Nafasi ya Muislamu kwa kutofautiana kwa marejeleo ya kisharia
Question
Nafasi ya Muislamu kwa kutofautiana kwa marejeleo ya kisharia
Answer
(utafiti wa misingi ya dini)
Muandishi: Hesham Rabii Ibrahim
Mtafiti katika idara ya utafiti wa kisharia
...
***
Muhtasari wa tafiti…
Kichwa cha habari cha utafiti huu ni [Nafasi ya Muislamu katika kufuata marejeleo tofauti ya kisharia). Tumeelezea kwa mtazamo mwepesi mambo tofauti yenye kushikamana na Fiqhi na misingi yake na kanuni zake.
Na utafiti huu umekusanya sehemu mbili:
Sehemu ya kwanza: nafasi ya Muislamu katika kufuata madhehebu tofauti ya kifiqhi. Nao unakusanya masuala mawili:
Suala la kwanza: Vidhibiti vya kushughulikia tofauti za kifiqhi kati ya Madhehebu.
Suala la pili: Madhehebu ya kifiqhi, na hukumu ya kuyafuata na kutoyafuata.
Sehemu ya pili: Nafasi ya muulizaji kwa kutofautiana anaowauliza (Mufti wengi walio tofauti) na tukamalizia utafiti huu kwa kutoa matokeo ambayo tuliyoyafikia, na tukayachunguza hayo yote kwa wachunguzaji, moja wapo ni marejeo ambayo tumeyategemea na mengine ni maudhui ambazo zimekusanywa katika utafiti huu.
***
Yaliyomo katika maudhui
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, rehma na amani zimshukie Mtume Muhammad mfunguzi wa vilivyofungwa, mpigania ukweli kwa ukweli, muongozaji katika njia ya Mwenyezi Mungu iliyonyooka, rehma na amani zimshukie juu yake na masahaba zake wote.
Baada ya hayo:
Utafiti huu unalenga kutibu moja kati ya masuala ya muhimu sana ya kimsingi ambayo yamekuwa yakijotokeza wenyewe katika uwanja wa kielimu, kwa kuwa maneno yamekuwa mengi na mijadala, semina na vikao vingi vimefanyika kwa lengo la kufanya utafiti wake na kutaka kuleta rai moja yenye kujulikana; nalo ni suala la {marejeleo kuwa tofauti} lengo letu katika utafiri huu ni kujua nafasi ya Muislamu juu ya utofauti huu na kujua hali ambazo zimeambatana na kutofautiana kwa marejeleo.
Na hakuna shaka jambo linalohitajika katika utafiti wa kifiqhi kwa wakati tulonao ni kufikia namna ya kushughulikia tofauti na yanayoshikamana, na hatutaki kujua masuala na kutoa dalili zake, na kuyapa nafasi madhehebu yake na kuijibu rai ya anayepinga tu, isipokuwa tunataka pamoja na hayo yote kuweka kidhibiti muhimu katika utofauti huo. Na pasingelikuwepo na faida ya kujua jambo hilo basi ingekuwa ni sawa kwa mchango wake katika kuthibitisha ukweli wa hoja baina ya kauli wakati wa kutoa fatwa, kufanya hivyo kungekuwa na manufaa ya kutosha.
Na kutilia mkazo haja ya kutaka kupata kuelewa maelezo haya imetokana na undani unaojitokeza kwa mwenye kujitahidi au kwa uchache kwa kuwa kuna utafauti wa masuala kwenye jambo hili kupitia vitabu vya waliotangulia vilivyoandikwa kwa maelezo yao na pingamizi zao na havikukusanya kwa uwazi zaidi juu ya maudhui hii isipokuwa kwa uchache.
Na suala la marejeleo tofauti linagusa maeneo mengi katika masuala mengine madogo madogo na tumejaribu kukusanya sehemu zake katika tafiti hii ambayo tumeipa jina la {Nafasi ya Muislamu kwa kutofautiana kwa marejeleo ya kisharia}
Na tusemapo {marejeleo} katika utafiti huu tunamaanisha moja ya mambo mawili:
Kwanza: watu wenye kujulikana kwa ujuzi wa mambo ya kielemu au elimu ya kisharia nao ni wanazuoni.
Pili: mitaala ambayo hutegemewa katika kutoa maarifa au maono yaliyotoka katika mitazamo iliyo na vyanzo na dalili.
Pia inaweza kukusudiwa kwa {marejeleo} kwa mambo mengine ambayo hayamo katika utafiti wetu huu[1]. Kwa maana hiyo neno {marejeleo} kupitia utafiti huu limegaiwa katika sehemu mbili.
Sehemu ya kwanza: nafasi ya Muislamu katika kufuata madhehebu tofauti ya kifiqhi.
Sehemu ya pili: Nafasi ya muulizaji kwa kutofautiana anaowauliza (Mufti wengi walio tafauti)
Tunamuomba Mwenyezi Mungu atuwezeshe na kutuepusha na makosa.
***
Sehemu ya kwanza:
Nafasi ya Muislamu katika kufuata Madhehebu tofauti ya kifiqhi.
Ikikusanya masuala mawili
Suala la kwanza: Vidhibiti vya kushughulikia hitilafu za kifiqhi kati ya madhehebu.
Suala la pili: Madhehebu ya kifiqhi, na hukumu yakuyafuata na kutoyafuata.
Suala la kwanza:
Vidhibiti vya kushughulikia hitilafu za kifiqhi kati ya Madhehebu.
Utangulizi
Kuwepo kwa tofauti katika masuala ya kimtazamo wa kiakili kwa ujumla na kwa upekee katika masuala ya kifiqhi ni jambo la kawaida duniani, kutafautiana hakujaacha kuwepo kwa wanadamu tangu zama za Nuhu (AS) na hakuna umma uliosalimika na jambo hili. Na katika aliyojaalia Mwenyezi Mungu kwa umma huu wa Kiisilamu kuwa utatafautiana kama zilivyotafautina umma zilizotangulia, na hitilafu hizo ni kawaida ya kilimwengu. Na kwa hilo ameseme ﴾Na kama Mola wako Angalipenda, bila shaka Angaliwafanya watu kuwa umati mmoja. Nao wataendelea kuhitilafiana… Isipokuwa yule ambaye Mola wako Amemrehemu; na kwa (rehema) hiyo Amewaumba. ﴿ (Surat Hud 118-119).
Kisha ilivyokuwa kutofautina kupo baina ya wenye ukweli na kwenye mipaka maalumu ya kisheria na katika vidhiiti vyke huwa ni jambo lenye kufaa na wala si makosa. Na haikuwa misingi ya kushauriana isipokuwa ni kwa ajili ya kuweka kidhibiti muhimu ikitokezea kutafautiana (na shauriana nao katika mambo) (Al Imran 159). ni mara ngapi Mtume (S.W.A.) alikuwa akishauriana na masahaba zake na kusikiliza maoni yao, na hutokezea kutafautina mitazamo na masahaba zake lakini jambo hili halikupelekea kutowathamini au kutowaheshimiana kati yao.
Jahawiy anaseme katika kitabu cha (Al-fikri Al-Samy) “na upeo wa kuanza kwa kutofautiana ni kule kuitakidi kwamba mpinzani wake ni mkosa katika suala husika kwa ushahidi kuwa amekosea katika muono wake, na anaitakidi kuwa ana udhuru kwa ile dalili aliyoitoa na wala hakuna upungufu juu ya hilo, na walikuwa wakimpa kilamwanachuoni haki yake na kukiri ubora wake na kuheshimu maono yake, hapo haikuwa hitilafu ni yenye madhara kwa upande wao na wala haikuwa jambo la kuaibishana lakini huhesabika kuwa ni ufuatiliaji wa kutaka kuonesha ukweli na kwa ajili hiyo tukamuhesabu kuwa ni kijana mwenye nguvu.[2]
Na imepokewa kutoka kwa Abi Dardai amesema: amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehma na amani zimshukie (alichohalalisha Mwenyezi Mungu katika kitabu chake basi ni halali na alichokiharamisha basi huwa ni haramu na alichokinyamazia huo ni msamaha, basi upokeeni msamaha wake kwani Mwenyezi Mungu hakuwa ni mwenye kusahau. Kisha akaisoma Aya hii (Hakuwa Mola wako ni mwenye kusahau)[3].
Na yale yaliyonyamaziwa mara nyingi huwa ndio maeneo ya hitilafu, kwa kukosekana dalili katika jambo ndio hupelekea kuwepo kwa hitilafu.
Ama maelezo kuhusu ushahidi wa vipengele hivi upo mwingi sana na jambo linaloshikamana na kushirikiana ni kuwa hitilafu ipo kwenye matawi, na umma hauhitajii kushika rai moja, iwapo rai moja itakuwa ni vigumu atashikamana na rai ya Madhehebu mengine au kama atapata matatizo basi ataelekea kwengine kwa vidhibiti maalumu.
Na kwa kutafuta utaratibu wa kuzungumzia hitilafu hizo au kwa usahihi zaidi ni kuwa hatukupata kitabu cha kina kilichokusanya vipengele mbalimbali vya mada hii, isipokuwa ni vidokezo[4] tu vyenye kuhitahi juhudi kubwa hasa ukizingatia ni kama jiwe la kusagia ambalo fatwa huzunguka humo humo katika zama za kisasa au kwa uchache hiyo ni moja ya vipengele vyake. Na kwa utaratibu huu inapasa kufanya kuwa ni sehemu ya adabu za hitilafu, lakini kabla ya kuijumuisha inapasa kulazimika kueleza masharti ya kuzingatiwa katika hitilafu kwa kuwa kuanzisha mfano wa masharti ya adabu nako pia huzingatiwa ni hitilafu. Kwa ajili hiyo maualamma wameweka masharti yenye kuzingatiwa wakati wa kuhitilafiana nayo:
Mosi: isiwe kipengele cha hitilafu ni dhaifu, iwapo ni dhaifu basi haitozingatiwa. Na maana ya udhaifu ni kule kuhitilafiana aya au mkusanyiko wa wanavyuoni au kipimo cha uwiano (kiyasi).[5]
Darder nasema katika (Asharhu Lkabiir) naye anaelezea yenye kubatilisha hukumu na yasiyobatilisha “haifai kwa mwenye Mufti aliyejua hukumu ya Kadhi wake kujibu kinyume na Kadhi wake. Na hi ni kwa hitilafu yenye kuzingatiwa kati ya wanazuoni ama kwa kile ambacho ni dhaifu kueleweka kwake kwa kutafautina kwa dalili au kipimo cha uwiano (kiyasi) au makubaliano ya ulamaa (Ijmaa) hiyo hubatilika.[6]”
Na sharti hili amelielezea Imam Suyuty akasema: “awe na uhakikaka wa ufahamu wake ili isiwe ni kosa” kisha akatoa mfano wa hitilafu ya udhaifu wa ufahamu akasema “kwa ajili hiyo ikawa funga kwa msafiri mwenye nguvu ni bora, na wala hakujali kauli ya Daudi: kuwa haiswihi. Na imamu wa Haramain amesema katika masuala haya: “na wahakiki hawalipi uzito hata kidogo kwa kutofautina na Ahlu dhahir.[7]
Al-Khatib Alshibiny anasema: (Na wala Mwanachuoni hakanushi isipokuwa kuna maafikiano katika kilichokanushwa na wanazuoni, na si kile kilichohitilifiana isipokuwa muhusika akiona ni haramu.” Na ikisemwa “wameeleza Hanafiy humpa adhabu ya Hadi mlevi (aliyetumia kilevi cha zabibu) pamoja na kuwa makemeo ya kivitendo ni makubwa zaidi kuliko ya matamshi” ikajibiwa kuwa “dalili ya kutoharamisha ulevi (uliotengenezwa kwa zabibu) hazina nguvu. Na kwa ajili hiyo kuna tofauti kati ya kupewa adhabu kwa mlevi na kutopewa adhabu aliyeingilia katika ndoa isiyo na walii.[8]”
Ama kwa maelezo yaliyotegemea dalili zenye hitilafu katika kuyathibitisha, hitilafu inayojitokeza huwa haikubaliwi na kuzingatiwa isipokuwa iwapo dalili iliyopo inafaaa kuwepo hitilafu kwa kuthibiti kwake, mfano wa hadithi ambazo mlolongo wake umekatika wapokezi.
Pili: Mwenye kupinga awe ni katika wanazuoni wajulikanao. Na kwa ajili hii sheikh Mohamed Hasaneyn Makhluf anasema katika kitabu chake (Bulugh lsuul) kwenye anuani: kutegemea kauli za wenye kujitahidi katika masuala ya kisheria: “nawakashurutisha kwa mwenye kuleta matokeo aliyoyapata kwenye dalili za ujumla katika hukumu ya kisheria – ilivyokuwa ni dhana haitoleta matokeo isipokuwa dhana – hivyo anatakiwa Lazima awe na sifa maalum, nguvu maalum, na ujuzi mkbwa itakaomwezesha kuchunguza kwa kina dalili namna ambayo dhana yake iwe kama elimu ya uhakika ili kuhifadhi hukumu za dini kuepukana na makosa kadiri awezavyo.[9]”
Tatu: kauli inayohitilafiana isiwe katika zile walizowafikiana maulamaa katika suala moja, kwa maana kusiwe na kauli nyengine mpya, kwa sababu kuzunguka (kuwepo) kwa kauli mbili zenye hitilafu au tatu kwa mfano itapelekea kuwepo makubaliano kuwa haki haikosekani kati ya kauli hizo, na kwa kuwa umma haukusanyiki katika upotevu. Na kuitakidi kuwa haki haipo kupitia makubaliano hayo na wao wote wamekosea hii italazimu kuitakidi kuwa wamekusanyika (wamekubaliana) kwa jambo la upotevu[10].
Na kwa kuzingatia yaliyopita; hitilafu inagawanyika katika vigawanyo viwili:
Kwanza: Jambo la wazi lenye kwa kuzingatia ushahidi na sheria na limejengewa misingi ya kujitahidi na uelewa wa hukumu, nayo ni hitilafu iliyozoeleka, na ndani ya aina hii kuna masuala mengi sana yasiyohesabika. Kwa ajili hiyo Ashatiby anasema “hitilafu iliyozoeleka ipo katika masuala mengi ya kisheria na hitilafu isiyozoeleka ni chache[11].
Pili: Iliyo na udhaifu katika mtazamo wake, iliyopotoka katika njia ya kuithibitisha hoja yake, aina hii hurudishiwa mwenyewe (msemaji wake) na hupingwa. Sehemu hii inabeba ndani yake uhalisia ambao maimamu walikuwa wakijibizana wao kwa wao, na kupinga kwao ni katika kauli isiyo ya kawaida.
Na ili hitilafu iwe yenye kuzingatiwa kuna mambo mengi ya kuzingatia tumeweka kama ifuatavyo:
Kwanza: Adabu kwa unayempinga
Ikimaanisha kuwa na dhana nzuri kwa upande wa pili, kuitakidi kuwa lengo lake ni kuifikia haki, kujibu kwa upole ili kuepusha mtafaruku utakaopelekea fitina kwa wanaohitilafiana. Kwa ajili hiyo Ibn Taimia anasema: “walikuwa wakijadiliana masuala ya kielimu na kivitendo huku wakidumisha upendo na kuhifadhi undugu wa kidini. na laiti ingelikuwa kila wanapohitilafiana waisilamu wawili hutengana basi waislamu wasingelibakia na wala undugu usingelikuwepo.[12]”
Imepokewa na Abi Hubaybah Bwana wa Talha (RA) amesema: niliingia kwa Ali pamoja na Imran bin Talhah baada ya kumalizana na wamiliki wa ngamia, akasema, akamkaribisha na akasema” mimi nataraji Mwenyezi Mungu anijaalie na baba yako tuwe katika wale aliosema Mwenyezi Mungu Mtukufu ((Na tutaondoa chuki iliyo kuwamo vifuani mwao, wawe ndugu juu ya viti vya enzi wameelekeana[13])
Na Adaradauwdy amepokea amesema “nilimuona Aba Hanifa na Malik Ibn Anas ndani ya msikiti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (SWA) baada ya sala ya Isha nao wanakumbushana na kusomeshana, mpaka aliposimama mmoja wao juu ya kauli ambayo amesema na mwenye kauli yake mwengine akaipinga bila ya Bila ya ukali, kukunja uso au kukosoa, mpaka walisali Sala ya Alfajiri katika mkusanyiko wao huo[14].”
Na hitilafu haipaswi kuwa imekusidiwa dhati yake, nayo ni kule kufanya kwa wanaohitiliafiana kuwa lengo lao ni kuufikia ukweli kujiweka mbali na ria na majadiliano, hii inamaanisha kuleta suluhisho la mzozo na kuchunga kwake. Kama tutakavyoeleza baadae. Na katika matunda yake ni kukiri makosa na kuyakubali. Na katika ya kuchunga ni kutosema jambo bila ya ujuzi nalo, kwa ajili hiyo ni lazima kujua kile ukisemacho juu ya masuala ya hitilafu na yenye kutakikana vile vile kuthibiti juu ya kauli ya mwenye kupinga kabla ya kumnasibishia kauli hiyo kwa namna yoyote ile awayo mwenye kupinga.
Pili: kutoka katika hililafu
Wanawazuoni wameweka sheria inayohesabika ni yenye kuinua tabia njema na upendo wa kweli katika kuweka pamoja watu wa madhebubu tofauti, nayo ni “kujitoa katika hitilafu ni jambo lenye kupendeza” ni kanuni iliyoafikiwa na wanazuoni wote hata baadhi ya wafuasi wa Malik wameifanya sheria hii ni miongoni mwa dalili ambayo Madhehebu yao huitegemea katika kutendeana na uhalisia ambayo wameipa jina la (msingi wa Madhehebu). Hata Ibn Arafa aliiona kuwa ni miongoni mwa fadhila / mema ya madhehebu hayo[15].
