Hukumu na adhabu ya watumiaji wa dawa za kulevya
Question
Je, uharamu wa dawa za kulevya umekubaliwa katika sharia ya Kiislamu, au ni miongoni mwa maeneo yenye kutofautiana baina ya Wanachuoni wa Fiqhi? Je, ni ipi hukumu kwa watumiaji wa dawa za kulevya? Je, kuna adhabu maalumu ya kisharia, kama vile kunywa pombe, uzinzi, wezi na mengineyo?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Madawa ya kulevya ni neno lenye maana ya vitu vinavyosababisha usingizi au hali ya kuzima hali ya mwili au akili. Neno hili linatokana na neno "khadra" ambalo lina maana nyingi, ikiwa ni pamoja na: kuficha au kufunika, kwa mfano, kusema "mwanamke ni aliyesitirika" kumaanisha kwamba anafichwa kwa kanga yake. Pia lina maana ya giza zito, uchovu, kupungua nguvu na kulegea pamoja na mvua na mawingu. Pia kuchanganyikiwa.[i]
Hivyo, kutokana na maana hizi za kilugha na madawa ya kulevya kuna uhusiano mkubwa ikiwa ni hali ya kuzima akili, kutia giza katika moyo kama mawingu yanavoziba mwanga wa jua, na kuchochea uchovu. Hali ya mtumiaji wa madawa ya kulevya inaathiri akili, moyo, na mwili wake kwa njia ya giza na kuchanganyikiwa[1].
Hakuna tofauti kati ya ufafanuzi wa madawa ya kulevya katika istilahi ya kifiqhi na maana yake katika lugha. Imamu Al-Qarafi alielezea kuwa ni kile kinachofunika akili na hisia bila kuambatana na furaha au shangwe[2].
Vilevile, Mwanachuoni Ibn Hajar Al-Haytami alielezea kuwa madawa ya kulevya ni kila kinachosababisha kufunika akili na kupoteza hisia katika mwili au uchovu, na kinachochochea kinyume cha furaha, shamrashamra, hasira, na uchangamfu.[3]
Madawa ya kulevya katika istilahi ya kisayansi ya kisasa ni: "Kila aina ya malighafi, iliyotengenezwa au iliyozalishwa ambayo matumizi yake husababisha hitilafu katika kazi za mfumo mkuu wa neva, iwe kwa kuupooza au kuchochea mwili au kusababisha hali ya kuona au kusikia vitu visivyokuwepo (kuhisi maoni ya uongo) jambo ambalo huathiri akili na hisia, na kusababisha uraibu. (ulevi sugu)
Itagundulika kuwa maana za kifasihi, kifiqihi, na kisayansi kuhusu madawa ya kulevya zinakaribia kuwa ni sawa, na maana kuu ya pamoja kati ya maelezo haya ni kwamba madawa ya kulevya husababisha kupoteza hisia au uchovu.
Ni muhimu kutambua kwamba madawa ya kulevya hayakuwa yakijulikana wakati wa Wanachuoni wa Fiqhi wa awali hadi mwishoni mwa karne ya sita. Kuhusu hili, Sheikh Ibn Taymiyyah anasema: "Hawakuzungumzia waliotangulia hasa kuhusu madawa ya kulevya; kwa sababu utumiaji wake ulianza hivi karibuni, na kwa hivyo Maimamu wanne hawakusema juu yake, kwani yalijitokeza mwishoni mwa karne ya sita na mwanzoni mwa karne ya saba wakati wa kuibuka kwa Taifa la Watatari.[4]"
Na dalili za kisharia zinaonesha kwamba matumizi ya madawa ya kulevya ni haramu na ni marufuku…
Miongoni mwa dalili za kisharia ni kama ifuatavyo:
Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema katika Qur'ani Tukufu: {wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo} (Albaqarah:195) na {Wala msijiuwe, hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwarehemuni.} (Al Nisaa 29). Aya hizi zinakataza kudhuru nafsi, kuitia nafsi katika hatari, na kutaka kuilinda nafsi kutokana na madhara. Kwa kuwa kulinda nafsi na akili ni miongoni mwa malengo makuu matano katika Uislamu, kila kitu kinachoweza kuondoa akili au kudhuru nafsi kimeharamishwa katika Uislamu. Na kama inavyofahamika, matumizi ya madawa ya kulevya ni uharibifu wa wazi na kutia nafsi katika hatari.
