Hija na Umra kwa njia ya mashindano
Question
Mimi na baadhi ya rafiki zangu tumeshiriki katika mashindano ya kitamaduni ambayo huandaliwa na moja ya taasisi za misaada, na wakatangaza kwamba zawadi ya mashindano hayo ni safari ya Hija au Umra, je, kunajuzu kwangu kwenda Hija au Umra nitakaposhinda katika mashindano hayo?
Answer
Hija na Umra kwa njia ya kushinda mashindano hayo kunajuzu kisharia wala hakuna ubaya katika hilo, isipokuwa mashindano hayo yawe kwa njia ya halali kwa mujibu wa hatua za kuandaa jambo hilo.
Maelezo
Uwezo unaowajibisha Hija unapatikana kwa kuwa na nguvu za mwili na uwezo wa kuvumilia mashaka ya safari ya kutekeleza ibada, usalama wa njia, pamoja na kumiliki gharama za mahitaji ya safari kama chakula, kinywaji, malazi, na nauli za usafiri zitakazomfikisha katika Nchi Takatifu kwenda na kumrudisha nyumbani bila kubana kupita kiasi wala kufanya israfu.
Na mashindano kimsingi ni halali kisheria, kwa kuwa yanalenga kuhamasisha akili na juhudi, na kwa sababu ni miongoni mwa njia ambazo mtu anaweza kupata na kukusanya mali, iwapo yatakuwa kwa malipo au fidia (kwa thamani ya kushiriki).
Ushahidi wa uhalali wake ni kauli ya Mwenyezi Mungu: (Hakika tulikwenda kushindana na tukamwacha Yusuf penye vitu vyetu)[Yussuf: 17] na kauli ya Mwenyezi Mungu: (Na katika hayo washindanie wenye kushindana)[Al-Mutaffifiin: 26].
Na yaliyopokewa kutoka kwa mama wa waumini Aisha R.A. kwamba alikuwa safarini na Mtume (S.A.W,) akasema: “Nikashindana naye, nikamshinda kwa mguu wangu, niliponenepa nikashinada naye akanishinda, akasema hii nimelipa ulivyonishinda mwanzo” imetolewa na Imamu Ahmad katika Musnad wake.
Ikiwa mashindano ni bila malipo, au malipo yanatolewa na mtu asiye mshindani, basi hakuna shaka kuwa ni halali na yanaruhusiwa.
Ama ikiwa malipo yanatoka kwa mmoja wa washindani au kwa wote wawili, basi wengi wa wanazuoni wa fiqhi miongoni mwa Hanafi, Shafi‘i, Hanbali, na baadhi ya Malikiyya wanaona kuwa aina zote mbili zinaruhusiwa, kwa sharti la kuwepo muhallil — yaani mshiriki wa tatu anayeingia pamoja nao katika shindano; akishinda hupata malipo, na akishindwa halazimiki kulipa chochote. Sharti hili linahusu hasa aina ya pili.
Na Hadithi ya Mtume S.A.W. “Hakuna mashindo isipokuwa ya ngamia au farasi au kurusha mishale” ambayo imepokelewa na Imamu Ahmad katika musnad wake haina maana ya kuwa mashindano yamefungwa katika hayo tu yaliyoelezwa, hii kwa sababu mambo haya matatu yalikuwa yanahimizwa kipindi cha vita zama za Mtume (S.A.W) , hivyo Wanazuoni wa Fiqhi juu ya kujuzu mashindano katika mambo haya matatu kutokana na matokeo yake ya kupatikana kwa nguvu na maandalizi ya kiakili na kimwili.
Na kwa ufafanuzi huu yanaingia mashindano yaliyoulizwa hapa, na ikiwa zawadi yake ni safari ya Hija au Umra, na badali katika mashindano hayo ni zawadi inayotolewa na wasioshindana, pia mashindano ambayo yanakuwa katika mtindo huu, hayatoki kuwa ujumla wake na kile kinachotakiwa kisharia katika kuandaa nguvu ya kisaikolojia na kiakili au vyote kwa pamoja ambavyo huchangamsha mazingira ya elimu na kulinda akili kiubunifu.
Hivyo inajuzu Hija au Umra pale unaposhinda vyote viwili au kimoja chao katika mashindano haya, na hakuna ubaya katika hili, na kuwa yote haya kwa njia ya halali na kwa mujibu wa hatua za maandalizi maalumu katika suala hili.
Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:
Uwezo ni sharti katika kupasa Hija ikiwa pamoja na uwezo wa mwili kuvumilia tabu za safari katika kutekeleza ibada ya Hija, na njia kuwa salama, na kumiliki matumizi ikiwemo chakula, vinywaji, na malazi na matumizi na usafiri ambao utamfikisha mji mtukufu wakati wa kwenda na kumrudisha katika mji wake wakati wa kurudi pasina kujinyima au ubadhirifu
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
