Swala ya Ijumaa ikiafikiana na siku ya Idi
Question
Ni ipi hukumu ya Swala ya Ijumaa ikiafikiana na siku ya Idi? Je, Swala ya Ijumaa haitekelezwi ikiwa Idi ni siku ya Ijumaa? Na mnasemaje katika kutokutekeleza Swala ya Adhuhuri pia ikiwa Idi siku ya Ijumaa, kwa kutosheka na Swala ya Idi?
Answer
Ikiwa Idi siku ya Ijumaa, basi asili ni kuswali Swala ya Idi katika wakati wake, kisha kuswali Ijumaa katika wakati wake isipokuwa kwa wenye udhuru, ama asiyekuwa na udhuru na ameswali Swala ya Idi, basi asili kuziswali zote katika haki yake; ili kujiepusha kuwaacha Wanazuoni waliosema kutotekelezwa Ijumaa Swala ya Ijumaa kwa Swala ya Idi, kutoka katika tofauti kunapendeza, na mwenye kutaka kuchukua ruhusa ya kuacha Swala ya Ijumaa atakaposwali Idi katika jamaa, basi ataswali adhuhuri; kwa kufuata Madhehebu ya Hanbali.
Maelezo
Swala ya Ijumaa ni alama muhimu mno katika alama za Dini, nayo ni faradhi haitakiwi kwa inayompasa kuiacha au pasi na udhuru wa kisharia; Mwenyezi Mungu Anasema: (Enyi mlio amini! Ikiadhiniwa Swala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara….) [Al Jumaa:9].
Al Daar Qutny ametoa Hadithi katika Suna zake kutoka kwa Jabir bin Abdillah kwamba Mtume (S.A.W) amesema: “Mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya Mwisho basi adumu kuswali Swala ya Ijumaa, isipokuwa mgonjwa au msafiri au mwanamke, au mtoto mdogo au mtumwa, mwenye kuacha kuswali kwa upuuzi au biashara Mwenyezi Mungu naye atampuuza, na Mwenyezi Mungu ni Mkwasi Mwenye kusifiwa”.
Mwenye kuacha kuswali ijumaa pasi na udhuru anapata dhambi; kwa dalili iliyotangulia, na kwa Hadithi iliyopokelewa na Imamu Muslim katika Sahihi yake kwamba Mtume (S.A.W) amesema: “Watu ima waache kukosa Swala za Ijumaa, au Mwenyezi Mungu awapige mihuri katika nyoyo zao na kisha wawe ni wenye kughafilika”.
Kunapasa kwa Muslamu kuwahi kuhudhuria Swala ya Ijumaa baada ya kusikia adhana; kwa kauli ya Mwenyezi Mungu: (Enyi mlio amini! Ikiadhiniwa Sala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara.) [Al Jumaa:9].
Umma umekubaliana juu ya uwajibu wake kwa wanaume huru waliobaleghe wakazi, na umma umenukuu hilo kutoka kwa Wanachuoni wengi[1], na Swala ya Idi El Fitri na Idi Al Ad’haa, zimewekwa ili kudhihirisha furaha kwa kutimiza Ibada za funga na Hija, na Waislamu kukusanyika katika siku mbili hizi kwa kufurahia ibada mbili hizi, imepokewa kutoka kwa Anas (R.A) amesema: Mtume (S.A.W) alifika Madina na watu wa Madina walikuwa na siku mbili wakicheza katika siku hizo, akasema hizi ni siku za nini? Wakasema: Siku hizi tulikuwa tukicheza kabla ya Uislamu, Mtume (S.A.W) akasema: Hakika Mwenyezzi Mungu amewabadilishia siku nyingine bora zaidi kuliko hizi, siku ya Idi Al Ad’haa na siku ya Idi El Fitri” imepokelewa na Imamu Ahmad katika Al Musnad, na Al Hakim katika Al mustadrak na ameifanya kuwa sahihi.
Siku ya Idi ni siku ya furaha, pia ni siku ya kushukuru, Mwenyezi Mungu Anasema: (na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongoeni ili mpate kushukuru.) [Al Baqara:185], wanazuoni wamekubaliana juu ya uhalali wa Swala ya Idi.
