Mke anamsaidia baba yake kwa pesa zake mwenyewe.
Question
Je, mume ana haki ya kumzuia mke wake kutoa msaada wa kifedha kwa baba yake mzee ambaye hawezi kufanya kazi kwa pesa zake mwenyewe? Je, ni ipi hukumu ya Kiislamu kwa mume kutumia nguvu na jeuri kwa mkewe hadi kusababisha alama kwenye mwili wa mke na kutoa maneno yanayopingana na dini ya Kiislamu?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Ndoa katika Uislamu ni ahadi na mkataba baina ya wanandoa, yenye kufungamana kwa maisha yote, na kuunganisha baina ya wao kwa wao kikamilifu, kama Mwenyezi Mungu Asemavyo: {Wao ni vazi kwenu, na nyinyi ni vazi kwao.} [Al-Baqarah: 187] na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na mkitaka kubadilisha mke mahali pa mke, na hali mmoja wao mmempa chungu ya mali, basi msichukue katika hayo kitu chochote. Je, mtachukua kwa dhulma na kosa lilio wazi?} [20]. Na mtachukuaje na ilhali mmekwisha ingiliana nyinyi kwa nyinyi, na wao wanawake wamechukua kwenu ahadi iliyo madhubuti?} [An-Nisa: 20-21]
Mwenyezi Mungu Mtukufu aliifanya ndoa kuwa ni miongoni mwa neema zake na akaihesabu kuwa ni miongoni mwa ishara zake, kama alivyosema Mwenyezi Mungu: {Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri} (Ar-Rum: 21) na Mwenyezi Mungu akasema: {Na Mwenyezi Mungu amekuumbieni wake katika jinsi yenu, na akakujaalieni kutoka kwa wake zenu wana na wajukuu, na akakuruzukuni vitu vizuri vizuri. Basi je, wanaamini upotovu na wanazikataa neema za Mwenyezi Mungu?} [An-Nahl: 72], basi Mtunga sharia mwenye hekima aliamrisha kutendeana mema baina ya wanandoa, na akabainisha haki na wajibu wa kila mmoja wao katika mahusiano ya ndoa, hivyo ni wajibu kwa wanandoa wote wawili kumcha Mwenyezi Mungu Mtukufu katika yale ambayo ni wajibu kwa kila mmoja wao kwa mwenzake. Inafaa kuashiria hapa kwamba mke ana haki juu ya mumewe na wajibu kwake kwamba mke anastahiki kupata matunzo ya kisheria kutoka kwa mumewe, ambayo ni kila kitu ambacho mke anakihitaji kwa ajili ya maisha yake, kama vile chakula, mavazi, nyumba na huduma, na anachohitaji katika samani, blanketi, na vitu vingine vya nyumbani kulingana na desturi za watu. Sababu ya wajibu wa matunzo haya ni haki ya mume katika uhifadhi wa mke wake kwa ajili yake na kuingia kwake katika utiifu wake. Hii ni ili mume amfurahie mkewe na kupata matunda ya ndoa hii. Ikiwa uhifadhi huu hautafikiwa, basi mke hastahiki matunzo kwa mujibu wa sharia ya Kiislamu. Kwa sababu basi atakuwa anamuasi bila haki na hangestahili matunzo. Kwa hiyo, mke wa Kiislamu lazima amtii mumewe katika kila jambo lisilohusisha kumuasi Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Wanachuoni wa Fiqhi wengi wameamua kuwa mke ana utu wake wa kiraia na hadhi yake ya kifedha isiyotegemea utu na hadhi ya mumewe. Kila mmoja wao ana hadhi yake ya kifedha inayojitegemea. Mke ana uwezo wa kufunga mikataba na haki ya kumiliki mali. Ana haki kamili na uwezo kamili wa kubeba majukumu na kufunga mikataba mbalimbali, huku akihifadhi haki yake ya kumiliki mali mbali na mume wake.
Mfumo wa fedha za wanandoa katika Uislamu ni mfumo wa utengano kamili na uhuru wa kifedha wa kila mmoja wao kutoka kwa mwingine. Misingi hii imeanzishwa na Qur`ani Tukufu katika aya nyingi, kama vile Aya za 228 na 229 za Surat Al-Baqarah na Aya za 4, 20 na 21 za Surat An-Nisaa. Kwa hiyo, mume Muislamu hana haki ya kumzuia mke wake kumsaidia baba yake mzee ambaye hawezi kufanya kazi kwa msaada wa kifedha kutoka kwa pesa zake mwenyewe. Bali, mke ana haki ya kumtumikia baba yake ikiwa hatapata mtu mwingine wa kumtumikia, kumsaidia na kumtumikia, hata kama yeye si wa dini yake. Nasaha zetu kwa kila mume Muislamu ni kumtendea mema mke wake na kuchunga uadilifu na wema katika kuamiliana naye. Mwenyezi Mungu Anasema: {Na kaeni nao kwa wema, na ikiwa mmewachukia, basi huenda mkakichukia kitu, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ametia kheri nyingi ndani yake} [An-Nisa’: 19] Na Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) amesema: “Mcheni Mwenyezi Mungu juu ya wanawake, kwani mmewashika kwa ahadi ya Mwenyezi Mungu, na mmeruhusiwa kustarehe pamoja nao kujamiiana kwa maneno ya Mwenyezi Mungu, wao wana haki ya riziki na mavazi juu yenu, kwa wema”.
Nasaha zetu kwa kila mke wa Kiislamu ni kumtii mumewe katika mambo yote ya ndoa ambayo hayahusishi kumuasi Mwenyezi Mungu Mtukufu, na pia katika yale ambayo ni muhimu kuwatunza na kuwalea watoto watakaowapata. Ama mambo mengine ambayo ni ya siri kwake, si wajibu kumtii katika hayo, kama vile akimzuia asitoe pesa zake au kumwamuru azitoe kwa njia maalumu, kwa sababu hana ulezi juu ya fedha zake. Mwenyezi Mungu atusaidie sote kuelewa mafundisho na hukumu za Uislamu na atuongoze sote kwenye njia iliyo sawa.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
