Kuzitia Rangi Nyusi
Question
Ni ipi hukumu ya kuzitia rangi nyusi?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba zake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Makusudio ya ibara ya (kuzitia rangi nyusi) ni kuziweka rangi ncha mbili za nyusi, ambapo mtazamaji hudhani kuwa nyusi ni nyembamba na nyepesi; kwa sababu ncha mbili za nyusi ya juu na ya chini zinakuwa hazionekani, na kwa kawaida rangi inayotumika inalingana na rangi yenyewe ya ngozi, na pengine kutiwa rangi juu ya nyusi zote kwa rangi ya ngozi, kisha zinachorwa kwa kalamu nyusi nyembamba na nyepesi; na pengine michoro hii inatumika kwa njia ya tatuu ambayo; na pengine unatumika unga wa madawa na rangi za viwandani, na makusudio ya hayo yote ni urembo tu.
Lakini kama rangi hii inatumika kwa tatuu basi ni haramu kabisa, na mwenye kufanya hivyo amelaaniwa, na ni mwenye kufanya dhambi kubwa. Na dalili ya hili ni kama ilivyopokelewa katika Vitabu Sahihi vya Sunna vya Bukhari na Muslim, kutoka katika Hadithi ya Ibn Umar, kuwa mtume S.A.W, anasema: “Mwenyezi Mungu amemlaani mwenye kuunga na mwenye kuungwa (nywele), na mwenye kuchora tatuu kuchorwa tatuu”. Na ahadi ya laana ni alama ya kuwa dhambi hiyo ni kubwa.
Na kama rangi hii inayotumika kwa mada za mapambo kama vile rangi za viwandani, hakika mtazamo wa Fiqhi unatofautiana kuhusu msingi wake, na kwa katika hukumu yake. Ni dhahiri kuwa msingi wa tofauti ni mambo mawili:
Kwanza: je inakatazwa kufanywa; kwa kuwa ni sababu ya kuzichonga nyusi? hakika kuzitia rangi nyusi kwa kutumia mada za viwandani zinazojulikana, ambapo nywele za nyusi hazirejei katika hali yake ya kawaida bali huzidisha wingi wa nywele, na hukuwa kwa haraka, na hii hupelekea kuziondosha ziada, na hii ndiyo ni hali ya kuzichonga nyusi.
Pili: Je kuzitia rangi nyusi ni miongoni mwa maana ya kuzichonga nyusi na kwa maana yake huchukua hukumu yake au la?
Kuhusu ya kwanza: iliyotahadharishwa na kuhofiwa, kuongezeka ukubwa wa nywele, na hilo si jambo la kawaida wala la kuainishwa, kwani miongoni mwa masharti ya kufanyia kazi kuzuia uovu (Sadd Al dhariia) kuwa kunapelekea kufanya lililokatazwa kwa yakini au kwa asilimia kubwa.
Kuhusu ya pili: Kauli ya kuwa kuzitia rangi nyusi ni aina ya kuzichonga nyusi, kunanategemea kujua mambo haya mawili ni aina moja au la kwanza linalingana na la pili kwa njia ya Qiyasi. Linalokubaliwa na wanazuoni wa Madhehebu mnne kuwa kuzichonga nyusi kunaambatana na nyusi tu, mbali na sehemu ya uso iliyosalia, Kisha wamekubaliana, isipokuwa wafuasi wa madhehebu ya Hanbal, ni kwamba hilo ni kwa kunyonyoa au mfano wake miongoni mwa njia za kuziondosha, kinyume na wafuasi wa madhehebu ya Hanbal ambao wanaiainisha kuwa ni kunyonyoa, na siyo njia nyingine.
Kuna mtazamo wa kuelekea kuwa: Je makusudio ya hali ya kuziondosha yanaambatana na kuzifanya nyusi ziwe nyembembe, au ni hali ya kuziondosha tu bila ya kuwa nyembemba?
