Kuchinja Aqiqah katika nchi nyingin...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuchinja Aqiqah katika nchi nyingine

Question

Hivi karibuni, zimeibuka baadhi ya Taasisi za hisani zinazotangaza kufanya Aqiqah katika baadhi ya nchi masikini za Afrika kwa niaba ya yeyote anayetaka baada ya kukusanya bei yake, ikizingatiwa kuwa bei yake huko ni ya bei nafuu kuliko bei yake ya ndani. Tunataraji kufahamishwa kuhusu hukumu yake kisharia.

Answer

Inafaa kuchinja Aqiqah katika mji wa yule anayefanya Aqiqah na nchi yake. Ikiwa yule anayefanya Aqiqah amewakilisha kuchinja Aqiqah nje ya mji wake, itamtosha, na yote hayo kwa sharti la kuwatosheleza masikini wa mji wake na nchi yake, na hii haitapatikana isipokuwa kwa kushirikiana na Taasisi na vyombo vinavyohusika na hilo; kwa sababu ndivyo vinavyohusika na kutoa taarifa kuhusu kuwepo kwa ziada juu ya mahitaji ya nchi au kutokuwepo kwake.

Maelezo

Aqiqah katika asili yake ya lugha imetokana na neno la "ʿaqqi", ambayo ni: kupasua na kukata, na inatumika na inamaanishwa nayo nywele ambazo mtoto huzaliwa nazo; kwa sababu zinapasua ngozi yake ili zitoke ndani yake, na pia inatumika na inamaanishwa nayo mnyama anayechinjwa katika siku ya kunyoa nywele hizi kwa Sunna katika siku ya saba ya kuzaliwa kwake kama ilivyokuja katika Sunna ya Mtume yenye heshima, hivyo kuitaja mnyama aliyechinjwa kwa jina la Aqiqah ni katika kuitaja kitu kwa kile kinachoambatana nacho au kilichokuwa sababu yake.

Na Aqiqah katika asili yake ni moja ya desturi zinazojulikana kwa Waarabu, ambapo walikuwa wakifanya hivyo kwa upole kwa kueneza nasaba ya mtoto baada ya kuzaliwa kwake na kuwaheshimu watu na kuwalisha, hivyo akaja Nabii (S.A.W.) akaikubali na akaamrisha kwayo na akaifanya yeye na masahaba wake watukufu (R.A.) na masalaf na makhalaf baada yao bila ya kukanushwa.

Kutoka kwa Buraidah (R.A.) alisema: “Tulikuwa katika Jahiliyyah ikiwa mmoja wetu amezaliwa mvulana, alichinja kondoo, na akampaka kichwa chake damu yake, na alipokuja Mwenyezi Mungu na Uislamu, tulikuwa tukichinja kondoo, na tunamnyoa kichwa chake, na tunampaka zafarani” Imepokewa na Abu Dawud katika "Sunan", na At-Tahawi katika "Mushkil Al-Athar", na Al-Bayhaqi katika "Sunan al-Kubra", na Al-Hakim katika "Mustadrak".

Na kutoka kwa Salman bin Amir Ad-Dabbi (R.A.) kwamba Mtume (S.A.W.) alisema: “Pamoja na mvulana kuna aqiqah; hivyo mtoeni damu kwa ajili yake, na muondoeni uchafu kutoka kwake” Imepokewa na Al-Bukhari.

Na Wanazuoni wa Fiqhi wametofautiana katika hukumu yake; hivyo wakaenda wengi wa Wanazuoni wa Fiqhi kutoka Maliki, Imamu Shafi na Hanbali kwamba ni Sunna iliyokokotezwa, na hiyo ndiyo iliyopokewa kutoka kwa Bibi Fatimah Az-Zahra (R.A.) binti ya Mtume (S.A.W.), na Mama wa Waumini Bibi Aisha (R.A.), na Abdullah bin Abbas na Ibn Umar (R.A.), na Buraidah Al-Aslami na Urwah bin Az-Zubayr (R.A.), na Al-Qasim bin Mohammed na Ata na Az-Zuhri na Abu Az-Zinad.

Na Imamu Hanafi wakaenda kwamba ni katika aina ya Sunna' akipenda afanye, na akipenda asifanye, na imekuwa ikifanyika kwa vizazi vyote kuchinja Aqiqah katika mji wa yule anayefanya Aqiqah na kutohamishia katika nchi nyingine, hivyo kuchinja katika mji na nchi ya yule anayefanya Aqiqah ni bora na thabiti zaidi kuliko kuchinja nje ya mji wake, na ingawa kuwakilisha katika kununua na kuichinja inaruhusiwa hata kama katika mji mwingine.[1]

Na baadhi ya wachunguzi kutoka Wanazuoni wa Fiqhi wamechunguza upendeleo wa mahali penye sifa ya kuchinja na kugawanya Aqiqah kwa ajili ya mtoto aliyezaliwa, na je, inahusiana na mji wa mtoto au mji wa yule anayefanya Aqiqah ikiwa miji yao inatofautiana? Wakithibitisha uhusiano wa mji wa yule anayefanya Aqiqah na kuichinja humo na kuigawanya kwa watu wake ni bora; ili kutimia hekima ya kisharia ya Aqiqah, na kwa sababu yule anayefanya Aqiqah ndiye anayetakiwa kuitimiza.