Imamu Ibn Ashour akitoa maelezo kuhusu Aya ya kwanza alisema: Kutumika kwa neno “msijitie” katika muktadha wa katazo kunamaanisha kila aina ya kutia nafsi katika hatari kwa makusudi, na hivyo ni haramu isipokuwa kuwepo na jambo linalohalalisha kuondoa katazo hili[5]."
Hadithi hii ni uthibitisho wa kuharamisha matumizi ya madawa ya kulevya, kwa sababu ni miongoni mwa vitu vinavyoleta uchovu na kudhoofisha akili, na kanuni ya Wanazuoni wa kifiqhi wanasema kuwa wakati katazo linapotolewa kwa vitu viwili vinavyohusiana, na kisha sharia ikasisitiza kuhusu moja, basi nyingine inapaswa kupewa sharia hiyo hiyo kutokana na kuunganishwa kwao katika muktadha na katazo. Katika Hadithi hii, mufattir ameunganishwa na kinywaji kinacholevya, na kwa hivyo, kwa kuthibitishwa kwa uharamu wa ulevi kupitia Qur'ani Tukufu, Sunna, na Ijmaa, ni lazima mufattir pia ipate hukumu hiyo kwa kuunganishwa kwa katazo hilo[6].
Ikiwa kuunganishwa kati ya sentensi kamili huru, basi maana ya kuunganishwa kuhusu kushiriki katika habari au hukumu ni tofauti, na maoni ya Wanazuoni wengi ni kwamba kuunganishwa katika muktadha huu kuna maana dhaifu. Hata hivyo, kuunganishwa kwa sentensi isiyo kamili au maneno kwa sentensi kamili kunaonesha kwa nguvu kwamba kunahusisha kushiriki katika habari na hukumu.
Anasema Imam al-Zarkashi: "Lakini ikiwa kilichounganishwa hakina habari, hakutakuwa na tofauti katika kushiriki na cha kwanza, kama vile kusema: 'Zaynab ni mwenye kuachwa na Amru'; kwa sababu kuunganishwa kunalazimisha kushiriki, na mfano wake ni kuunganishwa kwa maneno[7]."
Sheria za Kiislamu pia zinasema kwamba matumizi ya madawa ya kulevya ni haramu, kwani imethibitika kupatikana kwa uraibu wa madawa haya na yanadhuru kiroho na kimwili, na kila kitu kinachodhuru ni haramu; kama ilivyo katika Hadithi: "Usijidhuru wala usidhuru wengine." (Imepokewa na Ahmad, Ibn Majah, na Al-Hakim na imeisahihisha). Pia, matumizi ya madawa ya kulevya yanapingana na malengo ya sharia ya Kiislamu katika kulinda akili, nafsi, na mali, ambayo ni miongoni mwa mahitaji ya lazima ya Kiislamu.
Wanawazuoni wa Kiislamu wamekiri kuwa matumizi ya madawa ya kulevya ni haramu, na Imamu Al-Qarafi Al-Maliki katika "Al-Furuq", Sheikh Ibn Taymiyyah al-Hanbali katika "Al-Fatawa", na alama Ibn Hajar Al-Haytami katika "Al-Zawajir[8]" wametaja hilo kama moja ya madhambi makubwa.
