Wito wa kukusanyika kwa ajili ya kumswalia Mtume wetu Mohammad (S.A.W.), siku ya Ijumaa
Question
Baadhi ya rafiki zangu wameniuliza kuhusu maamuzi ya Wizara ya Wakfu ya Misri ya "kumswalia Mtume" katika Misikiti yote baada ya Swala ya Ijumaa ijayo kwa dakika tatu au tano katika tamko la Kiibrahimu, na wanasema kwamba jambo hili ni Bidaa na wananihimiza niondoke Msikitini mara tu baada ya salamu ya Imamu kwa sababu nitashiriki katika kitendo hicho. Ningependa kunijulisha rai sahihi kuhusu jambo hilo
Answer
kukusanyika ili kumswalia Mtume (S.A.W.), baada ya Swala ya Ijumaa kwa sauti ni jambo halali na linalopendeza, linalowaleta watu pamoja kwa moja ya mambo muhimu zaidi ya ibada. Ikiwa makusudio ya kisharia yameunganishwa katika hilo, kama vile kuwatanabahisha wasiojali, kuwaondolea shida, na kuwafundisha na kuwaongoza vijana, basi inakuwa uhalali zaidi na inastahili kupendekezwa zaidi, na hakuna dhambi au Bidaa ndani yake, inapaswa kuzingatiwa kwamba sauti inapaswa kuinuliwa kwa kiwango cha wastani, isiyokuwa na kero, Pamoja na sauti kwenda pamoja katika njia sawa. Yote haya ni kwa kwa kuchunga taratibu za mamlaka husika zinazosimamia jambo hilo.
Maelezo
Bwana wetu, Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.), ndiye bora zaidi na ni baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya viumbe vyake, na neema kubwa zaidi alizowapa. Mola wake amemfanya kuwa ni rehema kwa walimwengu, na njia ya kuwakinga na maafa kutoka kwa viumbe vyake. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote} [Al Anbiyaa 107].
Hakuna baraka, iwe ya dhahiri au iliyofichwa, ambayo imetupata, ambayo kwayo tumepata sehemu katika dini na maisha ya kidunia, au ambayo kwayo kitu kisichopendeza kimeepushwa kutoka kwetu katika yote kati ya hayo, isipokuwa kwamba bwana wetu Mohamad (S.A.W.), ndiye alikuwa chanzo chake, kiongozi wa wema wake, mwongozo wa uadilifu wake, mlinzi dhidi ya maangamizi na vyanzo vya uovu kinyume na uadilifu, yule anayetutahadharisha kuhusu sababu zinazoongoza kwenye kuangamia, na yule anayetoa ushauri katika mwongozo na onyo ndani yake. Kumtakia rehma na amani ni miongoni mwa ibada, njia ya karibu zaidi ya kumkaribia Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ibada kuu zaidi ya utiifu. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamswalia Nabii. Enyi mlio amini! Mswalieni na mumsalimu kwa salamu} [Al Hzaab 56].
Na kutoka kwa Abdullahi Bin Amru amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W), amesema: “Yeyote anayeniswalia mara moja, Mwenyezi Mungu atamswalia mara kumi” Imepokelewa na Muslim katika "Al-Sahih".
Na kutoka kwa Obaiy Bin Ka’ab amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa ikipita Robo ya usiku, husimama na kusema: “Enyi watu, mtajeni Mwenyezi Mungu, baragumu la kwanza limepulizwa, linafuatiwa na baragumu la pili, kifo kimekuja na yote yanayohusika.” Nikasema, “Ee Mtume wa Mwenyezi Mungu, mimi hukutakia rehma kwa wingi, nikutakie rehma mara ngapi?” Akasema, “Kama unavyotaka.” Nikasema, “Robo?” Akasema, “Kama unavyotaka, lakini ukiongeza, ni bora zaidi kwako.” Nikasema, “Nusu?” Akasema, “Kama unavyotaka, lakini ukiongeza, ni bora zaidi kwako.” Nikasema, “Kisha theluthi mbili?” Akasema: “Kama unavyotaka, lakini ukiongeza, ni bora zaidi kwako.” Nikasema: “Je, nikutakie rehma wakati waote?” Akasema: “Basi mambo yako yatakuwa sawa, na dhambi zako zitasamehewa.” Imepokelewa na At-Tirmidhi katika "Al-Sunan" na ameifanya kuwa Hadithi hasan, na Al-Hakim katika "Al-Mustadrak" na ameifanya kuwa sahihi, na Al-Baihaqiy katika "Shu'ab Al-Iman."
