama na kushindwa kwenda sambamba na mabadiliko ya maisha, ni katika jambo lisilowezekana kubakia na kukosa uwezo, na maelezo ya kutowezekana kubakia kwake hukwamisha.

Imamu Al-Haramaini anasema: “Kinachoaminika ni kuwa haizingatiwi kutokea tukio na kubakia Sharia mgongoni mwangu nimeibeba isipokuwa Sharia yenye kushikamana na hukumu ya Mwenyezi Mungu iliyomo ndani yake” ([76]).

Hivyo haiwezekani kujitosheleza na uadilifu wenye udhibiti wenye kulinda na kutetea madhehebu ya Imamu wake, kwa sababu dharura itaendelea kuwepo mpaka kwa Mufti mwengine anayeweza kutoa hukumu za matukio kwa madhehebu za Wanajitihada.

Rai ya Sita: Kufaa kwa sharti la udhibiti na uadilifu pamoja na kumuiga Mwanajitihada aliye hai.

Baadhi ya Wanachuoni wamesema inafaa Fat’wa ya mwenye kuiga kwa njia ya kuelezea madhehebu ya Mwanajitihada kwa sharti la Muigaji kuwa ni mwenye udhibiti muadilifu na Mwanajitihada kuwa bado hai ([77]).

Wakatoa ushahidi kwa maelezo yafuatayo:

Dalili ya Kwanza: Mwanajitihada akiwa amefariki haifai kuchukuwa kauli yake, kwa sababu hakuna kauli kwa mtu aliyefariki kwa dalili makubaliano hayafikiwi kwa kutofautiana naye akiwa hai, hufikiwa kwa kufariki kwake, hii inaonesha kuwa hakuna kauli yake inayobakia baada ya kufa kwake ([78]).

Dalili hii inajibiwa kuwa, ikiwa kauli zinakufa kwa kufariki mwenye kauli basi makubaliano ya Wanachuoni yatakufa kwa kufariki Wanachuoni waliokubaliana, na kwa kuwa makubaliano hayafikiwi wakati wa uhai wa Mwanajitihada na hufikiwa baada ya kufa kwake, kwa sababu makubaliano ya Wanachuoni ni kukubaliana Wanajitihada wa Umma wa zama katika zama juu ya jambo miongoni mwa mambo ya kidini, na Umma wakati wa uhai wake hawakukubaliana kwa sababu yeye ni sehemu, baada ya kufariki kwake wamekubaliana wakati hakuna aliye kinyume, kukubaliana kwao kuna kinga ya kukosea…

Kwa vile makubaliano ya Wanachuoni yanapita moja kwa moja na Jitihada ni jambo la dhana, makubaliano ya moja kwa moja hayapingani na dhana, makubaliano huuwa kauli ya Mwanajitihada aliyekinyume ni sawa sawa aliyetangulia makubaliano hayo au aliyokutana nayo, kama vile tamko huuwa kauli yake, basi hakuna jitihada katika tamko, ikiwa hakuna tamko au makubaliano ya Wanachuoni, basi kauli ya Mwanajitihada inabaki wala haifi kwa kufariki mwenye kauli ([79]).

Hii ikiwa utakubalika usahihi wa kufanyika makubaliano ya Wanachuoni baada ya kuwepo tofauti, na kama si hivyo miongoni mwa Wanachuoni wapo wanaozuia makubaliano ya Wanachuoni ikiwa kutakuwepo tofauti katika masuala kati ya Wanajitihada ([80]), hivyo hubatilisha dalili yenu kwenye asili yake.

Abu Is-haq As-Shiirazy amesema: “Ikiwa Maswahaba walitofautiana katika tukio kwa kuwa na kauli mbili kisha Taabiina wakakubaliana na moja kati ya kauli mbili hizo, basi masuala hayana makubaliano yeyote kwa kauli za watu wetu” ([81]).

Dalili ya Pili: Mwanajitihada aliyefariki inafaa kubadilisha jitihada yake lau angekuwa hai, kwa sababu alikuwa analeta mitazamo mipya wakati wa kujirudia tukio, na huenda lau ataleta mtazamo mpya basi atafuta kauli yake ya kwanza, kumfuata kwake kunatokana na udanganyifu wa muono, au kusitasita, na kutoa kauli kwa hali hiyo haifai.

