Mitala

Egypt's Dar Al-Ifta

Mitala

Question

Nini hukumu ya Sharia kuhusu ndoa ya wake wengi?

Answer

Uislamu umeruhusu ndoa ya wake wengi, na ukaweka ukomo wa juu wa kukusanya wake kuwa wanne; kutokana na kauli ya Mtume  kwa Ghaylan Ibn Salama Al-Thaqafi (R.A) aliposilimu akiwa na wake kumi: «Chagua miongoni mwao wanne»; isipokuwa Uislamu umeifunga ruhusa hii kwa uwezo wa kutoa matumizi na uadilifu kati yao katika chakula, mavazi, kinywaji, makazi, kulala na matumizi. Atakayejijua mwenyewe kuwa hana uwezo wa kutekeleza haki hizi kwa uadilifu na usawa, basi anakuwa ni mwenye dhambi na mtenda kosa ikiwa ataoa mwingine; kutokana na kauli ya : {na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu} [An-Nisa: 3], na kauli ya Mtume : «Atakayekuwa na wake wawili kisha asifanye uadilifu kati yao, atakuja Siku ya Kiyama na upande wake mmoja umeanguka», na Wanazuoni walisema: Inapendekezwa kutosheka na mke mmoja ikiwa hakuna haja ya mwingine.

Maelezo

Sharia imemruhusu Muislamu kuoa zaidi ya mke mmoja, na ikaweka ukomo wa juu wa kukusanya wake kuwa wanne; kutokana na kauli ya Mtume  kwa Ghaylan bin Salama al-Thaqafi (R.A) aliposilimu akiwa na wake kumi: ((Chagua miongoni mwao wanne)) [1].

Hadithi imeamuru kuweka ukomo wa idadi ya wake kwa yule aliyekuwa anazidi wanne, na kinyume chake, hakukuja kinachoonesha kuwa ni wajibu kwa aliyeoa mmoja kuoa mwingine; hiyo ni kwa sababu ndoa ya wake wengi si lengo lenyewe, bali mwanamume huoa mara nyingine kwa sababu na maslahi ya kijamii.

Uislamu umeifunga ruhusa ya ndoa ya wake wengi kwa uwezo wa kutoa matumizi na uadilifu kati yao katika chakula, mavazi, kinywaji, makazi, kulala na matumizi, hivyo atakayejijua hana uwezo wa kutekeleza haki hizi kwa uadilifu na usawa, basi anakuwa ni mwenye dhambi na mtenda kosa ikiwa ataoa mwingine.

Dalili ya hilo: 1- Kauli ya : {na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu} [An-Nisa: 3]. 2- Kauli ya Mtume : ((Atakayekuwa na wake wawili kisha asifanye uadilifu kati yao, atakuja Siku ya Kiyama na upande wake mmoja umeanguka)) [2].

Na Wanazuoni wa Fiqhi wamesema: Inapendekezwa kutosheka na mke mmoja maadamu hakuna haja[3].

Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:

Kwamba kuoa kwa mwanaume mke mwingine mpaka wake wanne, hukumu yake katika Uislamu ni ruhusa (ibaha) ikiwa ana uwezo wa hilo, na haliathiri kwa ubaya na madhara makubwa maisha yake mengine.

 

[1] Imepokelewa kutoka kwa Ibn Majah katika “Sunan” yake.

[2] Imepokelewa kutoka kwa Al-Tirmidhi.

[3] “Radd Al-Muhtar” cha Ibn Abidin (10/340), “Al-Majmu’” cha Al-Nawawi (16/144), na “Al-Insaf” cha Al-Mardawi (12/204).

Share this:

Related Fatwas