Na kupitia sheria hii wanazuoni wengi na wenye kujitahidi wameifanyia kazi katika masuala mengi yenye hitilafu jambo lenye kujulisha maana halisi ya ufahamu wa sheria hii. Wanazuoni kutoka kwa Hanifa; imamu Ibn Najim na Ibn Hemaam na Ibn Abidin na kutoka kwa Shafii; Imam Alzarkashy, Al izzu bin Abdel salaam, Altaj alsabaky na Alsuyuty. Na kutoka kwa Hanbal; Almuwafiq ibn Qudama na Al bahyuty na wengineo[16].
Na wanaieleza wanazuoni sheria hii kwa kusema “kuchunga hitilafu” badala ya kusema “kujitoa katika hitilafu”, hizo ni taabira mbili kwa maana moja, tofauti na inavyoenea kuwa kuna tofauti ya taabira mbili hizi na kunasibisha na madhehebu ya imam Malik, na pengine sababu ya kutofahamika huko ni kupokea kwa baadhi ya wafuasi wa Malik kama Ibn Arafa na Shatiby katika kuielezea hitilafu. Ibn Arafa anasema “kuitendea kazi hoja bila ya kubadilika dhumuni lake ambalo ushahidi mwengine ulitumiwa kuipinga hoja nyingine.[17]”
Alshatiby anasema “Kuipa kila moja wapo, yaani, ushahidi wa rai hizo mbili, kile ambacho nyingine inahitaji, au baadhi ya kile inachohitaji, hiyo ndio maana ya kuzingatia kutofautiana.[18]”
Na kupitia maana hizi mbili za kueleza hitilafu, ibara za waliotangulia katika dhehebu la Malik kama imamu Alqabbab[19] inamaanisha kuifanyia kazi mwanachuoni dalili ya mwenye kumpinga katika kuthibiti kinachopingwa, kwa mfano; kuthibiti urithi kati ya wanandoa ndoa isiyo na mahari (Ashighaar) pindi mmoja wao atakapofariki, pamoja na kuwa wanasema kuwa ndoa isiyo namahari (shighaar) huwa ni batili. Hii ikawa sababu ya kusema kuwa madhehebu ya Malik hawachungi hitilafu isipokuwa pale linapojitokeza suala lenye hitilafu, aidha, kwa kusoma tu kidogo matawi ya kielimu itaeleweka kuwa wanazuoni wa Malik huonekana wapo kinyume na hayo, au madhehebu ya Malik ni kama madhehebu mengine kuwa yanachunga hitilafu kabla au baada ya kutokea tukio.
Kauli ya wanazuoni na wanazuoni wa Usul zinakaribia kukubaliana kuwa malumbano haya katika kujadiliana na masuala ya hitilafu ni jambo jema isipokuwa kupendeza inaweza ikawa kidogo au kukubwa itategemea na suala lililopo na dalili zake zinazozingatiwa. Kwa ajili hiyo Alzarkashy amesema “hitilafu inashikamana na utafiti: kwanza ni; inapendelewa kujitoa kwenye hitilafu.[20]”
Izzu ibn Adulsalam anasema: “Iwapo ushahidi utakaribiana katika mzozo uliopo kwa namna ambayo kauli ya mwenye kupinga ipo mbali, basi katika hali kama hii inapendeza kujitoa katika hitilafu[21].”
Na ibn Abidin anasema: “kwetu tunahitajika kuzingatia hitilafu[22].”
Ibn Abidin anamnukuu mwandishi wa “An-Nahr Al-Fa’iq” akisema: “Viwango vya mapendekezo vinatofautiana kulingana na nguvu au udhaifu wa ushahidi wa mpinzani.[23]”
Faida tuipatayo kupitia ibara za Wanazuoni na Wanazuoni wa usuli ni kuwa; maana ya kuchunga hitilafu au kujitoa kwenye hitilafu hukusudiwa; kufanya kinachohitajika kwa mujibu wa hitilafu au kwa mwenye kujitahidi kuifanyia kazi dalili ya mpinzani wake; ikimaanisha kupanga athari za kuifanyia kazi – nayo ni; kuweza kuifanyia kazi na kuitolea hukumu juu yake au kwa mwenye kuitakidi kufaa kwa jambo na akaacha kulitenda hata kama mwengine ataitakidi kuwa jambo lile ni haramu, hivyo hivyo kwa upande wa jambo la lazima itapendeza kwa aonae kuwa ni jambo linalofaa kulifanya, alifanye hata kama Maimamu wataliona kuwa ni la lazima kulifanya.
Na wanatoa ushahidi wa kufaa kwa sheria hii kwa hadithi ya Aisha (RA) amesema; Utba bin Abi Waqas alikuwa amemuahidi ndugu yake Saad in Abi Waqs kuwa Ibn Walidat Zamgha anatokana na mimi hivyo mkamateni. Akasema: “Ulipofika mwaka wa ukombozi (wa Maka) Saad bin Abi Waqas akamchukua. Akasema “mtoto wa kaka yangu amenikabidhi huyu, Abdallah bin Zamgha akasimama akasema; “ndugu yangu na mtoto wa Walidat mtoto wa baba yangu alizaliwa kitandani mwake. Wakaenda hadi kwa Mtume (S.A.W), Saad akasema; “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, mtoto wa ndugu yangu alikuwa amenikabidhi. Abdallah bin Zamghat akasema ndugu yangu na mtoto wa Walidat mtoto wa baba yangu alizaliwa kitandani mwake. Mtume (S.A.W) akasema “huyo ni wa kwako ewe Abdalla bin Zamghat” kisha Mtume (S.A.W.) akasema “Mtoto ni wa mwenye tandiko; ama mzinifu lake ni jiwe (adhabu ya kupigwa mawe). [24]”
Mtume (S.A.W.) alichukua hadhari na akazizingatia hukumu zote mbili, hukumu ya tandiko (kitanda) na hukumu ya kufanana, kumpa mtoto kwa muhusika wake – ambaye ni Zamghat – alizingatia hukumu ya tandiko. Na kwa kumuamrisha Sawda, Mungu amuwie radhi, azuiwe na kutopewa mtoto aliyeshikamana na baba yake, alizingatia kanuni ya kufanana. Imam Nawawy anasema kwa namna ya kuchukua tahadahari “alimuamrisha – kumzuia – kwa hali ya tahadhari, kwa kuwa, kwa kuzingatia mtazamo wa nje ndugu yake kwa kuwa ameambatana na baba yake, lakini alipoona mfanano ni mkubwa mno kwa Atabat bin Abiy Waqas akaogopea asije akawa ni katika damu yake akawa mtu mgeni kwake, akaamuru kumzuia ikiwa kama ni tahadhari[25]..
Na katika hadithi ya Aisha (R.A) hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.) amesema; “mwanamke yeyote anayeolewa bila ruhusa ya walii wake basi ndoa yake ni batili (haisihi), ndoa yake ni batili, ndoa yake ni batili, (Mume) akimuingilia mwanamke huyo ana haki ya kupata mahari kwa alichohalalishia tupu yake.[26]
Mtume (S.A.W.) amehukumu katika kubatilisha mapatano ya ndoa na kwa mujibu wake yale yote yanayoamabatana na ndoa hayatazingatiwa kwa kuwa yatatendeka baada ya kufungwa ndoa nayo ni kuwepo kwa mahari, na kwa maana nyengine Mtume (S.A.W.) kila mmoja amempa hoja katika dalili mbili kama inavyotakiwa.
Isipokuwa kuna hadithi ya Al-Nuuman bin Bashir (R.A.) amesema; nimemsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani zimshukie ) akisema: "Hakika halali iko wazi, na hakika haramu iko wazi na kati ya halali na haramu kuna mambo yenye kutatiza, hawayajui mambo hayo wengi miongoni mwa watu, atakaye yaepuka mambo yenye kutatiza, basi atakuwa kaihifadhi dini yake na heshima yake, na atakayeingia katika mambo yenye kutatiza atakuwa kaingia katika haramu, ni kama mfano wa mchunga mifugo mwenye kuchungia kando kando ya mipaka wanahofiwa (mifugo wake) kuingia humo, tambueni na hakika kila Mfalme ana mipaka yake, na tambueni kuwa mipaka ya Mwenyezi Mungu ni makatazo yake…[27]”
Kuna baadhi ya utata wanazuoni wametofautiana katika kuhalalisha na kuharamisha kwake
Lakini si kila hitilafu ni huwa ni dalili tosha ya kusema ichungwe kwni kufanya hivyo itapelekea kwa watu kufuata ruhusa ya yaliyoharamishwa. Na ilivyokuwa madhehebu yametoa kauli ya kifiqhi iliyowazi kwa kuwa hakuna suala katika masuala isipokuwa ndani yake kuna hitilafu, hata katika yale waliyokubaliana wanazuoni wapo ambao wameyakataa. Anasema Azzarkashy katika kitabu cha (Albahru Almuhit): “elewa kwamba chanzo cha kutoelewana hakitoi mashaka wala kuzingatiwa, isipokuwa huangaliwa chimbuko na nguvu zake[28].”
Na Alrubani akasema katika mlango wa ‘ushahidi’ “lau kama hitilafu yenyewe ingelikuwa ni ya utata basi masuala mawili yengelikuwa sawa, ikimaanisha suala la kuwepo kwa adhabu kwa upande wa Madhehebu ya Hanifa kwa kunywa ulevi (uliotengenezwa kwa zabibu) na ushuhuda wake, lakini utata upo katika dalili.” Na kwa ajili hiyo kauli za wasioona hoja huchukuliwa kuwa ni hitilafu na kwa hivyo wanazuoni wakaweka sharti ambalo ni lazima liwepo ili sheria hii iweze kufanya:
Ikiwemo: Chanzo cha kutokubaliana lazima kiwe na nguvu kikiwa ni dhaifu, haitozingatiwa, imam Asuyuty ameeleza ibara hii akasema “awe na uhakikaka wa ufahamu wake ili isije kuhesabika ni kosa.[29]” Kwa ajili hiyo mlevi (aliyekunywa kilevi cha zabibu) atapewa adhabu. Abu Hanifa hakuchunga hitilafu kwa kuwa dalili za kutoharamisha zabibu hazina nguvu[30]. Pia Ataa bin abiy Rayah hakuchunga hitilafu katika kuhalalisha kumuingilia mjakazi asiye na nguo kwa kukosa rai hii dalili iliyo sahihi yenye kuzingatiwa, hivyo aliyefanya hivyo atapewa adhabu.
Na ukweli ni kuwa udhaifu wa chanzo ni jambo gumu kutokea kwa ajili hiyo anasema Altaj Alsabaky” nguvu za chanzo na udhaifu wake watu binafsi ndio pekee wenye kuweza kufahamu.[31]” Katika masuala mengi ambayo ndani yake kuna ikhtilafu, mitazamo ya wanazuoni (mafaqihi) hubadilika-badilika katika kuzingatia kile kinachoonekana kuwa chenye nguvu au udhaifu, yaani ni mambo ya yanayojitokeza mara chache sana. Lakini kilichodhihiri udhaifu wake huwa hakizingatiwi hata kidogo. Na tutaeleza katika somo lijalo baadhi ya alama za mitazamo dhaifu.
Pia hakuna athari kwa mtu asemaye iwapo kauli yake inachukuliwa kuwa yenye nguvu au dhaifu, hakuna utakaso wa watu na hakuna kuzingatia sifa zao bali kauli na ushahidi wao, yeyote aliye na nguvu katika hoja yake itazingatiwa hitilafu yake hata kama cheo chake katika jitihadi kiko chini ya daraja ya mpinzani, na iwapo mwenye kutoa hoja dhaifu, kinyume chake haitazingatiwa hata kama daraja yake ni kubwa zaidi. Na pengine mmoja wao ana hoja ya nguvu na anajua maswala kadhaa lakini sio yote, lakini hali hii lazima awe nayo mwenye kujitahidi[32] kwani utakaso upo kwenye ukweli hata kwa mtu yeyote.
Ikiwemo: Hitilafu isipelekee kukiuka yale waliyokubaliwana wanazuoni wengi au au kuzusha jambo lililoharamishwa. Hivyo aliyeoa bila ya walii wala mashahid ndoa yake huwa ni batili, kwani ingawa Abu HAnifa amejuzisha ndoa bila ya walii, na Malik amejuzisha ndoa bila ya mashahidi, hivyo elewa mtazamo huu umewafikiwa hakuna yeyote kati ya madhehebu manne aliyesema.
Ikiwemo: isipelekee kuanzisha hitilafu nyengine, tukahitaji kujiondoa kwani kufanya hivyo kutakuwa na mzunguko. Mfano wake; kuunganisha sala za witri na kutenganisha hali ipi ni bora? Imam Abi Hanifa anasema kuunganisha ni bora zaidi, hapa yeye hakuchunga hitilafu kwa kuwa madhehebu ya Malik wao wanaona hiyo (kuunganisha) inachukiza (Makruhu).
Altaj Sabaky anasema kuhusu mfano huu: “kuitenganisha witri ni bora zaidi kuliko kuunganisha kutokana na hadithi (msiifananishe na sala ya Magharibi). Na imam Abu Hanifa akazuia kuunganisha ila katika mtazamo mwengine kuunganisha ni bora zaidi, hii ni kutoka katika hitilafu, ila ni mtazamo dhaifu kwa kuwa wanazuoni wengine waliobaki wanajuzisha kuunganisha, na kama si hivyo basi kutoka katika hitilafu hakutopatikana[33].
Na baadhi ya wanazuoni wa Usul wakazidisha sharti nalo ni: iwe kuna uwezekano wa kukusanya rai za madhehebu yote, vinginevyo, haitoachwa kile anachokiitadiki yeye kwa kuchunga kinachotiliwa nguvu, kwa sababu huku ni kuachana na yale ambayo alilazimika kufuata kile alichofikiria na hiyo haifai kabisa.
Sharti hili ameliezea pia Azzarkashy[34] katika kitabu (Almanthur) amepokea kutoka kwa Abi Is-haq Al isfirany na akataja mifano mitatu juu ya sharti hili na wenye nguvu ni ule wa kwanza kuwa “haijuzu hata kidogo” katika hili kuna mwonekano ndani yake. Kwani kuchunga hitilafu si zaidi ya kuacha kauli yenye nguvu na kuifuata yenye nguvu zaidi kwa muda uliopo au muda ujao hali ya kuchunga sharti lililotajwa hapo awali. Na hii haina maana kama kauli yenye nguvu ni dhaifu moja kwa moja, kwa kuwa kama ingelikuwa ni dhaifu isingezingatiwa kama ilivyosemwa lakini haiachi kuwa ipo kati ya kiwango cha dhana na dhana yenye nguvu, na dhana yenye nguvu haijumuishi upande mwingine ambao ni dhana (isiyo na nguvu.)
Imamu Alqabab Almaliky anasema: “Ushahidi wa kisheria upo ule ambao nguvu zake zimedhihirika wazi, ambapo kwa mwangalizi anapata uhakika wa kusihi kwa moja ya dalili mbili za ushahidi, na kuitendea kazi moja wapo katika hali hii hakuna haja ya kuchunga hitilafu.
Na kuna miongoni mwa dalili ambazo moja kati ya dalili mbili ina nguvu na ambapo dalili moja kati ya hizo mbili inashinda kwa nguvu na uthabiti fulani, kiasi ambacho nafsi haisiti kuikubali navimeibuka. kmashaka kuhusiana na dalili nyingine katika hali hii ni bora kuzingatia hitilafu hiyo, kwa hivyo Imam anasema itaanza kufanyiwa kazi ile yenye ushahidi ulio na nguvu zaidi kwa kuwa dhana yake imemtangulia[35].
Na iwapo kuna makubaliano au ibada kwa mujibu wa ushahidi mwingine, makubaliano hayo hayatabatilika na wala ibada hiyo haitabatilika kwa sababu hayo yametokea hali ya kuafikiana na ushahidi ulio na mazingatio, na sio kutokukubalika ni kwa ajili ya utashi wa nafsi yake.” Mbali na hayo, kauli iliyo na nguvu inaweza kufanya kuwa na nguvu zaidi, namna hii kudhibiti hitilafu inajumuisha nafasi ya mtu na fatwa.
Mbinu hii katika kukabiliana na kutokukubaliana ni pamoja na kazi binafsi na fatwa. Ama upande wa fatwa matokeo yanaweza kuamuliwa kwa kauli yenye nguvu. Na Izzu bin Abdulsalaam ameweka wazi mahusiano haya yenye utata katika kitabu (Qawaid Kubra[36]) aliposema: “Hitilafu zina vigawanyo; kigawanyo cha kwanza: hitilafu inayohusu kuharamisha au kujuzisha, kujitoa katika hitilafu kwa kujiepusha huwa ni bora. Kigawanyo cha pili: Hitilafu iwe inahusu kupendezesha (istihbab) au uthibitisho, kuendelea nayo ni bora zaidi. Kigawanyo cha tatu: Hitilafu iwe inahusu uhalali, kuendelea nayo ni bora zaidi.
