Kusajili tarehe nyingine katika Fom...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kusajili tarehe nyingine katika Fomu ya kuzaliwa.

Question

Mtoto wa kike amekuja London pamoja na wazazi wake kwa njia ya kisheria wakiwa na pasipoti, lakini baadae wazazi wakamwambia mtoto huyo (mwenye miaka 12) kuwa abadili tarehe nyingine ya (mwezi wa) kuzaliwa katika fomu rasmi ili azidishe mwaka, mtoto huyo ambaye ni wa kike, akalipinga jambo hilo lakini mwisho wake akawakubalia wazazi wake, na tangu siku hiyo akawa anatumia tarehe hiyo isipokuwa akawa anahisi tabu na masikitiko, kwani hivi sasa keshabaleghe. Na alipotengeneza pasipoti kwa mara ya pili tarehe hiyo hiyo ikaandikwa tena, na alitaka kueleza ukweli, na kuwaambia kuwa tarehe sahili (mwezi) wa kuzaliwa kwake lakini wazazi wake wakamwambia kuwa iwapo atafanya hivyo atatusababisha matatizo. Mtoto huyu afanye nini?

Hakika kwamba tarehe hiyo sasa iko kwenye pasipoti yake ya Uingereza, na msichana huyo amechanganikiwa baina ya kusema ukweli na kutii wazazi wake. Anahisi kwamba anatumia pasipoti hiyo isivyofaa na ana wasiwasi kuhusu adhabu ya Mungu kwake na kwa wazazi wake, hasa kwao, ikiwa atasema ukweli. Afanye nini?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Uandishi wa nambari hizi huwa si jukumu la mtoto, kwani yupo chini ya himaya ya wazazi wake au muusiwa, na ufuatiliaji uliopo hautoi nafasi ya kujaza nambari isipokuwa mara chache, na iwapo kuna makosa yeyote basi kwa upande wa muulizaji hana kosa lolote, si mbele ya Mwenyezi Mungu wala mbele ya watu. Na mambo haya ni katika ufuatiliaji ambao kiukweli hauharibu ukweli uliopo, kwa mfano shahada uliyoipata kwa njia ya ukweli kabisa baada ya kumaliza masomo na mfano wake. Pamoja na kuwa tunamkataza aliyetuuliza – kabla ya kuingia katika kosa hili- atendae mambo kama haya sisi huwa hatumlazimishi mtu kile asichokiweza kwa ajili ya kurekebisha makosa ambayo kimsingi hayana athari yeyote, si kisheria, kidesturi wala kikanuni. Na wasomi wa Fiqhi wamelielewa jambo hili na wakaliwekea maelezo yasemayo: “Husamehewa hukumu ambayo haijatimiza baadhi ya mambo kisheria, na kama hukumu hiyo imetimiza mambo ya kisheria basi huwa haisamehewi.” Na hii ni moja ya mifano yake. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.

Share this:

Related Fatwas