Hukumu ya msichana aliyefika umri w...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya msichana aliyefika umri wa kubaleghe kulala kitanda kimoja na baba yake au mvulana aliyebaleghe kulala kitanda kimoja na mamake

Question

Je! Qur`ani Tukufu inasema nini kuhusu suala la kijana wa miaka 21 anayelala kitanda kimoja na mama yake, na pia msichana wa miaka 21 anayelala kitanda kimoja na baba yake?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Miongoni mwa adabu za Kiislamu za jumla ambazo yafaa kuzingatiwa na kuhifadhiwa ni kwamba mwanaume aliyebaleghe awe na sehemu yake ya kulala tofauti na dada yake, mama yake, au maharimu wengine. Vivyo hivyo kwa mwanamke aliyebaleghe. Hii ni kwa ajili ya kuziba milango ya fitna na kuondoa shaka. Hata hivyo, ikiwa kuna ulazima kama vile msongamano wa nafasi au kukosekana kwa kitanda kingine, na hakuna hatari yoyote ya fitna au shaka kwa hali yoyote ile, basi jambo hilo halitakuwa haramu.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi

Share this:

Related Fatwas