Mwanafunzi wa udaktari kutibu wagonjwa
Question
Je, kunajuzu kwa daktari mwanafunzi kufanya kazi ya kutibu wagonjwa kwa malipo kipindi cha mafunzo ya kivitendo, kukidhaniwa kwa ukaribu kuwa hatomdhuru mgonjwa, na kwamba amefikia uwezo unaotakiwa katika upande sehemu ambayo anafanya kazi yake? Kwa kujua kuwa mafunzo yanagawanyika katika sehemu mbalimbali: miezi miwili katika sehemu ya magonjwa ya tumbo, miezi miwili au zaidi sehemu nyingine… na kuendelea, je, anaweza kufanya kazi aliyoifanyia mafunzo kabla ya kumaliza mwaka wa majaribio?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Kufanya kazi ya utabibu kupo chini ya vidhibiti na kanuni hasa kipindi hiki cha jamii ya sasa na hali ya sasa, na asili katika hili ni jambo lisiloegemea upande wowote, na halikuwekwa dhidi ya mtu fulani au kwa masilahi ya mtu fulani, bali anayelisimamia na kulipanga ni masilahi ya umma, na kanuni ya kisharia inasema kwamba panapogongana masilahi ya umma na masilahi binafsi, hutangulizwa masalahi ya Umma, na kanuni ya kisharia pia inasema kwamba utendaji wa kiongozi unategemea masilahi, mtu mwenyewe anaweza kuona kwamba ana uwezo wa kutibu na kufanya kazi ya madawa au kujenga majengo au mengineyo katika kazi amabazo zinamgusa mtu mwingine, lakini mtu anavyojiona mwenyewe hakutoshi kuweza kuwauguza wengine na kuchezea mili na roho za watu kwa mtazamo wake binafsi, kwani ni wajibu kuheshimu viumbe vikavu na viumbe hai, mbali na mwanadamu ambaye Mwenyezi Mungu Amemwelezea: {Na hakika Tumewatukuza wanaadamu}[Al Israa:70], na Mtume S.A.W. amesema: “Muislamu ni yule ambaye wamesalimika Waislamu wenzake kutokana na ulimi wake na mkono wake”. Imepokelewa na Bukhari na Muslim, na akasema katika Hija ya kuaga: “Kila Muislamu kwa Muislamu ni haramu, damu yake, mali yake na heshima yake” imepokelewa na Muslim na wengineo, na miongoni mwa kuheshimu viumbe vya Mwenyezi Mungu ni kutokuwa sehemu ya majaribio ya mwingine kwa dhana yake hata kama yupo sahihi kwa upande wake, bali kunapasa kurejea katika hilo katika vidhibiti vya kikazi vinayotambulika kwa masilahi ya wote, ambavyo asili yake ni kujitahidi kufika kiwango kikubwa cha Masilahi na kuwepo makosa madogo, lakini shetani humwingia mwanadamu na kujali masilahi yake binafsi na huyaweka nyuma masilahi ya umma, na kama jambo hili litaachwa kwa makadirio ya kila mtu na dhana yake, basi watu wangehalalisha damu za watu na mali zao, huku wakidhani kuwa wanafanya wema, na vipimo vya ustaarabu na maendeleo ya umma hupimwa kwa vidhibiti vya watu kwa masilahi ya jamii, na kuanguka kwa nchi na kuharibika kwake kunakuwa kwa watu kutoka katika mifumo ya jamii na sheria zinazoongoza.
Hivyo basi hakujuzu kwa daktari aliye mafunzoni na mwingineo katika wale ambao wanaweza kuwa na maarifa makubwa na uzoefu na akili kubwa katika elimu ya tiba kufanya kazi nje ya mfumo wa kanuni na adabu za kazi.
Naye Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Zaidi
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
