Kuishi kwa mwanamke aliyeachwa pamoja na mume wake katika nyumba moja
Question
Je, mwanamke aliyeachwa kwa talaka tatu kamili[1] (talaka ya mara tatu) anaweza kuishi pamoja na mume wake katika nyumba moja ili kulea watoto wao?
[1] Talaka ya Ba’in: ni talaka ambayo mume hataweza kumrudisha mke wake isipokuwa kwa ridhaa yake na kwa makubaliano mapya.
Answer
Mwanamke aliyeachwa talaka ya kurudi (talaka ya mara moja au mbili) anaweza kuishi pamoja na mume wake katika nyumba moja, na kwa hakika kumaliza eda (kipindi cha kusubiria baada ya talaka) katika nyumba ya ndoa ni wajibu kisharia, kwa kutarajia matumaini ya maridhiano baina yao.
Ama kwa aliyeachwa kwa talaka kuu – kaachika mara tatu - hairuhusiwi kwa mwanamke aliyeachwa talaka ya ba’in kuishi na mumewe katika nyumba moja baada ya kumalizika kwa kipindi chake cha eda, hasa katika zama hizi ambapo uovu umeenea, na kila mmoja wao anapaswa kupanga muda maalumu wa kulea watoto wake upande wake bila kupuuza haki zao.
Maelezo
Mwanamke aliye aliyeachwa talaka kuu – aliyeachwa kwa talaka tatu - anakuwa mgeni[1] kwa mume wake, hivyo si halali kuchanganyikana. Lakini mwanamke huyu anaweza kwenda katika nyumba ya ndoa kwa kuwepo kizuizi kati yake na mume wake, ili kuepuka uwepo wa wawili hao pekee[2];wawapo katika nyumba moja katika kipindi cha mwanamke kuwepo katika eda. Na wasikutane kama wenza wa ndoa, na wala kusiwe na hofu yeyote ya vishawishi. Dalilia ya hayo yote ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Ewe Nabii! Mtakapo wapa talaka wanawake, basi wapeni talaka katika wakati wa eda zao. Na fanyeni hisabu ya eda. Na mcheni Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi. Msiwatoe katika nyumba zao, wala wasitoke wenyewe, ila wakifanya jambo la uchafu ulio wazi. Hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu, msiikiuke. Na mwenye kuikiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi amejidhulumu nafsi yake. Hujui; labda Mwenyezi Mungu ataleta jambo jengine baada ya haya} [At-Talaaq: 1]
Na: akasema pia {Wawekeni humo humo mnamo kaa nyinyi kwa kadiri ya pato lenu, wala msiwaletee madhara kwa kuwadhiki. Na wakiwa wana mimba, wagharimieni mpaka wajifungue. Na wakikunyonyesheeni, basi wapeni ujira wao, na shaurianeni kwa wema. Na mkiona uzito kati yenu, basi amnyonyeshee mwanamke mwengine.}[At-Talaaq: 6]
Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaamuru waume kuwa wasiwatoe wake zao katika nyumba zao, na amewaamuru wake wasitoke. Na amri hii inahusisha wake alioachwa talaka ya kurudiwa na talaka tatu kamili[3] ikikusanya talaka ya kwanza na ya tatu, na muda wa eda unapomalizika mwanamke anatakiwa kuondoka kwenye nyumba ya eda kwenda kwake au kwa wazazi wake, kwani Sharia ya Kiislamu imeharamisha mchanganyiko wa mwanamke na mwanaume asiye maharimu wake, na mume aliyemtaliki huwa ni mgeni kwake. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema katika Qur’ani:
{Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, wala wasioneshe uzuri wao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawake wenzao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, au wafwasi wanaume wasio na matamanio, au watoto ambao hawajajua mambo yaliyo khusu uke. Wala wasipige chini miguu yao ili yajuulikane mapambo waliyo yaficha. Na tubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa.} [An-Nur: 31]
Pia katika Hadithi: kwamba Mtume (S.A.W) alisema: “Jihadharini na kuingia kwa wanawake. Mwanamume mmoja kutoka kwa Ansari alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, vipi kuhusu shemeji? Akasema: mkwe ni kifo.” (Bukhari na Muslim).
Mkwe ni mmoja wa jamaa wa mke au mume ambaye hana uhusiano wa damu au ndoa. Ikiwa hii inamhusu jamaa ambaye hana uhusiano wa damu au ndoa, basi inamhusu zaidi mgeni wa mbali, kama vile mume ambaye amemtaliki mkewe bila kubadilika na amekuwa mgeni kwake.
Malezi ya watoto, kuwajali mambo yao, kuwatunza, kuwarekebisha, kuwalea kimaadili, na kuwalisha kimwili, kiakili na kiroho, pamoja na kuwapatia misingi, kanuni za mwenendo, na vigezo vya kidini na kijamii ili kuwafikisha katika kiwango cha ukamilifu, ni amana na jukumu lililo juu ya wazazi ambao wataulizwa juu yake mbele ya Mwenyezi Mungu; hata hivyo, hiyo si sababu ya kuruhusu kukaa pamoja kwa mwanaume na mwanamke wageni katika nyumba moja. Na juu ya wanandoa, wakati wa kupanga talaka ni vema wakakubaliana juu ya namna ya kuwatunza watoto wao na kuchagua kilicho bora kwao kati ya kukaa kwao na mama yao nyumbani kwake au na baba yao nyumbani kwake.
Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:
1-Mwanaume anatakiwa kuepuka kuishi na mke wake aliyempa talaka tatu, na mke vile vile awe mbali na mumewe na wala hawaruhusiki kuishi katika nyumba au chumba kimoja baada ya kumalizika kwa eda, hasa kwa zama hizi zilizo na uovu uliosambaa kwani achungae karibu na mipaka kuna hatari ya kuvuka mipaka hiyo.
2-Wakati wa kupanga talaka, wanandoa wanapaswa kukubaliana jinsi ya kuwalea watoto wao na kuchagua yaliyo na maslahi kwao
[1] “Mwanamke mgeni" inamaanisha mwanamke ambaye si jamaa wa karibu wa mwanamume huyo, wala mtu ambaye anaruhusiwa kumuoa kupitia ndoa, kama vile mke. Ndugu wa karibu wa mwanamume ni mwanamke yeyote ambaye amekatazwa kumuoa kabisa, kama vile mama yake, dada yake, shangazi yake, shangazi yake, na kadhalika.
[2] “Khalwa (kuwa faraghani)”: ni hali ya mwanaume na mwanamke kuwa katika sehemu moja ambayo hakuna anayewaona, wala hakuna mwingine anayeingia kwao, kama chumba cha kulala na mfano wake. Kuwa faragha inaweza kuwa haramu; kama pale kunapotokea kukutana kati ya mwanaume na mwanamke mgeni kwa namna ambayo kwa kawaida haipo salama dhidi ya shaka.
[3] Mwanamke aliyepewa talaka kamili: ni mwanamke ambaye mumewe amempa talaka mara tatu, na akaharamika kwake.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
