Wanawake wakuwasomesha wanaume
Question
Je, kunajuzu wanawake kuwasomesha wanaume Qur`ani Tukufu, kusoma kuandika msahafu na matini na mengineyo kwa kukosekana wanaume wanaoujua kusomesha elimu hii katika sehemu hiyo?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Wanaume kusoma kwa wanawake na wanawake kusoma kwa wanaume ni katika mambo ambayo hayakatazwi kisharia; Waislamu wa zamani na wa sasa wamekubaliana kuwa kuwepo wanawake na wanaume sehemu moja jambo hili si haramu, na uharamu unakuwa katika aina ya mkusanyiko ukiwa unapingana na Sharia Tukufu; kama wanawake kuonesha kisicho halali kwao kuonesha kisharia, na kuwa mkusanyiko wa jambo la haramu, au kuwa katika faragha iliyoharamishwa. Watu wa elimu wameeleza kwamba kuchanganyika kuliko haramu kwenyewe ni katika kubanana na kugusana, si kwa kuwepo tu sehemu moja.
Katika hili Hadidthi tukufu zimetoa Ushahidi, imekuja katika sahihi mbili kutoka kwa Suhayl bin Al Saady R.A. amesema: “Abu As’ad Al Saaidy alipofanya harusi, alimualika Mtume S.A.W. na Masahaba zake, alipowapikia chakula alikipeleka mke wake Mama Asyad”. Boukhary ameifasiri kwa kauli yake: “Mlango wa mwanamke kusimama mbele ya wanaume katika harusi na kuwahudumia”. Al-Qurtuby amesema katika kutafsiri: Wanazuoni wetu wamesema: katika Hadithi hii kunajuzu bibi Harusi kumuhudumia mume wake na marafiki zake katika arusi yake”.
Ibn Battala amesmea katika sherehe yake Bukhari: “Katika Hadithi tunapata kwamba kutenganisha wanawake na wanaume katika sehemu au katika muamala wa moja kwa moja si faradhi kwa wanawake wa waumini, bali ni maalumu tu kwa wake wa Mtume S.A.W., pia hili amelitaja Mwenyezi Mungu katika Qur`ani Tukufu kwa kauli yake: {Na mnapo wauliza wakeze haja waulizeni nyuma ya mapazia} [Al Ahzab:53]”.
Hafidh Bin Hajar amesema katika Fat’hi Al bary: “katika Hadithi hii kunajuzu mwanamke kumuhudumia mume wake na aliowaalika, na hakufichiki kwamba sehemu ya hili ni pale kunapokuwa na uhakika wa kutokuwepo fitina na kuchunga yanayopasa kustiri, na kujuzu mwanamume kumtumia mke wake katika jambo kama hilo”.
Imekuja kutoka katika sahihi mbili kutoka kwa Abu Hurayra R.A. katika kisa cha Talha Al Ansary katika kulisha kwake wageni: “Kwamba wao walijifanya waonekane kama wanakula ilhali walilala na njaa” na katika riawaya nyingine ya Ibn Abi Dunia katika Qira Al Dayf katika Hadithi ya Anas R.A: “Kwamba mtu mmoja alimwambia mke wake: Ujaze nyama mkate huu kisha utie samli kisha ulete, na mwambie mtumishi azime taa, na wakawa wanatafuna tafuna yeye na mke wake ili mgeni aone kuwa wanakula”. Na hali ilivyo ni kwamba wao wamekusanyika sehemu katika Sahani moja.
Mtume S.A.W. amesma: “Mwenyezi Mungu Amependezwa na mlichokifanya kwa mgeni wenu usiku”. Na ikashuka katika tukio hili Aya hii:{bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji} [Al Hashri:9].
Na katika sahihi mbili kutoka kwa Abu. Juhayfa R.A. amesema: “Mtume S.A.W. aliwaunga undugu Salman na Abu Dardaa, Suleyma akamtembelea Abu Dardaa, akamuona Mama Dardaa amevaa nguo chakavu, akamuuliza: una nini? Akasema: ndugu yako Abu Dardaa hana haja na dunia. Akaja Abu Dardaa akampikia chakula…” mpaka mwisho wa Hadithi. Al Hafidh bin Hajar amesema katika Fat’h Al Bary: katika Hadithi kuna faida… kujuzu kuzungumza na mwanamke wa kando na kumuuliza yenye masilahi”.
Ama kuhusu wanaume kuchukua elimu ya kisharia na mawaidha kutoka kwa wanawake wasomi, wanawake wa Mtume S.A.W. walikuwa wanatoa elimu na kusambaza Dini, na kuna Hadithi nyingi katika riwaya zao pia na tabaka la wanawake walio baada yao katika wale waliopokea Hadithi kutoka kwao wanaume na kuchukua elimu kwao, Alhafidh bin Hajar Al Asqalany amewafafanua peke yake katika kitabu chake Al Isaba fee tamyiiz Al Sahaba wanawake elfu moja miatano arobaini na tatu, miongoni mwao Wanazuoni wa Fiqhi, Hadithi na fasihi.
Mwanamke wa Kiislamu alikuwa anashirikiana na wanaume katika Maisha ya jamii, pamoja na kudumu na vazi lake la kisharia na kulinda mipaka ya amani na adabu zake; mpaka kulikuwa na wanawake wa Masahaba walioshika wadhifa wa uhasibu, katika hili ni Hadithi iliyopokelewa na At-Tabarany katika Al-Muujam Al-Kabir kwa Sanadi ya watu wake waaminifu, kutoka kwa Abu Balh Yahaya bin Abi Sleem, amesema: “Nimemuona Samraa bin Naheek na alikuwa amemuwahi Mtume S.A.W. na masahaba zake, akiwa na ngao ngumu na mtandio mkubwa mkononi mwake anawapiga watu na kuamrisha mema na kukataza mabaya”.
Kwa haya, basi hakuna nafasi kwa yeyote kukemea hali hii thabiti katika Hadithi za Mtume tukufu na historia ya Uislamu, wala hakusihi kufanya mila na desturi zilizorithiwa hapo zamani au sehemu yoyote kuwa ndiyo msaidizi wa kuhukumu katika Dini na Sharia, bali Sharia inakuwa juu wala haiwi chini ya chochote, wala hakujuzu kwa mtu anayefuata njia ya kujichunga kuwalazimisha watu katika njia hiyo au kuwabebesha, au kufanya ugumu au kubana katika yale ambayo Mwenyezi Mungu ameyafanya kuwa na wepesi ndani yake.
Na Mwenyezi MunguMtukufu ni Mjuzi Zaidi
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
