Hukumu ya kusheherekea siku ya mama...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya kusheherekea siku ya mama

Question

Hukumu ya kusheherekea siku ya mama, je, ni bidaa?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Mwanadamu ameumbwa na Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu amemtukuza kwa ubinaadamu wake; akamuumba kwa mikono yake na akampulizia roho yake, na Malaika wake wakamsujudia, na akamfukuza Ibilisi katika rehema zake kwa sababu alifanya kibri na kutotii amri ya Mwenyezi Mungu ya kumsujudia mwanadamu, ikiwa kumuheshimu mwanadamu ni sifa ya Kimalaika ambayo ustaarabu ulisimama kwayo, na kukawa kudharau mwanadamu na kumdhalilisha ni sifa ya shetani na ibilisi, iliyoteteresha ustaarabu ambao umejengewe juu yake, {Dari zikawaporomokea juu yao, na adhabu ikawajia kutoka wasipo kujua} [Annhli:26], { Na mwenye kumfanya Shet'ani kuwa ni mlinzi wake badala ya Mwenyezi Mungu, basi huyo amekhasiri khasara ya dhaahir} [119], {Je! Mnamshika yeye na dhuriya zake kuwa marafiki badala yangu, hali wao ni adui zenu? Ni ovu mno badala hii kwa wenye kudhulumu} [Al-Kahf:50]

Kama Uislamu ulivyokuja na kumtukuza mwanadamu kama alivyo, pasi na kuangalia aina yake, jinsia yake au rangi yake, hakika Mwenyezi Mungu ameongeza kumtukuza kwingine kunakofungamana na wadhifa ambazo amempa kutokana na umaalumu ambao Mwenyezi Mungu amemuumba nao, katika hilo ni kuwatukuza wazazi wawili ambao Mwenyezi Mungu amewafanya kuwa sababu ya uwepo, na akakutanisha kuwashukuru kwao na kumshukuru yeye; Akasema Mwenyezi Mungu: {Na tumemuusia mtu kwa wazazi wake wawili. Mama yake ameichukua mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu, na kumwachisha ziwa baada ya miaka miwili. (Tumemuusia): Nishukuru Mimi na wazazi wako. Ni kwangu Mimi ndiyo marudio} [Luqman: 14], na akajaalia amri ya kuwatendea wema wazazi baada ya amri ya kumwabudu yeye Mwenyezi Mungu Akasema: {Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema} [Al Israa: 23], hii imekuwa hivyo kwa sababu Mwenyezi Mungu amewafanya wazazi kuwa sababu ya uwepo wake; ikiwa tukio hili kubwa la kiulimwengu ndilo linadhihirisha sifa ya uumbaji, mbali na utukufu juu ya utukufu.

Mtume S.A.W. amemfanya mama ndio mbora zaidi wa watu kwa kuishi naye vizuri, pia akamfanya kuwa mbele ya baba, katika hilo; Hadithi iliyopokelewa na Abu Hurayra R.A. amesema: “Mtu mmoja alikuja kwa Mtume S.A.W.  akasema: Mtu gani ana haki zaidi ya kuishi naye vizuri? Akasema: Mama yako, akasema: kisha nani? Akasema: kisha mama yako, akasema: kisha nani? Akasema: kisha mama yako, akasema: kisha nani? akasema: baba yako”. Hadithi hii imepokelewa na Bukhari na Muslim.

Sharia ya Kiislamu imethibitisha kwamba mahusiano kati ya mtoto na mama yake ni mahusiano ya kiviungo ya kiasili, hayaishii kwa kuyanasibisha na kuwepo kwake amemleta kwa ndoa au zinaa, bali huyu ni mama yake kwa kila hali, kinyume na ubaba ambao hauthibitiki isipokuwa kwa njia ya kisharia.