Wanazuoni wa Fiqhi wametofautiana zikikutana Swala ya Idi na Ijumaa katika siku moja, na hili lipo katika kauli nne kwa kuzingatia hali za wanaosali:
Kwanza: Kwamba Swala ya Ijumaa ni wajibu na inatekelezwa haiachwi kwa Swala ya Idi, au moja yake kwa nyingine isipokuwa katika hali ya kuwepo dharura ya kisharia, kama maradhi, safari au mfano wa hayo, na haya ni Madhehebu ya Jamhuri ya Wanazuoni wa Hanafi, Malik na Shafi wamewafikiana nao kwa mkazi wa mjini na asie msafiri na katika njia nyingine kwa wakazi wa vijijini na maeneo ya mbali pia[2].
Pili: Ijumaa inatekelezwa kwa aliyeswali Swala ya Idi na akaenda maeneo ambayo hakukusaliwi Swala ya Ijumaa, kama majangwani na maeneo ya mbali na miji na vijiji hao tu pasi na wengine, na kwa sharti waswali Adhuhuri, na hii ni kauli ya Othman bin Affan (R.A) na Imamu Malik katika riwaya, na madhehebu kwa Shafi[3].
Tatu: Inatekelezwa kwa kuhudhuria Ijumaa kwa aliyeswali kwa sharti ya kuswali Adhuhuri, na haya ni Madhehebu ya Hanbali[4].
Nne: Adhuhuri na Ijumaa zinatekelezwa zote na hii ni kauli ya Ataa, na hii inachukuliwa kwa kuingiliana Swala mbili kwa pamoja kwa kujuzu kutanguliza wakati wa Ijumaa[5]. Na dalili yake ni Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Abou Daoud katika Al Sunan amesema: “Ibnu Zubeyr alituswalisha siku ya Idi katika siku ya Ijumaa asubuhi kisha tukaenda kuswali Ijumaa, hakutokea, tukaswali pekeyetu, ibnu Abbas (R.A) alikuwa Taif, alipokuja tukamwambia jambo hilo, akasema: Amepata Sunna”.
Na hii haifai kuwa dalili kwa kuwa ina shaka, na chenye mashaka kinabatilika kutolea dalili, kwani hii haijulishi kuwa hajaswali Adhuhuri nyumbani kwake, bali katika kauli ya Ataa kwamba wao wameswali peke yao, kwa maana Adhuhuri, inafahamika kuwa Adhuhuri haporomoki wakati huo.
Pia inaweza kuchukuliwa kuwa kuingia Swala ya Idi pamoja na Swala ya Ijumaa, kwa mujibu wa kauli ya waliojuzisha kuswali Ijumaa wakati wa Idi, na hili limepokewa kutoka kwa Imamu Ahmad, pia kutoka kwa Ataa mwenyewe ambao imenukuliwa kutoka kwake kauli yake: “Kila Idi inaswaliwa wakati wa Dhuhaa: Ijumaa na Idi Al Ad’haa na Idi El Fitri”.
Na uwelekezi huu unasisitiza kwamba riwaya ya Wahb bin Kaysaan kutoka kwa Annasaaiy aliposema: “Zimekutana Idi mbili zama za Zubayr, akachelewa kutoka mpaka ulipofika mchana, kisha akatoka akahutubia, akarefusha hotuba, kisha akashuka akaswali”. Na hakuwasalisha watu Ijumaa; kwani inajulikana kwamba hotuba ya Ijumaa inakuwa kabla ya Swala, na hotuba ya Swala ya Idi baada ya Swala, si kabla ya Swala.
Na asili ni kutoaporomoka Ijumaa kwa Swala ya Idi au moja yao kwa nyingine, ujumuishi umepokewa katika kauli ya Mwenyezi Mungu: : (Enyi mlio amini! Ikiadhiniwa Swala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu.) [Al Jumaa:9], haikutolewa katika hukumu hii si siku ya Idi wala siku nyingine.
Na asili ya kutofautiana katika Swala ya Ijumaa inapokutana na Swala ya Idi: tofauti katika usahihi wa Hadithi na mapokezi yaliyopokewa katika hilo kwa upande mmoja, na katika yale yanayotolea dalili kwa upande mwingine.