Mifano iliyotajwa na Al-Zarkashi inatokana na kigezo hiki,
Hilitafu katika kushartisha sala ya Ijumaa katika miji mikubwa inawezekana kuchungwa hitilafu kwa kusema kwamba Swala ya Ijumaa ni wajibu. Na huu ndio mfano wa kwanza ambao tumesema kuwa ndio wenye nguvu. Pia ametaja mifano mengine miwili nayo; imamu ametangulia kwa kusoma Alfatiha na mwanzo wa kuingia wakati wa sala ya Alasiri. Hoja hizi zikajibiwa; ya kwanza, pengine huzingatiwa kauli ya aliyesema sala hubatilika kwa mwenye kusoma alfatiha kwa kuwa kwake hana udhuru na kauli ya pili kama ilivyo kauli ya Al istikhry kuwa wakati wa mwisho wa sala ya Alasiri ni kufanana kivuli cha kila kitu kuwa mfano wake na atakaesali baada ya muda huo huwa anasali sala ya kulipa na hii kauli ni dhaifu haizingatiwi.
Tatu: kutomkana mpingaji
Ikimaanisha kuwa haipasi kwa mtu mzima (aloyekalifishwa na sheria) kumpinga mwengine au kumkataza kutoendelea na rai (mawazo) yake kwa sababu hayalingani na mtazamo wake au kuinasibisha kauli ya mpingaji kuwa ni kauli zenye upotovu kwa kutumia njia tatu za makatazo zilizotajwa katika hadithi – mkono, ulimi na moyo – kama njia ya kubadilisha upotovu au kupinga kazi inayokubaliana na rai/mawazo ni ya mwenye kujitahidi (mwanachuoni) anayekubalika kuhusu masuala hayo yenye utata
Na maana ya “Kupinga” amesema Ibn Faris: “ina maana ya kinyume cha ujuzi ambao hukaa moyoni, na kupinga kitu ina maana ya moyo wake haujakubali jambo hilo na wala ulimi wake haulikiri.[37]”
na jambo baya (ovu) ni lile lisilokuwa jema, na kila ambalo sheria imeliharamisha na kuliichukia hilo ni jambo baya[38].
Kujificha: mabadiliko. Al-Nakir ni jina la kukana, ambalo linamaanisha mabadiliko
Na kukana (kanusho) ni kinyume cha kukubali (kukiri) ambalo linatumika kwa kukubali kitu na kukitthibitisha, aidha katika maana za kupinga ni pamoja na kutokushukuru, kutojua kitu, na kukataza[39].
Na mfuatiliaji wa maana za matumizi ya neno kukana (kanusho) kwa mujibu wa wanazuoni wa kifiqhi atagundua kuwa halitoki kati ya moja ya maana mbili za kiisimu, nazo; mabadiliko na kukataza. Imepokewa kwa mtumizi ya kukana katika maelezo ya wanazuoni katika maana nyingi na zote hurelea katika maana hizo mbili, na katika maana zake pia ni kupinga, kuzuia, kueleza udhaifu wa hoja, kutokukiri neno au kitendo, dosari kwa apingaye na kumpinga, kulaumu na kutumia nguvu, mawaidha, amri na makatazo na adhabu, na pia kupita maana nyengine kunajitokeza sura tofauti ambazo zinaleta maana ya mabadiliko na makatazo.
Na ni wazi kwa kupitia maana tulizozitaja kwamba sisi tunakusudia kutokemea kitu chochote kimatendo, si kwa kauli ya hukumu, kwani majadiliano huwa katika matendo maalumu, kwa maana hiyo, majadiliano ya kisayansi hayatoingia katika masuala ambayo tupo nayo, kwani mijadala ya kisayansi haikanushi kauli ya hukumu pamoja na kuwa pande zote mbili hazipasi kukana matendo yanayosemwa na upande mwingine.
Neno Khilaaf (utofauti) limechukuliwa kutokana na kitenzi khaalafa Husemwa amepinga kitu ikimaanisha amekiasi au kukitenda baada ya kuwa kimekatazwa. Na neno khilaaf (utofauti) na Al ikhtilaaf (kutokubaliana) yana maana moja kilugha na kiistilahi. Kwani maana hiyo huonekana kupitia matumizi ya baadhi ya wanazuoni wa lugha, wa usul na wanazuoni wa sheria, kwani baadhi ya wakati hutumia maneno hayo mawili kwa maana moja, mfano wanazuoni wa madhehebu ya Abu Hanifa; “wakitafautina waliotangulia kwa kauli / rai mbili, kisha waliofuata wakaipa nguvu moja wapo, basi makubaliano hayo huondosha tofauti ya waliotangulia.[40]” Hapa tunaona taabira ya mwanzo imetumika neno ihktilaaf na ya pili imetumika khilaaf zote zikiwa na maana moja.
Na wapo wanazuoni waliotafautisha kati ya maneno hayo kwa kuzigatia kuwa neno Al ikhtilaaf linategemea dalili ama khilaaf hailitegemei dalili, na kwa maana hiyo ikawa wanatumia neno Al ikhtilaaf katika masuala yenye kuhitaji jitihada na sio neno khilaf. Na kama ilivyo kuwa al ikhtilaaf ni ile hali ya kuwa na kusudio moja ila njia zake ni tofauti, lakini khilaaf makusudio ni tafauti na njia pia. Mara nyingi al ikhtilaaf hutokana na kutofautina kwa mitazamo katika suala moja, na khilaaf ni kule kuweka wazi rai pasi na dalili[41].
Amesema katika al dar mukhtaar {asili ni kuwa kuhukumu inafaa katika maeneo yenye utofauti na si maeneo wasiyokubaliana, na tafauti yake ni kuwa katika Al Ikhtilaaf kuna dalili na sio katika Al khilaaf. Na hii tofauti ni ya kimazoea ukiacha hivyo Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema {na hawakuhilitafiana kwacho ila wale waliokipewa..} Albaqarah 213. {na hawakufarikiana wale waliopewa kitabu ila baada ya kuwafikia (dalili) bayana} [Al bayyina 4]. Hawana dalili kwao, ikimaanisha kuwa khilaaf isiyo na dalili kwa mujibu wa anayepinga kinyume cha hivyo msemaji atakuwa ametegemea dalili[42].
Al tahanawy anasema: “kauli iliyopewa nguvu ikikutana na yenye nguvu husemwa kuwa ni khilaaf na sio Ikhtilaaf na kinachofahamika ni kwamba kuthibitika kwa udhaifu kwa upande wa anayepinga, kwa kule kupinga kwake rai za wanazuoni wengi (Ijmaa) na kutokuwa dhaifu kwa upande wake kwa upande wa Ikhtilaaf [43].
Katika kitabu cha {Alkulliyaat} cha Abi Albaqaa Al kafawy: “Al ikhtilaaf iwe njia yake imetafautina ama malengo yawe mamoja. Na Al Khilaaf ni ile ambayo njia yake na malengo yake ni tofauti. Al ikhtilaaf ni katika athari rehema ama Al khilaaf ni katika athari za uzushi. Na iwapo hakimu akitoa hukumu kwa njia ya Al khilaf I nafaa kukata rufaa, tafauti na kutumia njia ya Al ikhtilaaf kwa kuwa Al khilaaf ni ile iliyotokea katika hali ambayo haifanyi ndani yake kufanya jitihada jambo ambalo ni kinyume na kitabu (Quran) na sunna na rai za wanazuoni (Ijmaa)[44].
Alraaghib Al asfahaniy anasema: “Al ikhtilaaf na Al mukhaalafa kila moja kati ya haya iwe ina njia zake tafauti na ya mwenziwe katika hali yake na matamshi yake. Na Alkhilaaf ina maana kwa ujumla (inakusanya) kuliko kinyume, kwa kuwa kila kilicho kinyume basi kimetafautina, na sio kila kilichofatautiana huwa ni kinyume na mwenziwe[45].
Matokeo yake ni kuwa utofauti wa maneno hauhesabiki kuwa ni jambo tu la kiistilahi ambalo halina kupingika.
Na tuliyoyataja ya kuwa haipasi kupinga katika masuala yenye hitilafu ni madhehebbu ya wanazuoni (Al fuqahaa)[46].
Na imepokewa kutoka kwa imamu Ahmad kwamba yeye anapinga kilichotafautiana[47]. Na imamu Ibn Taimiyya na Ibn Alqayyim wametafautisha kati ya masuala yenye hitilafu na masuala yenye kuhitaji jitihada[48].
Na tukiangalia na kufanya uhakiki juu ya masuala haya, tutagundua kuwa ni kuna tafauti ya kimatamshi, na maelezo yake ni kuwa katika masuala ya Al khilaaf kwa upande wa wanazuoni ni yale masuala ambayo dalili zake haziko wazi, ima kwa sababu hakukuwa na rai za wanazuoni au kwa kukosekana kwa dalili kabisa. Suala lolote ambalo halikupokewa dalili au imepokewa dalili yenye kukata maamuzi katika kuthibiti kwake hii itahesabika ni sehemu ya hitilafu, nayo ni kwa kuwa dalili yoyote yenye kukata maamuzi haimaanishi kuwa inaondoa hukumu kwa upande wa kutoa dalili isipokuwa pindi wanazuoni wakichagua moja ya maana zinazokusudiwa juu ya jambo husika, kama umuhimu wa kauli ya Hakimu katika kutatua mzozo.
Na udhibiti huu unafanya kazi katika masuala mengi ya elimu ya mantiki na masuala mengi katika elimu ya kifiqhi. Kwa kuwa jambo lenye kueleweka ni kuwa, wenye kujitahidi huwa hawaathiriki na hitilafu iliyo na dalili yenye kukata maamuzi lakini hitilafu yao ni katika masuala ambayo hayana dalili yenye kukata maamuzi, na katika masuala ambayo dalili yake ni ya kudhania kwa dalili na kuthibiti au masuala ambayo masuala yake ni kwa dalili ya kudhania au kwa kuthibiti pasi na dalili au kinyume chake. Na wanazuoni wakaelezea kuwa hii huwa ni hitilafu yenye kuzingatiwa, na tumeelezea hapo kabla masharti ya hitilafu yenye kuzingatiwa.
Na wanazuoni wamevua kwa kutokataa masuala yenye utata, ikiwa ni pamoja na: udhaifu wa mtambuzi, ambao tumeelezea hapo kabla.
Ikiwa pamoja na: hukumu ya hakimu, iwapo wamehitilafiana kwa jambo kati ya uhalali wake na uharamu wake na akapelekewa hakimu, ni juu yake kuhuhumu kwa kile anachoitakidi, na hukumu yake itaondosha hitilafu katika masuala yenye kuhusu tukio hilo kwa kuondosha mzozo ndani ya mipaka yake[49].
Ikiwa pamoja na: iwe kwa mwenye kukana ana haki katika jambo lenye hitilafu. Mume amzuie mkewe kunywa mvinyo japo kidogo, iwapo (mke) anaitakidi kuwa mvinyo ni halali, pamoja na kuwa utambuzi ni dhaifu, kama ilivyoelezewa.
Ikiwa ni pamoja na: kuitakidi mtu kuwa tendo la haramu na akalifanya nayo ni kwa kuvunja miko ya uharamu kwa upande wa itikadi yake na si kama anaitakidi kuwa tendo hilo ni halali (limehalalishwa).
Na wanazuoni wanatoka hoja kuwa haifai kukana katika masuala ya hitilafu kwa kuwa hakuna kati ya dalili mbili iliyo bora kushinda nyengine, kwani masuala ya kifiqhi hayakosekani kuwa ni masuala ya kudhania, na dhana inakubali kupingika, na hakuna kuipa mkazo dhana moja na kuiacha nyengine, na kwa kuwa kila mwenye kujitahidi anaweza akawa sahihi, au akawa sahihi katika hoja mojawapo na mkosaji (katika wenye kujitahidi) hana madhambi, lakini kama atajiepusha na hitilafu itakuwa ni vizuri sana.
Al jarhaziy anasema: “wanasema kinachohitilafiana hakipingwi” hii ni sheria muhimu yenye vigawanyo vizuri sana, kwani kunasibisha kwa mwenye kuharamisha si bora kuliko kunasibisha kwa mwenye kuhalalisha.
Alfadaniy anasema katika kuelezea: “ (kwa kuwa kukinasibisha) ikikusudiwa jambo lenye hitilafu (kwa aliyeharamisha) ikimaanisha; kwa aliyejitahidi ambae amesema uharamu ya jambo hilo, mfano imam Shafii, ambae amesema uharamu wa mvinyo (kwa kukinasibisha kwake) kwa maana; jambo lililohitilafiana (kwa mwenye kuhalalisha) ikimaanisha; mwenye kujitahidi ambae amesema uhaliali wake mfano imam Abi Hanifa ambae amesema uhalali wa mvinyo[50].
Sheikh Zakaria Answari anasema: “(wala hapingwi) msomi (isipokuwa kwa jambo lililokubaliwa na wote) ikimaanisha, kulipinga kwake jambo hilo, na silo lile walilohitilafiana ndani yake isipokuwa kwa mtendaji aone kuna uharamu ndani yake, na kwa kuwa kila mwenye kujitahidi anaweza akawa sahihi, au akawa sahihi katika hoja mojawapo tusilolijua na mkosaji (katika wenye kujitahidi) hana madhambi[51],
Na imepokewa kutoka kwa imam Ahmad kuwa anachukia jambo lenye hitilafu linalofuatwa kutoka kwa mwenye kufuata (maimamu) na wala hachukizwi hilitafu inayotokana na mwenye kujitahidi[52]. Na mapokezi haya yamefungamanishwa na yaliyotangulia, kuwa mapokezi yaliyotangulia ambayo yanajuzisha kukana jambo lenye hitilafu ndani yake – na Ibn Muflih anapinga kauli yenye hitilafu yenye dalili nzito au kauli moja na Ibn Rajab anasema kinyume na hivyo akasema: “na imeelezwa kutoka kwa Imam Ahmad kuchukizwa kucheza chesi (mchezo wa ubao) na Kadhi akaifasiri kauli hii “kwa achaye bila ya kufanya juhudi au kwa wigo mzuri. Kwani kilichoelezwa kutoka kwake ni mnywaji wa mvinyo hupewa adhabu ambayo kauli yake kuna hitilafu na kupewa adhabu ni jambo kubwa katika kukataza, pamoja nakuwa hatokuwa katika watu waovu, hiyo ikajuulisha kwamba anachukizwa na jambo lenye hitilafu ndani yake, kwa hoja iliyo ya sunna iliyo dhaifu katika kuharamisha kwake na mtendaji wa kosa hilo hawezi kuepukana na adhabu[53].
Ama kutafautisha Ibn Taymiya na Ibn Qayim na Al shaukany na waliowafikiana nao katika masuala ya hitilafu na masuala ya kujitahidi. Ibn Taymiya anasema: “wanaposema masuala ya hitilafu kuwa hakuna kukana hiyo siyo sawa, kwani kukana itapelekea kusema juu ya hukumu au matendo, ama ikipelekea kusemwa juu ya hukumu yenye kupingana na sunna au makubaliano ya wanazuoni walotangulia hii italazimika kuikana bila shaka. Na kama haipo hivyo basi hukanushwa kwa maana ya kuonyesha udhaifu wake kwa mujibu wa wale wanaosema kuwa mtu aliye sahihi ni mmoja, na wao ni katika kundi la waliotangulia (Salaf) na mafaqihi. Ama ikisemwa kuhusu matendo, ikawa yanahitilafiana na sunna au makubaliano ya wanazuoni italazimika kuyakana vile vile kwa mujibu wa kiwango cha kukana, na vile vile hukumu itatenguka ikienda kinyume na sunna na hata kama kuna baadhi wa wanazuoni watakuwa wameifuata.
Na iwapo hakuna sunna au makubaliano ya wanazuoni katika masuala juu ya suala hilo, kuna uhalali wa ijtihadi ndani yake, basi haikatazwi kwa yeyote anayeifanyia kazi, awe mwenye kujitahidi au muigaji (mfuataji wa madhehebu). Kwani mkanganyiko huu umekuja kwa sababu msemaji anaamini kwamba masuala ya kutokubaliana ni masuala ya kujitahidi, kama makundi ya watu wengine yanavyoamini.
Na usahihi ni kuwa ile rai waliyonayo viongozi (maimamu) kwamba katika mambo ya ijtihadi yasiyokuwa na dalili za wazi yanapaswa kufanyiwa kazi mfano Hadithi sahihi isiyo na ukinzani wa aina yake, linapokosekana hilo, basi inajuzu kwake kuitumia ijtihadi kwa kupingana ushahidi kama huo au kwa kufichikana kwa dalili.
Na si kwa kutaja kuwa suala hilo ni la uhakika hii haimaanishi pingamizi kwa wanazuoni (mafakihi) wanaohitilafiana nalo, kama ilivyo katika masuala mengine yote ambayo waliotangulia (salaf) walikhitalifiana, na tukawa na uhakika juu ya uhalali wa moja kati ya rai mbili zinazohusu suala hilo[54].
Na mfano kama huo Ibn Qayim anasema: “na vile vile amesema katika kuelezea kutolea ushahidi wa rai yake: “iweje Faqihi aaseme, "Hakuna kukanusha" katika masuala yenye hitilafu, wakati mafaqihi wa madhehebu yote wameweka wazi kuwa hukumu ya Hakimu ikipingana na kitabu au Sunnah hubatilishwa[55]?
Na shaukany anasema kuhusu maudhui hii – akikusudia kauli ya mtunzi: (Ni wajibujuu ya kila muislamu aliyebaleghe kuamrisha mema ajuayo na kukataza maovu ayajuayo… na sio katika yaliyohotilafiana ndani yake katika Madhehebbu yake.)- na imekuwa ni kisingizio kikubwa zaidi cha kufunga mlango wa kuamrisha mema na kukataza maovu. Na hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amewajibisha kwa umma huu kuamrisha mema katika yanayojulikana kuwa ni mema katika sheria na kukataza yaliyo maovu na kigezo cha yote ni kitabu na sunna. Ni juu ya muisilamu aamrishe alichokiona humo (ndani ya kitabu na sunna) au kimoja wapo, na akataze maovu alichokiona humo kuwa ni katika maovu au kimoja wapo. Na hata kama akisema msemaji katika walio na elimu kipingacho hayo, basi maneno yake yatakataliwa inapaswa kuyakana kwanza, pili kwa ayatendeaye. Hii ni sheria iliyotukuka ambayo tumeamriwa kuamrishana mema yake na kukatazana mabaya yake, na haya yote yamo kwenye kitabu na sunna[56].