Dalili hii inajibiwa kuwa, lau ingekuwa kufaa kubadilisha Jitihada ni kizuizi cha kuchukuwa kauli ya Mwanajitihada, basi ingezuiliwa kufaa kuiga ni sawa sawa Mwanajitihada akiwa hai au amekufa, sura ya muunganiko ipo wazi, na kuzuia moja kwa moja kuiga ni batili ([82]).

Dalili ya Tatu: Mwenye kujitahidi baada ya kufariki kwake hawi katika Wanajitihada, mfano mwenye kurudi tena ufasiki wake baada ya uadilifu wake hukumu ya uadilifu haitobakia, hivyo haifai kukubalika ushahidi wake vile vile Mwenajitihada baada ya kufa kwake haifai kufuatwa kwa kutokewa kwake na kifo.

Dalili hii inajibiwa kuwa, ushahidi uliothibiti kabla ya kutokewa na ufasiki ni wenye kukubalika, vile vile Jitihada iliyothibiti kabla ya kutokewa na umauti ni yenye kukubalika ([83]).

Dalili ya Nne: Kumuiga Mwanajitihada aliye hai ni dhana yenye nguvu zaidi, kutokana na kupitia kwake mambo ya wakati na mambo mengine ambayo fat’wa hubadilika kwa kubadilika kwake, na kufuata dhana yenye nguvu ni jambo la lazima, hivyo haifai kumuiga Mwanajitihada aliyefariki.

Dalili hii inajibiwa kuwa, madhehebu za Wanajitihada waliotangulia hasa Maimamu wanne, walianzisha misingi na kanuni kuu zinazowezesha wafuasi wa madhehebu haya kuendana na sura zote zinazotokea katika kila zama, na kuleta hukumu zake sawa na kanuni hizo pamoja na misingi hiyo, hivyo madhehebu yanaendelea kuwa hai na siku zote kufaa kuendana na matukio hata kama waasisi wake wamefariki, kwa mfano tukichukulia Mwanajitihada hai kufikia daraja ya Maimamu wa madhehebu akaanzisha madhehebu mapya, basi haichukuliwi yeye kuwa wa mwisho kidhana kwa sababu dalili nyingi za maandiko hujengewa madhehebu yake hayachukuliwi kuwa za kidhana, lau zingekuwa za kukata moja kwa moja basi Maimamu waliotangulia wasingepingana nazo, mambo yakiwa hivyo basi madhehebu ya Mwanajitihada aliye hai yanakuwa sawa na madhehebu ya Wanajitihada waliotangulia, wala hayafikiriwi kuwa kwake na nguvu isipokuwa kwa moja ya mambo mawili:

Jambo la Kwanza: Kupitia yale yasiyopitiwa na waliotangulia miongoni mwa “Maandiko ya Sharia” … lakini hili lipo mbali ambapo maandiko yaliyofika kwetu ni kupitia wafuasi wa madhehebu haya, ni jambo lipo mbali kupatikana andiko halijapitiwa na Wanajitihada waliotangulia au wafuasi wao kwa utafiti na mitazamo.

Jambo la Pili: Kupitia yasiyopitiwa na waliotangulia miongoni mwa “Mabadiliko ya wakati” … na hii hata kama imetokea, isipokuwa muigaji anaweza kutoa hukumu kwa madhehebu ya Imamu wake, anaweza pia kuendana na mabadiliko hayo katika wigo wa jitihada ya kimadhehebu.

Imamu Al-Haramain anasema:

“Huenda Mwanachuoni huru wa madhehebu ya Imamu ni mwenye uwezo zaidi wa kufahamu misingi ya Madhehebu ambayo yameasisiwa na Mwananjitihada katika jaribio lake la kufahamu misingi ya Sharia, Imamu muigaji amefanya juhudi zake kubwa katika udhibiti na kitabu kukipangilia milango na kuandaa mifumo ya Qiyasi “Uwiano” na sababu za kuandika Madhehebu ambayo yameandaliwa na Mwanajitihada katika jaribio lake la kufahamu misingi ya utaratibu wa milango, mwanajitihada ambaye anapaswa kurudisha jambo kwenye asili ya Sharia hapingani na maandalizi na kununi anazozikuta mnukuu wa madhehebu katika asili ya madhehebu yaliyopangiliwa” ([84]).