Miongoni mwayo: Yaliyopokewa na Abou Daoud, Annasaaiy, Ibnu Majah na Al Hakim kutoka kwa Iyas bin Abee Ramla Al Shamy amesema: “Nilimshuhudia Muawiya Bin Abou Sufyan akimuuliza Zayd bin Arqam R.A: Je, Ulishuhudia ukiwa na Mtume (S.A.W) Idi mbili zikikutana katika siku moja: akasema, ndio, akasema: Alifanya nini? Akasema: Aliswali Idi kisha akatoa ruhusa katika Swala ya Ijumaa akasema: “Mwenye kutaka na aswali”.
Na imepokewa kutoka kwa Abouhurayra (R.A) kwamba Mtume (S.A.W) amesema: “Siku yenu ya leo zimekutana Idi mbili, mwenye kutaka anaweza kutosheka na Swala ya Idi akaacha Ijumaa, na sisi tunakusanya (tunaswali zote). Imepokelewa na Abou Daoud, Ibnu Majah na Al Hakim.
Baadhi ya Wanazuoni wanaeleza kuwa kuswali Swala ya Idi hakuruhusu kuporomoka Ijumaa; wakitoa dalili kwamba dalili ya wajibu wa Saala ya Ijumaa ni inakusanya masiku yake yote, na kwamba zote mbili ni alama inayojitegemea haitegeme nyingine, na kwamba Hadithi na mapokezi yaliyopokea katika hilo hayana nguvu ya kuihusisha kutokana na Sanadi yake kuwa na shaka, na haya ni Madhehemu ya Wanazuoni waliowengi kama ilivyotangulia.
Pia haya mapokezi yanachukuliwa katika njia mbili, kwanza: Kuporomoka Ijumaa kwa watu wa mjini na wengineo na wanaswali Adhuhuri, na kauli nyingine: Kwamba ruhusa imepokewa katika hilo kwa watu wa majangwani na wale ambao Swala ya Ijumaa kwao si wajibu.
Hii pamoja na kuzingatia kwamba watu kuja kutoka sehemu za mbali ili kuhudhuria Ijumaa na Idi katika Msikiti na Mtume (S.A.W,) hakika ilikuwa kwa haja ya kukutana na Mtume (S.A.W,) na hii kwa sababu Sahaba zake walikuwa wanaona kusililiza hotuba zake, na kuhudhuria mkusanyiko wake hata kama makazi yao yapo mbali; kwa sababu yeye anafikisha kutoka kwa Mtume (S.A W,) na Mtungaji wa sharia na hukumu, na haja ilipopelekea hilo katika Amsaar wakaswali katika maeneo mbalimbali na hakukemea,ikiwa Ijumaa. Na maana hii ni ya Ibnu Qudama”.
Pia Swala ya Ijumaa ilikuwa ikisaliwa katika Msikiti mmoja na si Misikiti Mingi, kwa namna wanakusanyika watu wa mji na miji iliyokaribu katika zama za Mtume (S.A.W) na Makhalifa waongofu waliokuja baada yake, na hilo ni gumu kwa sasa kutokana na wingi wa Majengo na uwepo wa misikiti mingi ya Ijumaa katika maeneo mengi ya makazi yaliyo karibu karibu, pia kunafaa kuchuliwa maneno ya wanazuoni wa Fiq’hi yaliyopokewa katika kutofautisha kati ya vijiji na miji na miji mikubwa ni katika kupatikana au kutopatikana uzito katika kuhudhuria watu Ijumaa kutoka maeneo ya mbali katika wale ambao maeneo yao hayasaliwi Swala ya Ijumaa.
Na hili linaoneka katika tamko la Hadithi na Wanazuoni wa Fiqhi wakatoa sababu kwamba ruhusa katika kuporomoka kuhudhuria Ijumaa pamoja kuiswali Adhuhuri imepokewa kwa watu wanaokuja kutoka nje ya Madina yenye Nuru kipindi hicho, na ambao Swala ya Ijumaa kwao si wajibu; kwa kuwa kwao ni wakazi wa maeneo ya mbali na nje ya miji, hawa wakisubiri mpaka waswali Ijumaa itakuwa tabu kwao, pia lau wakirudi katika familia zao kisha wakaja tena kuswali Ijumaa pia.