Na akasema: “…na pengine mtu anataka kusahihisha uwongo akawa anamwambia kuwa hakuna ukanushaji katika mambo ya ijtihadi, basi atajibiwa kwa kuambiwa, na ni lini Mungu alimuidhinisha mtu anayedai kuwa ni mwenye jitihada juu ya Sharia aliyomteremshia Mtume wake na kumfanya kuwa ni hakimu ndani yake kwa akitakacho na juu ya amtakae. kwani kwa hakiki huu ni utume hakuna kujitahidi na sharia ni ya sasa (mpya) sio sharia ya mwanzoni, Mwenyezi Mungu hakumtuma katika umma huu Mtume isipokuwa Mtume mmoja tu[57].
Akasema: "hakika kukana maovu hata kama yalizuiliwa na kizuizi hiki - ikimaanisha: kwa dalili iliyothibiti maamuzi kwa namna ambayo hakuna hitilafu ndani yake" - basi mlango huu ungebatilika na kufungika mara moja na yeyote yule angefanya akitakacho, kwa kuwa hakuna kauli ya kitu kilichoharmisha na sheria - mara nyingi - kuna kauli ya msemaji au mfano mfanano wa mifanano[58].
Na upambanuzi wa msingi kati ya Ibn Taymiya na Ibn Alqayim unakuja katika masuala ya kutofautiana na mambo ya ijtihadi ni kwamba mambo ya ijtihadi ni yale ambayo hayana ushahidi (dalili) katika Qur-aan au, Sunnah, au makubaliano ya wanazuoni. na masuala ya Khilaaf ni kinyume chake. na inakatazwa kwa hali ya pili na siyo hali ya kwanza, kwa maana nyengine: masuala ya jitihadi ni yale ambayo huwa hitilafu ndani yake ina nguvu na inachukuliwa kuwa inastahiki kuzingatiwa.
Makundi mawili yamekubaliana kuwa masuala ambayo ndani yake yana dalili au makubaliano - ikikusudiwa dalili yenye kukata maamuzi - inakatazwa kupinga, na wote wanaita masuala yenye hitilafu. lakini iwapo masuala ambayo wanahitilafiana hayana dalili yenye kukata maamuzi yamewafikiana vilevile kutompinga anayekwena nayo kinyume hata kama wanazuoni wanayaita masuala yenye hitilafu - kama ya mwanzo- naye Ibn Taymiya na Ibn Alqayyim wanayaita masuala yenye kukubali jitihada. na istilahi zote ni sawa, kwa kuwa ni masuala ya hitilafu, na kwa kuwa kwake si makubaliano ya pamoja. na masuala ya jitihadi inafaa - inajuzu- kujitahidi ndani yake kwa kuwa ni eneo la kujitahidi.
Kisha masuala yote katika masuala ya hitilafu huzingatiwa kuwa ni miongoni mwa masuala ya jitihadi kwa sharti iwe hitilafu inazingatiwa - kama ilivyotangulia - ama itakapokuwa hitilafu haizingatiwi basi haitohesabika kuwa ni katika masuala ya jitihadi. mazingatio ni kuwa suala la hitilafu iwe hitilafu inazingatiwa na iwapo kuna tofauti, basi iwe ni baina ya masuala ya ijtihadi na masuala ya kutofautiana yasiyozingatiwa…
Kupitia kauli ya Ibn Taymiyya iliyotangulia: Na kama haipo hivyo basi hukanushwa kwa maana ya kuonyesha udhaifu wake kwa mujibu wa wale wanaosema kuwa mtu aliye sahihi ni mmoja, nao ni wengi katika madhehebu ya Salaf na wanazuoni. <Nje yamipaka ya mzozo, kwani mzozo upo katika matendo maalumu kama ilivyotajwa hapo awali.>
Matokeo ni: kauli ya msemaji kuwa masuala ya hitilafu yanakusanya kila kilichotafauti hata kama ni kwa dalili dhaifu au ngeni au yale yenye kuzingatiwa kama ni makosa (kukosea ulimi) kutoka kwa wanazuoni, kauli hii inakataliwa. Kwani kusudio la masuala ya hitilafu ni ile ambayo inazingatia masharit yaliyotajwa hapa juu.
**
Suala la Pili:
Madhehebu ya Kifiqhi na hukumu ya kuyafuata na kutoyafuata
Utangulizi katika kukua kwa madhehebbu ya kifiqhi
Kurani Tukufu imeteremshwa kwa Mtume Muhammad (S.W.A.), akawafikishia masahaba zake, akawafasiria yaliyofichikana, akawabainishia aya za ujumla, akaweka vizuizi kwa aya zilizowazi, akafikisha amana ya ujumbe kama itakiwavyo, akawaacha masahaba katika hoja zilizo wazi, na akawa anaeneza kwa masahaba zake roho ya kufanya jitihada, na hadithi ya Muadh alipomtuma kwenda Yemen ni hoja iliyo nzuri juu ya hili[59], na kama alivyotoa bishara njema kwa atakaepatia katika jitihada zake ana malipo mara mbili na wakati huo huo hakumnyima malipo kwa atakaekosea.
Na baada ya kuondoka kwake masahaba wake walibeba amana ya kufikisha ujumbe wake na kuitikia kauli yake: <Mwenyezi Mungu humuangalia mja kasikia maneno yangu akayahifadhi kama alivyosikia, huenda mweye ujuzi akawa hana ujuzi na huenda mwenye ujuzi akawepo mwenye ujuzi zaid yake.[60]> wakasimama kuitumikia Kuran na Sunna huduma kubwa. Wakaikusanya Kuran katika zama zao, wakayafikisha maneno ya Mtume kama yalivyo bila ya kuvuruga au mabadiliko yoyote, na wakatao fatwa kwa watu – kwa Kurani na Sunna- au wakatoa kutokana na hivyo yale ambayo hayana dalili.
Na Matabiina baada yao wakafuata nyayo zao, na kila sahaba akawa na baaadhi ya kuwafunza, na wakachukua (elimu) kutoka kwao. Imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas amechukua kutoka wote wawili kutoka kwa bwana wake Ikrimah, na kutoka kwa Omar amechukua Sa`ed Bin Musayyab pamoja na wengine walioshi zama hizo. Na mtoto wa Omar amepokea elimu kutoka kwa bwana wake Nafi`i. na kwa upande wa Iraq amepokea elimu Abdallah in Mas-ud Alqamah na Ibrahim Nakh`i. na jamaa wa Mtume (S.W.A.) na wengineo walipokea elimu na zaidi ya waliyokuwa wakiyajua baina ya masahaba katika fatwa zinazotolewa kwa kufuata kina cha ukweli, na kama kuna jambo lina rai basi huchomoza na kuwa wazi, mpaka Omar alikuwa akisema: kila jambo linapokuwa gumu“ Haya ni masuala ya ikhtifa au Mtume ameshayazungumzia"[61]
Na kwa kumalizika zama za masahaba na kuja waliobeba elimu yao katika tabiina, mitazamo ya kifiqhi ikaanza kupambanuka kwa sura iliyo wazi. Kila mmoja katika Tabiina akaanza kudhihirisha elimu yake aliyochukua kutoka kwa sahaba wake, wakapita katika njia zake pamoja na jitihada zao kutokana na yale ambayo hawajayachukua kutoka kwa Masahaba, na kutafautiana kwao katika njia ya kutoa fatwa kwa yale yasiyo na dalili – ikimaanisha: kutoka kwenye Kuran au Sunna au kauli ya Sahaba -. Kisha pamoja na kutafautiana miji ilikuwa ni mwanzo ulio wazi wa kuanza kwa madhehebu ya kifiqhi. Kikawepo chuo (madrasa) cha Hadithi katika mji wa Hijaz, na chuo cha rai Iraq.” Na sharia zao zilichangiwa kutokana na mazingira ambayo vyuo viwili hivyo vimeibuka.
Mji wa Madina ulihifadhi tamaduni (mila) nyingi za Kiislamu ambazo zilikuwa za kawaida wakati wa zama za Mtume, hivyo kulikuwa na matukio machache mapya na mabadiliko ya dharura ambayo yanahitaji hukumu. Ama Iraq, pamoja na wingi wa uwepo wa wasomi (mafaqihi) wa hadithi miongoni mwao, ila mazingira yake yalikuwa na desturi nasura ambazo zinazohitaji hukumu za Kiislamu ndani yake.
Na katika sura hii mpya, kuna utulivu kwa akili katika kutoa hukumu na uhuru wa mawazo[62]. “Haya ni pamoja na kile ambacho Ahlul-Bayt walikuwa wakiandika Hadith za Ali na wanawe naFiqhi zao..
Na walikuwa miongoni mwao maimamu mashuhuri waliochangia pakubwa katika uanzishwaji wa fiqhi wakiongozwa na Zaid bin Ali Zain al-Abidin na ndugu yake Mohammah Albaqir na Ibn Ja`afar Assadiq.
Na kutoka kwa Ubadah vyuo viwili vya hadithi na rai, pamoja na muda kusonga vikaanza kujidhihirisha katika upande wa fiqhi zaidi kuliko ilivyokuwa zama za Tabiina. Kwa upande wa Madina akaonekana Imam Malik, Iraq maimamu wawili Abu Hanifa na Ahmad na upande wa Misri Imam Shafii. Na ikawa ndani ya kila dhehebu katika madhehebu hayo kuna maimamu wenye kujitahidi walioweka misingi na matawi yake hata ikawa vitabu vyao tulivyonavyo ni ushahidi mzuri zaidi kwa juhudi walizozitoa katika kuutumikia uisilamu na mpaka vikatufikia sisi vikiwa safi kama ilivyoteremshwa kwa Mtume wetu Muhammad (S.A.W.)
Inafaa kusema: Madhehebu ya kifiqhi ambayo yamejitokeza - iwe kutoka kwa Sunni au kwa wengine – mengi yao ni kutokana na jitihada ambayo inatofautiana katika nguvu na udhaifu kulingana na nguvu na udhaifu wa mtambuaji.
Na madhehebu manne ya kifiqhi yalijaliwa kwa namna ya kipekee kupata bahati kutokana na sifa kadhaa - pamoja na kutofautiana miongoni mwao – yalipata kuongoza miongoni mwa madhehebu mengine ya kifiqhi. Kwa kuwa na wafuasi, utunzi wa vitabu, uhakiki, Kwa upande wa ufuatiliaji, utungaji, marekebisho, uhakiki, kutoa hadithi, uwekaji matawi na mambo mengine ambayo hayapatikani kwa maimamu wengine wenye kujijtihad, hata baadhi ya wanazuoni waliotangulia walichukulia kuwa, hukumu hurudishwa iwapo imekwenda kinyume na kile walichokubaliana juu yake madhehebu manne.[63]
Lakini madheheu manne kuwa ndio yenye nafasi kumezusha masuali mawili:
Kwanza: je hii ina maana kwamba rai za manazuoni wa madhehebu mengine yasiyokuwa haya manne huwa hazifai, hurudishwa?
Pili: na je kwa maana hiyo haifai kutoka (kuacha kufuata) madhehebu ya kifiqhi manne na kufuata madhehebu mengine na rai nyengine?
Kila suali katika hayo tumeweka nafasi ya majibu yake kama ifuatavyo:
Kwanza: Je rai za wanazuoni wa madhehemu mengine yasiyokuwa madheheu manne inarudishwa na wala haifai kuitumia?
Imam al-Hafiz Zain al-Din Abd al-Rahman bin Rajab al-Hanbali alilittenga kipekee suala hili katika tafiti yake aliyoiita: “Jibu kwa ambaye anafuata madhehebu mengine yasiyokua madhehebu manne ” anasema sababu ya kuandika tafiti hii: Nimesikia kwamba baadhi ya watu wamelaani kukanusha kwangu baadhi ya wale wanaojinasibisha na madhehebu ya Imam Ahmad na madhehebu mengine ya maimamu mashuhuri katika wakati huu wanaokengeuka kutoka katika mafundisho yao juu ya masuala, na wakati kwamba jambo hilo halipaswi kukanushwa kwa aliyefanya hivyo., na aliefanyalo jambo hilo” Na anayefanya hivyo anaweza kuwa ni mtu mwenye kufanya jitihada ya kufuata haki iliyomdhihirikia, au muigaji (mfuataji) mtu mwingine mwenye kuitahidi, jamboo hilo huwa halikatazwi.[64] .”
Na katika ujumbe huu mzuri alitaja yale ambayo yanaunga mkono aliyoyajadili, na tunaweza kuyafupisha aliyoyasema kuhusiana na sababu ya kukatazwa kufuata madhehebu mengine manne kuwa madhehebu yasiyokuwa ya maimamu wane mbali na maimamu wanne hayakuwa mashuhuri na hayakudhibitiwa.na pengine yamenasibishwa kitu ambacho hawajakisema au au wamefahamika kwa kitu ambacho hawajamaanisha, na madhehebu yao hayana mtu wa kuwatetea na kuonyesha kasoro zozote zinazojitokeza ndani yake tofauti na madhehebu haya manne yaliyo mashuhuri...
Imam Ibn al-Salah alizungumzia sababu kama hiyo katika kitabu chake: “Adabul Mufti” akasema kuhusu wale ambao hawajafikia kiwango cha ijtihadi:
“Hana haki ya kushikamana na madhehebu ya yeyote katika maimamu wa Maswahabah na wengineo waliotangulia, hata kama walikuwa wajuzi zaidi na wana daraja la juu kuliko wale walio baada yao, kwa sababu hawakujishughulisha na kuratibu elimu na kudhibiti chimbuko lake na matawi yake, na hakuna hata mmoja kati yao aliye na madhehebu yaliopangwa, yaliyo haririwa na yaliyo imara. Lakini hilo lilifanyika kwa waliokuja baada yao katika maimamu waliochimbua madhehebu kutoka kwa masahaba na tabiina, walisimamia kutanguliza hukumu juu ya matukio kabla ya kutokea, walio na mwamko wa kufafanua asili yake na matawi yake, mfano Imam Malik na Abi Hanifa na wengineo[65].
Na maneno ya Ibn Rajab yaliyotangulia, bali inafaa kutumika kwa maneno ya Mujtahid wa Tabiina ambao mafundisho ya madhehebu yao hayakupata umaarufu na wanafunzi wao hawakuyajali, mfano Al Awza`I, na Allayth, hayo ni katika aliyoyasema Ibn Salah.
Ama wale ambao mafundisho yao yameandikwa na matawi yake yakaelezwa, Ibn al-Salah hakujibu hilo. Wakati Ibn Rajab ameeleza kuwa yeyote ambaye ana sifa hii, maoni yake hayakatazwi, anasema: (na ikisemwa: Mnasemaje juu yamadhehebu ya imamu asiyekuwa wao, ikawa mafundisho yake yameandikwa, yamedhibitiwa na kuhifadhiwa kama vile mafundisho ya madhehebu mengine yalivyohifadhiwa?
Ikajibiwa: kwanza: Jambo hili halijulikani kama lipo hivi sasa, hata ikidhaniwa kuwa limetokea kwa sasa na ikakubaliwa kuwa inajuzu kulifuata na kushirikiana nalo, hilo halitajuzu isipokuwa kwa yule ambaye amedhihirisha kushikamana nalo, akatoa fatwa kutokana na maneno yake, na akatetea madhehebu yake.
Ama Yule anayedhihirisha kujinasibisha kwake kwa baadhi ya maimamu mashuhuri, lakini ndani yake anakuwa na uhusiano na wengine na anaamini madhehebu mengine yasiyo kuwa hayo jambo hilo halimpi haki hata kidogo na hii ni aina ya unafiki na kujifanya mchamungu na hasa wale waliochukua mali zilizowekwa maalumu kwa watu wa imamu huyo maarufu kutoka wakfu au kwingineko, au aliwapotosha watu na kuwafanya wafikirie kuwa aliyoyatolea fatwa ni kutoka kwenye madhehebu ya anayejinasibishia naye kwa siri ni dhehebu la imamu huyo mashuhuri, jambo hili kwa hakika halikubaliki. Hii ni itakuwa ni kuudanganya umma na kuwaongopea wanachuoni wa umma, na yeyote anayewahusisha maimamu wa Uislamu yale wasiyoyasema au anayoyajua kwamba wanasema kinyume chake huyo atakuwa ni muongo na anastahiki kuadhibiwa kwa hilo[66].”
Imebainika kutokana na maneno ya Ibn Rajab kwamba tukilazimisha kauli kwa mtu aliye na nafasi ya chini ya mwenye kujitahidi, kama vile mtu wa kawaida na mfwataji, lakini yeye hatokuwa hivyo. Kwani ni juu ya mwenye kujitahidi kuchagua kile ambacho bidii yake imempeleka, na hairuhusiwi kwake kuacha yale anayofikiria kuwa yana uwezekano mkubwa wa kufanyiwa kazi ndani ya dhana yake.
Na katika rai nyengine: Suala la usahihi wa rai za wanazuoni wa fiqhi wa madhehebu mengine yasiyokuwa madhehebu manne linatokana na suala jengine ambalo Al-Taj Al-Subki alilitolea mukhtasari kwa maelezo mafupi yaliyohaririwa akisema: “mwenye nguvu katika ufahamu wake hitilafu yake itazingatiwa hata kama daraja lake la kujitahidi lipo chini ya mwenye kumpinga, na iwapo ufahamu wake ni dhaifu hatozingatiwa hata kama daraja yake ni kubwa, kwani hutokezea ikawa ufahamu wa mmoja wapo ni mkubwa katika suala moja pasi na suala jengine, ila jambo hili haliepukani na mwenye kujitahidi[67]..
