Kuoga kutokana na janaba na hukumu ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuoga kutokana na janaba na hukumu ya kujichua sehemu za siri (kupiga punyeto)

Question

  1. Ni namna gani mwanaume anaoga kutokana na janaba baada ya kufanya tendo la ndoa?
  2. Ni ipi hukumu ya kujichua sehemu za siri kwa ufafanuzi zaidi.

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:

  • Yule anayetaka kuoga kutokana na janaba anapaswa kutia nia ya kuoga janaba, kisha aanze kwa kuosha mikono yake na sehemu iliyotoka janaba. Baada ya hapo, asukutuwe na kupandisha maji puani, kisha anyunyuzie maji juu ya mwili wake wote, akihakikisha kuwa maji yamefika kwenye kila sehemu ya mwili. Mwishowe, atamaliza kwa kuosha miguu ikiwa amesimama katika mahali ambapo maji yamekusanyika (yametuama).
  •  Hukumu ya kujichua sehemu za Siri.

 Jibu:
Uislamu umewahimiza wafuasi wake kushikamana na maadili mema, tabia njema, na kujiepusha na maovu na vishawishi, na hasa kwa vijana, kwani wao ni nguzo ya taifa na nguvu yake. Uislamu umekataza kila jambo linaloweza kuleta madhara kwa watu, kiimani (kidini) na kijamii (kidunia). Sharia ya Allah imeamuru ndoa ili kuzuia kutenda maovu, na Mtume wetu Muhammad (S.A.W) amewahimiza vijana waoe pale ambapo kuna uwezo wa kufanya hivyo, na ikiwa hakuna uwezo basi wanapaswa kufunga saumu. Alisema Mtume (S.A.W): "Enyi vijana, yeyote ambaye ana uwezo wa kuoa basi na aoe, kwani hiyo itamfanya aweze kuweka macho chini na ni hifadhi ya sehemu ya siri. Na yeyote ambaye hana uwezo basi na afunge, kwani hiyo itakuwa ni kinga." Hadithi hii imepokelewa na Imamu al-Bukhari na Imamu Muslim kutoka kwa Ibn Mas'ud (R.A). Ikiwa vijana wana uwezo wa kifedha na kiroho wa kuoa, basi wanapaswa kuoa.

Na kama mtu atashindwa kifedha kuoa, basi inampasa afunge, kwani kufunga kunapunguza tamaa za kimwili kwa mwanaume. Kwa hivyo, kujichezea sehemu za siri kama wafanyavyo vijana ni haramu kisheria, kwa sababu sio jambo lililohalalishwa na Allah, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Qur'ani: {Na ambao wanazilinda tupu zao,5 Isipo kuwa kwa wake zao au kwa iliyo wamiliki mikono yao ya kulia. Kwani hao si wenye kulaumiwa.6 Lakini anaye taka kinyume cha haya, basi hao ndio warukao mipaka..} [Al-Mu’minun: 5-7]
Mwenyezi Mungu anatanabahisha katika Aya hizi kuwa sehemu ambayo mwanaume anapaswa kutoa mbegu zake ni kwa wake zao au kwa wale ambao mikono yao inamiliki na yeyote anayemwaga mbegu zake kinyume na hayo, basi anakuwa amekiuka na kufanya madhambi. Tunamuomba Allah atuokoe na ghadhabu yake na kutovunja heshima za sharia Zake.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.

 

 

 

Share this:

Related Fatwas