Wito wa Jihadi dhidi ya Dola

Egypt's Dar Al-Ifta

Wito wa Jihadi dhidi ya Dola

Question

Nini hukumu ya kulingania jihadi dhidi ya dola?

Answer

Dhana ya jihadi katika Uislamu haikufungika katika vita na mapigano pekee, bali inajumuisha mambo mengine pia kama kupambana na nafsi, matamanio na shatani. Hivyo maisha ya Muislamu yote ni jihadi, iwe katika ibada zake, au ujenzi wa nchi, au katika kuitakasa nafsi yake.

Jihadi ya maadui ni katika faradhi za kutosheleza (Fardh Kifaya) ambazo utaratibu wake unarejeshwa kwa wenye mamlaka, na inafanywa na majeshi na taasisi za dola ili kuhifadhi mipaka na usalama wa ndani, na kuimarisha nguvu ya ulinzi.

Ama yale yanayofanywa na makundi ya kigaidi kama uharibifu, kuua askari, polisi na raia na kubomoa nyumba za ibada, hiyo si jihadi, bali ni uchochezi, uasi na ufisadi katika ardhi ambao unamstahiki mtendaji wake adhabu ya uchochezi, na ni wajibu kwa viongozi kuwakabili ili kuvunja nguvu zao na kuondoa shari yao.

Maelezo

Dhana ya jihadi[1]  haikufungika katika vita na mapigano; bali inajumuisha kupambana na nafsi, matamanio na shetani. Mwenyezi Mungu anasema: {Na wanaofanya juhudi kwa ajili yetu, Sisi tutawaongoa kwenye njia zetu. Na hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na watu wema.} [Al-Ankabut: 69]. Mwenyezi Mungu anasema: {Basi usiwat'ii makafiri. Na pambana nao kwayo kwa Jihadi kubwa} [Al-Furqan: 52]. Maana ya {Na pambana nao kwayo} yaani kwa Qur`ani. Na Mtume  (S.A.W) aliifanya Hija kuwa ni Jihadi; kutoka kwa Aisha (R.A) amesema: ((Tulisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, tunaona Jihadi ndicho kitendo bora zaidi, je hatupigani Iihadi pamoja nawe? Akasema: Hapana, bali jihadi bora zaidi ni Hija iliyokubaliwa)) (Imepokelewa kutoka kwa Al-Bukhari).

Kama ambavyo dhana ya Jihadi inatumika kwa maana zilizotajwa, pia inatumika kwa ajili ya kupigana na adui ambako kunakusudiwa kuondoa uchokozi na uonevu. Aina hii ya Jihadi ina sharti zake; ni faradhi ya kutoshelezana ambayo utaratibu wake upo mikononi mwa viongozi na wanasiasa ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu amewapa mamlaka, na kuwafanya kuwa na uwezo zaidi wa kujua matokeo ya maamuzi haya ya kukata shauri, ambapo wanaangalia haja inayopelekea hilo, hivyo uamuzi wa Jihadi unakuwa umesomwa kisayansi na kiuhalisia, kukiwa na usawa kati ya maslahi na madhara. Inajulikana kisharia na kiakili kuwa mgawanyiko na kukosekana kwa bendera (uongozi mmoja) hupoteza nidhamu ya mapigano na kuondoa thamani na utukufu wake.

Yale yanayofanywa na makundi ya kigaidi na kuyaita Jihadi si jihadi ya kweli; bali ni uchochezi, uasi na ufisadi katika ardhi ambao unamstahiki mtendaji wake adhabu ya uchochezi; Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Basi malipo ya wale wanao mpiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakawania kufanya uchafuzi katika nchi, ni kuuwawa, au kusalibiwa, au kukatwa mikono yao na miguu yao kwa mabadilisho, au kutolewa nchi. Hii ndiyo hizaya yao katika dunia; na katika Akhera watapata adhabu kubwa.} [Al-Maidah: 33].

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema kuhusu wachochezi: {Kama wanaafiki na wale wenye maradhi nyoyoni mwao, na waenezao fitna katika Madina hawatoacha, basi kwa yakini tutakusalitisha juu yao, kisha hawatakaa humo karibu yako ila muda mchache tu, Wamelaanika! Popote watakapo onekana watakamatwa na watauliwa kabisa.  Hii ni ada ya Mwenyezi Mungu iliyo kuwa kwa wale walio pita zamani. Wala hutapata mabadiliko katika ada ya Mwenyezi Mungu}[Al-Ahzab:60-62].

Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:

Kwamba dhana ya Jihadi haikufungika katika vita na mapigano pekee, bali inajumuisha mambo mengine pia kama kupambana na nafsi, matamanio na shetani; hivyo maisha ya Muislamu yote ni Jihadi, iwe katika ibada yake kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, au katika ujenzi wa ardhi, au katika kuitakasa nafsi.

Kwamba Jihadi ya maadui ni katika faradhi za kutoshelezana (Fardh Kifaya) ambazo utaratibu wa kuzipanga unarejeshwa kwa wenye mamlaka (viongozi), na inafanywa na majeshi na taasisi za dola, ili kulinda mipaka na usalama wa ndani, na kwa ajili ya kuimarisha nguvu ya ulinzi.

Yale yanayofanywa na makundi ya kigaidi kama uharibifu na kuua askari wa jeshi, polisi na raia na kubomoa nyumba za ibada si Jihadi, bali ni uchochezi, uasi na ufisadi katika ardhi ambao unamstahiki mtendaji wake adhabu ya uchochezi, na ni wajibu kwa viongozi wa Waislamu kuwakabili kwa namna itakayovunja nguvu zao na kuondoa shari yao.

 

[1] «Jihadi»: Ni kutoa nguvu katika kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa nafsi, mali, ulimi au mengineyo.

Share this:

Related Fatwas