 Na kwa hali hii hakuna madhehebu ya Mwanajitihada hai yanayopewa nguvu zaidi ya Madhehebu ya Mwanajitihada aliyefariki kwa kipimo cha uhai na kifo, lakini kupewa nguvu kunakuwa kwa kipimo cha kupatikana dalili na kiwango gani cha kufikia makusudio ya Sharia katika maisha ya watu na matukio.

Kupewa nguvu na uzito.

Kwa mara nyengine tunafupisha rai na mitazamo mbalimbali ya Wanachuoni tuliyoielezea kwa kina katika masuala ya Fat’wa ya mtu mwenye kuiga au (Mufti wa lazima) kisha tunataja kwa ufupi kila rai, tunasema Wanachuoni wametafautiana kwa rai mbalimbali…

Rai ya Kwanza: Haifai kabisa.

Rai ya Pili: Inafaa anapokosekana Mwanajitihada.

Rai ya Tatu: Anafaa kwa sharti la Jitihada ya madhehebu.

Rai ya Nne: Anafaa kwa sharti la kufahamu dalili za Mwanajitihada.

Rai ya Tano: Anafaa kwa sharti la udhibiti na uadilifu.

Rai ya Sita: Anafaa kwa sharti la udhibiti, uadilifu, na kumuiga Mwanajitihada aliye hai.

Tunafupisha kuwa rai ya kwanza inaoondolewa, kwa sababu ipo kinyume na uhalisia na kubana watu, jitihada kuiwekea sharti hivi kwa Mamufti, kunaondoa mahitaji ya Umma kwa uwingi wa nchi na uwingi wa waulizaji wakati wote.

Ama rai ya pili, yenyewe pamoja na kuwa karibu zaidi ya rai ya kwanza isipokuwa kufungamanisha kufaa kwa kukosekana Mwanajitihada ndani yake kunaleta uzito pia kama rai ya kwanza, kwani huenda akapatikana Mwanajitihada mmoja au uchache wa Wanajitihada lakini hawakidhi mahitaji ya Umma.

Rai ya tatu, ambayo ni kuiwekea sharti nafasi yake Mufti, isiwe chini ya Jitihada katika madhehebu, ni rai yenye nguvu na ya kuzingatiwa…kinachoweza kusemwa ni kuwa wakati haukosi muigaji anayefikia cheo cha Jitihada katika madhehebu ya Imamu wake, kwa sababu kujirudia kwa matukio kunapelekea Umma kuwa na mahitaji ya Jitihada, na kama si hivyo basi kunaondoa kuwa dini ya ulimwengu na kufaa kwake kuhukumu, nalo ni jambo lisilowezekana, hivyo haiwezekani Fat’wa kuwa huru kabisa mbali na marejeo ya Mwanajitihada walau jitihada ya kimadhehebu, ambapo yenyewe si yenye kuhitajika sana kubainisha hukumu za mambo yanayotokea.

Imamu Zarkashy anasema: “Ukweli ni kuwa wakati unaweza kukosa kabisa Mwanajitihada, si Mwanajitihada ndani ya moja ya madhehebu ya Maimamu wa nne” ([85]).

Lakini kama ilivyosemwa katika rai mbili zilizopita… huenda akapatikana Mwanajitihada mmoja au zaidi wa kimadhehebu lakini hawakidhi mahitaji ya Umma kutokana na uwingi wa miji na nchi pamoja na uwingi wa wataka fat’wa kwa siku, kuhusisha nafasi ya Fat’wa kwa Mwanajitihada peke yake au Mwanajitihada wa madhehebu ni sehemu ya uzito, hivyo kauli yenye nguvu zaidi ni kutofaa kuiondoa nafasi ya utoaji fat’wa kwa Mwanajitihada wa kimadhehebu, pamoja na kufaa kufanya kazi hiyo Mamufti wengine ambao hawajafikia cheo chake ambapo anakuwa ni marejeo yao, kwa Jitihada zao za kimadhehebu katika mambo yanayojitokeza hutoa fat’wa.

