Kutoka katika Chumba cha Mtihani kwa Ajili ya Kuswali
Question
Kuna Chuo kikuu kimoja miongoni mwa Vyuo Vikuu vilivyopo hapa Cairo huwa kinatoa shahada ya uzamili katika Idara za Kazi za Kimataifa, na hufanyika mitihani kila ufikapo nusu ya muhula wa masomo na mwisho wake. Na aina ya wanafunzi wa chuo hiko ni wafanyakazi, na mitihani hiyo hufanyika kuanzia saa moja usiku mpaka saa tatu usiku, na baadhi ya wanafunzi huwa wanataka kutoka wakati wa mtihani ili kwenda chooni kutia udhu; jambo ambalo wanafunzi wengine ndani ya chumba cha mtihani na walio nje hupata shaka, na wengine hupiga simu au kughushi katika mtihani. Hivyo ninaomba nipate jibu iwapo kuna ulazima wa kutoka kwenye chumba cha mtihani kwa ajili ya Swala au hapana. Na pia ninaomba kujuwa iwapo mfumo kama huu upo katika Chuo Kikuu cha Al Azhar au haupo?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, Jamaa zake, Masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Swala ni nguzo ya Dini nayo ni nguzo ya pili baada ya Shahada mbili, na Mwenyezi Mungu Ameiwekea wakati maalumu ili itekelezwe na kuwalazimisha Waumini kuitekeleza katika nyakati hizo, nayo ni lazima na haina budi isipokuwa kuswaliwa tu. Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema, {kwani hakika Swala kwa Waumini ni faradhi iliyowekewa nyakati maalumu}[AN NISAA: 103]. Na Mwenyezi Mungu hakuiondosha kwa yeyote na kwa hali yeyote, kwa kuwa mtu baleghe, mwenye akili timamu na anayekalifishwa na sharia, hata katika hali ya ugonjwa ambayo mtu huwa hawezi hata kuinua kitu, na hata katika hali ya vita baina ya makundi mawili yanayozozana, haya yote ni kwa sababu ya umuhimu wa Swala katika maisha ya Muislamu.
Na sharia imeruhusu kupunguza Swala (idadi ya rakaa za Swala) na kuzikutanisha kwa baadhi ya mazingira, kwa mfano safari, na imeruhusu kuzikutanisha katika mazingira mengine kwa mfano kuwa na hofu kuwa ya mvua na wasiwasi (hali ya kuogopa) mkubwa. Na baadhi ya wanazuoni wakaliweka jambo hili kwa upana zaidi, wakasema kuwa inafaa kukusanya Swala mbili (kwa wakati mmoja) iwapo kuna usumbufu kwa mtu, kwa kuifanyia kazi Hadithi ya Mtume – rehema na amani zimshukie- iliyopokewa na Ibn Abbas– radhi za Mwenyezi Mungu ziwashukie- katika kitabu cha Muslim: "Mtume -rehema na amani zimshukie– amekusanya pamoja (ameziswali kwa wakati mmoja) baina ya Adhuhuri, Alasiri, Magharibi na Isha alipokuwa Madina bila ya hofu wala mvua." Ibn Abbas akaulizwa: “Kwa nini kafanya hivyo?” "Akajibu: “amefanya hivi ili asimweke mtu yeyote katika usumbufu (matatizo) katika watu wa umma wake.”
Imamu An Nawawiy anasema katika kitabu cha: [Sharhu Muslim 5/219, Ch., Dar Ihyau At Turath Al Arabiy]: "Baadhi ya kundi la Maimamu wamekubaliana kukusanya Swala kwa mkazi (asiye msafiri) kwa dharura isiyo ya kawaida, nayo pia ni kauli ya Ibn Sayriyn na Ash bah katika Wanazuoni wa Madhehebu ya Malik. Na Al khatwabiy ameeleza kutoka kwa Al qafali na Sha shiy Al kabiyr katika Wanazuoni wa Madhehebu ya Imamu Shafi kutoka kwa Is haq Al Maruziy kutoka kwa kundi la Wanazuoni wa Hadithi, na ameichagua Ibn Al-Mundhir na kuyatilia nguvu maneno ya Ibn Abbas: “Amefanya hivi ili asimweke mtu yeyote katika usumbufu (matatizo) katika watu wa umma wake.” Hapa hakuna tatizo la ugonjwa au kitu kingine chochote, Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye Ajuaye zaidi. "
Na Madhehebu haya ingawa ndiyo yatumikayo na inafaa kuyafanyia kazi wakati wa matatizo lakini kwa sharti la kwamba hatakiwi Muislamuu kufanya kuwa ndio kawaida –kama ilivyoelezwa katika maneno ya Imamu An Nawawiy– na haifai kuendelea na kitendo hicho isipokuwa wakati wa udhuru mkubwa wa kipindi cha Swala na mtu akalazimika kuichelewesha Swala ya Adhuhuri na kuiswali wakati wa Alasiri, Magharibi au Isha, namna ambayo atasali Sala zake ndani ya wakati wake kwa mfano iwapo mtu huyo anahofia Swala isije ikatoka katika wakati wake na akawa anahofia pia asije akapoteza kitu ambacho hataweza kukipata tena.
Na kwa hayo na kwa mujibu wa swali: Chuo kilichotajwa ni lazima kipange wakati maalumu wa mitihani wa nusu ya muhula na mwisho, kwa kutopingana na nyakati za Swala, kwa kufanya mwisho wa kumaliza mtihani iwe kabla ya kuingia kwa Swala nyingine kwa muda unaotosha ambao utamwezesha mwanafunzi kutia udhu na kuswali. Kwa mfano utatangulizwa mtihani kabla ya kuingia wakati wa Swala ya Magharibi ili waweze kuiwahi Magharibi na kabla ya kuingia Swala ya Isha. Au mtihani utacheleweshwa kidogo kwa ajili ya Swala ya Magharibi (wataswali, kisha wataingia katika chumba cha mtihani) ili waiswali Swala kwa wakati wake, na ikiwa haiwezekani kufanya mabadiliko ya wakati wa mtihani kwa kuchelewesha au kutanguliza na Chuo Kikuu kikawa hakiwezi kuwapa wanafunzi muda wa kufanya ibada ya Swala pamoja na kutoweza kuwazuia wasifanye kughushi basi kwa hali kama hiyo itafaa –kwa kuzingatia haja ya dharura iliopo– kufanyika mtihani kwa wakati wake na wala asiruhusiwe mwanafunzi kutoka, na wanafunzi wanaweza kukusanya kati ya Swala mbili –kwa kutanguliza au kuchelewesha. Kwa kuifanyia kazi Hadithi ya Ibn Abbas –radhi za Mwenyezi Mungu ziwashukie yeye na Baba yake– iliyokwishatajwa. Na kwa kuzingatia kuwa mitihani katika Chuo Kikuu cha Al-Azhar inachunga nyakati za Swala pamoja na nyakati za kufanyia mitihani.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