Wanazuoni wengi, isipokuwa wafuasi wa madhehebu ya Hanbal, wameeleza kuwa ni kuziondosha pamoja na kuwa nyembamba, na Ibn Al-Humam katika kitabu cha [Fat-h Al-Qadiir] anasema: “Mwenye kuchonga nyusi ni yule anayenyonyoa nyusi kwa ajili ya kuwa nyembamba”. [6/426]; na katika kitabu cha: [Al-Mjmuu’ na An-Nawawiy: “mwenye kuchonga nyusi ni yule anayechukua sehemu ya nywele za nyusi na kuifanya nyembamba ili iwe nzuri’. [3/141]; na katika kitabu cha [Hashiyat Al-jamal]: “ Kuchonga nyusi kumekatazwa kwa mwanamke aliyekwenye eda”. [4/460]; na An-Nafarawiy mfuasi wa madhehebu ya Malik katika kitabu cha [Al-Fawakih Ad-Dawaniy] anasema: “kuzichonga nyusi ni kuzinyonyoa nywele za nyusi ili ziwe nyembamba na nzuri”. [2/314].
Inapaswa kuzingatiwa kuwa kinachoathiri katika unyonyoaji wa nyewele za nyusi - kwa kauli ya Wanazuoni wengi - ni kupunguza unene wala si kuondoa tu. Hukumu ya kisharia kuhusu kuchukua sehemu ya nyusi kwa ujumla bila kuzipunguza unene ni tofauti na hukumu ya unyonyoaji; kwa sababu si kila kuchukua sehemu ya nyusi kunachukuliwa kuwa ni unyonyoaji. Wanazuoni wa madhehebu ya Hanafi na Hanbali wamesema kuruhusu kuchukua sehemu ya nyusi ikiwa zimekuwa ndefu sana. Ama Wanazuoni wa Madhehebu ya Maliki na Shafi wamesema kuchukiza kufanya hivyo wala si kuharamisha.
Na ikiwa unyonyaji wa nyusi ni kuondoa nywele za nyusi kwa lengo la kupunguza unene, basi haingii katika maana yake upigaji rangi, kama isivyofichikana.
Kuhusu kauli ya kusihi kufanya Qiyasi cha kuzitia rangi nyusi kwa kuzichonga nyusi, kauli hii inategemea kuelewa sababu ya kuharamisha kuzichonga nyusi, ambayo Wanazuoni wametofautina.
Na kwa kurejea Vitabu vya Fiqhi vya Madhehebu manne, tunaona kuwa wao wametofautina katika kubainisha sababu; wanazuoni wa madhehebu ya Hanafi walitaja kuwa sababu ni kuonesha mapambo, na kwa mujibu wa hayo haiharimishwi ila katika hali ya mapambo; na baadhi ya wafuasi wa Madhehebu ya Shafi na ya Hanbal walitaja kuwa sababu ni kughushi; na baadhi ya wafuasi wa madhehebu ya Hanafiy wanaona kuwa sababu ya kuharamisha ni kuwa kuna maudhi; na baadhi ya wafuasi wa madhehebu ya Hanbal wanasema kuwa: Ni alama ya wanawake waovu; na baadhi ya wanazuoni wanaona kuwa sababu ni kubadilisha uumbaji wa Mwenyezi Mungu, na dalili ya hayo ni muktadha wa Hadithi ya Ibn Masu’ud: “Mwenyezi Mungu amewalaani wenye kuchora tatuu, na wenye kupigwa chale, na wanaochonga nyusi, na wanaochonga meno, wakaacha mwanya kwa sababu ya uzuri, wanaobadilisha maumbile aliyoyaumba Mwenyezi Mungu…”. [Muttafaq].
Kwa kuchukuliwa kuwa sababu ya kukataza kuzichonga nyusi ni kudhuru ya mwili, hakika hayo hayadhihiriki katika hali ya kuzitia rangi nyusi, hasa katika hali ya maendeleo ya ufundi wa watu wanaoshughulika na kazi hii.
