Ulaji wa nyama zinazoingizwa kutoka nje
Question
Ni nini hukumu ya ulaji wa nyama zinazoingizwa kutoka nje ya nchi?
Answer
Nyama zinazoingizwa kutoka nje ikiwa ni nyama za wanyama wanaoliwa na zimechinjwa au kuchinjwa koo kwa namna ya kisharia, na mchinjaji akawa ni Muislamu au miongoni mwa Watu wa Kitabu; basi hizo ni nyama zinazojuzu kuliwa na hazina uharamu wowote.
Lakini ikiwa zinatoka katika nchi ambazo si za Waislamu wala si za Watu wa Kitabu, kwa kuwa zinatoka katika nchi za waabudu masanamu na wapagani, basi haijuzu kuzila. Kadhalika, ikiwa ni nyama za wanyama wasioliwa kama vile nguruwe, mbwa, na punda, haijuzu kula nyama zao hata kama zimechinjwa na Muislamu au mtu wa Kitabu.
Au ikiwa nyama hizo zilizoingizwa hazikuchinjwa, kama vile kufa kwa njia ya kupigwa shoti ya umeme, kunyongwa, au mambo mengine yanayofanywa na wale wanaoharamisha uchinjaji; ikiwa hilo limejulikana kwa yakini, basi haijuzu kula nyama hizo, kwani ni mzoga ambao ni haramu kuula.
Maelezo
Hairuhusiwi kisharia kula nyama za ndege na wanyama wanaoruhusiwa kuliwa isipokuwa idhibitike kuchinjwa kisharia; kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu (S.W.): {Mmeharamishiwa nyama ya mzoga, na damu, na nyama ya nguruwe, na mnyama aliyekufa kwa kutajwa jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na aliyekufa kwa kunyongwa, na aliyekufa kwa kupigwa, na aliyekufa kwa kuanguka, na aliyekufa kwa kupigwa pembe, na aliyeliwa na mnyama wa mwitu, isipokuwa wale mliowachinja (kabla hawajafa), na waliochinjwa juu ya vilinge (vya masanamu)} [Al-Maidah: 3].
Kuchinjwa kishari (Tadhkiya[1]) ya kisheria ina maana ya: Kumuua mnyama anayeliwa kwa kumchinja kooni, au kumchinja kifuani (nahr), au kumjeruhi kwa ajili ya kumuua (aqr) kupitia Muislamu au mmoja wa Watu wa Kitabu[2].
Ili iwe halali kula nyama ya mnyama aliyechinjwa, yanahitajika masharti matatu:
Sharti la Kwanza: Mnyama awe miongoni mwa wanaoliwa kama vile ngamia, ng'ombe, mbuzi, sungura, kuku na ndege Nk. Ikiwa mnyama haliwi, kama vile nguruwe, mbwa, punda wa kufugwa, na nyumbu, basi ni haramu kula nyama yake.
Sharti la Pili: Mnyama achinjwe kooni mwake, au kwenye kidimbwi cha koo (kifuani) ikiwa anaweza kudhibitiwa, au kwa jeraha lolote linaloondoa roho ikiwa hawezi kudhibitiwa kama vile mawindo.
Ni lazima mnyama achinjwe kwa moja ya njia tatu: Dhabhu (kooni), Nahr (kifuani), au Aqr (jeraha la kuua) ili iwe halali kumla. Ikiwa mnyama atauawa kwa njia nyingine tofauti na hizo, basi nyama yake ni mzoga na haijuzu kuila, sawa awe aliyemuua ni Muislamu, mtu wa Kitabu, au mwingineyo.
Sharti la Tatu: Mchinjaji au mwindaji awe miongoni mwa Waislamu au Watu wa Kitabu (Mayahudi na Wakristo). Sharia imeruhusu kichinjwa cha Muislamu au mtu wa Kitabu; Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na chakula cha wale waliopewa Kitabu ni halali kwenu, na chakula chenu ni halali kwao} [Al-Maidah: 5]. Na neno «Chakula» katika Aya hii ni la ujumla, linajumuisha wanyama waliochinjwa na vyakula vilivyotengenezwa kwa malighafi halali. Na jamhuri ya wafasiri (wa Qur`ani Tukufu) na Wanavyuoni wa Fiqhi wanaona kuwa makusudio ya "Chakula" katika aya hii ni wanyama waliochinjwa au nyama; kwa sababu hizo ndizo zilizokuwa sehemu ya shaka, ama aina nyingine za vyakula zilikuwa halali kwa mujibu wa asili yake[3].
Kulingana na hayo: Ikiwa mchinjaji si Muislamu wala si miongoni mwa Watu wa Kitabu — kwa kuritadi[4], mwabudu masanamu, mpagani[5], au muabudia moto (majusy) — basi kichinjwa chake si halali.
