Kumpa Jina Mtoto

Egypt's Dar Al-Ifta

Kumpa Jina Mtoto

Question

Je, haki ya kumpa mtoto jina kisharia ni ya baba au mama?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

kinachokusudiwa kuhusu jina la mtoto ni kumtambua na kumwekea anwani itakayomtofautisha kwa namna inayolingana na heshima yake kama mwanadamu. Hili linaonekana kutoka kwenye asili ya neno jina, ambapo imesemwa: limetokana na alama.

Na Ibn Hazm amepokea Ijmaa (makubaliano ya wanazuoni) juu ya wajibu wa kumpa jina, akasema: “Wamekubaliana kwamba kumpa jina mwanamume na mwanamke ni wajibu[1].”

Ama kuhusu haki ya kumpa jina mtoto: asili yake ni kwamba ipo kwa baba, si kwa mama; kiasi kwamba wakigombania, baba ndiye anayetangulizwa. Kwani mtoto ananasibishwa kwa baba yake duniani, na husemwa kumhusu na kumwita: “Ewe mwana wa fulani”, na katika kumtaja: “Fulani bin fulani”, wala hasemwi: “Mwana wa fulani (mama)”; amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{Waiteni kwa baba zao, maana huo ndio uadilifu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu} [Al-Ahzab: 5], yaani: wanasibisheni kwa baba zao na muwahusishe kwao.

Na Siku ya Kiyama watu wataitwa kwa majina ya baba zao, na itasemwa: “Fulani bin fulani”; na Imepokelewa na Al-Bukhari katika Sahihi yake kutoka kwa Ibn ‘Umar — radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao — kwamba Mtume (rehma na amani zimshukie) amesema:

“Hakika msaliti atainuliwa kwake bendera Siku ya Kiyama, na itasemwa: Hii ni hiana ya fulani bin fulani.”

 

Na imepokelewa na Abu Dawud katika Sunan yake kutoka kwa Abu Dardaa (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) kwamba Mtume (rehma na amani zimshukie _ amesema:
“Hakika nyinyi mtaitwa Siku ya Kiyama kwa majina yenu na majina ya baba zenu, basi yafanyeni majina yenu.”

Na kwa kuwa mtoto anamfuata baba yake katika ukoo, na kutaja jina ni sehemu ya kufafanua ukoo na anayehusiana nao, basi baba anastahili kuwa na haki ya kumpatia jina mtoto. Kama ambavyo, baba ndiye mwenye jukumu la kumwongoza mkewe na kuwa na mamlaka juu ya mtoto wake, na hili linaimarisha haki hii.

Imepokelewa na Al-Bayhaqi katika “Shu’ab al-Iman” kutoka kwa mama wa waumini, Aisha R.A) radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake — kwamba Mtume — (rehma na amani zimshukie) alisema: "Haki ya mtoto juu ya baba yake ni kumpatia jina zuri, kumtunza vizuri kwa mlezi wake na kumfundisha adabu nzuri." Ingawa Hadithi hii ingawa ina udhaifu, bado inatoa ushahidi wa ujumla kwa maana hii.

Imepokelewa na Muslim kutoka kwa Anas bin Malik — radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake — kwamba Mtume — rehma na amani zimshukie — alisema: "Leo usiku nilipata mtoto mvulana, nikamwita kwa jina la baba yangu Ibrahim."

Hii ni kwa mujibu wa kauli za Wanazuoni wa Fiqh kutoka kwa Madhehebu tofauti, na baadhi yao walikubaliana kuhusu hili kama hukumu ya pamoja.

Sheikh Al-Alish Al-Maliki alisema: "Kumpa jina mtoto ni haki ya baba yake.[2]"

Na Al-SharwaniAl-Shafi alisema: "Inapaswa kuwa kwamba haki ya kumpa jina ni ya yule mwenye mamlaka juu ya mtoto, ambayo ni baba, hata kama hakupaswi kumtunza kwa sababu ya umasikini, kisha babu.[3]"

Na Al-Mardawi Al-Hanbali alisema: "Inapendeza kumpatia jina mtoto siku ya saba... na haki ya kumpatia jina ni ya baba, sio mama.[4]"

Na Ibn Qayyim alisema: "Kumpa jina mtoto ni haki ya baba, sio mama. Hili ni jambo lisilo na mgogoro miongoni mwa watu, na kwamba ikiwa wazazi wataingia kwenye mzozo kuhusu kumtaja jina mtoto, basi haki hiyo ni ya baba.[5]"

Lakini inapaswa kuzingatiwa kuwa hii ni sehemu ya haki, wakati sehemu ya makubaliano kati ya mume na mke ni pana zaidi, na inafaa zaidi kwa adabu njema; ikiwa mume hatochagua jina pekee na kumshirikisha mke wake katika uchaguzi, hii itakuwa ni sababu ya kudumisha upendo, kupatikana haki, upatanisho, na rehema kati yao. Imepokelewa na At-Tirmidhi kutoka kwa Aisha (Radhi Mwenyezi Mungu) - kwamba Mtume (Rehma na amani zimshukie juu yake) alisema: "Miongoni mwenu bora ni yule ambaye ni bora kwa familia yake." Rehema ya Mwenyezi Mungu kwa mwanaume kwa mke wake, kuzingatia maoni yake na kuifariji nafsi yake, bila shaka ni miongoni mwa mambo mema yanayosifiwa katika Hadithi hii

Na Mweneyzi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.

 

[1] Maratib Ijmaa, Uk. 154, chapa Dar Kutub Elmiyah.

[2] Manhu Ljaliyl, 2/2, chapa Dar Fikr.

[3] Hashiyat Sharwany Ala Tuhfat Minhaj, 9/372, chapa, Dar Ihyaa Turath Al araby.

[4] Al inswaf 4/111, chapa, Dar Ehyaa Turath Al araby.

[5] Tuhfat Al mauluud, Uk 96 chapa Maktabatl Quran.

Share this:

Related Fatwas