Na katika riwaya nyingine: Mtume wa Mwenyezi Mungu, (S.A.W), amesema: “Basi Mwenyezi Mungu atakutosheleza yale yanayokushughulisha maisha yako ya kidunia na akhera.” Imepokelewa na Imamu Ahmad katika “Al-Musnad”.
Amri ya kisharia ya kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu na kumswalia Mtume (S.A.W), imekuja kiujumla. Imethibitishwa kwamba amri ya kiujumla inahitaji ujumla wa nyakati, mahali, watu, na hali. Amri hiyo ni pana katika wigo, ikiwa Mwenyezi Mungu ameweka amri kwa njia ya kiujumla, na inawezekana kwamba kitendo chake na jinsi ya utekelezaji wake vinaweza kuwa na vipengele zaidi ya kimoja, basi inachukuliwa kwa maana ya kiujumla na pana, na hairuhusiwi kuiwekea mipaka kwa njia kimoja pasina nyingine isipokuwa kwa Ushahidi au dalili. Na kumtaja Mwenyezi Mungu kwa pamoja kuna siri inayojidhihirisha katika kuinua pazia, tofauti na dhikri ya mtu peke yake. Vivyo hivyo, kwa upande wa thawabu, kila mmoja ana thawabu ya dhikri yake mwenyewe na thawabu ya kusikia dhikri ya wenzake.
Na dalili za kisharia zimetaja katika Qur’ani Tukufu na Hadithi za Mtume (S.A.W) zikihimiza baraza za dhikri na kukutana kwa ajili yake, ikiwa ni pamoja na maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu akimueleza Mtume wake mtukufu (S.A.W): {Na isubirishe nafsi yako pamoja na wanao muomba Mola wao Mlezi asubuhi na jioni, hali ya kuwa wanataka radhi yake} [Al Kahf 28]. Haifichiki kwamba kufuata amri, pamoja na wale wanaomlingania Mwenyezi Mungu, hupatikana kupitia kushirikiana pamoja katika dua.
Na kutoka kwa Abu Hurairah R.A., kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W), alisema: “Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: Mimi nakuwa katika dhana ya mja wangu, na mimi niko pamoja naye anaponitaja. Akinitaja moyoni mwake, nami namtajia moyoni Mwangu, na akinitaja katika mkusanyiko, nami namtaja katika mkusanyiko bora kuliko wao”. Na dhikri katika mkusanyiko haitendwi isipokuwa waziwazi tu.
Na kutoka kwa Abu Hurairah na Abu Saeed Al-Khudriy, kwamba walimshuhudia Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W), akisema: "Hakuna watu wanaokaa pamoja wakimtaja Mwenyezi Mungu, isipokuwa malaika wanawazunguka, rehema inawafunika, utulivu unawashukia, na Mwenyezi Mungu anawataja kwa wale walio pamoja naye." Imepokelewa na Imamu Muslim katika "Al-Sahih".
Na kutoka kwa Abu Hurairah R.A., Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W), amesema: “Mwenyezi Mungu ana Malaika wanaozunguka-zunguka barabarani wakiwatafuta watu wa dhikri. Wanapowakuta watu wakimtaja Mwenyezi Mungu, huitana, ‘Njooni kwenye mnachokitafuta!’ akasema: Kisha huwazunguka kwa mabawa yao hadi mbingu ya dunia …” (Hadithi). Imepokelewa na Imamu Bukhari katika Sahih yake.
