Hukumu ya vitendo vya kujiripua dhi...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya vitendo vya kujiripua dhidi ya raia

Question

Ni Ipi hukumu ya mashambulizi ya mabomu yanayotokea katika baadhi ya nchi, ambayo yanawalenga raia wasio wapiganaji dhidi ya Waislamu? Na mashambulizi haya yamenasibishwa na baadhi ya makundi yanayodai kuwa ya Kiislamu, na baadhi ya wanaoyaunga mkono wametamka uhalali wake. Je, anayefanya mashambulizi haya anahesabiwa kuwa shahidi?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Hapana shaka kwamba matendo ya kulipua yanayowalenga raia ni haramu kisharia, na hayana uhusiano na Uislamu kwa njia yeyote ile (ya mbali wala ya karibu). Badala yake, ni miongoni mwa madhambi makubwa ambayo sharia imemuahidi mtendaji adhabu kali, kwa sababu kadhaa, ikiwa ni pamoja na:

Kwanza, ni kumwaga damu kwa njia ya haramu (kinyume cha haki), na kuua raia wasio na hatia, Waislamu au wasiokuwa Waislamu, ambao Allah ameharamisha kuwaua isipokuwa kwa haki. Sharia inatilia mkazo na kuogopesha kumwaga damu ya mtu au kuingilia uhai wake bila haki, kama ilivyoelezwa katika Qur'ani Tukufu: {wala msiue nafsi ambayo Mweneyzi Mungu ameharamisha ila kwa haki} [Al-An'am: 151].  Na mwenyezi Mungu akafanya kuua nafsi sawa iwe ya Muisilamu au asiye Muisilamu bila ya haki ni kuua nafsi zote.

na pia amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {kwa ajili hiyo, tumeandika juu ya wanaisraeli kuwa yule anaeua nafsi bila sababu ya haki au ufisadi katika ardhi, ni kama aliyeua watu wote, na yule anaehifadhi (anayehuisha) maisha yake ni kama anavyohifadhi maisha ya watu wote} [Al-Ma'idah: 32]

Pili: Kwamba inahusisha kuua wasio na hatia, kwani Abu Dawood na Al-Hakim wamepokea kutoka kwa Abu Huraira - Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - akisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.) amesema: «Muumini hawezi kutekeleza fitna, kwani imani inazuia fitna».

Akasema Ibn al-Athir katika kitabu chake "An-Nihaya": «Fitna ni mtu kumjia mwenzake akiwa ameghafilika na hajui kinachoendelea, kisha kumshika na kumuuwa».

Maana ya Hadithi hii ni kwamba imani inazuia fitna kama vile pingu inavyoshikilia na kuzuia mtu kutenda vitendo vibaya. Na maneno ya Mtume (SAW): “Mumini hawezi kutekeleza fitna” ni taarifa ambayo ina maana ya kukataza, kwani inahusisha hila na udanganyifu, au ni katazo lenyewe.

Na Waislamu wa mwanzo walifahamu haya maadili ya juu na kuyazingatia, walipiga mifano bora zaidi katika historia. Miongoni mwa hayo ni Hadithi ya Khubaib Al-Ansari - Radhi za Mweneyzi Mungu ziwe juu yake - ambayo imepokelewa na Bukhari katika Sahihi yake, ambapo alikamatwa na washirikina kama mfungwa pamoja na Ibn Dathina, kisha akauzwa Makkah, na akanunuliwa na familia ya Banu al-Harith bin Amir bin Naufal bin Abd Manaf. Khubaib alikuwa ndiye aliyemuuwa Al-Harith bin Amir siku ya Vita vya Badr, na alikaa kwao kama mfungwa. Siku moja aliazima jembe kutoka kwa binti ya Al-Harith ili kujitunza, akamuazima, akalichukua mtoto wake hali ya kuwa ameghafilika, na alipokuja binti yake aliona jambo hilo na alishtuka sana, kisha akamwambia Khubaib: "Je, unadhani nitaweza kumuua?" Khubaib akajibu: "Sijawahi kufanya hivyo." Binti ya Al-Harith alisema: "Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, sijawahi kuona mfungwa bora zaidi kuliko Khubaib…"  hadi mwisho wa Hadithi. Hii ni Hadithi ya mtu mfungwa wa Kiislamu aliye mikononi mwa maadui zake wanaopanga kumua, lakini hata hivyo, wakati alipokuwa na nafasi ya kulipiza kisasi kwa kuua mtoto wao, alikataa kufanya hivyo kwa sababu maadili ya Muislamu hayawezi kujumuisha hila au kudanganya wale walioghafilika.

Na ikiwa haifai wakati wa vita halisi kuua wanawake wasiokuwa wapiganaji, watoto, wazee wanyonge, na wafanyakazi wasiohusika na vita, basi katika hali nyingine ni makato zaidi.

Mwenyezi Mungu anasema: {na piganeni katika njia ya mwenyezi mungu wale wanaokupiganieni, na msizidi hipa (msifanye uadui), kwani Mwenyezi Mungu hawapendi wafanyao uadui} [Al-Baqara: 190]. Hii inamaanisha kwamba msiwauwe wazee, wanawake na watoto.

