Haki za kifedha kwa mwanamke aliyea...

Egypt's Dar Al-Ifta

Haki za kifedha kwa mwanamke aliyeachika

Question

Ni zipi haki za mwanamke aliyepewa talaka baada ya kuingiliwa?

Answer

Mwanamke aliyepewa talaka baada ya kuingiliwa ana haki tano: ana haki ya matumizi ya kipindi cha eda, ambayo huamuliwa kwa makubaliano ya pande mbili au huamuliwa na kadhi, na hutofautiana kulingana na hali ya mtoa talaka kwa upande wa utajiri au umasikini; ana haki ya matumizi  ya kumfaiji, kwa sharti kwamba talaka haikuwa kwa ridhaa yake wala kwa sababu iliyotokana naye, ana haki ya pete ya uchumba[1]  kwa sharti iwe imezoeleka au imekubaliwa kati ya pande mbili kuwa ni mahari au sehemu yake; ana haki pia ya orodha ya vitu vya nyumbani kwa sharti iwe imezoeleka au imekubaliwa kati ya pande mbili kuwa ni mahari au sehemu yake; na ana haki ya mahari yote ikiwa ni pamoja na sehemu ya mahari iliyocheleweshwa.

Maelezo

Mwanamke aliyepewa talaka baada ya kuingiliwa anastahiki yafuatayo:

1- Mahari[2] yote, ikiwa ni pamoja na sehemu ya mahari yake iliyocheleweshwa, ambayo ni sehemu ya mahari iliyothibiti kwa mkataba wenyewe; na sehemu hiyo iliyocheleweshwa hulipwa kwa mojawapo ya muda ulio karibu zaidi kati ya talaka au kifo.

2- Orodha ya vitu vya nyumbani [3] na pete ya uchumba, kwa sharti kwamba iwe imezoeleka au imekubaliwa kati ya pande mbili kuwa ni mahari au sehemu yake.

3-Matumizi[4] kipindi cha eda [5], ambayo ndani yake hustahiki aina zote za huduma zinazompasa mke; na kadhi hurejea kauli ya mwanamke katika kubainisha muda wa eda yake kutoka kwa mumewe, kwa sharti kwamba muda huo usizidi mwaka mmoja tangu tarehe ya talaka.

4- Huduma za kumfariji[6], kwa sharti kwamba talaka haikuwa kwa ridhaa yake wala kwa sababu iliyotokana naye; kama vile talaka ya kujivua (khul‘u) au kwa kuachiliwa haki. Na huduma hii hukadiriwa kulingana na hali ya mtoa talaka kwa utajiri au umasikini, na huamuliwa na kadhi kwa mujibu wa anavyoona inafaa kwa hali iliyowasilishwa mbele yake, au kwa makubaliano ya pande mbili. Na wala huduma isipungue chini ya miaka miwili kama kiwango cha chini kwa kuzingatia muda wa ndoa na mazingira ya talaka; hayo ni kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Lakini wapeni cha kuwaliwaza, mwenye wasaa kadiri awezavyo na mwenye dhiki kadiri awezavyo - maliwaza kwa mujibu wa dasturi kuwa ni haki juu ya watendao mema} [Al-Baqara: 236], na pia kauli Yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na wanawake walio achwa wapewe cha kuwaliwaza kwa mujibu wa Sharia. Haya ni waajibu kwa wachamngu } [Al-Baqara: 241].

 

Na hili ndilo liliamuliwa na  sheria katika nchi ya Misri; kwani kifungu cha 18 (kilichoongezwa) kilichosisitizwa na Sheria Na. 25 ya mwaka 1929, kilichoongezwa kwenye Sheria Na. 100 ya mwaka 1985, kikisema kuwa:
“Mke aliyeingiliwa katika ndoa sahihi, mume wake akimpa talaka bila ridhaa yake wala bila sababu iliyotokana naye, anastahiki matumizi ya eda yake kumfariji (mut‘a) itakayokadiriwa kwa huduma ya angalau miaka miwili, kwa kuzingatia hali ya mtoa talaka kwa utajiri au umasikini,, na mazingira ya talaka, na muda wa ndoa; na inafaa kuruhusiwa kwa mtoa talaka kulipa tafrija hii kwa awamu.” Mwisho wa nukuu.

Basi tafrija hukadiriwa na kadhi kwa msingi wa matumizi yaliyo wajibu kipindi cha ndoa au matumi ya eda inayomlazimu, kulingana na hali ya mtoa talaka kwa utajiri au umasikini; kwa muda wa miaka miwili kama kiwango cha chini, kwa kuzingatia muda wa ndoa na mazingira ya talaka, kwa mujibu wa anavyoona kadhi inafaa kwa hali lililowasilishwa mbele yake.

Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:

Kuwa mwanamke aliyepewa talaka baada ya kuingiliwa ana haki tano: nazo ni huduma za eda, ambayo huamuliwa kwa makubaliano ya pande mbili au na kadhi, na hutofautiana kulingana na hali ya mtoa talaka kwa utajiri au umasikini; na matumizi ya tfrija (mut‘a) kwa sharti kwamba talaka haikuwa kwa ridhaa yake wala kwa sababu iliyotokana naye; na ana haki ya pete ya uchumba(shabka) kwa sharti iwe imezoeleka au imekubaliwa kati ya pande mbili kuwa ni mahari au sehemu yake; na ana haki pia ya orodha ya vitu vya nyumbani kwa sharti iwe imezoeleka au imekubaliwa kati ya pande mbili kuwa ni mahari au sehemu yake; na ana haki ya mahari yote ikiwa ni pamoja na sehemu ya mahari iliyocheleweshwa.

 

[1] Shabka; Pete ya uchumba ni mkusanyiko wa vito vya dhahabu au zawadi za thamani ambazo bwana harusi humpa bibi harusi wakati wa uchumba, kama ishara ya kujitolea na ahadi.

[2] Ni jina la mali anayostahiki mke kutoka kwa mumewe kwa sababu ya kufunga ndoa naye au kwa kuingiliwa.

[3] "Orodha ya mali inayohamishika": Hii ni tamko kutoka kwa mume kwenda kwa mkewe, kwenye hati yenye sahihi ya mume, ikisema kwamba amepokea vitu vya nyumbani (mali ya ndoa).

[4] Ni kukidhi mahitaji ya chakula, mavazi, makazi, na yanayoambatana nayo.

[5] Ni muda maalumu ambao mwanamke husubiri na hukaa katika nyumba ya ndoa baada ya kuachana na mume wake kwa sababu ya talaka au kifo.

[6] Ni jina la mali anayopaswa mwanaume kumlipa mke wake kwa kumuacha; kwa ajili ya kumtuliza moyo wake na kumsaidia.

Share this:

Related Fatwas