Kutoa nyama au mali badala ya kuchi...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutoa nyama au mali badala ya kuchinja Udh’hiya

Question

Tumesikia kwamba bwana wetu Abdullah bin Abbas R.A. alikuwa akinunua nyama badala ya kuchinja mnyama, na anasema: “Hii ni Udh’hiya yetu”. Je, kunajuzu kubadilisha nyama kwa udh’hiya?

Answer

Katika yale waliyokubaliana Wanazuoni katika Madhehebu ya Fiqhi yanayotegemewa ni kwamba miongoni mwa sharti za kusihi Udh’hiya nikuwa katika wanyama: ngamia, ng’ombe, mbuzi na kondoo, mbuzi au kondoo anatosha kwa mtu mmoja, na ngamia na ng’ombe wanatosha kwa watu saba, wala hakutoshi kunua nyama au kitu kingine, au kutoa sadaka ya mali; kwa kuwa hii ni ibada inayokusudiwa yenyewe.

Ama kununua nyama na kuitoa sadaka au kuwapa fedha mayatima na wahitaji miongoni mwa mafukara na masikini, jambo hili linapendeza kisharia na Muislamu anapata thawabu kwa kulifanya, lakini halitoshelezi kuchinja wala halichukui nafasi yake.

Maelezo

Udh’hiya ni alama katika alama za dini na Sunna yenye kusisitizwa, ameifanya Mtume (S.A.W) na ameamrisha kuifanya, na akaipendekeza kwa Masahaba zake, imepokewa Hadithi kutoka kwa Anas R.A amesema: “Mtume (S.A.W.) alichinja kondoo wawili weupe na mapembe, aliwachinja kwa mkono wake, na akasema Bismillah Allah Akbar, na akaweka mguu wake juu ya shingo yake” Hadithi hii imepokelewa na Bukhari na Muslim.

Na ni karaha kuacha Udh’hiya kwa mwenye uwezo, kwa kauli yake (S.A.W.)“Mwenye kuwa na uwezo na hajachinja, basi asikaribie sehemu yetu ya kuswali Swala ya Idi” imetolewa na Imamu Ahmad katika Musnad  na Ibn Maja katika Al Sunan.

Na Udh’hiya hatoshi isipokuwa Ngamia, ng’ombe au mbuzi na kondoo, na kinachosihi kuingia katika hawa kama nyati, na imesimuliwa makubaliano ya hilo isipokuwa Mwanazuoni mmoja, kama Imamu Ibn Abdul Al-Barr.

Na muktadha wa hilo ni kwamba haitoshi katika Udh’hiya kutoa pesa au kununua nyama au mfani wake na kutoa sadaka kuwa hiyo ni udh’hiya, na yale yaliyopokewa kutoka kwa baadhi ya wema waliotangulia katika kutoa sadaka kwa pesa badala ya udh’hiya, hilo linachukuliwa kwamba baadhi yao walikuwa wanaona kwamba kuwapa sadaka mayatima na

wahitaji kwa thamani ya udh’hiya ni bora kuliko kuchinja, na kwa kauli hii amesema Al Shaaby na hii ndio kauli ya  Imamu Malik na Abii thawr.

Na yaliopokewa kutoka kwa Ibn Abbas katika yaliyotolewa ushahidi katika swali ni kwamba alikuwa ananunu nyama na anachinja: hili halimaanishi kuwa kununu nyama inatosheleza na ibada ya kuchinja ina inaingia nafasi yake, bali hili lilikuwa kwa kukusudia kuwataaarifu watu kwamba udh’hiya si wajibu wa moja kwa moja, bali ni Sunna iliyosisitizwa ya hiyari kwa haki ya mwenye uwezo, na kunajuzu kuwa amechinja na ametoa sadaka nyama yake yote na akaenda kujinunulia nyama mwenyewe, na akasema hii ni Udh’hiya ya Ibn Abbas yaani ni  badala ya fungu langu lake la udh’hiya.

Pamoja na kwamba yeye alikuwa anachinja sana kila siku kama zinavyoeleza taarifa na simulizi, iweje awe anachinja kila siku na asichinje siku ya idi?! Bali alikuwa akifanya hivyo ili watu wasifikiri kuwa ni wajibu, na alikuwa ni Imamu anayefuatwa.

Kununua nyama na kuitolea sadaka kwa kuwapa mayatima na wahitaji katika masikini na mafukara ni jambo zuri kisharia na linathawabu, lakini halitoshi kuacha kuchinja na wala halichukui nafasi yake.

Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:

Udh’hiya ni ibada katika ibada za dini na alama katika alama zake thabiti.

Mnyama anayetosha katika ibada ya Udh’hiya anaweza kuwa ngamia, ng’ombe au mbuzi na kondoo, wala haitoshi kununua nyama au kitu kingine, au kutoa sadaka ya pesa; kwakuwa hii ni ibada inayokusudiwa yenyewe,

Anayetaka kuchinja anaweza kutoa sadaka ya pesa akiwaona watu wanaomzunguka wanahitaji mali zaidi kuliko nyama, isipokuwa hiyo sadaka haihesabiwi kuwa ni Udh’hiya, bali ni sadaka katika sadaka.

Share this:

Related Fatwas