Na maana ya kuzingatiwa hitilafu yake, inamaanisha haijuzu kuchukua rai yake wala kutomkana yule aliyeichukua, nguvu na udhaifu wa ufahamu vinazingatiwa katika kusihi rai za madhehebu ya fiqhi mengine yasiyokuwa madhehbu manne.
Na udhaifu wa ufahamu unaweza kuwa kutokana na sababu nyingi hakuna aliyepinga hata mmoja, zikiwemo, kwenda kinyume na aya (kurani au sunna) au makubaliano ya wazuoni (ijmaa). Kauli yoyote au rai yoyote inayakwenda kinyume na Kurani au sunna au walichokubaliana wanazuoni huwa haizingatiwi, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu. {Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume} [Anisaa, 59]. Na kauli yake Mtukufu {Basi hukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu} Al maida 48. Na akasema {Na mkikhitalifiana katika jambo lolote, basi hukumu yake iko kwa Mwenyezi Mungu} AShuura 10.na akasema {mwenye kuzusha katika jambo letu hili lisilotokana nalo basi (jambo hilo) linarudishwa[68].}
Kwa ajili hiyo, kupingana na Qur’ani, Sunnah sahihi, au maafikiano katika mambo yenye kukanusha habari za kuaminika, hata kama mlolongo wa mapokezi yake yameshikamana yakawa hayana uthibitisho, na vilevile hukumu ya Hakimu hubatilishwa.
Na hapa tunakusudia aya ya Kurani na sunna zilizo dhahiri katika uthibitisho na dalili, kama ilivyoelezwa katika masuala ya uthibitisho kwa njia ya dhana na ushahidi wake au aya iliyothibiti kwa dhana na uthibitisho pasi na dalili au kinyume chake nayo ni katika masuala ambayo inafaa kutendea ndani yake, na wala haipasi kukana kwa anayeyatendea, ikimaanisha kuzingatia hitilafu kuwa ina nguvu ndani yake.
Ama kwenda kinyume na Qiyass kuna maelezo kuhusu hilo; kwani Qiyass ima iwe ya wazi, nayo ni ile dalili zake zilizozungumzia kasoro husika, au iliyokatwa shauri kwa kukataa utofauti kati ya mzizi na tawi, kwa maelezo mengine ya kina nayo:ni ile yenye maana ya asili pekee, nayo huitwa Alqiyass Al qat`I – inagwa baadhi wanasema ni miongoni mwa dalili za aya- mfano wake; : kuambatisha uharamu uharamu wa kuwapiga wazazi kwa kukataza kuwadhulumu kwa hoja za kujiepusha na kuwadhuru. Na kufanya qiyass ya kulinganisha usimamizi wa ndoa juu ya usimamizi wa mali katika kufanya usimamizi wa mtoto mdogo kwa ila ya utoto kwa wote wawili...,
Na aina ya pili ya Qiyass: ni ile iliyojificha au ya kudhani; nayo ni ile ila (sababu) yake iliyokadiriwa au iliyozingatia kukanusha mtengamano baina ya asili na tawi kwa kupitia dhana ya mwenye kujitahidi. Mfano wake; kupima – kukisia mchele kwa ngano kwa kuzingatia kuwa vyote ni vyakula, na kuthibiti uharamu wa kuboresha baina yao. Ila (sababu) iliyopo katika ngano haijawa dalili iliyothibiti kuwa kwake ni chakula mpaka ilinganishwe (ifanyiwe Qiyass) lakini kuna hitilfu ndani yake, tafauti na ila ya Qiyass iliyo wazi.
Na makubaliano ya wanazuoni wamekubaliana kuwa udogo ni ila katika kuthibiti uongozi, na kutowafanyia maudhi wazazi wawili ni uelewa wa wazi wa aya, hata Sheikh Issa Mannuwn anasema katika kuelezea masuala ya Qiyass Alqat`I na Dhaniy…) ...katika kubainisha ila (sababu) ya kuruhusu kuharamishwa kuwakemea wazazi pekee pasi na kulaani kuwapiga hii inachukuliwa kuwa ni upuuzi wa kiakili[69]. Kwani haitofaa kusema {basi usimwambie hata: Ah!} Al israa, 23. Haioneshi kuharamishwa isipokuwa neno la kuwakemea, si kwa njia Qiyass na wala si kwa dalili ya neno, kwani ila (sababu) ya kukemea imepatikana kutokana na aya ambayo haifai kwenda nayo kinyume kwa msomi yeyote sembuse kwa mwenye akili.
Na wasomi wengi wa Usuli ya kuwa mwenye kwenda kinyume na kauli za wanazuoni wa Fiqhi juu ya Qiyass iliyo wazi hii ni ishara ya udhaifu wake, hata wamefikia kubatilisha kauli ya Hakimu pindi akihukumu kinyume na Qiyass. Na makubaliano ya wanazuoni hayavunjiki kwa kupinga kauli hii yenye hitilafu. Na amepokea Azamakhshary katika Albahru Muhiyt; “kutoka kwa Abi Is-haq Al asfaraniy ya kuwa rai hii ni ya wanazuoni wengi (jamhuri) wenye elimu[70].
Namna hiyo hiyo ametaja Alqurtuby katika kuelezea juu ya kitabu cha Sahih Muslim kwamba kauli hii ndivyo wasemavyo wasomi wengi wa Usuli na wanazuoni wa kifiqhi[71]. Hii ni katika muktadha wa mazungumzo yao juu ya kwenda kinyume na madhehebu ya Dhahir juu ya makubaliano ya wanazuoni na kwamba kwenda kinyume haitozingatiwa. Na sababu ya kutozingatiwa ni kile walichoshangaza katika misingi ambayo walijitenga nayo na wanazuoni wengine, na katika hizo ni Qiyass Al jiliyy (wazi) ambazo Ibn Hazim amezikataa kabisa. Na kupitia sababu hii Kadhi Abu Bakar Albaaqaniy na Abu Ishaq Al isfirayiyn na Imam Alguwayny na mwanafunzi wake Al Ghazaly wameeleza[72]: “Basi, yaweza kusemwa kwamba wanazuoni wa Usuli hawamzingatii asemaye jambo ambalo linapingana na Qiyass Jiliyy (ya wazi).
Na aliyotaja Alisfaraniy na Alqurtubiy ni kauli zaidi ya moja kutoka kwa wanazuoni: Kutoka kwa Shafii: Nawawy, na Al zarkashy na Ibn Daqyq al eid na Abi Hurayra na Au Alhuseyn Almarwazy na imam Haramayn na Abu Hamid Alghazaly na Ibn Salah[73].
Na kutoka kwa Malik: Kadhi Abu bakr Al baqalaniy, Ibn Batal, Ibn Alaraby, Dardery [74]na maneno ya Alshawqaniy yanajulisha hilo[75].
Ama kuhusu Qiyass Khafiy ilyofichikana wengi wao wanasema kutozingatiw kwa kule kuhalifu Qiyass Ajaliyy wakasema vile vile kutozingatiwa chenye kwenda kinyume na Qiyass Khafiy.
Isipokuwa Ibn Salah akawapinga katika hilo akasema katika fatwa zake;[76] “ambacho amekichagua mwalimu Abu Mansur katika hili na akataja kuwa ni sahihi katika madhehebu kuwa inazingatiwa hitilafu yake – akimaanisha Abu Suleiman Daud Al Asfahaniy – katika fiqhi ambayo anaendana nayo,jambo hilo katika kile kinachotokea mara nyingi na na kujulikana katika safu ya maimamu waliotangulia ambao wamepokea madhehebu ya Daud katika kutihibitsha vitabu vyao mashukuri katika matawi mfano Sheikh Abi hamid Al Asfaraniy na mwenziwe Al Mihamily na wengineo Mwenyezi Mungu awawie radhi kwani lau asingezingatia kupinga kwao (kupingana naye) basi wasingelitaja mafundisho yake katika kazi kama hizi kwa kule kupingana na maudhui kwa hilo.
Na kwa hili nilijibu, nikitafuta msaada wa Mwenyezi Mungu na kutumia kile ambacho Daudi alijenga kutoka katika madhehebu yake kuwa asili yake ni kukataa mlinganisho wa wazi Qiyass Jiliyy na yale waliyokubaliana juu yake wasomi wa Qiyass katika aina zake au katika njia nyengine za misingi yake ambazo dalili ya kuthibiti imesimama juu ya kubatilisha jambo hilo, basi kwa makubaliano ya wasiokuwa yeye kuhusiana na kumpinga jambo kama hilo basi makualiano yatafanyika, na kauli yake kuhusiana na jambo kama hilo inahesabika kuwa ni kuvunja makubaliano ya wanazuoni.”
Na maneno ya Ibn As sabaky yanatupa faida kwa yale aliyoyasema Ibn Salah pale aliposema katika kitabu cha “Atabakaat[77]” “kwa upande wa Madhehebu ya Dhahiriya wana masuala ambayo hayazingatiwa katika kumhalifu – akimaanisha Daudi –ndani yake, kwani si kwa sababu Daudi hana sifa ya kuangalia, lakini kwa sababu ya uvunjaji wake wa makubaliano, na akatoa udhuru wake kwamba hakuifikia, au ushahidi wa wazi kabisa[78]. .
Na ushahidi aliposema: “na ushahidi wa wazi” hakuna ndani yake Qiyass iliyofichikana bila ya malumbano.
Na ushahidi wa maneno ya Ibn Salah; “Wanachuoni wa Qiyass wamekubalina aina zake“ na Qiyass Alkhafiy ni katika aina hizo kwa kule kutafautiana wanazuoni katika aina zote za Qiyass Alkhafiy katika ila (sababu) ya msingi ambayo imejengewa kwake Qiyass. Kwa mfano muuwaji kwa kutumia kitu kizito na muuwaji wa kutumia kitu kilicho na ncha, hakuna dalili iliyothibiti ya moja kwa moja kutokana na utafauti uliojitokeza kati ya hali hizi mbili, mpaka isemwe ni lazima kisasi kifanyike katika hali zote hizo mbili kwa maana hiyo imam Abu Hanifa Hakuona kuwa kuna kisasi kwa muuaji kwa kutumia kitu kizito.
Na maneno ya Ibn Salah ni moja ya njia walizotaja wanazuoni, kwani Qiyass imejengewa kutokana na ila (sababu) za msingi, na inapokuwa haikujengewa dalili au kuwepo makubaliano hutoko kuwa yakinifu na kuwa ya dhana, na kilicho na misingi ya dhana hiyo ni dhana, na mwenye kupinga dhana huwa hakanushwi, kwa kuwa hapingani na dalili iliyothibiti. Kwa ajili hiyo AS Shatibiy anasema katika “Al muwafaqaat” dhana ambayo haijulikani asili yake wala haipingi asili ilothitibiti hii itaangaliwa[79], akimaanisha ni jambo la kuangaliwa katika utendaji wake.
Na inapasa kuweka wazi kwa kile alichokitaja Daudi katika maneno ya Ibbn Salah na Ibn As sabaky huo ni mfano tu, iwapo mwanachuoni mwengine amehitilafiana na aliyoyataja Ibn Salah na Ibn As sabaky katika ibara zao, hakuna shaka katika kuwarudi –kuwajibu – kauli zao na kutozitilia maanani, kwa kuwa hakuna haja ya kuingilia kauli ya mtu kwa kuona kauli yake ina nguvu au ina madhaifu, kwani hatukuzwi yeyote na wala haiangaliwi sifa zake lakini kwa maelezo yake na ufahamu wake.
Pili: Je, inajuzu kutoka katika Madhehebu manne ya Kifiqhi na kwenda (kufuata) Madhehebu mengine rai ningine?
Kwa kuzingatia yale yaliyotangulia, kauli ya mwanachuoni yeyote (faqihi yeyote), ikiwa anategemea hoja iliyo na nguvu, na sahihi kisha na akaijumuisha katika mizani yenye kutilia nguvu kwa mujibu wa kinachomdhihirikia kuwa na nguvu, na hata ikidhoofika hoja yake kwa sababu yoyote ile haitozingatiwa kuwa ni sahihi ..
Kwa ajili hiyo, kauli nyingi zilizo nje ya Madhehebu[80] manne zilikuwa ni ngeni na dhaifu. Hivyo, Al Mawirdy anasema “"Mzunguko wa Uislamu na tegemeo la watu wake vimebakia kwa hawa maimamu wanne na wafuasi wao, na mafundisho yao, maneno na vitendo vyao vimedhibitiwa, na kuhaririwa, na kunakiliwa bila shaka juu ya hilo.”
Kinyume na madhehebu mengine, hata kama ni katika maimamu wanaotegemewa, isipokuwa wao haijayadhibiti kikamilifu, na hata kama kuna baadhi ya kauli ni sahihi, basi ni kiasi kidogo tu na nahakitomtosheleza. Nayo kwa kutofuatwa pia kauli zao ima zinaafikiana na maimamu hawa wanne au haziwafikiani, na ikiwa ziwameafikiana, basi yale yaliyokusudiwa yatakuwa yamepatikana na kutilia mkazo.
Na iwapo haziwafikiani, mara nyingi zisizokubalika huwa ni kauli ngeni zisizo za kawaida na zisizokubalika. Ama maimamu wengine viongozi wa uzushi (bidaa), kama vile Rafidhi, Khawariji, Mu’tazila, na wengineo, maneno yao hayazingatiwi yenye kupinga kauli za maimamu na wafuasi wao. lakini kauli zao zikitajwa hiyo ni kwa ajili ya kuielezea kujitegemea na wanazuoni hutokezea kutaja kwa malengo ya kumjibu msemaje wake na kujiepusha nae na kuwafunza wengine kuweza kuepukana na fitina zilizomo ndani[81] yake.
Una mfano juu hili rai kutoka madhehebu ya Dhahiria katika masuala ya Alqiyass Al jiliyyah (Qiyas iliyo wazi: ni ile ambayo ila – sababu - yake imethibitishwa kwa ushahidi wa aya/hadithi au makubaliano ya wanazuoni au ilikuwa dhahiri –wazi- kwa kukataa tofauti kati ya asili na tawi) masuala ambayo yaligandishwa kwa maana ya wazi. Yakiashiria kwamba masuala ambayo walioenda kipekee kinyume na wanazuoni wanne ambayo hakuna mtu aliyewafuata kutokana na kauli zilizoachwa, kama vile kusema kwao kujisaidia katika maji yaliyotuama na kuyamiminia maji na kusema hapana Riba isipokuwa katika makundi maalum yalioainishwa kupitia aya / hadithi.
Kama inavyojulisha vilevile juu ya yale waliyokwenda kinyume baadhi ya wanazuoni wa madhehebu manne inaweza kuweza kuwa imekubaliwa na wanazuoni wengine. Kuchukua rai yao katika hali kama hii haitozingatiwa kuwa ni rai pekee ya madheheu ya Dhahiria lakini pia itanasibishwa na madhehebu mengine. Tofauti na (rai) iliyotafautiana katika Al Qiyas Al khafiyy (ni ile ambayo haikani utafauti baina yake – baina ya asili na tawi lake.) kwa kuwa hii imejengeka kwa dhana – kama ilivyoelezwa – Aldhahabi Ashafii anasema katika kuelezea maneno ya Daud bin Ally Imamu wa Dhahiria: “hapana shaka kuwa kila suala (jambo) la kipekee alilolitaja na akatoa kauli ya kulibatilisha jambo hilo huzingatiwa kuwa ni la uwongo kabisa ni la upotevu, lakini tunalisema kwa kustaajabisha tu. Suala lolote ambalo lina ushahidi wa aya / hadithi na kuungwa mkono na muhusika wa suala hilo au mfuasi aliyetangulia hilo ni jambo lenye hitilafu, kwa hivyo suala hilo halipaswi kuonekana kuwa ni la upotoshaji. Kwa ujumla Daud bin Ally ni mtambuzi wa Fiqhi na mjuzi wa Qurani amehifadhi historia kichwani katika kujua hitilafu kutokana na vyanzo vya elimu, ana utaalamu mkubwa na mshika dini. Hivyo hivyo katika madhehebu ya Dhahiria kuna wanazuoni wenye elimu kubwa na akili yenye nguvu, ukamilifu ni jambo zuri na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kuwafikisha.
Nasi hapa tunaelezea kauli ya Ibn Abass katika ndoa ya Mut`a na katika matumizi na pia katika kukataa Al Aul (ni hali ya kuongeza idadi ya mafungu na kupungua sehemu ya hisa za warithi.) na kauli ya kundi la masahaba katika kuacha kuoga kwa kuingiza uume katika tupuya mwanamke (na mfano wake, hivyo haijuzu kwa yeyote kuwafuata katika hayo[82].”
Anasema Al-Shawkani katika “Irshad al-Fahul[83]” : “Yeyote anayejua vyema matini (maandiko) ya sharia, akatafakari aya za Kitabu kitukufu, na akazama katika elimu ya Sunnah tukufu, na akaelewa kwamba matini za Shari'a hutekeleza – hutosheleza – katika yanayohitajika katika matukio yote, na wanazuoni wengi wa madhehebu ya Dhahiria wapo miongoni mwao maimamu wakubwa waliohifadhi Sharia na wakashikamana nayo, na hakuna ubaya kwao isipokuwa kuacha kutekeleza rai za upotovu ambazo hazijaashiriwa na kitabu, wala Sunnah, au Qiyass yenye kukubalika… ndio, walidumaza mas-ala ambayo walipaswa kuyaacha kama yalivyo, lakini kuhusiana na yaliyotokea katika madhehebu mengine katika kufanya mambo ambayo hayana ushahidi hata kidogo, ni masu-ala machache sana.