Ama rai ya nne, ambayo inaweka sharti la Mufti muigaji kufahamu dalili ya Mwanajitihada katika kila masuala anayoyatolea fat’wa ni rai ya kutupwa, kwa sababu muigaji hafikiriwi kufahamu dalili, kwa sababu kufahamu dalili kunahitaji kufahamu vyanzo na hoja zake na njia za uletaji dalili, na kufikia hilo kunakuwa kwa mtazamo na kujadili, mwenye kuiga si mtu wa mtazamo na kujadili, hivyo hafikiriwi kufahamu dalili.

Rai ya tano, yenye kusema inafaa Fat’wa ya muigaji akiwa ni mdhibiti muadilifu na kunukuu kwa Mwanajitihada, inafahamika kuwa rai hii haikutenganisha kati ya kuwa mnukuu kutoka kwa Mwanajitihada aliye hai au aliyefariki, tuchukulie kuwa huyu Mufti mwenye kuiga hana uwezo wa kufanya jitihada katika madhehebu ya Mwanajitihada au kuleta hukumu, jambo linalomaanisha kuwa matukio mapya yatawezekana kutolewa fat’wa kama Imamu Mwanajitihada hatokuwa hai, hivyo Sharia itakwama na wala hakuna umuhimu wa kuwa na Mufti kama huyu, hivyo rai hii pia ni ya kuachwa.

Ama rai ya sita, yenye kusema kufaa kwa sharti la udhibiti uadilifu na kumuiga Mwanajitihada aliyehai, ni rai bora kukubalika isipokuwa kuweka sharti la Mwanajitihada aliyehai ikiwa inayokusudiwa ni Jitihada basi ni rai ya kuwekwa mbali, kwa kukosekana kwake ndani ya zama hizi, au kwa makadirio ya chini ni kutokana na ugumu wa kumfikia Mwanajitihada huyu ikiwa anapatikana.

Ama ikiwa inakusudiwa Jitihada tu basi hapo anaingia Mwanajitihada wa madhehebu, na hii inakuwa ndio rai yenye nguvu kutokana na ndani yake kuwemo wepesi kwa Umma wa kuwa na Wanafat’wa wengi, na Sharia kuendelea kubainisha hukumu ya matukio na mambo mapya kwa njia ya kurejea kwa hawa Mamufti wenye kuaminika kwa Wanajitihada wa madhehebu na fat’wa zao kwa yale waliyoyafikia.

Yaliyopitishwa kwa mujibu wa yanayoonekana kwetu.

Ikiwa rai ya sita haichukui tafasiri ya Mwanajitihada hai kwa zaidi ya Mwanajitihada kamili na Mwanajitihada wa kimadhehebu, basi hakuna ubaya wa kukusanya kati ya rai ya tatu na sita pamoja na kuepusha yanayoleta matatizo kwenye rai hizo mbili.

Kwa maelezo haya kinachochukuliwa kinakuwa ni: Kufaa kwa Fat’wa ya muigaji (Mufti wa lazima) akiwa ni mdhibiti na muadilifu, kwa sharti la kurejea kwake kwa Mwanajitihada aliye hai ni sawa sawa akiwa Mwanajitihada kamili au Mwanajitihada katika moja ya madhehebu ya Maimamu wanaofuatwa, humuiga katika utoaji hukumu za matukio kwa kanuni za Mwanajitihada kamili, na katika kufahamu kauli zenye nguvu na sura mbalimbali katika madhehebu.

Hili ni kuwa kuhusisha fat’wa kwa Mwanajitihada ni sawa sawa akiwa Mwanajitihada kamili au wa kimadhehebu ndani yake kuna ugumu kwa Umma kusikoendana na uhalisia wake na mahitaji yake, vile vile haifai kumtegemea muigaji mwenye kunukuu tu kutokana na kushindwa kwake kutoa hukumu za matukio, hivyo kauli iliyopitishwa ni kufaa Fat’wa ya mwenye kunukuu kwa sharti la kumuiga Mwanajitihada aliyehai ni sawa sawa akiwa Mwanajitihada wa madhehebu au Mwanajitihada kamili.

Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi

Ewe Mwenyezi Mungu tunakuomba umteremshie rehma na baraka Mtume wetu Muhammad pamoja na kwa watu wake na Maswahaba zake na wanaowafuata kwa wema mpaka Siku ya Malipo.

Imeandikwa Na:

Mtafiti / Ahmad Mahmoud Ally.

30 / 09/ 2009.