Wanazuoni wameeleza kwamba inaruhusiwa kuinua sauti yako katika dhikri na kufanya hivyo kwa sauti ya wazi, hasa ikiwa watu wanaodhikiri ni kundi. [1] Kukutana kwa wanaoswali baada ya Swala ya Ijumaa ili kumswalia Mtume (S.A.W), kwa sauti kunaruhusiwa kwa sababu kadhaa:
Kwanza: kuiingia katika jumla ya dalili za kisharia za Kiislamu zinazohimiza kumtaja Mwenyezi Mungu baada ya Swala kwa ujumla, kama ilivyoelezwa katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mkisha swali basi mkumbukeni Mwenyezi Mungu mkisimama, na mkikaa, na mnapojinyoosha kwa kulala} [An Nisaa 103]. Na jambo la ujumla lisilo na kikomo huchukuliwa kwa ujumla wake mapaka lipatikane litakaloliwekea kikomo katika sharia ya Kiislamu.
Pili: Kufanya hivyo ni kufuata amri ya Mtume (S.A.W), Waislamu kwenye mikusanyiko na mikutano yao wasiache kumswalia Mtume (S.A.W), kinyume na hivyo itakuwa ni masikitiko kwa wale ambao hawafuati amri hii Siku ya Kiyama, kama ilivyoelezwa katika Hadithi iliyopokolewa na Abu Hurairah, R.A., kwamba Mtume (S.A.W), amesema: "Hakuna watu watakaa katika mkusanyiko ambao hawamtaji Mwenyezi Mungu na hawamswalii Mtume wao, isipokuwa kwamba itakuwa chanzo cha hasira kwao. Akitaka, atawaadhibu, na akitaka, atawasamehe." Imepokolewa na Al-Tirmidhiy katika "Al-Sunan", na akasema: "Hiyo ni Hadithi hasan ... na maana ya msemo wake: 'chanzo cha majuto'."
Na kutoka kwa Jabir Bin Abdullah R.A., Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) amesema “Watu hawaka katika mkusanyiko kisha wakatawanyika bila kumswalia Mtume (S.A.W) isipokuwa kwamba wanatawanyika katika hali mbaya zaidi kuliko harufu ya mzoga.” Imepokelewa na Al-Nasa’iy katika “Al-Sunan Al-Kubra”.
Na tamko la kukataza kuacha kumswalia Mtume (S.A.W) katika mkusanyiko ni kauli ya jumla. pia mkusanyiko usio wa kumswailia Mtume (S.A.W) ulivyo ni chanzo cha hasira kwa waliohudhuria, basi kusanyiko lenye kumswalia Mtume linakuwa ni sehemu ya rehma na ridhaa za Mwenyezi Mungu Mtukufu, na sehemu inayotazamwa na kuchungwa Mtume Wake (S.A.W) hasa kwa vile yeye (S.A.W) alitumia neno "watu/kaumu," ambalo linatumika tu kwa kundi.
Bila shaka, mikusanyiko ya dhikri hushuhudiwa na Malaika watukufu, na ni mahali pa baraka, zinazowazunguka wale wanaohudhuria kwa kukubalika, rehema, neema, na msamaha. Basi kutoka kwa Abu Hurairah kwamba Mtume (S.A.W) amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu ana Malaika wa msafara ambao, wanaposikia mikusanyiko ya dhikri, baadhi yao husema: Kaeni chini. Kisha, watu wanapoomba dua, husema Amina kwa dua zao, wanapomswalia Mtume (S.A.W) humswalia pamoja nao hadi watakapomaliza. Kisha, huambiana: Mwisho mwema kwa watu hawa, watarudi wamesamehewa.” Imepokelewa na Abu Al-Qasim Al-Tamimi katika "At-Targhib wa At-Tarhib".
