Kuhiji kwa niaba ya marehemu mmoja na kufanya Umra kwa niaba ya marehemu mwingine katika safari moja.
Question
Nataka kujua hukumu ya kisharia kwa mtu aliyekwenda Hija, na akatia nia ya umra kwa niaba ya mama yake aliyefariki, na nia ya Hija kwa niaba ya baba yake aliyefariki, na mwaka wa pili akafanya kinyume, kwa maana akatia nia ya Hija kwa niaba ya mama yake aliyefariki na umra kwa niaba ya baba yake aliyefariki, je, hili linafaa?
Answer
Hija na Umra zote ni ibada zinazojitegemea, zina nguzo zake na sharti zake, na wala hakujawekewa sharti katika safari moja kufanya Hija na Umra kwa mtu mmoja, kunajuzu kumfanyia umra mtu mmoja na Hija mtu mwingine.
Maelezo
Hija na Umra zote ni ibada zinazojitegemea, zina nguzo zake na sharti zake, na wala hakujawekewa sharti katika safari moja kufanya Hija na Umra kwa mtu mmoja, kunajuzu kumfanyia Umra mtu mmoja na Hija mtu mwingine.
Kunajuzu kwa Muislamu mwenye uwezo kuwafanyia Hija ndugu zake waliofariki au wagonjwa wasioweza kuhiji wenyewe, ikiwa yeye mwenyewe ameshatekeleza ibada ya Hija, au amuwakilishe mtu mwingine kuwafanyia Hija, na hii kwa Fatwa iliyochaguliwa katika uhalali wa kutekeleza ibada ya Hija kwa niaba ya mtu mwingine, kwa maana Hija ni katika ibada ambazo zinafaa kumwakilisha mtu anaposhindwa kwa mujibu wa makubaliano ya Wanazuoni wa Fiqhi wa Imamu Hanafi, Shafi na Hanbali, imepokewa kutoka kwa Imamu Bukhari na Muslim katika sahihi zao katika Hadithi ya Ibn Abbas R.A. amesema:” Alikuja mwanamke kutika Khath’am mwaka wa Hija ya kuaga, akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Hakika faradhi ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake katika Hija imemkuta baba yangu akiwa mzee sana, hawezi kupanda mnyama na kusafiri, je, inatosha kuhiji kwa niaba yake? Akasema: ndiyo”.
Na imepokewa kutoka Ibn Abbas R.A. amesema: “kwamba mwanamke kutoka Hujayna alikuja kwa Mtume (S.A.W.) akasema: Hakika mama yangu aliweka nadhiri kuhiji, hakuhiji mpaka amekufa, je, nimfanyie Hija kwa niaba yake? Akasema: ndio hiji kwa niaba yake, waonaje kama mama yake angekuwa na deni ungemlipia? Akasema: ndio. Akasema: basi mlipie deni la Mwenyezi Mungu, kwani Mwenyezi Mungu Ana haki zaidi ya kumtekelezea” imepokelewa na Bukhari katika Sahihi yake.
Na imepokewa kutoka kwake pia: “kwamba Mtume (S.A.W.) alimsikia mtu akisema: Nimekuitika Mwenyezi Mungu kwa niaba ya Shabruma. Akasema: Shabruma ni nani? Akasema: kaka yangu au ndugu yangu, akasema: Umetekeleza ibada yako mwenyewe? Akasema: Hapana. Akasema: Fanya Hija yako mwenyewe kisha mfanyie Hija shabruma” imepokelewa na Abu Daud na Ibn Maja katika Sunan yake na Al-Bayhaqy katika Sunan kubraa.
Kutoka na hayo kuna juzu kwa muulizaji kumfanyia Umra mama yake au baba yake waliofariki na thawabu za Hija na Umra zinawafikia kaburini pasina kupungua, isipokuwa Wanazuoni wa Fiqhi wametofautiana kuielezea Hija hii kwa namna hii iliyopokelewa katika swali, kwa upande wa kujuzu alichokielezea muulizaji katika hali ya AT-TAMAATUU, je kunapasa kwake kuchinja mnyama au laa?
Maana ya AT-TAMAATUU ni anaye hiji kuhirimia umra katika miezi ya Hija katika eneo la kuhirimia katika mji wake au sehemu nyingine katika maeneo anayopita au anayokaribiana nayo, kisha anatekeleza ibada ya umra na kuimaliza, kisha anaanza Hija katika mwaka wake pasina kurudi katika maeneo ya kuhirmia Hija.