Hivyo basi katika jambo hili kuna nafasi muda wakuwa na mas’ala yenye hitilafu na wala Madhehebu mamoja hayapingi Madhehebu mengine, Ijumaa inaswaliwa Misikitini kwa kufuata kitendo cha asili, na yule ambaye kumekuwa uzito kwake kuhudhuria Ijumaa au akataka kufuata ruhusa kwa kufuata kauli ya kuporomoka wajibu wa Ijumaa kwa kuswali Swala ya Idi basi anaruhusiwa kufanya hivyo, kwa sharti aswali Adhuhuri badala ya Ijumaa pasi na kumlaumu aliehudhuria Ijumaa au kumkemea aliyesali msikitini, vilevile pasi na kuibua fitina katika jambo lenye hitilafu pana tangu zamani.
Na ufahamu wa hilo unajengewa katika kanuni tau maarufu ya kuendesha hitilafu za Kifiqhi zinazonigatiwa ambazo wamezipitisha Wanazuoni, kwamba: “Hakuna kukemea katika masala ya hitilifu” na kwamba: “Mwenye kufanya kitu chochote katika masuala yenye hitilafu basi amfuate aliejuzisha” na kwamba: “Kutoka katika hitilifu kunapendeza kwa kila hali”pia katika “Kanuni za hukumu katika maslahi ya waja”.
Pia hakuna katika Sharia kwamba Swala za faradhi ni nne katika hali yeyote hata katika hali ya maradhi makubwa, bali hata katika vita, bali Swala ni tano kwa hali zote kama ilivyoelezwa na Matini za kukataza kama kauli yake alipomwambia bedui katika idadi ya Swala za Faradhi katika Uislamu: “Swala tano kila siku na usiku” imepokelewa na Bukhari na Muslim katika Hadithi za Talha bin Abdillah R.A.
Na kauli yake Mtume S.A.W alipomwambia Muaadh bin Jabal alipomtuma kwenye Yemen: “Wafundishe kwamba Mwenyezi Mungu amewafaradhishia Swala tano kila siku na usiku”. imepokelewa na Bukhary na Muslim katika Hadithi za Ibnu Abbas (R.A.) na kauli yake Mtume (S.A.W) “Swala tano amezifaradhisha Mwenyezi Mungu kwa waja” imepokelewa na Abou Dawoud na Annasaaiy katika Hadithi za Ubbada bin Samit (R.A) na nyinginezo katika Matini zilizokithiri.
Ikiwa Swala ya Faradhi haiporomoki kwa Swala nyingine ya Faradhi, basi vipi itaporomoka kwa kuswali Swala ya Idi ambayo ni Faradhi ya kutoshelezana kwa wote na Sunna kwa ngazi ya mtu mmoja mmoja?!
Sharia imewajibisha Swala tano kwa kutofautiana nyakati na sehemu na watu na hali, isipokuwa katika maeneo iliyovua, kama Hedhi na Nifasi kwa mwanamke, mpaka Mtume (S.A.W) alipoelezea muda wa Masih Dajjal kukaa duniani akasema: “Siku aroubaini: siku moja kwama mwaka, siku moja kama mwezi, na siku moja kama Ijumaa, na siku zilizobaki kama masiku yenu, Masahaba wakamuuliza: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, siku ambayo kama mwaka mmoja itatutosha kusali Swala ya siku moja? Akasema” Hapana, ikadirieni kiasi chake”. Imepokelewa na Muslim, na hii ni kama Matini ya kutoporomoka Swala ya Faradhi kwa hali yeyote na katika zama zozote.
Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:
Asili ni kwamba Swala ya Idi iswaliwe katika wakati wake, kisha iswaliwe Swala ya Idi katika wakati wake, isipokuwa kwa watu wenye udhuru, ama asiye na udhuru na akahudhuria Swala ya Idi, basi asili ni kusali Swala zote ili atoke kwenye hitilifu za jamhuri ya Wanazuoni wasemao kwamba Swala ya Ijumaa haiporomoki kwa Swala ya idi.
Kutoka kwenye hititlsfu kunapendeza, na mwenye kutaka kufuata ruhusa ya kuacha kuswali Ijumaa atakapokuwa ameswali Idi katika jamaa, basi huyo ataswali adhuri badala ya Ijumaa, kwa kufuata madhehebu ya Hanbali.
[1] Al Ijmaa cha Ibnu Al Mundhir Uk 40. Al Istinkar 2/56.
[2] Radd al Mukhtar 2/166.
[3] Al Dhakira 2/355, Al Umm 1/274.
[4] Al Kashaf Al Qanaa 2/43.
[5] Heelt al ulamaa fee maarifat madhaahib al fuqhaa, 2/226.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