Tatu: Kutaraji fadhila kwa kumswalia Mtume (S.A.W) siku ya Ijumaa, ambazo hazipatikani katika siku nyingine, na kutumaini kwamba itaambatana na saa ya kukubaliwa dua, na kwa sababu Ijumaa ndiyo bwana wa siku, jambo bora zaidi la kutumia juu yake ni kumtumikia bwana wa wanadamu, rehma na amani zimshukie.
Imepokewa kutoka kwa Abu Darda’ R.A., amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) amesema: “Nitakieni rehma kwa wingi siku ya Ijumaa, kwani ni siku inayoshuhudiwa na Malaika wanaishuhudia. Na hakuna yeyote atakaye nitakia rehma isipokuwa dua yake huawasilishwa kwangu hadi atakapoimaliza.” Akasema: Nikasema: “Hata baada ya kifo?” Akasema: “Hata baada ya kifo. Hakika, Mwenyezi Mungu ameharamisha ardhi kula miili ya Manabii, kwa hivyo Mtume wa Mwenyezi Mungu yuko hai na anaruzukiwa.” (Imepokelewa na Ibn Majah) "Sunnah".
Imepokewa Hadithi utoka kwa Anas R.A, Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) amesema: “Nitakieni rehama kwa wingi siku ya Ijumaa na usiku wa Ijumaa, atakaenitakia rehma mara moja, Mwenyezi Mungu atampa rehma mara kumi.” Imepokelewa na Al-Baihaqiy katika “Al-Sunan Al-Kubraa” na “Shu’ab Al-Iman,” na Al-Qati’i katika “Juz’ Al-Alf Dinar.”
Amri ya kupendekeza kumtakia rehma bwana wetu, Mtume wa Mungu (S.A.W) katika siku ya Ijumaa na usiku wake ni kauli waliyokubaliana Wanazuoni wa Fiqhi, na zimepokewa matini za Maimamu wa Madhehebu yanayofuatwa, Imesimulwa kutoka kwa wanazuoni wa umma huu na mawalii zake kwamba wameitenga siku ya Ijumaa na usiku wake kufanya mabaraza maalumu ya kumtakia rehma Mtume (S.A.W) kwa kuigawa kwa nyakati za siku hiyo, kama baada ya Swala ya Ijumaa, kama vile "Majlis Al-Mahya" ambayo ilifufuliwa na Imamu Nur Ad-Din Ali As-Shuni (aliyefariki 944 AH/1538 BK) kwenye kaburi la Shekhe, Sayyid Ahmad Al-Badawi, katika mji wa Tanta kwa miaka ishirini mfululizo, kisha ikahamia kwenye Msikiti wa Al-Azhar huko Kairo.
Tunapata faida Kutokana na yaliyotangulia:
Kumtakia rehma Mtume (S.A.W) ni miongoni mwa Ibada bora, njia ya karibu zaidi ya kumkaribia Mwenyezi Mungu, na ibada tukufu zaidi katika kumtii Mwenyezi Mungu.
Kukutana kwa ajili ya kumswalia Mtume (S.A.W) kwa sauti baada ya Swala ya Ijumaa ni jambo linalopendeza ambalo huwaleta watu pamoja katika mojawapo ya ibada tukufu zaidi.
kunachungwa katika mikusanyiko hiyo, kuwa sauti inapaswa kuinuliwa kwa kiwango cha wastani, isiyo na kero, pamoja na sauti kuwa sambamba kwa njia ya pamoja. Yote haya ni kwa mujibu wa taratibu za mamlaka husika zinazosimamia jambo hilo.
[1] - Kitabu cha: “Muftaahu Al Falaah na Muswbah Al Arwaah 9Uk. 13, Mtwba’at As Saadah]. Na kitabu cha: (Al Fatawa Al Fiqhiyah Al Kubraa 176/1)
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