Na haya ndiyo masharti yanayofanya nyama kuwa halali na kujuzu kuliwa. Kwa kuyatumia maelezo haya kwenye nyama zinazoingizwa kutoka nje (imported meats); ikiwa ni nyama za wanyama wanaoliwa na zimechinjwa au kuchinjwa kifuani (nahr) kwa sifa iliyotajwa, na mchinjaji au mwindaji akawa ni Muislamu au miongoni mwa Watu wa Kitabu; basi hizo ni nyama zinazojuzu kuliwa na hazina uharamu wowote.
Njia ya kujua kuwa mchinjaji ni Muislamu au miongoni mwa Watu wa Kitabu ni kwa kupitia dhana yenye nguvu au uwezekano unaokubaliwa zaidi; kwa mfano, ikiwa wakazi wengi wa nchi hizo ni Waislamu, Wakristo au Mayahudi, na inajulikana kuwa wao huchinjaji na hawaharamishi kuchinja kufuata madai ya wale wanaoharamisha uchinjaji. Hata kama haijulikani kwa yakini kuwa ni kichinjwa chao, bali kwa kupitia tu habari zao (maelezo yao), na inatosha kwa hilo kuwepo kwa maneno yasemayo: «Wamechinjwa kwa njia ya Kiislamu»; kwani hiyo inachukuliwa kama aina ya taarifa kutoka kwa yule ambaye ana sifa za kuchinja.
Lakini ikiwa nyama zinazoingizwa kutoka nje zinatoka katika nchi ambazo si za Waislamu wala si za Watu wa Kitabu, kwa kuwa zinatoka katika nchi za waabudu masanamu na wapagani, basi haijuzu kuzila. Kadhalika, ikiwa nyama zinazotoka nje ni za wanyama wasioliwa kama vile nguruwe, mbwa, punda, na nyumbu, haijuzu kula nyama zao hata kama zimechinjwa na Muislamu au mtu wa Kitabu. Au ikiwa nyama hizo zilizoingizwa hazikuchinjwa, kama vile kufa kwa njia ya kupigwa shoti ya umeme, kunyongwa, au mambo mengine yanayofanywa na wale wanaoharamisha uchinjaji na kuua wanyama kwa shoti ya umeme au kwa kuwapiga kichwani; ikiwa hilo limejulikana kwa yakini, basi haijuzu kula nyama hizo, kwani ni mzoga ambao ni haramu kuula.
Tunapata faidia Kutokana na yaliyotangulia:
1- Hairuhusiwi kisharia kula nyama za ndege na wanyama wanaoruhusiwa kuliwa isipokuwa idhibitike Tadhkiya (uchinjaji wa kisharia) yao.
2- Uchinjaji wa ya kisharia ni kuondoa roho ya mnyama anayeliwa kwa njia ya Dhabhu (kuchinja kooni), Nahr (kuchinja kifuani), au Aqr (jeraha la kuua) kupitia kwa Muislamu au mmoja wa Watu wa Kitabu.
3- Inajuzu kula nyama zinazoingizwa kutoka nje ikiwa zinatoka nchi za Waislamu au nchi za Watu wa Kitabu; kwa sababu machinjio yao mengi huandikwa maneno: «Wamechinjwa kwa njia ya Kiislamu».
Ikiwa nyama hizo zinatoka katika nchi ambazo si za Waislamu wala si za Watu wa Kitabu, kwa kuwa zinatoka katika nchi za waabudu masanamu na wapagani, basi haijuzu kuzila.
5- Ikiwa nyama hizo ni za wanyama wasioliwa kama vile nguruwe, mbwa, punda, na nyumbu, haijuzu kula nyama zao hata kama zimechinjwa na Muislamu au mtu wa Kitabu.
6-Ikiwa nyama hizo hazikuchinjwa, kama kuwa mnyama amekufa kwa njia ya kupigwa shoti ya umeme, kunyongwa, au mambo mengine yanayofanywa na wale wanaoharamisha uchinjaji na kuua wanyama kwa mshtuko wa umeme au kwa kuwapiga kichwani; ikiwa hilo limejulikana kwa yakini, basi haijuzu kula nyama hizo, kwani ni mzoga ambao ni haramu kuula.
[1] "Tadhkiya": Inamaanisha kuondoa roho ya mnyama anayeliwa, kwa kumchinja shingoni (kwenye kidimbwi la koo) ikiwa ni ngamia, au kumchinja kooni ikiwa ni ng'ombe, mbuzi na mfano wao, au kumjeruhi sehemu yoyote ya mwili wake kama vile mawindo ikiwa hawezi kudhibitiwa isipokuwa kwa kufanya hivyo.
[2] "Watu wa Kitabu": Mayahudi na Wakristo.
[3] «Al-Mughni cha Ibn Qudamah» (13/293).
[4] «Murtadi»: Ni yule anayeacha Uislamu baada ya kuingia ndani yake.
[5] «Mkanamungu (Mulhid)»: Ni yule anayekataa kuwepo kwa Mwenyezi Mungu, Mitume, na jumbe za mbinguni.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