Na ingawa kuna tofauti katika Aqiqah je, inachinjwa katika mji wa mtoto au mji wa yule anayefanya Aqiqah? Basi kuitoa katika mji wa nje yao wawili ni mbali zaidi na kusudio lake.

Na hekima katika hili ni kwamba kusudio la Aqiqah ni kuwalisha watu wa mji wa yule anayefanya Aqiqah, na kuwasaidia mahitaji na kufurahia zawadi iliyotolewa, na kueneza nasaba yake kati yao, na kueneza shukrani kwa Mtoaji Mwenyezi Mungu Mtukufu, hivyo kuchinja katika mji wake mbele ya watu wake na jamaa zake na majirani zake ili wale kutoka humo ni bora na thabiti zaidi, kama vile watu wa kila mji wana haki zaidi ya sadaka yao kutokana na asili.

Inaongezwa kwa hayo yaliyo ndani yake ya kutunza haki ya ujirani; kwani maandishi ya kisharia yameenea katika kudhihirisha ukubwa wa haki ya jirani na Sunna ya kumtunza kwa wema; miongoni mwa hayo: kauli ya Mwenyezi Mungu (S.W.): {Na muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote, na kwa wazazi wema, na kwa wenye ukaribu na mayatima na masikini na jirani wa ukaribu na jirani wa mbali na mwenzako wa karibu} [An-Nisaa: 36].

Na miongoni mwake: yaliyopokelewa na Ibn Umar (R.A.) kwamba Mtume (S.A.W.) alisema: “Hakukoma Jibril kuniusia kuhusu jirani, hata nilidhani kwamba atamrithisha” Imepokelewa na Masheikh wawili (Bukhari na Muslim).

Na kutoka kwa Abu Dharr (R.A.) kwamba Mtume (S.A.W.) alisema: “Ee Abu Dharr, unapopika mchuzi, zidisha maji yake, na utunze majirani zako” Imepokelewa na Al-Bukhari.

Hivyo kuchinja kwa yule anayefanya Aqiqah katika mji wake kunajumuisha maana ya kumuheshimu jirani na kumtunza kwa wema, hivyo wema ndani yake ni mpana zaidi na fadhila ndani yake ni kamili zaidi.

Na ikiwa jirani ni mwenye ukaribu, basi njia za wema zimegawanyika ndani yake wakati huo, kwani wakati huo inajumuisha fadhila ya Aqiqah, na wema kwa jirani, na kushikamana na jamaa, kama ilivyodhihirishwa na Hadithi ya Salman bin Amir Ad-Dabbi R.A. kwamba Mtume (S.A.W.) alisema: “Sadaka kwa masikini ni sadaka, na kwa mwenye ukaribu ni mbili: sadaka na kushikamana” Imepokelewa na Ibn Majah katika "Sunan" yake, na ndani yake kuna tamko wazi kwamba tendo linaweza kukusanya thawabu ya matendo mawili kwa kutimia makusudi yao kwa hilo, hivyo kwa mfanyaji wake yote yaliyokuja katika thawabu zao kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na neema zake.

Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:

Aqiqah ni fadhila mojawapo ya fadhila na mema ambayo mfanyaji wake atapewa thawabu na asiyeweza kuifanya hapati dhambi.

Inafaa kuchinja Aqiqah katika mji wa yule anayefanya Aqiqah na nchi yake.

Ikiwa yule anayefanya Aqiqah amewakilisha kuchinja Aqiqah nje ya mji wake, itamtosha, na yote hayo kwa sharti la kuwatosheleza masikini wa mji wake na nchi yake, na hii haitapatikana isipokuwa kwa kushirikiana na Taasisi na vyombo vinavyohusika na hilo; kwa sababu ndivyo vinavyohusika na kutoa taarifa kuhusu kuwepo kwa ziada juu ya mahitaji ya nchi au kutokuwepo kwake.

 

[1] «An-Nawādir wa Az-Ziyādāt» ya Ibn Abi Zayd Al-Qayrawani (4/332, ch. Dar Al-Gharb Al-Islami), na «Al-Kāfī» ya Ibn Abdul-Barr (1/425, ch. Maktabah Ar-Riyadh Al-Hadithah), na «Al-Majmū'» ya An-Nawawi (8/426-447, ch. Dar Al-Fikr), na «Al-Mughnī» ya Ibn Qudāmah (9/459, ch. Maktabah Al-Qahirah), na «Mukhtasar At-Tahāwī» (7/292, ch. Dar Al-Bashā'ir Al-Islamiyyah), na «Al-'Uqūd Ad-Durriyyah» ya Ibn 'Ābidīn (2/212, ch. Dar Al-Ma'rifah).

Share this:

Related Fatwas