Kupaka (maji) juu ya «Soksi» katika...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kupaka (maji) juu ya «Soksi» katika Udhu

Question

Je, udhu unatenguka kwa kuvua tu «soksi» baada ya kupaka maji juu yake?

Answer

Kupaka juu ya soksi katika udhu ni jambo linalojuzu, lakini inapendekezwa ziwe nzito na isiyoonyesha ndani, na inajuzu kwa aliye katika hali ya dharura kama msafiri wakati wa harakati zake katika vyombo vya usafiri, au mfanyakazi katika sehemu yake ya kazi ambaye hawezi kuvua soksi, au askari jeshini akiwa amesimama katika ulinzi wa sehemu yake akilinda nchi yake na hawezi isipokuwa kupaka juu ya soksi nyepesi inayoonesha ndani; basi hakuna ubaya kwake katika hilo kwa kufuata waliolijuzisha hilo miongoni mwa Wanazuoni, na haifai kumkataza, kwa sababu kanuni ya kisharia zimepitisha kuwa: "Hakuna kukataza katika jambo lenye ikhitilafu".

Ama kuhusu muda wa kupaka, unaanza tangu wakati wa kupatwa na hadathi baada ya kuvaa soksi ukiwa na twahara, na ni kama ifuatavyo:

Inajuzu kwa mkazi katika nchi yake kupaka juu ya soksi mchana mmoja na usiku mmoja (saa 24).

Inajuzu kwa msafiri wa umbali wa kufupisha Swala -unaokadiriwa takriban kilomita (85)- kupaka juu ya soksi siku tatu na masiku yake (saa 72). Na baada ya kwisha muda huo, ni wajibu kwake kuvua soksi ikiwa anataka kutawadha. Ama kwa aliyevua soksi wakati wa muda wa kupaka akiwa bado ana twahara, hukumu yake ni: kwamba udhu wake hautenguki, bali inatenguka kwa hilo twahara ya miguu miwili tu bila viungo vingine vya udhu, na ni wajibu kwake wakati huo kuosha miguu miwili ikiwa anataka kuvaa soksi mara nyingine.

Maelezo

Uislamu ni dini ya wepesi na upole, na zimekuja hukumu za Sharia ya Kiislamu zikizingatia hali za watu, na kuendana na maumbile ya mwanadamu ambaye Mwenyezi Mungu alijua udhaifu wake; Mwenyezi Mungu anasema: {Mwenyezi Mungu anataka kukupunguzieni taabu, na mwanaadamu ameumbwa dhaifu.} [An-Nisa: 28], na imepokelewa kutoka kwa Anas Ibn Malik (R.A), kutoka kwa Mtume (S.A.W) amesema: ((Fanyeni wepesi wala msifanye uzito, na bashirini kheri wala msiwafukuze watu[1])).

Kwa hiyo Sharia ya Kiislamu imezingatia baadhi ya hali ambazo ni vigumu kwa mtu kuvua «soksi» kwa sababu ya baridi kali au kwa ugumu wa jambo hilo katika sehemu ya kazi au wakati wa harakati katika vyombo vya usafiri, au kama askari jeshini akiwa amesimama sehemu yake ya ulinzi kwa ajili ya kuilinda nchi na mfano wa hayo, basi Sharia tukufu imeruhusu katika hali hizo mtu kupaka juu ya «soksi» akitaka kutawadha badala ya kuosha miguu; kutoka kwa Al-Mughirah Ibn Shu'bah (R.A): «Kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) alitawadha na akapaka juu ya soksi mbili (jawrabayn) na viatu viwili»[2]. Wanazuoni wamekhitilafiana katika sharti za kupaka juu ya soksi katika rai mbili:

Ya kwanza: Rai ya jamhuri ya Wanazuoni (wengi) nayo ni kwamba ili kujuzu kupaka juu ya soksi kuna  sharti mbili ambazo ni lazima zipatikane:

Soksi iwe nzito kiasi cha kuzuia maji kufika kwenye ngozi.

Isiwe inayoonesha ndani kiasi cha kuonekana kilicho chini yake katika miguu.

Ya pili: Rai ya baadhi ya Wanazuoni nayo ni kujuzu kupaka juu ya soksi bila kuwekewa sharti mbili zilizotajwa, hivyo inajuzu kwao kwa anayetaka kutawadha kupaka juu ya soksi hata kama ni nyepesi inayoonesha ndani.

Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:

Na Fatwa iliyotolewa na Ofisi ya kutoa  Fatwa ya Misri  (Dar Al-Ifta Al Misri) ni kujuzu kupaka juu ya soksi, lakini inapendekezwa iwe nzito na isiyoonesha ndani, na inajuzu kwa aliye katika hali ya dharura kama msafiri katika vyombo vya usafiri au mfanyakazi sehemu ya kazi ambaye hawezi kuvua soksi, au askari jeshini akiwa amesimamia ulinzi na hawezi isipokuwa kupaka juu ya soksi nyepesi inayoonyesha ndani; hakuna ubaya kwake katika hilo kwa kufuata waliolijuzisha hilo miongoni mwa Wanazuoni, na haifai kumkataza; kwa sababu kanuni ya kisharia imethibiti: «Hakuna kukataza katika jambo lenye ikhitilafu».

Ama kuhusu muda wa kupaka, unaanza tangu wakati wa kupatwa na hadathi baada ya kuvaa «soksi» ukiwa na twahara, na ni kama ifuatavyo:

Inajuzu kwa mkazi katika nchi yake kupaka juu ya «soksi» mchana mmoja na usiku mmoja.

Inajuzu kwa msafiri umbali wa kufupisha unaokadiriwa takriban kilomita (85), kupaka juu ya «soksi» siku tatu na masiku yake.

Na baada ya kwisha muda huo, ni wajibu kwake kuvua «soksi» ikiwa anataka kutawadha.

Ama kwa aliyevua «soksi» wakati wa muda wa kupaka akiwa bado ana twahara, hukumu yake ni: kwamba udhu wake hautenguki, bali inatenguka kwa twahara hiyo miguu miwili tu bila viungo vingine vya udhu, na ni wajibu kwake wakati huo kuosha miguu miwili ikiwa anataka kuvaa «soksi» mara nyingine.

 

[1] Imepokelewa na Al-Bukhari.

[2] Imepokelewa na Abu Daud.

Share this:

Related Fatwas