Namna ya kuunga udugu

Egypt's Dar Al-Ifta

Namna ya kuunga udugu

Question

Je, kuunga udugu kati ya jamaa kunaishi tu kwenye kutembeleana, au kunaweza kuwa kwa njia nyingine?

Answer

Kuunga udugu ni miongoni mwa dalili za jinsi Uislamu unavyojali kuimarisha mafungamano ndani ya jamii; Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na tahadharini na Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana, na jamaa zenu.} [An-Nisaa: 1], yaani: ogopeni kuvunja udugu.

Mtume (S.A.W) amebainisha kuwa kuunganisha udugu wa kifamilia, kuwafanyia wema ndugu wa karibu na kuwapenda, malipo yake ni baraka katika umri na riziki; akasema (S.A.W) : «Anayependa kufunguliwa katika riziki yake au kuongezewa katika athari yake (umri wake), basi aunge udugu wake.»

Vilevile sharia imeonya dhidi ya kukata udugu wa kifamilia, na imetaja kuwa hilo ni miongoni mwa sifa za kijinga na kujitenga na dini ya Mwenyezi Mungu; amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Je, Basi yanayo tarajiwa kwenu mkitawala ndio mfisidi katika nchi na mwatupe jamaa zenu?} [Muhammad: 22]. Kwa ajili hiyo, wanazuoni wamesema kuwa kuunganisha udugu wa kifamilia (jamaa) ni wajibu; lakini hakuishii pekee na kutembeleana tu, bali kunaweza kufanyika kwa njia nyingine za kuwasiliana; kama vile kupeana zawadi, kupigiana simu, kuandikiana barua, kutuma salamu na njia nyinginezo.

Maelezo

Kuunganisha udugu wa jamaa[1] ni miongoni mwa dalili za jinsi Uislamu unavyojali kuimarisha mafungamano ndani ya jamii. Qur’ani Tukufu imeashiria umuhimu wa kuhifadhi uhusiano wa jamaa na kuendeleza mawasiliano yao; amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na tahadharini na Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana, na jamaa zenu. } [An-Nisaa: 1], ikimaanisha;  Ogopeni kuvunja uhusiano wa jamaa.

Aidha, Mwenyezi Mungu Mtukufu amewausia waja wake kuwafanyia wema wazazi, ndugu wa karibu, majirani na wahitaji; na hili ni baada ya kuwaamrisha wamuabudu Yeye peke yake; kuonyesha umuhimu wa kuimarisha maadili haya na kubainisha nafasi yake katika mtazamo wa Kiislamu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wawili na jamaa na mayatima na masikini na jirani wa karibu na jirani wa mbali, na rafiki wa ubavuni na mpita njia, na walio milikiwa na mikono yenu ya kulia. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wenye kiburi wanao jifakhiri,} [An-Nisaa: 36].

Mtume )S.A.W) amebainisha kuwa kuunganisha udugu wa jamaa, kuwafanyia wema ndugu wa karibu na kuwapenda, malipo yake ni baraka katika umri na riziki; akasema (S.A.W): «Anayependa kufunguliwa katika riziki yake au kuongezewa katika athari yake basi aunganishe udugu wake[2].»

Pia Sharia imeonya vikali kukata udugu, na imetaja kuwa jambo hilo ni miongoni mwa sifa za kijinga na kujitenga na dini ya Mwenyezi Mungu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Je Basi yanayo tarajiwa kwenu mkitawala ndio mfisidi katika nchi na mwatupe jamaa zenu?} [Muhammad: 22]. Na katika hadithi ya Abu Huraira (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake), Mtume(S.A.W) alisema: «Mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi aunganishe udugu wake[3].»

Na kutoka kwa Abu Huraira R.A kwamba Mtume (S.A.W) amesema: «Mwenyezi Mungu aliumba viumbe; alipomaliza, udugu  ukasimama na ukashika upande wa Ar-Rahman. akauwambia: Acha! Ukasema: Hapa ni mahali pa anayejilinda Kwako dhidi ya kukatwa. Akasema: Je, huridhii niwaunganishe wanaokuunganisha na niwakate wanaokukata? Ukasema: Ndio, Mola wangu. Akasema: Basi ndivyo hivyo.» Abu Huraira akasema: «Someni mkitaka: { Je, Basi yanayo tarajiwa kwenu mkitawala ndio mfisidi katika nchi na mwatupe jamaa zenu?[4]}»

Kwa sababu hiyo, Wanazuoni wamesema kuwa kuunga udugu ni wajibu; lakini hakujifungi tu na kutembeleana peke yake, bali kunaweza kufanyika kwa njia nyingine za kuwasiliana; kama vile kupeana zawadi, kupigiana simu, kuandikiana na kutumiana salamu, na njia nyinginezo.

Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:

Kuunga udugu ni wajibu, na ni miongoni mwa sifa za watu wa imani.

Kuunga hakujifungi na aina maalumu inayopatikana kwa njia moja tu; kama kunavyopatikana kwa kutembeleana, pia kunatimia kwa njia nyinginezo; kama zawadi, mawasiliano na kuandikiana ujumbe kwa njia ya simu.

 

[1] Al-Arhamu: Ni jamaa wa upande wa wazazi wote wawili.

[2] Amepkea imami Bukhari.

[3] Imepokewa na Imam Bukhari.

[4] Bukharin a Muslim.

Share this:

Related Fatwas