Miongoni mwa hali za kumtukuza mama kumuheshimu na kumfanyia wema, na hakuna katika sharia yoyote kinachozuia kuwepo sherehe ambayo Watoto wanaonesha furaha yao kwa mama zao, jambo hili ni lakimfumo halina ubaya, na halina mahusiano na mambo ya bidaa ambayo yanazungumzwa na watu wengi; kwani bidaa inayozungumzwa ni ile iliyozushwa kinyume na Sharia kwa mujibu wa kauli ya Mtume S.A.W.: “Mwenye kuzusha katika jambo letu hili lisilokuwepo basi hilo ni lenye kurudishwa”. Hadithi hii imepokelewa na Bukhari na Muslim katika Hadithi za mama Aisha R.A.

Na maana ya Hadithi hii ni kwamba mwenye kuzusha katika Dini lililokuwepo basi hilo linakubalika halikataliwi, na Mtume S.A.W. amekiri sherehe za Warabu kwa kumbukumbu za mataifa yao na ushindi wao ambao walikuwa wakiimba mazuri ya kabila lao na masiku yao ya kumbukumbu ya ushindi, kama ilivyokuja katika Hadithi ya sahihi mbili kutoka kwa Aisha R.A. “kwamba Mtume S.A.W. aliingia akamkuta na vijakazi wawili wakiimba wimbo wa siku Buaath”, na imekuja katika Hadithi kwamba Mtume S.A.W. alizuru kaburi la mama yake Bi. Amina akiwa na askari elfu mbili walivaa ninja, hakuwahi kuonekana akilia sana kuliko siku hiyo”. Imepokewa na Hakim na amefanya kuwa sahihi na asili yake ni katika Hadithi za Muslim.

Maana ya Umama ni maana kubwa sana kwa Waislamu, ni maana wazi katika turathi zao za kilugha; Mama katika Lugha ya Kiarabu kiasili ni jina la nyumba, jina la Rais na mtumishi wa watu ambaye anasimamia chakula chao na huduma zao, na maana hii ya mwisho imekuja kutoka kwa Imamu Shafi R.A. ambaye ni mtaalamu wa Lugha ya Kiarabu, amesema Ibn Durayd: “Kila kitu kinachokusanya vitu vingi, basi Waarabu wanakiita hicho kitu “Mama”. Hivyo basi Makka ikaitwa Ummul Quraa (mama wa miji) kwa sababu ipo katikati ya Dunia na kwa sababu ni kibla kinachoelekewa na watu, na kwa sababu mji mtukufu zaidi”.

Na kwakuwa lugha ya Kiarabu imekuwa ndiyo chombo cha fikra hivyo athari ya neno hili kwa Waislamu inahusiana na huyo mwanadamu mtukufu ambaye Mwenyezi Mungu amemfanya kuwa asili kuumba wanadamu, kisha akampa nchi ambayo ndiyo nyumbani kwake, kisha akamuelekeza sera zake na malezi yake, na akampendekesha huduma zake na kusimamia mambo yake; mama katika hayo yote ndiyo sehemu ya upole na huruma ambayo Watoto wake wanaipata.

Kama maana hii ilivyo  wazi katika asili na muweko wa kilugha, na mnyumbuliko kutoka katika sili ya neno katika lugha, basi urithi wetu wa kitamaduni unauzidishia uzuri na uwazi, na katika hilo matumizi changamano ya “Kuunga udugu” ambapo sifa hii ya kiviungo imewekwa kwa mama kuwa ni alama ya mawasiliano ya kifamilia ambayo imekuwa ndiyo msingi wa kujenga jamii ya kibinaaadamu; kwani hakuna mwenye haki zaidi ya mahusiano haya kuliko mama ambaye kwake ndiko kunaendelea maana ya Maisha na inadhihirika maana ya huruma.

Na jambo hili linakamilika kwa maana hii ya kidini nzuri ambayo Mtume S.A.W. anabainisha katika kauli yake: “Udugu umefungamanishwa na Arshi, unasema: Mwenye kuniunga Mwenyezi Mungu amuunge, na mwenye kunikata Mwenyezi Mungu Amkate”. Hadithi hii imepkelewa na Bukhari na Muslim.