 

 

[1] Imepokewa na Abu Daud Hadithi nambari 3641. Na Tirmidhy Hadithi nambar 2682. Na Ibn Maja Hadithi nambari 223…..

[2] Kitabu cha Ghayya Al-Umam ukurasa wa 285.

[3] Imekubaliwa na Jamhuri ya Wanachuoni wa Hadithi: Na imepokewa na Imamu Bukhary Hadithi nambari 6858. Na Imamu Musliamu Hadithi nambari 1337,

[4] Angalia kitabu cha: Lisaanul Arabi mada ya fat’wa 15/145.

[5] Angalia kitabu cha: Al-Majmui 1/74.

[6] Angalia: Kamusi elezi ya fiqhi chapa ya Kuweit, msamiati wa fat’wa 27/32, na Imamu An-Nawawi anasema: Mtu fasiki haikubaliki fat’wa zake na analazimika kufajifanyia yeye mwenyewe Ijitihada, kitabu cha Rawdhatul-Twalibina 8/87.

[7] Angalia kitabu Rawdhatul-Twalibiin.

[8] Angalia kitabu cha Hashiyatu Ibn Aabideen 5/359.

[9] Ni marejeo hayo hayo yaliyopita.

[10] Kitabu cha misingi ya fiqhi cha Dr. Wahbatu Az-Zuhaily 2/1156.

[11] Angalia: Kitabu cha Fat’hu Al-Qadiir 6/256.

[12] Angalia: Hashiyatu Ibn Aabidiin kwenye kitabu cha Ad-Durru Al-Mukhtar 5/365.

[13] Angalia: Kitabu cha Al-Bahru Al-Muhiitwu 6/306.

[14] Angalia: Bayaanul-Mukhtaswar cha Aswafahany 3/288.

[15] Kitabu cha Ghiyaabati Al-Umam kutoka ukurasa wa 289 mpaka 291.

[16] Angalia kitabu cha: Aqdu Al-Jayyid fii Ahkaami Al-Ijtihaad ukurasa wa 3.

[17] Kitabu cha Majmuui 1/74 – 75.

[18] Kitabu cha Aqdul-Jayyid fii Ahkaami al-ijitiihaad wa taqliid ukurasa wa 3.

[19] Kitabu cha Al-Mujmuui 1/75.

[20] Kitabu cha Aqdu Al-Jayyid fii Ahkaami Al-Ijtihaad wa Taqliid ukurasa wa 3.

[21] Kitabu cha Al-Majmuui 1/76.

[22] Kitabu cha Aqdul-Jayyid fii Ahkaami Al-Ijtihaad wa Taqliid ukurasa wa 3.

[23] Kitabu cha Ghaayatil-Umami ukurasa wa 306.

[24] Kitabu cha Al-Majmuui 1/76.

[25] Kitabu cha Aqdul-Jayyid fii Ahkaami Al-Ijtihaad wa Taqliid ukurasa wa 3.

[26] Kitabu cha Al-Majimuui 1/77 – 78.

[27] Kitabu cha Ghiyaatul-Umami ukurasa wa 300.

[28] Kitabu cha Majmuui 1/77 – 78.

[29] Angalia: Hashiyatu Al-Atwar sherehe ya Jamuu Al-Jawaamii 2/437.

[30] Imepokewa na Imamu Ahmad 1/313 Hadithi nambari 2867, na imepokewa na Ibn Maja Hadithi nambari 2340.

[31] Mapokezi yaliyotangulia.

[32] Angalia kitabu cha Al-Mahmuul 6/72, kitabu cha Al-Ihkaami 4/283, kitabu cha Al-Wasiitw 7/291 na kitabu cha Al-Bahriu Al-Muhiitw 6/207.

[33] Angalia kitabu cha At-Tahabiir 8/4059, kitabu cha sherehe ya Al-Kaukabul-Muniir 4/564.

[34] Imepokewa na Imamu Bukhary Hadithi nambari 100. Na imepokewa na Imamu Muslimu Hadithi nambari 2673

[35] Imepokewa na Imamu Bukhary Hadithi nambari 6653. Na imepokewa na Imamu Muslimu Hadithi nambari 2672.

[36] Kitabu cha Al-Mahsuulu 6/97, 98.

[37] Kitabu cha Al-Ibhaaji 3/269.

