Hasadi na jicho baya, na jinsi ya kujikinga navyo
Question
Je, jicho baya linaweza kusababisha hasadi kwa mtu na kumuua? Mtu anawezaje kujikinga na jicho baya na Hasadi?
Answer
Jicho baya au Hasadi: Ni Mtu mwenye Hasadi kutamani baraka za mtu anayemwonea Hasadi ziondoke, ambayo ni tabia ya kuchukiza na ugonjwa hatari ambao Mwenyezi Mungu Ametuamrisha kuomba atuhifadhi nayo. Mwenyezi Mungu Anasema: {Na shari ya hasidi anapo husudu} [Al-Falaq:5]. Hasadi humdhuru mtu mwenye Hasadi katika dini yake, Ikimfanya achukie qadar ya Mwenyezi Mungu, na humdhuru katika maisha yake ya dunia, ikimsababishia kuteseka kwa Hasadi Yake na kubaki katika taabu na matatizo.
Kuhusu Ghibtah au kushindana: Nako ni kutamani neema ile ile ambayo wengine wanayo, hakuna ubaya katika hilo kulingana na Sharia ya Kiislamu.
Sharia ya Kiislamu imetoa njia za kutibu na kuzuia Hasadi, ambazo ni kama ifuatavyo:
Kwanza, mtu mwenye Hasadi anapaswa kujitahidi kutomwonea Hasadi yeyote, na akiona kitu anachokipenda kwa wengine, anapaswa kumwaombea baraka.
Pili: yule anayehusudiwa anapaswa kujikinga kwa kusoma Sura mbili za kinga (Surat Falaq na Surat Annas), Surat Al-Fatiha (Al-Hamdu) Aya ya Kursiy na kusoma Ruqiyaa ya Qur`ani Tukufu na nyiradi kwa ujumla.
La tatu: Si sahihi kwa mtu kuwa na dhana potofu na mashaka kwa watu wengine, na kuwa tuhumu Hasadi kwa sababu tu ya matukio yanayomtokea, ambayo huenda hayahusiani kabisa na wale anaowadhania vibaya.
Maelezo
Hasadi na jicho baya ni sifa za kuchukiza na magonjwa hatari ambayo yameharamishwa na Sharia ya Kiislamu, tofauti na Ghibtah au ushindani, ambao ni kutamani neema zilezile ambazo wengine wanazo, na hakuna madhara katika hilo. Ndiyo maana Al-Fudayl bin Iyad alisema: "Ghibta hutokana na imani, na Hasadi hutokana na unafiki, Muumini huwa na Ghibtah na si hasadi, na mnafiki anahusudu na hana ghibtah." Imepokewa na Muslim
Mwenyezi Mungu Ametuamrisha kujikinga na hasaadi. Anasema: {Na Shari ya Hasidi anapohusudu} [Al-Falaq: 5].
Imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas (R.A) kwamba Mtume (S.A.W) amesema: "Hasadi kweli ipo, na kama kuna chochote kinachotangulia qadar, ni hasadi. Mnapooga, ogeni vizuri." Imepokewa na Muslim.
Kwa hiyo, Wanazuoni wanasema: "Ukweli ni kwamba mtu mwenye kijicho anapomtazama anayemshangaa na kumpenda, Mwenyezi Mungu hupeleka maumivu au uharibifu wowote anaoutaka, na anaweza kuzuia kabla haijatokea, ima kwa kuomba kinga (kwa Mwenyezi Mungu) au kwa njia nyingine, na anaweza kuuondoa baada ya kutokea kwa kusoma ruqya."
Hapa kuna swali muhimu linajitokeza: Je, Hasadi humdhuru mtu mwenye Hasadi na mtu anayemhusudu?
Kwanza: Hasadi humdhuru mtu mwenye Hasadi katika dini yake na maisha yake ya dunia zaidi kuliko inavyomdhuru mtu anayehusudiwa, humdhuru dini yake kwa sababu humfanya mtu mwenye Hasadi kuchukia qadar ya Mwenyezi Mungu, na kuchukia neema ambazo Amewagawia waja Wake. Inamdhuru katika maisha yake ya dunia kwa sababu inasababisha maumivu na mateso na kwa husda yake, na hubaki katika taabu na wasiwasi, hivyo kuharibu dini yake na maisha yake ya dunia bila faida yoyote.
Pili: mtu anayehusudiwa hadhuriki katika dini yake wala maisha yake ya dunia, kwa sababu baraka haizuiwi kwa sababu ya Hasadi; bali, chochote ambacho Mwenyezi Mungu Amewakadiria hakiwezi kuondoka, kwani kila kitu kipo kwenye kadari.
Tiba ya Hasadi na jinsi ya kujikinga nayo ni kama ifuatavyo:
Kwanza: Mtu mwenye Hasadi anapaswa kujitahidi kutomhusudu yeyote, na akiona kitu anachokipenda kwa mtu mwingine, anapaswa kumwombea baraka. Imepokewa kutoka kwa Abu Umamah bin Sahl bin Hanif kwamba alisema: "Amir bin Rabi'ah alipita karibu na Sahl bin Hanif alipokuwa anaoga, na akasema: 'Sijawahi kuona kitu kama hiki leo, wala ngozi iliyo laini hivi. Baada ya muda mfupi akaanguka chini, na akapelekwa kwa Mtume (S.A.W) akaambiwa, "Sahl amekutwa amekufa,?" Akasema, "Mnamtuhumu nani?" Wakajibu, "Amir bin Rabi'ah." Akasema: Kwa nini mtu kati yenu amuue ndugu yake? Atakaeona kati yenu kinachompendeza kwa ndugu yake, na amwombee baraka.”
Pili: Mtu anayehusudiwa anapaswa kujikinga kwa kusoma Sura mbili za kinga (Surat Falaq na Surat Annas), Sura ya Al-Fat’ha, Aya ya Kursy, Ruqiya na nyiradi kwa ujumla, na anapaswa kusoma dua za Mtume: kama vile: "Aaudhu bikalimatllah taammaat min sharri maaa khalaq."
Anapaswa pia kuongeza dua zake kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ili kuepukana na ubaya, jicho baya, na hasadi. Hakuna ubaya katika kutafuta ruqyah kutoka watu wema, imepokewa kutoka kwa Mama Aisha, Mama wa Waumini (R.A) kwamba amesema: (Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa akiniamuru nisome ruqyah dhidi ya jicho baya), na Asma bint Umays ameasema: (Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, watoto wa Ja'far wameathiriwa na jicho baya, basi niwatafutie ruqyah? Akasema: Ndiyo, kwani lau kama kuna kitu kinaitungulia kadari basi jicho baya).
La tatu: Sio sahihi kwa mtu kuwa na dhana potofu na mashaka kwa wengine. Haijuzu kwa Muislamu kuwadhania mabaya ndugu zake na kuwatuhumu kuwa wana Husda kwa sababu tu ya matukio yanayotokea kwa ghafla ambayo huenda hayahusiani na wale anaowadhania vibaya.
Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:
Jicho baya ni kweli lipo na lina athari watu kupitia hasadi, hivyo mtu anapaswa kujilinda kwa kusoma Qur`ani Tukufu, nyiradi kwa ujumla, na kutafuta ruqyah kutoka kwa watu wema.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