Lakini hali isiyo ya kawaida na udhaifu wa kauli hiyo sio uhalali wa kuiacha na kuipuuza, kuwa na nguvu kwa dalili kunaweza kutofautiana na kuwa na nguvu kwa matendo, kiasi kwamba kauli dhaifu hufanyiwa kazi kwa dharura, au kuleta masilahi ya uhakika, au kuepusha madhara. Hii ni pamoja na kuiga madhehebu mengine katika mojawapo ya hali zilizotajwa, na hili ni suala wamelizungumzia wanazuoni (mafaqihi) na wanazuoni wa Usul na kutaja katika udhibiti wake kuwa lisiwe na udhaifu mkubwa, ikimaanisha kauli iwe inazingatiwa kwa nguvu ya hoja na kama hoja iliyopo ni dhaifu basi haitozingatiwa kama ilivyotangulia.
Na miongoni mwa vidhibiti pia ni pamoja na kuwepo hali ya ulazima au maslahi ya moja kwa moja, au kufanya kwa ajili ya kuondosha ovu, au kuanguka katika majaribu.
Ushahidi ulio bora kabisa wa kuacha yale ambayo ni sahihi zaidi na kutenda yaliyowekewa mkazo ni vitabu vya fiqhi vilivyojaa matawi yanayoashiria hili, kwa mfano Ibn Qudama anasema: “Ama kwa wale wanaohitilafiana katika matawi, kama vile wafuasi wa madhehebu ya Abu Hanifa, Malik, na Al-Shafi'iy, kuswali nyuma yao ni sahihi na wala haikuchukizi. Akaeleza Imam Ahmad, ‘ kwani Maswahaba, matabiina na waliofuta baada yao hawakuacha baadhi yao wakifuata baadhi yao pamoja na kuwa wamehitilafiana katika matawi, hiyo ikajulikana kama ni makubaliano ya wanazuoni, kwani mwenye kwenda kinyume ima atakuwa amepatia katika jitihada zake naye atakuwa na malipo mara mbili; kwa jitihada zake na kwa kule kupatia kwake, au atakuwa amekosea naye atakuwa na malipo mamoja kwa kule kujitahidi kwake, na wala hatokuwa na madhambi kutokana na kosa lake kwani yeye ni aliyefanya ufupisho[84]. .
Imaam Ahmad anajuzisha swala nyuma ya mtu ambaye anaenda kinyume na rai - maoni yake, ijapokuwa anaweza kufanya ndani ya sala yake kile asichokiamini yeye kuwa ni sahihi.
Na katika kitabu cha Tuhfa ala Minhaj: “ni halali kutumia chombo chochote katika kujitahirisha …. Isipokuwa cha dhahabu na fedha… huharamishwa.” Kukitumia katika kula au matumizi mengine… hata kwa mwanamke akakitumia kwa kupakia wanja kwa mtoto bila ya dharura, kwa kule kukatazwa jambo hilo pamoja na kuwepo kwa makatazo ambayo huenda yakahesabika ni katika madhambi makubwa.” Asharwaniy anasema katika Alhashiy: “aliposema: (yakahesabika ni katika madhambi makubwa).. amenukuu Al Awazai kutoka kwa wanazuoni kuwa hilo ni katika madhambi madogo, na kauli hii huzingatiwa. Na amesema Daudi Adhahiriy huchukiza kutumia vyombo vya dhahabu na fedha machukizo ya kulazimika kujiepusha nayo ni kauli ya zamani ya imam Shafiy. Na ikasemwa ni uharamu ikihisisha katika ulaji na vinywaji pasi na jambo lengine... na kwa upande wa Imam Hanafy anasema inafaa kwa hali ya dharura ingawa kauli yenye kuzingatiwa kwao ni uharamu, hivyo inahitajika kwa yule aliyefikwa na mtihani huo kama yalivyofikwa wengi ajitahidi kujiepusha ili aisiingie katika uharamu[85].
.Miongoni mwa mifano ya kutendea kilichotiliwa nguvu ni kuacha mtu madhehebu yake na kuhamia madhehebu mengine kwa baadhi ya mas ala si kwasababu ya nguvu ya ushahidi au uhalali wowote wa kisheria inayokubalika lakini ni kwa utashi. Mfano ni kuchukua katika kila madhehebu kilicho chepesi sawa iwe katika dhehebu aliloenda katika madhehebu manne au nje ya hayo. Mfano wake iwe jambo ndani ya madhehebu yake wajibu au haramu kisha aache na kufanyia kazi madhehebu anayoona kuwa si wajibu wala si haramu kwa matamanio yake au awe anatafuta huruma ya jirani na akawa anaamini kuwa ni haki yake kisha akaombwa huruma ya jirani aliyoiamini kuwa si thabiti. Au iwapo ana adui anayefanya baadhi ya mambo yenye kwenda kinyume kama kunywa mvinyo ambao wametafautiana ndani yake au kucheza bao (shatranj) linalokemewa, hivyo rafiki yake akitenda hayo na akiiamni kuwa hayo ni katika masuala ya jitihada ambayo hayakatazwi.
Na wanazuoni wamehitilafiana katika jambo hilo kwa kauli zifuatazo:
Kauli ya kwanza: Ni haramu, na ni ubaya kwa atendaye ni (fasiki), kauli hii amesema imam Hanifa, Malik, Hanbal nayo ni kauli ya madhehebu ya Shafiy – isipokuwa – akimaanisha Shafiy – wamesema. Iwapo kuhama na kufuata madhehebu mengine miongoni mwa madhehebu yaliyohaririwa sahihi ni kuwa hahesabiki kuwa ni jambo baya (fasiki). Na Shehabu Aramly akayawekea mipaka iwapo utiifu wake utashinda maasi yake. Na iwapo atahamia katika madhehebu yasiyohaririwa hata kama ni katika zama za mwanzo – zama za masahaba – hatokuwa fasiki ama kinyume chake atakuwa fasiki. Na baadhi ya wanazuoni wamenakili – kama Ibn Abd Bar na Annafrawiy wa madhehebu ya Malik[86] – kukusanyika kwa jambo baya hilo ni kufuata ruhusa kimatamanio.
Na wakatoa ushahidi wa hilo kwamba hakuna ruhusa yeyote kuamini jambo kuwa ni wajibu au haramu kisha aliitakidi kuwa si wajibu wala haramu kwa matamanio yake. Haya ni yale aliyoyasema imama Ahmad kama alivyotaja Ibn Taymiya[87]. Kama lau tungelisema kujuzu kuhamia madhehebu mengine kwa kuchukulia kuwa kule kuchukua maneno ya baadhi ya wenye kujitahidi basi kukataza hilo kungekuwa ni bora zaidi, kwani nafsi humili katika wepesi na raha na kukimbia matatizo na mambo mzito.
Kwani hiyo mara nyingi hupelekea kuharibu hukumu za kisheria, ikawa ni wajibu kuzuia mwanya wa kupelekea matatizo na uharibifu. Naye Mwenyezi Mungu ameshutumu kufuata matamanio kwa ajili ya kutosheleza matamanio ya nafsi na utashi wake.{Hawafuati ila dhana tu na kipendacho nafsi.}Annajm 23.
Na kufuata ruhusa pasi na kuwepo haja au dalili ipelekeayo jambo hili huhesabika ni katika kufuata matamanio yenye kupelekea upotofu, na haya ndiyo aliyoyasema Ashatiby kwani ameweka wazi kuwa jambo hili litapelekea “kuifanyia mchezo dini, kwani kwa kufanya hivyo inakuwa ni kama mtiririko usioweza kudhibitika, ambao hauzuii nafsi kuepukana na matamanio yake na hautoweza kusimama katika mipaka..[88]
Ikiongezwa zaidi ya hayo, kuwa kufuata madhehebu mengine kimatamanio hupelekea kusemwa kwamba madhehebu yamebuniwa kwa njia ambayo yanakinzana na ushahidi wa wazi katika hoja zake au rai za makubaliano ya wanazuoni. Kwa mfano ukiwa unamfuata Imam Shafiy katika kauli ya kuwa mvinyo na ulevi ni vitu viwili vinavyofanana katika hukumu kisha ukamfuata imam Aba Hanifa ya kuwa mvinyo ni haramu, itakuwa amechangaya kauli mbili juu ya hukumu, nayo ni kuwa ulevi ni halali kwani mvinyo ni halali kwa upande wa Abiiy Hanifa, hali ambayo ni sawa kihukumu kwa upande wa imam Shafy (kuwa ni haramu). Hivyo, mkanganyiko huu ni batili wenye kwenda kinyume na makubaliano ya wanazuoni na kwa ushahidi wa wazi ambao umeharamisha ulevi[89].
Na inawezekana kutoa ushahidi kwa asemaye kuwa mtu anayefuata madheheu mengine hawi fasiki katika rai za masahabba: kwa kuwa masahaba si kama wengine, kwani wana ubora na upambanuzi usiokuwepo kwa wengine, wao wamemuona mtume na kuishi mazingira ya kuteremshwa wahyi na kitabu bila ya kuwepo kiunganishi kati yao na mtumu (S.W.A.). Ibbn Qayyim anasema kutoka kwa Imam Shafiy” {wao wapo juu yetu kielimu, juhudi, uchaji Mungu, kiakili, utambuzi wa mambo ya uchambuzi wake, na mawazo- rai zao kwetu ni bora na zenye kushukuriwa kuliko mawazo – rai zetu[90]}.
Kama ilivyowaombea Mtume (S.A.W.) baadhi ya masahaba kuwa na elimu na hifadhi na ufahamu au wameshuhudia hilo. Na Mwenyezi Mungu amewatukuza na akatuamrisha kupitia kuranai kuwafuata kwa ujumla. Jambo hili linatoa uyakini juu ya kauli zao katika suala moja hata kama rai zao zitahitilafiana, jambo ambalo sisi linatupa uhalali kuchukua moja wapo kwa wakati Fulani na kuchukua jengine kwa wakati mwengine.
Kauli ya pili: Hatozingatiwa kuwa ni fasiki kabisa, hata kama akifuata kimatamanio na kufuata ruhusa; hii ni kauli ya baadhi ya Hanafy na kupita hayo amesema Ibn AbdSalam, ibn Aby Hurayra wa Shafiy, Ahmad katika moja ya mapokezi yake, Abu Ishaq Almurzawy wa Hanbal katika moja ya kauli zake aliposema inafaa kufuata. Nayo pia ni katika madhehebu ya Omar Ibn AbdAziz aliposema inajuzu kuchukua kinachofaa iwapo kuna hitilafu na akaashiria kwamba hitilafu ni uwanja mpana (kuna wasaa) hivyo hivyo amesema Qasim bin Muhammad na Sufyan Athawry[91].
Wakatolea ushahidi juu ya hili kwa hadithi ya Mtume (S.A.W.) {Maswahaba zangu ni kama nyota, yeyote amtakaemfuata mtaongokewa[92].} na ushahidi unaopatikana ni kuwa ni ule mlinganisho unaopatikana kupitia kauli za wanazuoni kutokana na kauli za masahaba Mwenyezi Mungu awawie radhi, kwani kutokana na hadithi kuna ushahidi wa kujuzu kuchukua kauli za mmoja wao hivyo hivyo kwa wanazuoni.
Pia ushahidi mwengine imepokewa kutoka kwa Aisha Mwenyezi Mungu amwie radhi amesema: {alikuwa anapenda yale yaliyo mepesi kwao[93].} akimaanisha, mtume (S.A.W.) alikuwa akipenda yale yaliyo mepesi kwa umma wake na katika kuchukua neno la mwanazuoni kuna wepesi hivyo itakuwa imeingia katika hadithi hii. Na kama alivyokuwa Mtume (S.A.W.) ametumwa kwa unyenyekevu na usamehevu, hii haimzuilii mfuasi wake kuchukua ruhusa ilivyokuwa katika kuchukua huko kuna wepesi.
Ikiwemo hadithi ya Ibn Omar (R.A) amesema: amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.): “Mwenyezi Mungu anapenda kutimizwa ruhusa zake (alizowapa waja) kama apendavyo kutimiziwa wajibu wake[94].”
Ushahidi unaotolewa ni kuwa: kuchukua kilicho na wepesi ni jambo limpendezalo Mwenyezi Mungu Mtukufu kama kufanya yaliyo lazima ni jambo pia limpendezalo Mwenyezi Mungu, hivyo hadithi ikatoa ushahidi kuwa inafaa kuchukua ruhusa kwani kuna wepesi ambao Mwenyezi Mungu anaupenda.
Ikiongezwa juu ya hilo kuwa kufanya mkazo ambao wameutaja ni kuzuia wasifuate wengine moja kwa moja huko ni kuwazuia watu wasifuate ruhusa, na inapotenguka kinachotahadharishwa juu ya kuchukua ruhusa itafaa kuifanyia kazi.
Na kama ilivyo kwa watu tangu zama maswahaba hadi kutokea kwa madhehebu wanauliza kuhusu kuwapa wanazuoni wenye kutafautiana bila ya kukataa sawa wawe wanafuata ruhusa au wajibu, kwani wamejaalia mwenye kupatia ni mmoja[95] – naye yuko sahihi- ambaye hawajamtaja ni nani. Na aliyejaaliwa kuwa kila mwenye kujitahidi amepatia basi hakuna haja ya kukana katika kumfuata kwa kuwa yupo sahihi.
Saatiby anasema kutolea ushahidi wa rai hii: {kwa upande wa Qiyas. Mwenyezi Mungu ni Mkwasi Mkarimu, na waja ni wenye kuhitaji, na ikitokezea kutowafikiana baina ya pande mbili basi upande wa Ukwasi utakuwa ni bora[96].”}
Na kauli iliyo sahihi zaidi katika kauli mbili hizo itategemea hali ya anayehama na kufuata dhehebu jengine, itakuwa ni haramu kwake iwapo ni mwenye kujitahidi kwenda katika madhehebu mengine au kufuata kauli ya mwenye kujitahidi na kufuata kauli ya mwenye kujitahidi mwengine kwa kufuata matamanio na si kisheria, isipokuwa hatajulikana kuwa ni mfu fasiki kwa kufanya hivyo. Na sababu ya kuwa haramu ni makubaliano ya wanazuoni wa usul ya kwamba mwenye kujitahidi atakapojitahidi na dhana yake ikashinda hukumu haitompasa kumfuata mwengine ikimaanisha haitomfaa kwake kuacha dhehebu lake[97].
Ama kwa asiyekuwa mwenye kujitahidi, baadhi wamesema inafaa na wengine wakakataa. Alghazaly anasema baada ya kutaja hitilafu kwa asiyekuwa mwenye kujitahidi[98]: {masuala ya kudhani yenye kuhitaji kujitahidi} kwa maana tukisema kuwa inafaa kuhamia dhehebu jengine lingekuwa jambo la karibu – rahisi- lakini inashartishwa ili kufaa kuhamia dhehebbu jengine iwe kauli ya mwenye kuhamia inazingatiwa yenye nguvu ya kidalili, na iwapo dalili ni dhaifu haitozingatiwa. Na bora kwake ni ile isiyo na dalili kabisa. Sharti hili limewekwa si kwa kila mtu. Ama kwa (mwenye kujitahidi) anashartishwa kufuata kwa aliyemshinda kwa dhana yake na kuwa ni katika watu wenye kutoa fatwa, na njia atumiayo ni ile inayojulikana kuwa ni ya fatwa na anastahiki na si kwa matamatio (ya nafsi yake.)
Kama inavyoshartishwa kwa kila mtu na kwa mwengine katika wale wanaofaa kufuata madhehebu mengine – makusudio yao kufuata madhehebu mengine yasiwe kuepukana na kufuata wajibu wa kisheria au kuacha kufuata sehemu tu ya jambo hilo. Na madhumuni ya sharti hili ni kama alivyoashiria Ibn Abidin alipozungumzia kuhusu kuhamia madhehebu ya Hanafi kutoka madhehebu ya Shafiy, na baada ya maelezo mengi akasema: {tumerefusha katika hilo ili wasije wakapata hadaa baadhi ya wajinga kwa yale yaliyoandikwa katika vitabu kwa kusemwa baadhi ya taabira zenye kutatiza kinyume na ilivyokusudiwa na wakayachukua hayo kwa kuwadogesha wanazuoni wenye kujitahidi. Hakika wanazuoni – mwenyezi mungu awaepushe – hawakukusudia kudhalilisha madhehebu ya Shafiy au mengine, lakini wamesema ibara hizo kwa lengo la kuzuia kuhama hama kwa hofu ya kufanya mchezo ndani ya madhehebu, Mwenyezi Mungu atunufaishe na elimu zao na atufishe juu ya mapenzi yao.[99]}
***
Sehemu ya pili
Nafasi ya mwenye kuuliza fatwa juu ya kuwepo kwa majibu tofauti
Ndani ya nchi moja inaweza kutokezea idadi kubwa ya watoa fatwa maswali (mufti wengi), na inapotokezea kutatizwa kwa muulizaji juu ya suala ambalo anataka kujua hukumu yake ya kisheria, je anaweza kumuuliza yeyote (katika mufti) au achague aliye bora?