Hii ndio sehemu inayowakutanisha Wanazuoni wa Fiqhi katika kuelezea neno AT-TAMAATUU, lakini wametofautiana katika kutokea kwake: Wanazuoni wa Imamu Hanafi, na Shafi na Hambal katika yanayotegemewa wanaona kwamba: hakuna sharti katika kutekelezwa Hija na Umra katika safari moja kwa mtu mmoja ili mtu aitwe ni mwenye kufanya AT-TAMAATUU, bali kunasihi kutekeleza ibada ya Umra kwa mtu na kumfanyia ibada ya Hija mtu mwingine([1]). Ama Madhehebu ya Imamu Malik imenukuliwa mara nyingi kutoka kwa Wanazuoni wake, baadhi yao wanaona hakuna sharti la kuteleza ibada mbili kwa mtu mmoja ili aitwe AT-TAMAATUU, kama rai ya Jamhuri ya Wanazuoni, na sahihi kama alivyoeleza Imamu Ad-Dardeer, huku wengine wanaona kwamba ni sharti[2].
Pamoja na haya, Wanazuoni wa Fiqhi wamekubaliana kwamba kunapasa kwa mwenye kufanya AT-TAMAATUU kuchinja mnyama ikiwa hayupo katika Msikiti wa Makka, na makubaliano haya yamenukuliwa na Imamu Al-Mundhir([3]).
Na mnyama anayepaswa kuchinjwa katika hili ni mbuzi, ng’ombe au ngamia, kushirikiana watu saba katika ng’ombe au ngamia, kwa makunaliano ya Wanazuoni, asiyekuwa na uwezo basi afunge siku tatu katika Hija na saba atakaporejea katika mji wake, na sababu ya mtu aliyefanya AT-TAMATUU kuchinja mnyama, ni kukusanya kati ya ibada mbili katika safari moja, Mwenyezi Mungu Amesema: (Basi mwenye kujistarehesha kwa kufanya Umra kisha ndio akahiji, basi achinje mnyama aliye mwepesi kumpata Na asiye pata, afunge siku tatu katika Hija na siku saba mtakapo rudi; hizi ni kumi kaamili. Hayo ni kwa ajili ya yule ambaye watu wake hawako karibu na Msikiti Mtakatifu)[Al-Baqarah:196].
Na kwa Hadithi iliyopokewa katika sahihi Muslim katika Hadithi za Abdullah bin Omar R.A. amesema: Mtume (S.A.W.) alifanya AT-TAMATUU katika Hija ya kuaga kwa kufanya Umra halafu Hija kisha akachinja mnyama, kisha akawachukua wanyama kutoka dhul Hulayfa, na Mtume (S.A.W.) akazna kuhirimia Umra, kisha akahirimia Hija na watu wakafnaya AT-TAMATUU na Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa kufanya Umra kisha Hija, baadhi ya watu walichinja na baadhi yao hawakuchinja, Mtume (S.A.W.) alipofika Makkah akasema: Enyi watu: Aliyechinja miongoni mwenu basi si halali kwake kitu chochote kilichoharamishwa kwake mpaka amalize Hija yake, na yule ambaye hajachinja basi afanye twawaf katika Al-Kaaba na Safaa na Marwa na anyoe nywele zake na atoke katika Ihramu, kisha ahirimie Hija na achinje mnyama, aliyekosa mnyama, basi afunge siku tatu katika Hija na saba atakaporejea kwa jamaa zake”.
Kutokana na yaliyotangulia na kutokana na swali: Kunajuzu kwako kumfanyia Umra mama yako aliyefariki, na kumfanyia Hija baba yako aliyefariki katika mwaka mmoja, kisha mwaka wa pili ukamfanyia Hija mama yako aliyefariki na ukamfinyia umra baba yako aliyefariki, ukifanya hivyo katika miaka miwili kunaitwa Kutamatuu, na kunapasa kwako kuchinja mnyama.
Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:
Kunajuzu kwa Muislamu mwenye uwezo kuwafanyia Hija ndugu zake waliofariki au wagonjwa wasioweza kuhiji wenyewe, ikiwa yeye mwenyewe ametekeleza ibada ya Hija, au kumuwakilisha mtu mwingine kuwafanyia Hija.
Hakua sharti katika kutekeleza ibada mbili- Hija na Umra- katika safari moja kwa mtu mmoja ili kuitwa mtu Muatamatuu, bali kunasihi kutekelezwa Umra kwa mtu, na Hija kwa Mtu mwingine.
Top of Form
Bottom of Form
([1]) Al-Hidaya (1/179, Al Maj’mou 7/177, Al-Kashaf Al-Kinaa (2/413).
([2]) Al-Sharh Al-Kabeer (2/30).
([3]) Al-Ishraf ala Madhaahib Al_Ulamaa, (3/296.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