[38] Kitabu cha Al-Ihkaami fii Usuuli Al-Ahkaami 1/299.

[39]  Albahrul Muhiitw 6/209.

[40] Kitabu cha Ghayyat Al-Umam ukurasa wa 300.

[41] Kitabu cha Alwasiit 7/291.

[42] Kitabu cha Al-Majmuui 1/43.

[43] Al-Bahru Al-Muhiitw 6/209.

[44] Imepokewa na Imamu Muslimu.

[45] Imepokewa na Imamu Muslimu Hadithi nambari 1920.

[46] Imepokewa na Abu Daud Hadithi nambari 2484.

[47] Kitabu cha Ghayath Al-Umami ukurasa wa 306, 307.

[48] Maelezo yake yametangulia.

[49] Kitabu cha Nihaayatul- Wusuuli 8/3886.

[50] Rejea kitabu cha sherhe Al-Kaukabu Al-Muniir 4/557. Kitabu cha Attahbiir sherehe ya Attahriir 8/4070. Kitabu cha Adabu Al-Mufti wal Mustaftiy 1/38.

[51] Angalia kitabu cha Al-Haawi Al-Kabiir 16/50 – 53.

[52] Angalia kitabu cha Al-Muutamad 2/929.

[53] Rejea kitabu cha sherhe Al-Kaukabu Al-Muniir 4/563.

[54] Angalia kitabu cha Muutamid 2/932.

[55] Rejea kitabu cha Al-Muutamid 2/933.

[56] Kitabu cha Al-Mahsuul 6/70.

[57] Rejea kitabu cha Attahbiir 8/4059, na kitabu cha Nihaayatul-Wusuuli 8/3887.

[58] Angalia kitabu cha Bayaani Al-Mukhtasara cha Al-Asfahany 3/365.

[59] Angalia kitabu cha Al-Bahru Al-Muhiitw 6/299.

[60] Kitabu cha Attahbiir 8/4070.

[61] Kitabu cha Ghayyati Al-Umami ukurasa wa 297, 299.

[62]  Angalia kitabu cha: Nihayatul-Wusuuli 8/3883.

[63] Rejea kitabu cha Attahbiir: 8/3983

[64] Kitabu cha Ghayaat Al-Umami ukurasa wa 307

[65] Angalia kitabu cha: Al-Ihkaami 4/287, na kitabu cha Mukhtasar Ibn Al-Hajib kwa sherehe yake ya Aswfahany 3/365, pia kitabu cha Nihayatul-Wusuli 8/3885.

[66] Angalia kitabu cha Attahbiir 8/4072.

[67] Angalia kitabu cha: Fawatihul-Rahmuut 2/404.

[68] Angalia kitabu cha: Al-Ihkaami 4/287.

[69] Angalia kitabu cha Attahbiir

[70] Angalia kitabu cha Al-Hawii Al-Kabiir 1/21.

[71] Kitabu cha Rawdhatul-Twaalibina 4/114.

[72] Rejea kitabu cha Attahbiir 8/470.

[73] Rejea kitabu cha Fawatihi Rahmuut 2/404, na kitabu cha Bayani Al-Mukhtasar 3/366.

[74] Rejea kitabu cha: Al-Mahsuul 6/71, na kitabu cha Fawatih Rahmuut 2/404.

[75] Angalia kitabu cha: Al-Mahsuul 6/71. Na kitabu cha Nihayatul-Wusuul 8/3886.

[76] Ghayatul-Umami ukurasa wa 310.

[77] Rejea kitabu cha: Al-Mahsuul 6/71.

[78] Angalia kitabu cha: Al-Mahsuul 6/71.

[79] Rejea kitabu cha: Fawatih Rahmuut 2/407.

[80] Rejea kitabu cha: Nihayatul-Wusuul 6/2540.

[81] Kitabu cha Tabswirah ukurasa wa 378.

[82] Angalia kitabu cha: Bayani Al-Mukhtasar 3/362. Na utafiti wa hukumu ya muiga mwanajitihada aliyefariki kwa watu wa masomo ya misingi ukurasa wa 518.

[83] Ni marejeo hay ohayo yaliyotangulia.

[84] Kitabu cha Ghayatul-Umami ukurasa wa 307.

[85] Kitabu cha Al-BAhru Al-Muhitu /209.

Share this:

Related Fatwas