Jinsi ya kujua kwamba mwanamke aliy...

Egypt's Dar Al-Ifta

Jinsi ya kujua kwamba mwanamke aliye katika hedhi ametwaharika (amesafika)

Question

Kwanza: naomba kuelezwa ni namna gani mwanamke aliye katika hedhi anajua kwamba amepona?  Na usafi inamaanisha nini? Na inachukua muda gani? Na je baada ya kumalizika siku nne au kukatika damu atabaki (atapitisha) kipindi cha Swala mbili –Adhuhuri na Alasiri – ili kupata uhakika wa kuwa ametwaharika au kuna alama gani hasa? Naomba majibu na maelezo ya kutosheleza.

Pili: je Swala zilizompita atazilipa ambazo wakati wake umeingia hali ya kuwa hajajitwaharisha? Kwa kuwa yeye alikuwa akisubiri kupata uhakika wa kuwa ametwharika – mfano damu imekatika wakati wa Alfajiri naye hakuwa akielewa kuwa imekatika, kwa kuwa anatokwa na vitone au kitu hata kama ni nukta moja, kisha akaoga baada ya Magharibi kwa kuwa muda wa Swala ya Alasiri alihisi kuwa kuna kitu kimeteremka ikiambatana na damu- ni namna gani ataswali pindi akitwaharika muda was ala ya Isha kwa mfano.?

 

 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:

Kwanza: Mwanamke aliye katika hedhi anajua kwamba amepona ikiwa damu imeacha kutoka, au kama akiona majimaji meupe ambayo ni mwisho wa hedhi, na hii inadhihirisha kuwa kifuko cha uzazi kimekoma kutoa damu. Au pia, mwanamke anajua amepona kama damu imekauka kabisa.

Na maana ya "usafi" (twahara) kati ya hedhi mbili ni wakati ambapo mwanamke anakuwa ametakasika kutoka damu ya hedhi na nifasi. Hakuna muda maalumu wa mwisho wa twahara hii kwa mujibu wa Ijmaa (kufuatwa na wazo moja la wanazuoni), lakini kuna maoni tofauti kuhusu muda wake:

Muda wa chini wa twahara: Inasemekana kuwa muda wa chini wa twahara ni siku kumi na tano, wengine wanasema ni siku kumi. Wengine wanasema ni siku nane. wengine wanasema ni siku tano. Wengine wanasema inategemea pia na desturi ya mwanamke (ada yake) ikiwa desturi ya mwanamke ni kuona damu kwa siku tano, kwa mfano, na damu hiyo haikomi, basi inatakiwa aongeze siku tatu kama tahadhari (kujihakikishia kuwa ni kipindi cha twahara), na kisha ataoga na kuanza \Swala. Hii ni kwa mujibu wa Madhehebu ya Fiqhi ya Imamu Malik.

Pili: Ikiwa damu ya hedhi imekatika na mwanamke hajaoga (hajajitwaharisha), inampasa aoge mara damu itakapokatika, kisha aswali Swala zote alizokosa kuanzia wakati damu ilipokatika. Pia, inaruhusiwa kwa mwanamke kuswali akiwa na majimaji (kama vile majimaji meupe) kwa sharti kwamba atie udhu kwa kila Swala. Hatoswali Swala za Adhuhuri na Alasiri kwa udhu mmoja, hata kama udhu wake haujavunjika kwa sababu ya tukio lingine zaidi ya majimaji. Inampasa kuchukua udhu kwa kila Swala kisha aswali na kukamilisha Swala yake, hata kama majimaji yanaendelea kutoka.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.

 

 

 

Share this:

Related Fatwas