Na pia, imeripokewa na At-Tirmidhiy kutoka kwa Suleiman bin Bureida kutoka kwa baba yake kwamba alisema: "Mtume (S.A.W.) alipokuwa akituma  Amiri (kiongozi) wa jeshi, alimuhimiza hasa kumcha Mwenyezi Mungu na kuwa na huruma na Waislamu wakiwa pamoja naye, na alisema: 'Piganeni kwa jina la Mweneyzi Mungu Mtukufu, na katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, piganeni na wale wanaomkufuru Mwenyezi Mungu Mtukufu, piganeni lakini msichukue nyara, msivunje ahadi, msifanye udhalilishaji, na msimuue mtoto mdogo.'.

Imepokewa na Ahmad katika Musnad yake kutoka kwa Al-Marqaa' bin Sayfi kutoka kwa babu yake Raba' bin Al-Rabi' ndugu wa Hanzala, ambaye alimueleza: "kwamba alitoka na Mtume wa Mweneyezi Mungu (S.A.W.) katika vita moja ambayo mbele yake alikuwa Khalid bin Walid. Walipokuwa wanapita, waliona mwanamke aliyeuawa kutokana na mashambulizi ya mbele ya jeshi. Walisimama kumtazama na kushangaa juu ya muonekano wake, mpaka alipofika Mtume wa Mweneyzi Mungu (S.A.W.) akawafikia kwa ngamia wake na Alisimama juu ya huyo mwanamke na kusema: 'Huyu hakupigana.' Kisha akamwambia mmoja wao: 'Nenda kwa Khalid, umwambie asiue watoto wala wafanyakazi.'"

Na Imamu An-Nawawi katika sharh ya Sahih Muslim alisema: "Wanazuoni wamekubaliana kwamba ni haramu kuuwa wanawake na watoto kama hawapigani."

Ikiwa tutazingatia kwamba sababu ya vita ni mapigano, basi kila anayekosa kupigana atahesabiwa kama waliotajwa katika maandiko ya kisharia kama vile vipofu, wagonjwa wa kudumu, wendawazimu, wakulima na mfano wao. Hawa huitwa katika istilahi ya kisasa "raia." Hivyo, haitaruhusiwi kuwadhuru au kuharibu mali zao, mbali na kuwaua. Kuua raia ni miongoni mwa makosa makubwa.

Tatu: Kinyume na malengo ya kisharia:

Sharia tukufu imesisitiza umuhimu wa kulinda mambo matano ambayo dini zote zimekubaliana juu ya ulazima wa kuyatunza, nayo ni: dini, nafsi, akili, heshima na mali, na haya huitwa malengo matano ya kisharia.

Ni dhahiri kwamba mashambulizi ya kigaidi yanayohusika yanaenda kinyume na baadhi ya malengo haya muhimu ya kisharia, ikiwa ni pamoja na lengo la kulinda nafsi. Aliyeuawa ni raia ambaye hahusiki na ana uangalizi na hakufanya kosa lolote. Ana roho iliyo na heshima na ni haramu kumdhuru, na inahitajika kulindwa. Mwenyezi Mungu Mtukufu ameonesha ukubwa wa roho ya binadamu, akisema: {Mwenye kuua nafsi bila ya haki au kwa uharibifu duniani, basi ni kama aliyeua watu wote, na mwenye kuhuisha nafsi moja, basi ni kama aliyehuisha watu wote} [Al-Ma'idah: 32]

Vilevile, mashambulizi haya ya kigaidi yanakwenda kinyume na lengo la kulinda mali; hakuna shaka juu ya madhara yake ya uharibifu wa mali, majengo, na mali za umma na binafsi. Uharibifu wa mali na kupoteza mali ni jambo ambalo sheria imelifanya haramu, na uharamu huu unakuwa mkubwa zaidi na kuongezeka pindi mali iliyoharibiwa haimilikiwi na aliyeiharibu, bali ni mali ya mwingine kama ilivyo hapa. Hivyo, uharamu huu unahusiana na ukiukwaji wa amri ya sharia kwa upande mmoja, na haki za viumbe wengine kwa upande mwingine.

Kuhusu mtenda mashambulizi ya kujitolea ambaye anajiingiza mwenyewe kwenye kifo kwa kujifunga na mabomu au namna nyingine, yeye anahusiana na kauli ya Mtume (S.A.W) katika Hadithi iliyosimuliwa na Abu Awanah kutoka kwa Thabit bin Dhahhak R.A) ambapo amesema: "Anayejiua kwa kitu chochote duniani atateseka kwa hicho hicho Siku ya Kiyama."

Imam Muslim alisimulia kutoka kwa Abu Huraira (R.A) kwamba Mtume (S.A.W) alisema: "Anayejiua kwa chuma, basi chuma hicho kitakuwa kikiwa katika mkono wake, na atajichoma tumbo lake nalo, akiwa ndani ya moto wa Jahannam milele, na anayekunywa sumu na kujiua, basi atakuwa anainywa sumu hiyo katika moto wa Jahannam milele, na anayejitupa kutoka kwenye mlima na kujiua, basi atakuwa akijitupa katika moto wa Jahannam milele." Imamu Nawawi aliweka mlango kwenye Hadithi hii katika maelezo yake ya Sahihi Muslim, akisema: "Mlango: Ukubwa wa kuharamisha kujiua, na kwamba anayejiua mwenyewe kwa kitu atateswa kwa hicho katika moto."

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi

Share this:

Related Fatwas