Mwanzoni tunakiri kuwa: Haipasi kwa muulizaji atakapohitajia kujua hukumu ya mas ala kumuuliza (mufti) asiyejulikana. Lakini amuulize Yule ambaye dhana yake itampelekea kuhisi kuwa ni katika wenye kufaa kuulizwa, na haitoshi kuonekana kwake katika mtazamo wa wanazuoni, kwani si kila anayenasibishwa na elimu na akawa anasomesha anafaa kuulizwa, lakini hapana budi awe ni mwenye kustahiki kutoa fatwa na dhana yake impelekee kuhisi kuwa ana uwezo huo, na njia ya kujua hilo kwa kudhani ni kwa kuhisi kuwa ana sifa za kutoa fatwa na si kwa matamanio.
Nawawiy anasema: {inafaa kuuliza kwa mwenye sifa (aliyebobea) kwa kuwa kwake anastahiki kutoa fatwa. Wakasema baadhi ya waliokuja baadae: inazingatiwa kauli yake ‘mimi nina sifa ya kutoa fatwa si kwa kutaka umaarufu’ na wala haitoshelezi kule kubobea kwake wala kwa mtiririko, kwani kubobea na umaarufu kwa watu huwa hawaamini na huenda ikawa inatokana na mkanganyiko (kuchanganya mambo isijulikane uhalisia), ama kukosa mtiririko hainufaishi elimu ikiwa haitokani na elimu inayoonekana. na lililo sahihi ni lile la mwanzo[100].} na mifano ya kubobea ni kusimamisha imamu au naibu wake awe ni mufti au anayejuzu kutoa fatwa katika wale atakaowasimamisha kuwa maimamu.
Na mwenye kuangalia tafsiri ya wanazuoni wa Usul juu ya mifano ya kuwepo watoa fatwa (mufti wengi) ataona kwamba wamezingatia kidhibiti cha uwezekano (uwepo). Mufti asiyeweza kujibu suala la muulizaji kwa sababu ya umbali au hofu au kizuizi chengine katika vizuizi uwepo wake ni sawa na kutokuwepo hata kama ni katika mji mmoja na kinyume chake. Na kuendela kwa njia za mawasiliano kuna athari kubwa katika sharti hili la uwezekano (uwepo). Wakikusanyika ndani ya mji mmoja mufti zaidi ya mmoja wakawa na uwezo kamili kwa kumalika na masharti ya kutoa fatwa ima mwenye kutaka kuuliza ajue rai zao au hapana, ikiwapo hajui rai zao, wanazuoni wa usuli wamehitilafiana juu ya muulizaji kwa kauli mbili:
Kauli ya kwanza: nayo ndio iliyochaguliwa: Anaweza kumuuliza atakaye na wala halazimiki kutafuta aliye na elimu ya juu kuliko mwengine. Hii ni kauli ya wanazuoni wa usul.
Kauli ya pili: atalazimika kumchagua aliye bora wao. Wamesema hili baadhi ya wanazuoni wa usul akiwemo Ibn Alquswar, Shatiby katika madhehebu ya Malik, Ibn Sariyg, Qaffal Almarwazy, Qadhi Hussein, Asam `any katika madhehebu ya Shafiy na akachagua Ibn Uqayl na ibn Alqayyim katika madhehebu ya Hanbal.
Amir Batshah anasema: (Inafaa kumfuata aliyependekezwa kwa ubora pamoja na kuwepo kwa aliye bora.) walio wengi katika madhehebu ya Hanbal mfano Qadhi, Abi Khatwa, na Mwandishi wa kitabu cha Raudha na pia wakasema wafuasi wa madhehebu ya Hanafy, Malik na wengi katika madhehebbu ya Shafiy (na Imam Ahmad na kundi katika wanazuoni) wakiwafikiana (kukataza) mfano Ibn Sariyg, Qafal, Almarwazy na Ibn Sam`aniy na tafauti ipo katika mji mmoja kwa kuwa hakuna hitilafu kwamba halazimiki kumfuata aliye bora zaidi duniani. Namna hiyo hiyo ametaja Azarkashy katika maelezo yake na katika mapokezi ya Ahmad pamoja na wanazuoni[101].}
Akasema Azarkashy: {iwapo hakuna isipokuwa mufti mmoja na marejeo yake yanajulikana. Na wapo wengine wengi, je inafaa kumchagua aliye na elimu zaidi? Kuna mitazamo miwili; kutokana na hitilafu iliyotangulia katika kumfuata aliyependekezwa. Moja ya mitazamo hiyo ni aliyosema Ibn Siraj na Qafal atalazimika kufanya juhudi nyengine katika kumtafuta (aliye na elimu zaidi) kwani anaweza kumjua hata kwa njia ya kusikia kutoka kwa wakweli ikawa hana tatizo. Kauli hii ameisahihisha ustadh Abu Ishaq Al asfaraniy na Ilkiya. Lililo bora ni kuongokewa katika njia ya kisheria, na kauli uliyochaguliwa ni kwamba si lazima, isipokuwa atachagua ni nani wa kumuuliza kati yao. Rafi`i anasema: nayo kauli sahihi kwa wanazuoni wengi. Akasema ni kauli iliyo sahihi zaidi kama ilivyokuwa hailazimu kujitahidi katika kutafuta dalili. Na imam Shafii (RA) amesema katika Al Aa`m: “Kila Mwislamu anayeelekea Qiblah yuko huru katika kumfuata, na wala hatumuamrishi kufanya bidii katika yale yanayotegemewa zaidi.[102]”}.
Na imam Ghazaly anasema: {Mas ala iwapo katika mji hakuna isipokuwa mufti mmoja, italazimu kwa wote kumfuata, na iwapo wapo zaidi ya mmoja (muulizaji) anaweza kumuuliza amtakaye na halazimiki kumfuata ajuaye zaidi kama ilivyofanyika wakati wa zama za Masahaba, watu wa kawaida waliwauliza aliye na elimu zaidi na walio na elimu ya kawaida na wala hawakuzuiliwa watu wa kawaida katika kuuliza isipokuwa kwa Abi Bakr, Omar na wengineo katika makhalifa. Na wengine wakasema: ‘italazimu kumuuliza aliye na elimu zaidi, na iwapo watakuwa atachagua, na hili linakwenda kinyume na rai za wanazuoni maswahaba kwani wahakumzuia alieye na elimu zaid juu ya aliye na elimu ya kawaida katika kutoa fatwa, lakini haipasi isipokuwa kumwendea anayetambulika kwa elimu, uadilifu na kwa hilo waliwatambulikana[103].}
Na katika ‘Al usul ilaa Al usul’ cha Ibn Barhan: {wanazuoni wametafautiana kuhusu watu wa kawaida wakipatwa na jambo, je inafaa kwao kumfuata wamtakae au inapaswa kuchagua kwa mujibu wa uoni wa wanazuoni wenye kujitahidi. Wapo waliosema itamlazimu kugonga kila mlango katika milango ya elimu ya Fiqhi na masuala na kuhifadhi majibu yake na kumuuliza mjuzi, akipatia jawabu basi atamfuata. Wengine wakasema, isipokuwa atamfuata kwa kule kutajwa kwake kuwa na elimu ya fiqhi na kuenea kwa sifa zake. Aidha wengine wakasema, atamuuliza, je, wewe ni mwanachuoni mwenye sifa ya kujitahidi je, nikufuate? Akimjibu hilo, basi atamfuata, nayo ni kauli sahihi kwa madhehebu[104].}
Ya pili: anaweza kumfuata pindi akiamini ubora au usawa wa elimu, kauli hii imechaguliwa na Al-taj Asabaky, Albarmawi na wengineo.
Na maelezo yake: ni kwamba akiitikadi kuwepo aliyebora basi kauli yake itakuwa ni yenye kutiliwa mkazo, na wala hakuna katika sheria kulinganisha usawa kati ya kauli iliyobora kwa kauli iliyo bora zaidi. Ibn Uqayl anasema:
Itamlazimu kujitahidi, na itatangulizwa kauli iliyo bora zaidi, akimaanisha: kauli ya Al Kharqy na Al muwafaq katika kitabu cha Al muqni`i na venginevyo katika (mlango) wa kuelekea kibla. Na akasema hivyo Ibbn Sariyg na Qafal na Alqadhy Alhusein na Ibn Assam`any na Albaqalany na kwa upande wa madhehebu ya imam Ahmad kuna mapokezi mawili, kama yale ya mwanzo, kwa ajili hiyo, wametoa dalili ya kwanza kwa kusema: kilichokuwa bora kwa maswahaba na Alsalaf walikuwa wakiuliza masuala pamoja na kuwepo walio bora zaidi pamoja na kuwa mashuhuri na jambo hilo kufanyika mara kwa mara na hapakuwa na wa kulikataza, ikawa ni rai ya wanazuoni wote ya kujuzu kuuliza fatwa pamoja na uwezo wa kumuuliza aliye bora zaidi, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema {Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui} Al Nahl 43.
Na mtume Muhamad (S.A.W.) amesema {Maswahaba zangu ni kama nyota, yeyote amtakaemfuata mtaongoka} na wamo walio bora kuliko wengine; na vile vile watu wa kawaida hawawezi kuwajua nani ana elimu kubwa kuliko mwengine, na angelikalifishwa katika hilo basi ingelikuwa ni kumkalifisha juu ya kumtaka afanye bidii. Lakini Ibn al-Hajib alisema kwa kudogesha kwamba hili litatokea kwa kusikiliza na kuwarejea wanazuoni na wengineo kwa uwepo wa wingi wa wanaotoa fatwa na kuwatanguliza wanachuoni[105].
Na dalili za rai ya kwanza ni kama ifuatavyo:
1) Inafaa kumuuliza suala aliyependekezwa kwa ubora pamoja na kuwepo kwa aliye bora zaidi yake. Na dalili juu ya hilo ni hadithi ya Al-Asiyf, ikieleza kuwa; kuna kijana katika mabedui alienda kwa Mtume (S.A.W.) akasema; mwanangu alikuwa ni meajiriwa - mfanyakazi - kwa huyu hapa, akazini na mkewe, wakaniambia, mwanao ni lazima arembewe mawe, nikamkomboa kwa kondoo mia moja na ndama, kisha nikawauliza wenye elimu wakaniambia; mwanao apigwe bakora mia na kumhamisha mwaka[106].”
Na ushahidi uliopo hapa ni kuulizwa wenye elimu pamoja na kuwepo kwa Mtume Muhamad (S.A.W.) na Mtume (S.A.W.) hakukataza jambo hilo. Na kama ilivyo kuna masahaba walio bora na walio bora zaidi pamoja na yote alikuwa alilyeboreshwa akitoa fatwa pamoja na uwepo wa walio bora zaidi pasi na kukatzwa.
2) Mwenye kuuliza hawezi kujua ni nani aliye bora zaidi katika wenye sifa za jitihada na wala aliye na elimu kubwa, na kama tukimlazimisha hilo tutakuwa tumemuingiza katika mateso na masumbuko na hasa ukizingatia kuwa hatukumlazimisha kujitahidi katika kujua hukumu za kisheria. Namna hiyo hiyo hatumlazimishi kujitahidi katika kumjua mwenye elimu kubwa katika mufti au kumtafuta, ukiongezea kuwa muulizaji inamlazimu arejee kwa mufti aliyekusanya masharti na jambo hilo lipo kwa aliyependekezwa[107].
3) Kuwepo kwa Mufti aliyebora haibatilishi fatwa ya aliye bora (aliyependekezwa). hii haizuwii kutopata jibu kutoka kwa liyefadhilishwa.
Na wakatoa ushahidi wa kauli ya pili kwa kuwa kurejea kwa kauli ya mwengine haifai isipokuwa baada ya utambuzi kwa kuwa kwake anaelewa. Kwa dalili ya Hakimu na mtathmini wa bidhaa haipasi kurudi kwao mpaka kuelewa sifa zao, hivyo hivyo katika kufuata, na kama mwenye kuuliza hajui sifa za muulizwaji –mufti-
hakuwa na imani nae juu ya suala lake na kauli –jibu - lake halikuwa bora kuliko ya mwengine[108], kama ilivyo kwa mamufti katika mtazamo muulizaji, ni kama ushahidi unaokinzana dhidi ya mujtahid, na mujtahid, inapotokea mgongano, hutanguliza kile chenye nguvu, vivyo hivyo muulizaji wanapokuwa mamufti wengi, kwani jambo hili linazunguka katika nadharia ya dhana, mwenye kuitakidi kuwa Imam Shafiy (R.A.) ni mtambuliza zaidi na yupo sawa kwa madhehebu yake hatohitajika kuchukua madhehebu yanayopingana naye kwa matamanio, na namna kama hiyo.
Na dalili ya kwamba hairuhusiwi kurejelea kauli ya mtu mwingine isipokuwa baada ya kujua kwamba ana sifa ya kufanya hivyo, iko nje ya mgogoro. Kwa sababu asiyestahiki kutoa fatwa haijuzu kumuuliza hata kidogo, na swali letu linawekwa kwa aliyetimiza masharti ya kutoa fatwa pamoja na kuwa mamufti ni wengi.
Na kauli ya kuwa mamufti kwa mtazamo wa muulizaji ni sawa na dalili zinazokinzana za mwenye kijitahidi inabatilika kwa kuwa kauli yenye nguvu ni miongoni mwa kazi za mujtahid kutokana na wingi wa elimu yake na uimara wa akili yake, tofauti na muulizaji hivyo haizingatiwi nguvu yake hata ikiwa mwa mamufti wengi.
Na iwapo ni suala linaloulizwa ni katika mambo ya dhana - na ndio ilivyo, vinginevyo kusingekuwa na hitilafu baina ya mamufti kuhusiana na hilo - basi hakuna tatizo kwa mwenye kuchukua dhana – rai - ya mufti mmoja hata kama anapingana na rai ya mufti mufti mwingine.
Na wala haisemwi kuwa kumpa muulizaji chaguo baina ya kuomba fatwa kutoka kwa mmoja wa mamufti kunafungua mlango wa kufuata matamanio, kwa sababu hiyo ikiwa kwa hawa mamufti hawajatimiza masharti ya kutoa fatwa. Na ingelisemwa kufuata chaguo baina ya kila mwenye kunasibishwa na elimu au kujishughulisha na elimu bila ya maarifa kamili hii ingelikuwa ni kufungua mlango wa kufuata matamanio ya mamufti.
Ama hali ya pili, ni ile ya ujuzi wa muulizaji kuhusu rai za mamufti juu ya anachokiuliza, kama vile mmoja wao akisema haipendezi na mwengine akasema ni haramu, kwa mfano – na kauli ya wanazuoni wa Usuli imetafautiana pia ni nani kauli yake itachukuliwa – Azarkashy ameeleza kama kauli kumi katika suala hili, kauli ambayo tunaichukua ni kuwa atakuwa na hiari kuchagua kauli aitakayo na hata kama kauli atakayoiacha ni bora, na dalili ya hilo ni kuwa kumuuliza aliyebora pamoja na kuwepo aliye bora zaidi inafaaa, kama ilivyotangulia.
Na kwa ufupi ni kuwa mamufti wakikamilisha sifa zao za kutoa fatwa, basi muulizaji ana hiari katika kumuuliza yeyote na ana hiari ya kuchukua kauli ya yeyote.
.
.Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi
***
Matokeo ya utafiti
Mwisho wa utafiti tumegundua nukta zifuatazo:
kinachokusudiwa katika mareleo katika tafiti hii ni moja ya mawili:
kwanza: Watu wenye kujihusisha namambo ya kielemu au elimu za kisheria, nao ni wanazuoni.
Pili: Mitaala ambayo hutegemewa katika kupatia maarifa au maono ambayo yametolewa kutokana na vyanzo na dalili.
Wanazuoni wamehitilafiana kuhusu mweye kufuata madhehebu kuacha dhehebu yake na kufuata dhehebu mengine katika baadhi ya mas ala si kwa sababu ya nguvu ya dalili au kwa sababu yoyote ya kisheria yenye kukubalika juu ya kauli mbili. Na yenye nguvu; kuna maelezo kwa mujibu wa mwenye kuacha dhehebu lake, iwapo ni mwenye kujitahidi ni haramu kwake kufuata madhehebu na kwenda dhehebu jengine au kufuata kauli ya mwenye kujitahidi mwengine kimatamanio si kwa sababu za kisheria isipokuwa hatohesabika kuwa ni mtu muovu (fasik) kwa kufanya hivyo.
Ama asiyekuwa mwenye kujitahidi wapo waliosema inajuzu na wengine wakasema inakatazwa. Na tukisema inajuzu kuhamia madhehebu mengine jambo lingelikuwa ni karibu – jepesi – lakini inashartishwa ili kujuzu kuhamia dhehebu jengine hata kama si katika watu wa kawaida iwe kauli –dalili -ya mwenye kuhamia iwe na nguvu yenye kuzingatiwa. Ama kwa watu wa kawaida inashartishwa kufuata yule ambaye dhana yake itahisi zaidi kuwa ni mwenye sifa za kuweza kutoa fatwa, na njia ya dhana hii ni kubobea kwa kuwa kwake ni mwenye sifa za kutoa fatwa na si kwa umaarufu tu.
Na inashartishwa kwa wote wawili mtu wa kawaida na asiye wa kawaida kwa wanaofaa kuhamia dhehebu jengine lengo lao lisiwe kwa kuhamia huko kwenda dhehebe lengine ni kukimbia kutokana na kukalifishwa na sheria kwa kuiacha kabisa au kujiepusha na kutekeleza sehemu yake.
Na ili hitilafu iwe inazingatiwa ni lazima ipitie mambo kadhaa ikiwepo:
Moja: Adabu kwa unayepingana nae, ikimaanisha; kuwa na dhana njema kwa upande wa pili, na kuamini kuwa lengo lake ni kuifikia haki, na kuwa mpole katika kutoa na kupokea hoja kwa lengo la kujiepusha na malumbano yatakayopelekea fitina kwa wanaohitilafiana.