Na katika Hadithi Qudsy: “Mwenyezi Mungu Anasema: Mimi ni Allah, mimi ni Al Rahaman nimeumba udugu na jina lake limetokana na jina langu; mwenye kuungana nami ninamuunga na mwenye kuuukata basi nitamkata”.  Hadithi imepokelewa na Abu Dawoud na Al tirmidhy na amefanya kuwa sahihi katika Hadithi za Abdurrahman bin Auf R.A.

Na kutokana na utukufu wa maana hii ya Umama kwetu kiupande wa kilugha, kiurithi na kiutamaduni na kidini, tunaweza kugundua pengo kubwa na tofauti kati yetu na wengine ambao thamani ya familia kwao imetoweka, na imesambaratika katika uhalisia wake, ikawa wanaisaka tu katika minasaba hii na wanakuwa na hamu kuadhimisha ili wahisi kitu katika maana hii iliyopotea kwao, siku kama hizi zikawa karibu sana kwao kwa kile tunachoweza kukiita “Kuomba huruma” kutoka kwa Watoto ambao wanawazindua katika masiku hayo kukumbuka mama zao angalau kwa zawadi katika taabu zao za Maisha ambayo wanaangalia mbele tu wala hawatazami nyuma.

Pamoja na tofauti hii iliyopo kati yetu na tamaduni nyingine ambazo zimetenga uhalisia wake katika minasaba kama hii, isipokuwa kwamba hili halitengenezi kizuizi kisharia kusheherekea, bali tunaona kwamba katika kushiriki kuna kueneza wema kwa wazazi wawili katika zama ambazo kumedhihiri kutowatendea wema wazazi wawili ambako kunasikitisha, nasi tuna kigezo chema kutoka kwa Mtume S.A.W., ambapo yeye alikuwa anapenda tabia nzuri na kuzisifu katika kila kitu hata kama kikiwa si katika Dini yake; “Walipoletwa mateka wa kabila la Tayii binti wa Hatim Al Taayii alikuwa katika mateka; akamwambia Mtume S.A.W.: Ewe Muhammad! Naomba uniachie huru nisidhalilike kwa Waarabu; kwani mimi mtoto wa kiongozi wa watu, baba yangu alikuwa anasaidia watu, na kuwatatulia matatizo yao, anawasaidia chakula wasionacho, kuwapa nguo wasio na mavazi na kuwakirimu wageni, analisha chakula na kusalimia watu, na wala hakuwahi kumnyima mwenye kuomba haja hata siku moja. Mtume S.A.W. akasema: Ewe kijakazi! Hizi ni sifa za Waumini wa kweli, la kama baba yako angekuwa Muumini tungemwombea rehema; muacheni kwani baba yake anapenda tabia njema, na Mwenyezi Mungu Anapenda tabia njema, Abu Burda bin Niyar R.A. akasimama akasema: Ewa Mtume wa Allah! Mwenyezi Mungu anapenda tabia njema? Mtume S.A.W. akasema: Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu ni milki yake, hataingia Peponi yeyote isipokuwa kwa tabia njema”. Hadithi hii imepokelewa na Al Bayhaqy katika Hadithi za Ally bi. Abii Talib R.A.

Na Mtume S.A.W. amesema: “Nimeona nyumbani kwa Abdillah bin Judaan ushirikiano wa thamani mno, na lau Uislamu ungeliutaka ningeupendekeza”. Imetolewa na Al Bayhaqy kutoka kwa Talha bin Abdillah bin Auf.

 Hivyo basi, kusheherekea siku ya mama kunajuzu kisharia, hakuna kizuizi wala ubaya, na bidaa inayokataliwa ni bidaa iliyozushwa kinyume na Sharia, ama iliyoshudiwa na Sharia katika asili yake, basi hiyo haiwi bidaa inayokataliwa na wala hakuna dhambi kuitenda.

Na Mwenyezi MunguMtukufu ni Mjuzi Zaidi

Share this:

Related Fatwas