Ulemavu wa viinitete (Mtoto tumboni...

Egypt's Dar Al-Ifta

Ulemavu wa viinitete (Mtoto tumboni)

Question

Ipi hukumu ya kutumia njia za kisasa katika kuangalia ulemavu wa viinitete na matibabu yake?

Answer

Kutumia njia za kisasa ili kuangalia ulemavu ambao unaweza tokea kwenye kiungo chochote katika viungo vya mwili wakati kiinitete (Mtoto wa tumboni) akiwa bado yu tumboni mwa mama yake, ni jambo linaloruhusiwa, kwa vile tu wanaosimamia vipimo wawe ni madaktari wenye weledi na uwezo, isipokuwa kama kutapelekea madhara au kudhaniwa kutokea hayo madhara kwa mama au kwa mtoto (kiinitete), wakati huo itakuwa haifai Kisharia.

Vile vile njia za tiba ambazo hutumika kutibia ulemavu wa mtoto tumboni kama vile tiba ya dawa au kufanya upasuaji, hakuzuiwi kufanya hivyo isipokuwa ikiwa madhara yake yana nafasi kubwa, ambapo uharibifu wa kutumia kwake ni zaidi ya uharibu wa kuacha kwake.

Share this:

Related Fatwas