Haifichiki kuwa hii ni kwa dharura isiyo ya lazima; kwani uharamu huu unakwenda mbali ikiwa madawa ya kulevya yatatumika kama tiba, na hiyo hutolewa na daktari mtaalamu anayeaminika kwa ufanisi na uaminifu. Anasema Imamu Al-Nawawi: "Kila kitu kinachozuia akili isipokuwa vinywaji kama vile bangi ni haramu. Ikiwa kuna hitaji la kuondoa akili kwa ajili ya kukata mkono unaoathirika, je, inaruhusiwa? Nasema, inaruhusiwa kwa hakika, na kama kuna tiba inayohitaji kuondoa akili kwa madhumuni sahihi, basi ni halali kutumika bila shaka.[9]"
Na haramu ya madawa ya kulevya haiishii tu kwa matumizi yake, bali pia inajumuisha kilimo chake na biashara yake. Kwani Sharia ilipoharamisha divai, pia iliharamisha kila sababu inayosababisha kuenea kwake. ikilaani mtengenezaji wake, mnunuzi wake, mnywaji wake, thamani yake yake, mkamuaji wake, na kinachokamulia, na anayeibeba, na anayebebewa. Hivyo inafananishwa na madawa ya kulevya kwa vile vinashirikiana katika kumfanya mtu kutokuwa na akili.[10].
Anasema \Mwanachuoni Ibn Hajar: "Ikiwa imebainika kuwa hizi zote ni vinywaji vinavyolevya au madawa ya kulevya, basi matumizi yake ni dhambi kubwa na ni uovu kama vile divai. Kila kinachotajwa katika onyo la mnywaji wa divai kinahusu pia mtumiaji wa kitu chochote kati ya hivi vilivyotajwa, kwa sababu vyote vinashiriki katika kuondoa akili, ambayo ni lengo kuu la Sharia (Akili) iwepo, kwani ni chombo cha kuelewa yatokayo kwa Mungu Mtukufu na Mtume wake (S.A.W) na ndiyo kinachotofautisha binadamu na wanyama, na njia ya kufikia ukamilifu badala ya mapungufu. Hivyo, kutumika kwa kile kinachozuia akili kunahusisha adhabu ya divai.[11]"
Tumesema "kuzuia akili kwa jumla" kwa sababu kuna tofauti kati ya madawa ya kulevya na vilevya (vinywaji vinavyolevya). Madawa ya kulevya siyo miongoni mwa vilevya, na hili limewekwa wazi na Wanazuoni wa Madhehebu ya Maliki, na limeelezwa na Imamu Al-Qarafi katika "Al-Furuq" na Imamu Ibn Al-Hajj katika "Al-Madkhal". Imamu Al-Qarafi anasema: "Tofauti kati yake ni kwamba anayetumia haya ima hufichwa hisia zake au hapana. Ikiwa hisia kama vile kuona, kusikia, kugusa, kunusa, na kuonja zitapotea, basi ni mtu iliyeondoshwa akili. Ikiwa hisia hazitapotea, basi haikosi ima ataendelea na furaha na nguvu ya nafsi kwa mtumiaji wake, au la. Ikiwa sivyo, basi hicho ni kilevi; vinginevyo itakuwa ni uovu (uharibifu) wa akili, kama vile bangi na vinavyolewesha [12]"
Kwa hivyo, mtumiaji wa madawa ya kulevya hatakiwi kupewa adhabu ya kupigwa, bali atapewa adhabu kama atakavyoona hakimu kwa manufaa ya kijamii.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
[1] Lisan Arab 4/230 neno Khadara.
[2] Alruruq 1/217. Chapa Alem kutub.
[3] Azawajir, Uk. 356. Chapa Dar Fikr. Toleo la kwanza.
[4] Siyasat Alshariyah, Uk.101, chapa Wizara ya Mambo ya Kiisilamu na Wakfu na Ulinganio na Mwongozo, Saudi Arabia. Mwaka 1418H.
[5] Attahriyr wattanwer 2/215, chapa Dar Tunusiyah, washambazaji.
[6] Rejea. Hashiyat ibn Shat Al Furuuq, 1/216.
[7] Albahr Muhet 8/110, chapa, Dar kutuby.
[8] Azawajir, 1/354.
[9] Ar rawdhah, 10/171 chapa Almaktab islamiy.
[11] Azawajir, 354.
[12] Al ruuq 1/217.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
