Hukumu ya kusema “Harama” baada ya ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya kusema “Harama” baada ya sala

Question

Ni nini hukumu ya kusema “Harama” baada ya sala?

Answer

Waislbcm amu kusema wenyewe kwa wenyewe baada ya sala “Harama” ni dua kwa maana nakuombea usalie Msikiti Mtukufu, kwa hiyo waislamu kuombeana dua baada ya kumaliza sala ni jambo linaloruhusiwa kisheria, wala haijuzu kukataliwa, kwani dua katika asili yake ni mubaha, na kuitoa baada ya sala ni dalili ya kupendekezwa kwake zaidi, na hutarajiwa kukubaliwa ikitolewa na mwislamu kwa nduguye mwislamu mwingine, hivyo ndivyo walivyozoea waislamu katika zama zote, ama wale wanaodai kuwa dua hii au dua kwa jumla ni bidaa au ni jambo lisilokubaliwa katika sheria, basi ni dalili ya upotofu wa fikra na ufisadi wa maoni lisiloridhikiwa na Mwenyezi Mungu (S.W.) wala Mtume wake (S.A.W.).      

Share this:

Related Fatwas