Tofauti kati ya manii, madhii na wadii na hukumu ya kila moja.
Question
Unawezaje kutafautisha kati yake? Na ipi hukumu ya kila moja wapo kuhusu twahara ya mwili na nguo?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Wadii: ni maji meupe mazito yanayotoka baada ya kukojoa. Hukumu yake ni bila tofauti kati ya wanazuoni wa Fiqhi. Bi. Aisha (R.A) alisema: "Ama kuhusu wadii hutoka baada ya mkojo, hivyo anaosha uume wake na makende yake, na anatawadha wala haogi."
Madhii: Ni maji meupe, meupe meupe (mazito kidogo) na yenye ute, yanayotoka wakati wa mawazo ya matamanio au wakati wa kuchezeana na pengine asihisi mtu wakati wa kutoka kwake. Na hutokezea kwa mwanaume na mwanamke isipokuwa kwa wanawake hutoka mara nyingi zaidi. Hukumu yake ni najisi, kwa makubaliano ya Wanazuoni, yanapoingia mwilini inapasa kuosha.
Kutoka kwa Sahl bin Haniyf (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) alisema: "Nilikuwa nikikumbwa na madhii kwa shida na taabu, na nilikuwa nikioga mara nyingi. Nikamueleza hilo Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehema na Amani ziwe juu yake), akasema: “Inakutosha kuchukua kiganja cha maji na kunyunyuzia juu ya sehemu ya nguo uliyodhani imeguswa na madhii.”
Manii: Ni maji yanayotoka kwa nguvu wakati wa kilele cha raha kubwa, na ni miongoni mwa mambo yanayolazimu kuoga. Baadhi ya wanazuoni wamesema kuwa ni najisi, lakini inavyoonekana ni kuwa ni twahara, ingawa inapendekezwa kuiosha ikiwa bado ni majimaji na kuifuta ikiwa imekauka. Aisha (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) alisema: "Nilikuwa nikifutika manii kutoka kwenye nguo ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehema na Amani ziwe juu yake) ikiwa imekauka, na niliiosha ikiwa bado ni majimaji."
Na kwa yaliyotajwa, jibu la swali litakuwa wazi iwapo hali iko kama ilivyoulizwa.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
