Mke kusafiri na Mumewe Kwenda Nchi ya Uhamisho
Question
Muulizaji anasema kuwa ameolewa na mwanaume na ana binti naye. Alisafiri pamoja naye hadi Japani kwa muda wa mwaka mmoja, kisha akarudi Misri na kusafiri naye tena hadi Kanada kwa muda wa miezi miwili. Alirudi Misri kwa sababu ya kuogopa nafsi yake mwenyewe na binti yake kutokana na majaribu ambayo Waislamu wanakabiliwa nayo huko. Mumewe alikataa kumpatia matumizi yeye na bintiye kwa kisingizio kwamba hamtii. Afanye nini? Je, amtii na kwenda naye katika nchi ya uhamisho ambako Waislamu wanateswa na mateso ya kidini, huku akihofia majaribu kwa nafsi yake na binti yake, au afanye nini?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Uislamu umeweka wazi kwamba ndoa imejengwa juu ya utulivu, mapenzi na huruma. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema ndani ya Qur’ani Tukufu: {Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri} (Ar-Rum: 21)
Dini yetu ya kweli imeweka utiifu wa mume kuwa ni wajibu juu ya mke, na ikiwa mke hamtii mumewe, basi huyo ni muasi na hastahiki matunzo kutoka kwake. Kwa sababu mume anawajibika kutoa matunzo kwa mkewe kwa kumkabidhi nafsi yake mwenyewe kwa utiifu wa mumewe maadamu haihusishi kumuasi Mwenyezi Mungu.
Katika suala la swali, ikiwa safari ya mke na mume wake katika nchi ya uhamisho inahofiwa kuwa ni sababu ya kumtia mke katika majaribu kutokana na mateso ambayo yanaweza kusababisha kuacha dini, kufanya vitendo vilivyoharamishwa, na kulea binti mbali na mafundisho ya dini ya haki, basi inajuzu. Bali ni lazima mke asiende katika nchi ya majaribu ili kuhifadhi dini yake, na kwa kutosafiri naye si muasi. Kwa sababu sharti la kumtii mume ni kwamba isiwe katika kumuasi Mwenyezi Mungu - Mungu apishe mbali. Ndio maana Bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu – (S.A.W) – akasema: “Hakuna utiifu katika maasi, utiifu ndio ni katika wema tu”.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
