Kuhudhuria Mazishi ya wasiokuwa Waislamu na Kuwaombea Dua Ndugu zao
Question
Mimi ni mwanamke niliyesilimu, nina swali linalonitatiza kwa muda mrefu. Swali linahusiana na kuhudhuria mazishi ya ndugu wasiokuwa Waislamu na kuzuru makaburi yao na kuwaombea dua. Mama yangu ni Mkristo wa Prostenti na baba yangu alikuwa Mkatoliki amefariki miaka michache iliyopita. Nimehudhuria shughuli za mazishi Kanisani ili kumliwaza mama yangu, na nimesimama na nimekaa kama wanavyofanya, lakini nimemwomba Mwenyezi Mungu Awaongoze katika Uislamu wote waliohudhuria. Nimekwenda makaburini kwa ajili ya mazishi lakini nilikaa mbali na nikaomba dua hii kwa utaratibu: “Amani iwe juu yenu wakazi wa nyumba ya Waumini tunambo Mwenyezi Mungu Atupe afya sisi na nyinyi”. Je! Nilichofanya kilikuwa sahihi? Na je! Naweza kumwombea dua baba yangu moja kwa moja au kufanya hivyo itakuwa kama alivyofanya Nabii Ibrahim kwa mzazi wake, ambaye Mwenyezi Mungu Amemwamrisha asimwombee dua? Na baada ya yote haya Wakatoliki wanaamini Mungu watatu. Na je! Naweza kuwaombea dua ndugu wengine waliotangulia? Je! Inafaa kwangu kuzuru makaburi ya ndugu zangu wasiokuwa Waislamu?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Dada yetu mpendwa … Mwenyezi Mungu Anawahurumia zaidi waja kuliko wao wenyewe, na Mwenyezi Mungu Amemsifu kipenzi chake Muhammad S.A.W. kwamba ni rehema kwa ulimwengu wote, na kwamba yeye ana tabia ya juu, na Mtume S.A.W. anapenda tabia njema, na anamsifu mwenye nazo hata kama hakuwa Muislamu. Mateka wa vita wa kike walipoletwa bint wa Hatim alikuwa miongoni mwa mateka hao, baba yake alikuwa maarufu sana kwa ukarimu na tabia njema; Mtume S.A.W. akasema: “Mwacheni; kwani baba yake alikuwa anapenda tabia njema, na Mwenyezi Mungu Anapenda tabia njema, akasimama Swahaba mmoja na akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Hivi Mwenyezi Mungu Anapenda tabia njema? Akasema Mtume S.A.W.: Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu ipo mikononi mwake, hataingia Peponi mtu yeyote isipokuwa kwa tabia njema”. Imetolewa na Al-Bayhaqy katika Hadithi za Ali bin Talib R.A.
Hukumu za dunia zinatofautiana na hukumu za Akhera, inajulikana kwamba kila asiyemwamini Mtume wetu Muhammad S.A.W. basi huyo ni kafiri, lakini mtu anaweza akahukumiwa hapa duniani kidhahiri kuwa kafiri kwa sababu hakuingia katika Uislamu, na haikutokea kwake kuukadhibisha Uislamu hata kidogo, na hukumu hii hailazimu kuwa anayehukumiwa ukafiri kwa wazi kuwa katika watu wa Motoni pamoja na kuwa atakaa milele; anaweza kusamehewa kwa Mola wake Mtukufu kwa kutoweza kumfika Uislamu kwa njia ya kumvutia, au kwa kutosimamishiwa hoja juu ya Uislamu, hivyo basi, anakuwa katika watu wa mtihani katika matukio ya Siku ya Kiyama, Mwenyezi Mungu Anasema: {Haimpasi Nabii na wale walio amini kuwatakia msamaha washirikina, ijapo kuwa ni jamaa zao, baada ya kwisha bainika kuwa hao ni watu wa Motoni}[Al Tawb:113]. Uharamu wa kumwombea msamaha umetegemezwa kwa yule anayeombewa msamaha kuwa amebainika kuwa katika watu wa Motoni, na maana ya hilo ni kwamba ikiwa haikubainika kwa anayeombewa msamaha, basi hakuna kizuizi cha kumwombe msamaha, pia anaweza kumwombea dua yule ambaye hakubaini ukafiri wake; kama kumpunguzia adhabu kama atakuwa katika watu wa Motoni; imepokewa kuwa baadhi ya watu wa Motoni watapunguziwa adhabu kwa baraka za Mtume S.A.W. hivyo hakuna kuzuia kutamani ukarimu wa Mwenyezi Mungu, bali hilo ni jambo halali, hivyo basi, hakuna kizuizi kumwombea baba yako na ndugu zako, wala hakukatazwi kuzuru makaburi yao.
Naye Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
