Kutoa Takbira Wakati wa Moto
Question
Je, imethibitishwa katika Sharia kwamba kutoa Takbira huzima moto unapotokea? Na nini maana yake?
Answer
Imethibitishwa mwongozo wa Mtume (S.A.W) wa kusoma Takbira wakati wa moto, na hiyo ni katika Hadithi hasan kutokana na ushahidi wake. Kwa hivyo, Wanazuoni wametaja kupendeza kutumia Takbira na Dua katika kuzima moto, pamoja na kuwa ni wajibu kisharia kwa mtu, kunapotokea moto, kuchukua hatua za kivitendo zinazofaa kwa hilo, kama zilivyopangwa na mamlaka husika kwa ajili ya kukabiliana na jambo hili.
Maelezo:
Sharia Tukufu imeamrishia utegemezi mzuri kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu pamoja na kuchukua sababu, na hakuna mgongano kati ya haya mawili. Tawakkul (Kumtegemea Allah) ni katika matendo ya moyo, na kuchukua sababu ni katika matendo ya mwili. Na Uislamu umeamrisha kukusanya haya mawili. Imepokelewa kutoka kwa Anas Ibn Malik (R.A) amesema: Mtu mmoja alisema: Ee Mtume wa Mwenyezi Mungu, nimfunge ngamia wangu kisha nitawakali, au nimwachie kisha nitawakali? Akasema: :Mfunge kisha tawakkal” Imepokelewa na Imamu At-Tirmidhiy katika Sunan yake.
Pamoja na kuchukua sababu na kuzipa kipaumbele hasa kunapotokea moto - kama ilivyo katika swali letu hilo - ni lazima pia kumkimbilia Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa dua na kujisalimisha kwa amri yake, na kusoma adhkar (nyiradi) zilizothibiti kwa hali hizi. Hakika Mtume (S.A.W) ametufundisha wakati wa moto kwamba mja anatakiwa kumtaja Mola wake na kusoma Takbira, na amebainisha Takbira (kusema Allahu Akbar) kwa sababu ndani yake kuna onyo kwamba Mwenyezi Mungu ni Mkubwa kuliko kila kitu, na Ana uwezo wa kuzima moto. Imepokelewa kutoka kwa Abdullah Ibn Amr Ibn Al-'As (R.A) amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu Amesema (S.A.W):” Mtakapoona moto, someni Takbir, kwani Takbir huuzima” Imepokelewa kutoka kwa Ibn As-Sunni katika 'Amal Al-Yawm wa Al-Laylah.
Na katika Hadithi ya Imamu At-Twabarani katika kitabu Ad-Du'a' kwa lafdhi: ((Ikitokea moto, kithirisheni Takbir; kwani inazima)).
Na katika Hadithi nyingine ya Imamu At-Twabarani katika Al-Mu'jam Al-Awsat kutoka kwa Abu Hurayrah (R.A) amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu Amesema (S.A.W): “Zimeni moto kwa kutoa Takbir”. Na katika Hadithi ya Imamu Al-Bayhaqi katika Ad-Da'awat Al-Kabir kutoka kwa 'Amr Ibn Shu'ayb, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) alisema: “Ombeni msaada katika kuzima moto kwa kutoa Takbir”.
Hadithi hizi zilizokuja kuhusu uhalali wa kusema Takbira wakati wa moto ingawa njia zake ni dhaifu; lakini zinapata nguvu kwa mkusanyiko wa njia zake katika kuashiria kufaa kuzifanyia kazi, hivyo Hadithi ni nhasan kwa ushahidi wake. Mwanachuoni Abu Al-Faydh Ahmad Ibn As-Siddiq Al-Ghumari Amesema: " Mtoa maelezo amesema: na isnadi yake ni dhaifu lakini ina ushahidi, nikasema: miongoni mwake ni ile iliyopokelewa kutoka kwa Ad-Dulabi katika Al-Kuna".
Na Hadithi ya Imamu Ad-Dulabi: kutoka kwa Ja'far Ibn Mohamad, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) Amesema: “Mtakapoona moto, somoni Takbir, kwani Mwenyezi Mungu (S.W) huuzima”.
Imamu Nawawi amesema: “(Mtakapoona moto, somoeni Takbir, kwani Takbir huuzima)), na inapendeleza kuomba pamoja na hayo dua ya karb (dhiki)". Na wanazuoji wa Fiqhi wa Madhehebu ya Imamu Hanafi wametaja uhalali wa kusoma Takbir kwa sauti wakati wa moto.
Lakini tunakumbusha kwamba Hadithi hii kwa mapokezi yake mengi ingawa ndani yake kuna mwongozo kutoka kwa Mtume (S.A.W) kwamba kutoa Takbir ni miongoni mwa sababu zinazotumiwa katika kuzima moto, haikanushi kutegemea pia sababu za kivitendo zinazopangwa na mamlaka za usalama husika kama vile idara za ulinzi wa raia na zimamoto, bali ni wajibu kuzichukua sababu hizo. Si halali kwa mujibu wa Sharia kupuuza kuchukua hatua za kimwili za kuzima moto; kwa kuwa kuziacha kunatia doa katika dhana ya kumtegemea Mwenyezi Mungu (tawakkul). Hali hiyo hugeuza tawakkul kutoka kuwa kitendo cha kupongezwa na kusifiwa, na kuifanya iwe uzembe na kulegalega kunakolaumiwa. Na jambo hili halikubaliwi na Sharia ya Kiislamu, bali linakatazwa.
Al-Hafidh Ibn Hajar Al-Asqalani amesema: "Na makusudio ya tawakkul ni kuamini yale yanayooneshwa na Aya hii: {Na hakuna mnyama yoyote katika ardhi ila riziki yake iko kwa Mwenyezi Mungu. Naye anajua makao yake na mapitio yake. Yote yamo katika Kitabu chenye kubainisha.}; na sio makusudio kuacha kuchukua sababu na kutegemea kile kinachokuja kutoka kwa viumbe; kwa sababu hiyo inaweza kupelekea kinyume na kile kinachotakiwa katika tawakkul".
Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:
1- Sharia Tukufu imeamrisha kumtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu pamoja na kuchukua sababu.
2- Imethibitishwa mwongozo wa Mtume (S.A.W) wa kusoma Takbir wakati wa moto, pamoja na kuwa ni wajibu kisharia kwa mtu, kunapotokea moto, kuchukua hatua za kimwili zinazofaa kwa hilo, kama zilivyopangwa na mamlaka husika kwa ajili ya kukabiliana na jambo hili.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
