Wasia kwa Hija ya Faradhi
Question
Baba yangu imemuwajibikia ibada ya Hija, na ameazimia kuitekeleza, isipokuwa hakuweza kutokana na maradhi yaliyompata kabla ya safari, na ameniambia kwamba akipona, basi atahiji mwenyewe mwaka unaofuata, na akatoa wasia kwamba akifariki nikahiji kwa niaba yake kwa mali yake, na aliendelea na maradhi mpaka akafariki, ni ipi hukumu ya kisharia katika hili?
Answer
Mtu aliyefariki akitoa wasia wa kufanyiwa Hija kwa mali yake, na hakukuwa na mvutano kwa warithi katika kuthibitisha wasia huu, kwa kuwa gharama za Hija zinatoka katika mali yake aliyoiacha katika mpaka wa theluthi yake kwa wajibu, wala haitoki nje ya theluthi isipkuwa kwa makubaliano ya warithi, na hii ni katika haki ya aliyekuwa miongoni mwao ni katika watu wa kutoa anejua kinachomtosha.
Maelezo
Wanazuoni wa Fiqhi wa Madhehebu ya Hanifa wameuelezea wasia kuwa ni “Milki inayoongezwa mpaka baada ya kifo” Madhehebu ya Malik wameulezea kuwa: “Ni mkataba unawajibisha haki katika theluthi ya aliyefunga mkataba, inayolazimu kwa kifo chake au kwa niaba yake baada yake” Madhehebu ya Shafi wameuelezea kuwa: “Ni sadaka inayotolewa katika haki ya kinachoongezwa japo kwa kukadiriwa baada ya kifo” Madhehebu ya Hanbali wameilezea kuwa: “Ni amri ya kuchukua hatua baada ya kifo, na wasia wa mali ni kuitoa sadaka baada ya kifo”.[1].
Katika maana hizi tunapata faida kwamba wasia unakuja kwa maana ya kujitolea mali na kuitumia, na inakuja kwa maana kuusia kitu au juu ya kitu, maana ya kwanza: Kunakuwa kutumia mali kunategemezwa na baada ya kifo, maana ya pili: Ni muusia kumueweka mtu mwingine sehemu yake katika jambo baada ya kifo chake, kama mtu kuusia kuozesha mabinti zake, au kupanga sehemu atakayozikwa, au watakaomsalia au kumuosha na mfano wa hayo.
Na wasia ni halali kwa Ushahidi wa Qur`ani Tukufu,Hadithi za Mtume (S.A.W) na makubaliano ya Umma.
Katika Qur`ani Tukufu ni kauli ya Mwenyezi Mungu: “Haya ni baada ya kutolewa alicho usia au kulipa deni” [An-Nisaa:11]. Na Kauli yake: “baada ya wasia waliyo usia au kulipa deni” [An-Nisaa:12].
Na katika Hadithi ni iliyopokelewa kutoka kwa Saad bin Abee Wiqas R.A “Kwamba Mtume (S.A.W) alikuja kumuona alipokuwa mgonjwa akiwa Makkah, akasema Saad R.A: Ewe mjumbe wa Allah, niusie mali yangu yote? Akasema: Hapana: nikasema nusu yake? Akasema: Hapana. Nikasema theluthi, akasema: basi Usia katika theluthi na theluthi ni nyingi”. Imepokelea na Bukhari na Muslim.
Na imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Umar R.A. kwamba Mtume (S.A.W) amsema: “haiwi sawa kwa Muislamu mwenye kitu anataka kuusia katika kitu hicho, zikapita siku mbili bila ya kuandika wasia huo” imepokelewa na Bukhari na Muslima.
Na tangu zama za Mtume (S.A.W.) mpaka sasa watu wanaendelea kuacha wasia na hakuna yeyote anayekemea, hili linakuwa ni makubaliano ya umma”, na Wanazuoni wamekubaliana katika zama zote na sehemu zote kuwa wasia unajuzu”.
Na wasia wa maiti unatekelezwa kwa mali, ukithibiti kwa kile kinachothibitisha haki za kulipa- katika mpaka wa theluthi ya mali kwa njia ya wajibu, sawasawa mtoa usia aliufunga wasia wake kwa theluthi au hakuufunga, na kunajuzu kutekeleza wasia katika zaidi ya theluthi ya mali kwa makubaliano ya warithi ikiwa ni katika watu wa kujitolea sadaka wanaujua wanachokifanya kwa makubaliano ya Wanazuoni wa Fiqhi.
“Wanazuoni wa Fiqhi wamekubaliana katika sehemu zote kwamba wasia zaidi ya theluthi ya mali warithi wakiuruhusu basi inajuzu, na kama warithi hawakuruhusu basi haifai isipokuwa theluthi”[2].
Hivyo basi, Aya ya 71 katika kifungu cha sheria ya urithi namba 71 katika shria ya mwaka 1946, kinaeleza kwamba: “Wasia unasihi kwa theluthi kwa warithi na watu wengine, na unatekelezwa hata kama warithi wakikataa, na unasihi kwa zaidi ya theluthi, na ziada ya theluthi haifanyiwi kazi isipokuwa kwa ruhusa ya warithi baada ya kifo cha mrithiwa na wakawa watu wenye uwezo na kutoa sadaka wanajua wanachokiruhusu”.
Hivyo basi mtu akiusia kufanyiwa Hija ya faradhi, basi Fatwa iliyochaguliwa ni kwamba wasia wake unatekelezwa kwa gharama za zilizo ndani ya kiwango cha theluthi ya mali yake kwa njia ya wajibu, na haya kwa mujibu wa Madhehebu ya Hanafi na Malik.
Na rai hii pia ni Madhehebu ya kundi la wema waliotangulia kama Hamad bin Abee Sulayman Al-Kkufy, Daud bin Abi Hind, Hamdaan bin At-Taweel, Abee Amr Al-Bintiy, Ibn Sireen, Al-Nakhee, Ash-Shaaby na Al-Thawry[3].
Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:
Wasia ni halali kwa Ushahidi wa Qur`ani Tukufu na Hadithi na makubaliano ya Umma.
Mtu akiusia kufanyiwa Hija ya faradhi, basi wasia wake unatekelezwa kwa gharama za Hija hii katika mpaka wa theluthi ya mali aliyoiacha kwa njia ya wajibu.
([1]) Badaaii As-Saanee, 7/330, Al-Mukhtasar 10/428.
([2]) Umdat Al-Qary, 8/91.
([3]) AlIshraf cha Imamu Inbu Al-Mundhir, 4/418.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