Na kuhusu maelezo ya baadhi ya wanazuoni kuwa kuzichonga nyusi ni alama ya mafasiki au inabadilisha uumbaji wa Mwenyezi Mungu, hakika hii haisihi iwe maelezo, lakini ni miongoni mwa hekima zenye faida kwa kuelewa kusudio la kukataza, na siyo sababu ya lazima. Kwa hiyo kundi la Wanazuoni waliyapinga maelezo kama haya, miongoni mwao ni Al-Qarafiy na Al-A’adawiy wafuasi wa Madhehebu ya Malik; katika kitabu cha: [Adh-Dhakhirah] cha Al-Qarafiy anasema: “Ilivyotajwa katika Hadithi kuhusu kubadilisha uumbaji wa Mwenyezi Mungu, hakika sikuifahamu maana yake, kwa sababu mabadiliko kwa ajili ya uzuri hakatazwi kisharia, kama vile: tohara, kukata kucha na nywele, kupaka Hina, kuzipaka hina nywele, na mengineyo”. [13/315; Ch. ya Dar Al-Gharb Al-Islamiy].
Na At-Twahir Ibnn A’ashuur katika Tafsiri yake anasema: “Hayazingatiwi kuwa kubadilisha uumbaji wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, yanavyofanywa katika kwa watu katika yale aliyoruhusu mwenyezi Mungu, na yanayoingia katika maana nzuri; hakika tohara ni kubadili uumbaji wa Mwenyezi Mungu lakini kwa faida ya kiafya, kuzinyoa nywele kwa ajili ya kuepusha madhara, kuzikata kucha kwa ajili ya kurahisisha kazi za mikono, kutoboa matundu ya masikio ya wanawake kwa ajili ya kuweka hereni na urembo.
Na kuhusu ilivyopokelewa katika Sunna kuambatana na kulaani wanaounga nywele, wanaochonga nyusi, wanaochonga meno kwa uzuri, hakika hayo yote miongoni mwa masuala ya kutofautiana”. Kisha akahitimisha kuwa kusudio la kukataza kuwa makatazo haya yalikuwa miongoni mwa alama za mafasiki wa zama hizo, au za washirikina. [5/205, Ch. ya Ad-Dar At-Tunusiyah Linnashr], na kwa mujibu wa hayo, ni dhahiri kuwa suala la kuzitia rangi nyusi halilingani na suala la kuzichonga nyusi hata kidogo katika katazo pia.
Ama kwamba kuzitia rangi nyusi kuwa ndani yake kuna maana ya kuonesha mapambo na aina ya kughushi ni sahihi, na kwa hiyo hupewa hukumu ya uharamu, kutokana na kauli ya wafuasi wa madhehebu ya Hanafi na ya Shafi, na Madhehebu haya mawili yameondoa hukumu ya uharamu wa kuzichonga nyusi ikiwa kwa ajili ya mume, na kauili ni hiyohiyo katika kuzitia rangi nyusi. Panaweza semwa: kipimo hili kinapinga maelezo ya wafuasi wa Madhehebu ya Shafi kumkataza mwanamke alie kwenye eda, kuzitia rangi nyusi, kutokana na ilivyotajwa katika kitabu cha: [Sharh Al-Manhaj] na Sheikh Zakariya Al-Answariy: “kuacha kutumia rangi zinazowekwa usoni, mikononi, miguuni, kama vile Hina na zafarani n.k… na hii inakusanya vidole, paji la uso, nywele, na nyusi”.
Katika kitabu cha Al-Bijirmiy: “Na kama mwanamke alie kwenye eda amekatazwa kufanya hivyo, hakika ni kwa kuwa hayo ni mapambo na siyo haramu, na hii inamaanisha kuwa inajuzu kwa asiye kwenye eda kulifanya, kwa sababu ikiwa ni haramu kimsingi, basi hakuna haja ya kuitaja katika maandiko haya ikiwa imekatazwa kabisa.
Hili linajibiwa kuwa, Pamoja na kukubali hilo, isipokuwa kujuzu kutia rangi nywele ni maalumu kwa mume na kwa ruhusa yake.
Kwa mujibu wa yaliyotangulia: tunaona kuwa rai yenye nguvu zaidi ni: Kujuzu kuzitia rangi nyusi, kwa kuangalia vigezo vilivyotajwa hapo juu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