Pili: kujitoa katika hitilafu, ikimaanisha; Kuzingatia yaliyomo kwenye mzozo wa hitilafu, au kuifanyia kazi kwa mwenye kujitahidi dalili ya mpinzani wake, ikimaanisha; kupanga athari za matendo yake - yaani, juu ya tabia – huku akitoa hukumu yenyewe kwa kutowa ni kinyume cha sheria au mwenye kuamini kujuzu kwa kitu na kuacha kukifuata hata kama wengine wanaamini kuwa ni haramu. Hivyo hivyo kwa upande wa mambo ya lazima inapendeza kwa anayejua kujuzu kwa jambo fulani kulitenda hata kama maimamu wanaona jambo lile ni la wajibu.
Tatu: kutokumkana mpinzani, ikimaanisha; haipasi kwa mtu aliyekalifishwa na sheria kumkana mwengine au kumkataza asitende kwa maoni yake kwa kuwa tu anatofautiana nae, au kumnasibishia kauli yenye kuchukiza kwa kutumia njia tatu zilizoelezwa katika hadithi – mkono au ulimi au moyo – kama njia ya kumbadilisha au kwa kumpinga kutokana na matendo yenye kuwafikiana na maoni ya mwenye kujitahidi hali ya kuzingatia kuwa jambo hili ni sehemu ya mas ala yenye hitilafu.
Mamufti wakiwa na sifa za kutoa fatwa basi kwa mwenye kuuliza ana hiari ya kumuuliza yeyote na ana hiari pia ya kuchukua kauli ya mmoja wapo amtakae.
***
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi
[1] . Na miongoni mwa maana ambazo haziingii katika utafiti weru: Mfumo wa kijumla na msingi wa kimitaala wa fundishaji katika madhehebu au mwelekeo au mawazo. Kwa kutaka ziada rejea utafiti wa »Marejeleo na maana zake na vigawanyo vyake « Dkt. Said Alghamidy. Utafiti uliofanyiwa uhakiki na uliosambazwa kupitia gazeti la Jami Umm Qura – elimu za sheria za Kiisilamu. Toleo (50) Rajab 1431 H.
[2] . kitabu “Alfikru Asamy fiqhi Al Islamy (2/20)
[3] . Hadithi ya Abiy Dar dai ameitoa Alhakim katika AlMustadrik (2/375), akasema “Sahih Isnad” ameitoa Albayhaqy (2/196) anaifanya bora Alhaythamy katika Almujama`a (1/208).
[4] . kuna tafiti imesambazwa hivi karibuni za Mtunzi/ Thawar Ibn Ashally, yenye anuani “Al Asas fiy fiqhi alkhilaf … Utafiti wa kinadharia, wa kiasili unaotumika, uliochapishwa na Dar Al-Salam - Cairo.
[5] . tutaelezea kwa kina tukifikia kuelezea mas ala ya pili.
[6] . Asharhu lkabiyr (4/156)
[7] .Al ashbah wanadhair (uk. 137). Ang. Almuwafaqaat cha Ashatiby (4/172)
[8] . Almughny Almuhtaj (6/11)
[9] . Bulugh Assul katika Madkha Elm Usuul (Uk. 15)
[10] .Rejea: Al ibhaj (2/413). Na Hashiyat Albany (2/197)
[11] .Almuwafaqaat (1/105)
[12] . Almagmuu fataway(4/173)
[13] . Ameitoa Alhakim katika Almustadrik (3/424) na akasema “sahihi isnad”. Albayhaqy katika Sunan (8/173)
[14] . Rejea: Namudhaj min Rasail Aimah Assalaf wa-adabuhum al elmy cha Sheikh/ Abdulfattah Abi Ghudah. (Uk.45).
[15] .Iswal saalik fiy Usul Al imam Malik pamoja na ufafanuzi wa Muhamad bin Omar Ashanqiyty (Uk30.)
[16] .Rejea: Albahr Araiq (1/52). Na Fath Alqadir (3/151). Na Adur Almukhtar (1/147). (3/8). Na Manshur cha Azarkashy (2/127-128). Na Alqawaid Kubra cha Ezz Ibn Abd salaam (1/370). Na Alashbah wanadhair cha Assuyut (Uka36). Na Alashbah wanadhair cha Taaj Asabaky (1/110-111). Na Almughny (1/135)(2/11). Na Sherh Almuntahy (1/16).
[17] .Hudud in Arafah pamoja na ufafanuzi wake cha Araswagh (Uk.177).
[18] .Almuwafaqaat (5/107).
[19] .Rejea: Al miiyar alma`arab cha Alwanshariyny (6/388).
[20] .Al manshur (2/127).
[21] .Alqawaid Alkura (1/370).
[22] .Rad Almukhtar (1/131)
[23] . Rad Almukhtar (1/147).
[24] .Mutafaq Alayh. Ameito Bukhary katika kitabu bha “Tafsir Ashubuhat. Na Muslim katika kitabu cha “Aridhaa” Mtoto wa kitanda na kujiepusha na yenye kutatiza.
[25] . Muslim (10/39)
[26] .Ameitoa Ahmad (6/65-66). Na Abu Daud katika kitabu cha Anikah; mlango wa Waliy. Na Tirmidhy katika kitabu cha Anikah mlango wa “hakuna ndoa isipokuwa kwa walii. Na ameitoa Ibn Majah katika mlango wa Ndoa: hakuna ndoa bila ya walii, kutoka katika hadithi ya Aisha RA.
[27] .Bukhari na Muslim. Ameitoa Bukhary katika kitabu cha Al iyman, mlangowa uboro wa kujitakasa kwa dini. Na ameitoa Muslim katika mlango wa kunyoshelezea. Ktika mlango wa kuchukua halali na kuacha yenye kutatiza”
[28] .(8/311).
[29] .Ashbah wanadhair (Uk137)
[30] .Almughny muhtaj (6/11)
[31] . Ashbah wanadhair (1/113).
[32] . Ashbah wanadhair cha Taj Asabaky (1/112-113)
[33] . Ashbah wanadhair (1/112). Rejea: Ashbah wanadhair cha Asuyut (Uk137)
[34] Rejea: Almanthur (2/131)
[35] Rejea: Almiiyar Muurab (6/366)
[36] .(1/369)
[37] Rejea; Muujam maqayes llugha (5/383) heruf i ( Na-Ka-Ra)
[38] Rejea: Lisan Arab (10/232) Herufi (Na-Ka-Ra)
[39] Rejea: Tahdheeb Allugha Lil azhar (10/191) Herufi (Na-Ka-Ra) Na Taaj Al Aruus (14/287) Mlango wa hereufi ya Ra, Nu. Na kitabu cha Misbah Almunir (Uk. 625) Herufi (Na-Ka-Ra)
[40] Alfataway Al hindiyah (3/312)
[41] Rejea: Adabu Likhtilaf fiy masael elm wa Deen, ust;/ Mohamed Awwamah (Uk 8-10)
[42] Rad Mukhtar (5/403)
[43] Rejea: Kashaaf Istilahat wal funuun (1/116)
[44] (1/73)
[45] Mufradaat Alfaadh quran (uk156)
[46] Rejea: Aqdi Jayyid fiy Ahkaam Ijtihad wa Taqleed cha Dahlawiy (Uk26). Na Alfuruq cha Al quraafy (4/257). Na Almanthuur cha Azarkashy (3/364). Na Ashabaah wanadhair cha Assuyut (Uk137) na Alfawaid Al jiniyyah cha Alfaadaaniy (2/333). Na Alfuru`u cha Ibn Muflih (2/17). Na Kashaf Alqina`a cha Albahutiy (1/479).
[47] Rejea: Al adab Ashariyah cha Ibn Muflih (1/166)
[48] Rejea: Alfataway kubra cha Ibn Taimiyyah (6/96) Na I`lam muwaqi`en cha Ibn Qayyim (3/288).
[49] Rejea: Al hukmu kadhai wa atharuhu fiy raf`I khilaaf cha Ust; Dkt; Shauqy Abdelkarem Alam
[50] Alfawaed jiniyah a`la madhaheb suninnyah (2/333).
[51] Asnaa Matwaalib (4/180)
[52] Rejea: Al adab shareyah (1/166)
[53] Rejea: Jami`I Al ulum Wal hekam (Uk325).
[54] Alfataway kubra (6/96)
[55] I`ilam muwaqeen (3/288)
[56] Asayl Jaraar Almundafiq A`la hadaiq Azhar (4/588) pamoja na mabadiliko kidogo.
[57] Asayl Jaraar (4/218).
[58] Asayl Jaraar (3/81).
[59] Hadithi ya Muadh ameitoa Ahmad (36/333) na Abu Daud katika kitabu cha Al Aqdhiya; malnago wa Ijtihad Ra`I fiy qadhaa. Na Tirmidhy katika kitabu cha Ahkam; Mlango; yaliyokuja kuhusu Kadhi na namna ya kuhukumu.
[60] Imepokewa na idadi kubwa ya maswahaba wakiwemo; Zaid bin Thabit, amepokea kutoka kwake Ahmad (35/467). Na Abu Daud ktika kitabu cha: Elm; mlango wa fadhila za elimu. Na Ibn Majah katika Muqadimah sunanih. Mlango wa Aliyefikiwa na elimu. Akiwemo pia Ib Masuud, amepokea kutoka kwake Ahmad (7/221). Na Tirmidhy katika mlango wa Elm, mlango yaliyokuja katika kushajiisha kufikisha kwa kusikia. Amepokea Ahmad kutoka kwa Anas (21/60). Na Mut im Bin Ady (27/301).
[61] Rejea: Muqadimat Sheikh/ Mohamed Abi Zahrah kitabu cha / Ahmad Taimur Basha: {Nadhratu taarikhiya fiy huduth almadhaheb al fiqhiyah ar`aa wantisharuha `inda jamhur muslimeen}
[62] Rejea: Etijah fiqhiyah i`nda As hab hadith fiy qarn thalith hijriy, dkt/ Abdulmaged Mahmoud. Uk (44) pamoja na mabadiliko kidogo.
[63] Rejea: Ashbah wanadhair cha Ibn Nageem (Uk92).
[64] Majmuu`u rasailIbn Rajab (2/619).
[65] Adab Mufty (Uk163).
[66] Majmu`u Rasail Ibn Rajab (2/627)
[67] Ashbah wanadhair Ibn Asabaky (1/112-113).
[68] Mutafaq Alayh. Ameitoa Bukhary katika kitabu cha “Sulhu” mlango wa wakisulihishwa juu ya suluhu ya mjeuri basi suluhu hiyo hukataliwa. Na amepokea Muslim katika kitabu cha Hukumu, mlango wa Kubatilika hukumu iliyo batili na kumrudi anayezusha mambo.
[69] Nabras Uquul fiy tahqiq qiyas i`nda ulamaa usul (Uk182)
[70] Albahr muhet (4/271).
[71] Al mufhim lima Ushkila min talkhes kitab muslim (1/543)
[72] Al burhan (2/819). Na Bahr muhet (4/471-472)
[73] Angalia: Sherh nawawi – Sahih Muslim (1/142) bahr Muhet (4/472-474) na (6/291) Sherh Elmaam In Daqyq Eid (1/413) Na Burhan (2/819) Na Fatawa Ibn Salah (Uk69).
[74] Al mufhim lima Ushkila min talkhes talkhes kitab muslim cha Qurtuby (1/543). Na sherh saheh Bukhary Ibn atal (1/352) Na Aridhat Ahwadhiy (10/111) Na Bulghat Saalik (2/389).
[75] Irshad Fuhuul (1/215).
[76] (1/207)
[77] (2/290)
[78] Bdae`i sanae`I (7/234).
[79] (3/25).
[80] Zingatia, hapa sisi tunakusudia matamshi kutoka kwa madhehebu ya Kifiqhi kwa ujumla wake, na sio matamshi sahihi pekee.
[81] Atahbeer (1/128-129)
[82] Sayru A`lami Nubalaa (13/106/107)
[83] (1/215)
[84] Rejea: Almughniy (2/11)
[85] Tuhfatul minhag Bihashiyat Sharwaniy (1/118)
[86] . Rejea: Jami`I bayan elm wafadhlih (2/927) Na Fawakih dawaniy (2/356)
[87] . Rejea: fatawy Kubra (20/220-221)
[88] Rejea: Almuwafaqat (5/102)
[89] Rejea: Mausua Fataway Al muuswila: kilichoandaliwa/ Idara ya Tafiti za Kisheria, Dar Iftaa Masriya (1/393)
[90] Elam Muwaqieen (2/150)
[91] . Rejea: Fathul qadeer (7/258) Na Faidh Alqader (1/209) na Jami bayan elm (2/898). Na Tahbeer (8/4091-4093). Na Sharh kaukab al muner (4/578) Na Sherh Jalal Bihasheyet A`tar (4/441).
[92] Angalia maelezo juu ya mshikamanowa mlolongo wa hadithi katika; Atalkhes haber Ibn Hagar (4/462). N Badr muner Ibn Almultaqin (9/584)
[93] Ameitoa Bukhari katika kitabu: Nyakati za sala. Mlango wa zinazosaliwa pamoja na Alasiri kwa sala zilizopita.
[94] Amepokea kutoka hadithi ya Ibn Omar: Abayhaqy katika Alkubra (3/200). Na Ibn Haban (2/69). Na kutoka kwa hadithi ya Aisha: Tabrany katika “Al awsat” (8/82). Na kutoka hadithi ya Ibn Abas: Ibn Haban (8/333)
[95] Na hii ni kauli ya wanazuone wengi. Ameelezea Al mawirdy – kama ilivyo katika Al bahr muhet cha Azarkashy (8/283) kutoka kwa Shafy na Abi Hanifa na Malik na wanazuoni wengi.
Na Sheikh Ishaq Shabrazy anasema katika “Sherh Luma`a” (2/1046) chapa Dar Algharb islamy” haya ndio yaliyotajwa kutoka kwa Shafy katika kauli za zamani na mpya, na hana kauli nyengine zaidi ya hiyo, na sielewi katika wafuasi wake walioenda kinyume na madhehebu yake” na amenukuu pia (2/1048) kutoka kwa Tabary kuwa yeye amesema “Al-Muzani alilizungumzia hili kwa kina katika kitabu chake “Al-Targhīb fi al-'Ilm” na akahitimisha kuwa ukweli uko ndani ya mtu mmoja, na akatolea ushahidi nayo ni madhehebu ya Malik na Al-Layth, nayo ni Madhehebu ya kila aliyeandika katika madhehebu ya Al-Shafi'i, wa mwanzo na waliochelewa na kwa hilo wamelipokea pia madhehebu ya a Ashaera, Abu Bakr ibn Mujahid na Abu Bakr ibn Furak, na Abu Ishaq Al-Isfarayini.
Hivi ndivyo Ibn al-Subki alivyosahihisha katika “Jami’ al-Jawami’”; Imekuja ndani yake kwa maelezo yake Al-Allamah Al-Mahalli (2/428, 429): “(Ama suala ambalo halina uamuzi ndani yake) kutokana na masuala ya kifiqhi...( sahihi ni kuwa kwa mujibu wa wanazuoni wengi ni kwamba yuko sahihi) ndani yake (ni mmoja, na Mwenyezi Mungu Mtukufu) ana hukumu ndani yake kabla ya kujitahidi Ikasemwa (hakuna ushahidi juu yake), bali ni hazina ambayo huipata kwa atakae Mwenyezi Mungu (na sahihi ni kuwa kuna dalili juu yake, na kwamba yeye - yaani mwenye kujitahidi - (anawajibika kuifikia) - yaani hukumu -; Kwa kuwezekana kwake ... (na kwamba mwenye kukosea hapati dhambi, bali ana thawabu); kwa kule Kufanya juhudi ya kuitafuta.
Kama ilivyo kwa Maswahabah, Mungu awawie radhi, nao walijadiliana katika masuala, na kila mmoja wao akatoa dalili kwa kauli yake, na baadhi yao wakapata makosa kutoka kwa wengine. Na hii inapelekea kila mmoja alikuwa akiitafuta kuifikia haki. Kinachothibitishwa ukweli wa tusemayo ni makubaliano ya wanazuoni wa umma juu ya ulazima wa kutafakari, na kujitahidi, na kupanga ushahidi na kujenga baadhi yake juu ya nyinginezo na lau kama wote wangelikuwa wamepata (wako sahihi) basi kutafakari na kujitahidi kusingekuwa na maana yoyote.
Rejea: hapo juu katika: Fatwa ya Dar Al-Iftaa ya Misri No. 209 ya 2011 AD, ya tarehe: 5/18/2011 AD.
[96] Rejea: Almuwafaqat (5/104-105)
[97] Rejea: Al mustaswfa (uk368). Na Ehkam cha Amidee (4/204). Na Qawate`e adellah cha Ibn Sam`any (2/341).
[98] Al mustaswfa (uk369).
[99] Rad Almuhtar (4/80)
[100] Adab fatwa cha Nawawiy (Uk72).
[101] Tayseer tahrer (4/251).
[102] Abahr Muhet (8/365).
[103] Almustaswfa (Uk373).
[104] . Alwusul ila Usul (2/363-364).
[105] . Atahber (8/4080-4084)
[106] . Bukhari na Muslim; Imepokewa na Al-Bukhari katika Kitabu cha Hukmu, Sura: Je, inafaa kwa mtawala/hakimu kumtuma mtu peke yake kuangalia mambo? Na Muslim katika mlango: Mipaka, Sura: Anayekiri kwa nafsi yake juu ya uzinzi.
[107] Rejea: Allam`a Aby Ishaq (Uk256).
[108] Rejea: Alwadheh Ibn Akeel (5/466).