Hukumu Swala ya Jamaa Mwanamume na Mwanamke
Question
Je! Kunajuzu kisharia mume na mke kuswali Swala ya jamaa - kwa kufuata Madhehebu ya Imamu Hanifa -? Wazazi wangu na wazazi wa mke wangu wamesoma Dini ya Uislamu nchini Urusi kipindi cha kabla ya mapinduzi, kipindi hiki mafunzo ya Kiislamu nchini Urusi yalikuwa katika kiwango kizuri sana, wakati huo walikuwa hawaswali kama hivyo, hali iliendelea kuwa hivyo mpaka nikawa kijana na tukawa tunaswali jamaa sisi watatu, mimi baba na mama, baba akanieleza kuwa Swala ya jamaa inahitaji kuwepo wanaume wawili hata mmoja wao akiwa kijana mdogo. Naomba majibu yatakayoungwa mkono na dalili na kutaja vyanzo vya dalili hiyo, asanteni sana.
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Hili si sahihi, na hakuna Mwanachuoni yeyote wa Fiqhi alisema hilo, si katika Madhehebu ya Hanafi wala wengineo. Inawezekana amechanganya na suala la mwanamke kusimama sawa na mwanaume katika Swala akinuia Imamu, basi hilo linabatilisha Swala katika Madhehebu ya Hanafi. Mwanazuoni Abdurahman Shaukhy Zaadahu Al-Hanafi anasema katika “Majamaa Al-Anhar Sharh Multaqa Al-Abhar”: “mwanamke akisimama sawa na mwanamume na wakawa sawa kwa kiungo kimoja na mwanamume hata ikiwa mwanamke yupo kwenye kivuli na mwanamume kwa kiatu chake chini yake kikiwa kinalingana sawa na mwanamume, basi Swala yake ni batili, Az-Zualy amesema kinachozingatiwa katika kulingana sawa ni kisigino na mguu kwa kauli sahihi, na katika kueleza kwake kwamba kulingana kidogo kunaharibu Swala kama alivyosema Abu Yousuf, ama kwa Muhammad ameweka sharti la kuwa kiasi cha nguzo moja ijapokuwa akihirimia katika Swala na akarukuu katika safu nyingine, na kusujudu katika safu ya tatu Swala inabatilika aliye kuliani kwake, kushoto kwake na nyuma yake na safu yote”.
Naye Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
