Biashara katika vitu vyenye matumiz...

Egypt's Dar Al-Ifta

Biashara katika vitu vyenye matumizi mawili

Question

Ni ipi hukumu ya kutengeneza, kuuza au kukodisha vitu vinavyoweza kutumiwa kwa matumizi mawili: matumizi halali na matumizi haramu? Je, mtu anayefanya hivyo anapata dhambi?

Answer

Kutengeneza, kuuza au kukodisha vitu vyenye matumizi mawili kunajuzu kisharia, mradi tu uharamu haujathibitika moja kwa moja au kutajwa wazi. Kilichoharamishwa ni mtu kutumia kitu hicho katika haramu, si kitu chenyewe, madamu kina manufaa na hakijakatazwa kiasili. Kikiwa kimetumiwa katika haramu, basi dhambi inamhusu mtumiaji pekee, si mtengenezaji, muuzaji, wala mkodishaji.

Maelezo

Sharia imeweka kuwa biashara kiasili ni halali mradi hakuna dalili ya kuikataza. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Enyi mlioamini! Msiliane mali zenu kwa batili isipokuwa iwe ni biashara kwa ridhaa yenu wenyewe} [An-Nisā’: 29]. Kwa hiyo biashara yoyote inayotokana na ridhaa na isiyokatazwa, ni halali kisheria. Pia Mwenyezi Mungu amesema: {Na Mwenyezi Mungu ameharamisha riba na kuhalalisha biashara} [Al-Baqara: 275]

Uhalali huu unahusu aina zote za biashara isipokuwa zile ambazo sharia imezitaja wazi kuwa haramu, kama zilizojumuisha riba na mfano wake.

Inajulikana wazi kuwa lengo la biashara ni kupata manufaa kwa kubadilishana mali, huduma au faida kwa madhumuni ya kupata faida.

Kwa hivyo, Wanazuoni wameweka kwamba chochote chenye manufaa halali, ambacho hakikatazwi, ambacho masharti yake ya kisharia yanatimia—kutoka pande mbili zinazofanya makubaliano (mnunuzi na muuzaji), kitu kinachouzwa au kununuliwa, na tamko la makubaliano—na hakina kitu kinachokiharibu, basi makubaliano hayo ni sahihi na kujuzu kuuza na kununua[1].

Kuhusu biashara katika kitu chenye matumizi ya halali na haramu kwa wakati mmoja, maoni ya kutolewa Fatwa katika mlango huu ni ya Madhehebu ya Imamu Hanafi. Wao wamesema kuwa kufanya hivyo kunajuzu bila kuchukiza, kwa sababu madhambi hayako katika kitu chenyewe, bali katika kukitumia kwa njia ya maasi. Kwa hivyo kinachoharamishwa ni matumizi ya haramu, si muamala wa kuuza au kutengeneza kitu hicho.

Kwa hivyo kutengeneza kitu chenye matumizi mawili, kukiuza, kukikodisha au kuhusika katika kukiuza, jukumu la dhambi linabaki kwa mtumiaji. Akikitumia katika halali, ni halali; akikitumia katika haramu, basi ni haramu kwake. Hii inalingana na kanuni za sharia kwamba: “Uharamu usipothibitika moja kwa moja, kitu hubaki katika uhalali wake,” na “Kitu chenye matumizi mawili, uharamu unatokana na matumizi ya haramu tu na humhusu aliyeyafanya -aliyekitengeneza.” Na hakuna dhambi kwa mtengenezaji wake, mzalishaji wake, mjenzi wake, au mpangaji wake kwa hilo, kwa kuwa ipo katika hali ya kuuza na kufanya biashara. Aidha, ushahidi wa kujuzisha biashara katika vitu vyenye matumizi mawili ni kwamba vitu hivyo haviko chini ya hukumu ya haramu kwa asili; kwa sababu uharamu hauhusiani na vitu vyenyewe, bali unahusiana na vitendo vya watu kwa kauli za Wanazuoni. Vitu havisemwi kuwa haramu au halali isipokuwa kwa namna vinavyotumiwa. Pia sharia haikulazimisha muuzaji kuuliza mnunuzi anataka kukitumia vipi kitu anachokinunua. Hivyo, bidhaa zinazoruhusu matumizi ya halali na haramu zinajuzu kuuzwa.

Na mnunuzi ni mtu mwenye uchaguzi, na dhambi humhusu anayefanya, si mwingine, kwa kauli ya Mwenyezi Mungu: {Hakuna nafsi itakayobeba dhambi ya nyingine} [Al-An‘ām: 164].

Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:

Kutengeneza, kuuza au kukodisha vitu vyenye matumizi mawili kunajuzu kisheria, mradi uharamu haujathibitishwa moja kwa moja au kutajwa wazi.

 

[1] “Al-Istidhkār” (juzuu 1, ukurasa 164, chapa ya Dār al-Kutub al-‘Ilmiyyah), “Nihāyat al-Maṭlab” (juzuu 5, ukurasa 499, chapa ya Dār al-Minhāj)

Share this:

Related Fatwas