Dalali kuchukua malipo kutoka kwa muuzaji na mnunuzi bila mnunuzi kujua kuwa muuzaji analipa malipo
Question
Kuna kijana anafanya kazi kama dalali, na anapokea malipo kutoka kwa muuzaji na mnunuzi, huku mnunuzi haelewi kuwa muuzaji anamlipa malipo ya kazi yake. Ni ipi hukumu ya kisharia juu ya suala hili?
Answer
Dalali kupokea malipo yaliyokubaliwa kutoka kwa muuzaji na mnunuzi, huku mnunuzi asielewe kuwa anachukua malipo ya kazi kutoka kwa muuzaji au kinyume chake, ni jambo linaloruhusiwa kisharia, wala hakuna dhambi au kosa katika hilo, mradi anachunga kanuni na taratibu zinazosimamia miamala ya aina hii, na kulazimika kwa uaminifu na ukweli katika yote hayo.
Maelezo
Dalali (Simsar): ni neno la Kipersia lililodoholewa na kufanywa kuwa la Kiarabu, na kusudio lake katika uuzaji ni: mtu anayejihusisha kati ya muuzaji na mnunuzi kama kiunganishi wa kufanya muamala, ambapo anaonyesha bidhaa kwa mnunuzi na anaonesha bei kwa muuzaji. Maana ya kisharia ya neno hili lipo karibu sawa na maana ya kifasihi, kwani wanasheria wanamtambua dalali kama mtu ambaye huuza au kununua kwa niaba ya mwingine kwa malipo.
Kama ilivyofafanuliwa katika Kifungu cha 192 cha “Sheria ya Biashara ya Misri” namba 17 ya mwaka 1999, udalali ni: "mkataba ambao mtu dalali anajitolea kutafuta upande wa pili kwa ajili ya kufanikisha mkataba fulani na kushiriki katika upatanisho wake." Mwisho.
Udalali ni mapatano kati ya watu ulioanza tangu nyakati za Mtume Muhammad (S.A.W). na ni muamala unaokubalika kisharia mradi bidhaa au kile kinachofanana nacho ni halali; kwa kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Enyi mlio amini, timizeni ahadi} [Al-Maida: 1].
Na kwa hadithi ya Amru bin Auf al-Muzani (R.A), Mtume (S.A.W) alisema: "Waislamu wako ahadi zao, isipokuwa kama ahadi itakayoharamisha halali au kuhalalisha haramu" Imetolewa na maimamu: At-Tirmidhi – alisema ni sahihi na nzuri, Ad-Daraqutni, Al-Baihaqi katika Sunan zao, na Al-Hakim katika Al-Mustadrak na akaisahihisha.
Na kutoka kwa Qais bin Abi Gharazah (R.A) alisema:: Mtume wa Mweneyzi Mungu alitujia nasi tunaitwa madadali, akasema: ‘Enyi wafanyabiashara, Shetani na dhambi hudhuria katika mauzo, basi changanya mauzo yenu kwa sadaka’" Imetolewa na maimamu: Abdul Razzaq katika Al-Musannaf, Ahmad katika Musnad yake, Abu Dawud, na At-Tirmidhi katika Sunan zake, akasema ni sahihi na nzuri.
Wanazuoni wamekiri kukubalika kwa udalali na kuchukua malipo kutoka kwa mmoja wa waliopatana (muuzaji au mnunuzi) au kwa wote wawili. Wanachuoni wa madhehebu ya Hanafi, Maliki, Shafi’i na Hanbali wanasema kuwa dalali ni halali na anaweza kuchukua malipo kutoka kwa mmoja wa waliokuwa wakitenda muamala au wote wawili; kutokana na hitaji la watu kwa hili. Ikiwa kazi na malipo yanajulikana kwa pande zote mbili zinazofanya muamala, basi ni kama kukodisha, na ikiwa yamefichika au ni moja tu ndio inayojulikana, basi huo muamala ni kama ni kama malipo ya shukrani (kwa kufanyiwa kazi) au malipo yanatathminiwa kulingana na mfano wa kawaida wa dalali, kulingana na maelezo ya wanazuoni, nayo ni kauli ya Maimamu; kama Ibn Sirin, Ata, Ibrahim Al-Nakha’i, na Al-Hasan Al-Basri.
Udalali ni kama makubaliano mengine yoyote ile ya miamala; ingawa asili yake ni halali na kuruhusika, isipokuwa ni lazima uwe umetakasika na kuepukana na vizuizi vya sharia kama hadaa,lutojilikana, udanganyifu, hila, uharamu ya kile kinachofanyiwa kazi, na sababu nyingine za kisheria na mahakamani. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: { Enyi mlio amini! Msimfanyie khiana Mwenyezi Mungu na Mtume, wala msikhini amana zenu, nanyi mnajua.} [Al-Anfal: 27].
Na kutoka kwa Abu Huraira (RA) alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) amekataza kuuza kilichorembewa jiwe[1], na kuuza kisichojulikana”, na pia kutoka kwake (RA) kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) alisema: “Mwenye kudanganya si katika sisi” — Amezitoa Imamu Muslim katika Sahihi yake.
Kupokea malipo na dalali kutoka kwa muuzaji na mnunuzi ni kweli inahusisha miamala miwili tofauti, mmoja pamoja na muuzaji ili ampatie mnunuzi, na mmoja pamoja na mnunuzi ili amtafutie kile anachokusudia kununua. Ikiwa inatokea kwamba mnunuzi anataka kile kutoka kwa muuzaji ambaye amekubaliana na dalali, basi kutokuwa na ufahamu kwamba dalali anapata malipo kutoka kwa muuzaji au mnunuzi hakuvunja uhalali wa miamala yoyote kati ya hiyo miwili, kwa sababu si wakili wa yeyote. Kwa kuwa kama angekuwa wakili, basi wakili ni mwenye kubeba dhaman, na kuchukua malipo bila idhini ya mteule wake ni aina ya khiyana.
Kama ambavyo mazingatio katika makubaliano na miamala ya kifedha ni kupatikana kwa maridhiano kutoka kwa pande mbili, na hakuhitaji kujulikana na yeyote zaidi yao. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Enyi mlioamini, msile mali zenu baina yenu kwa batili, isipokuwa iwe biashara kwa kuridhiana kati yenu} [An-Nisa: 29].
Na ishara ya maridhiano ni ni kupatikana kwa kukubali na kukiri kutoka kwa pande mbili.
Wala haijifichi kwamba kukiri na kukubali havihusiani na yeyote asiye wahusika katika makubaliano; hivyo pindi ridhaa inapotoka kwao wawili, mali inayostahiki kutokana na muamala huo haitakuwa ulaji wa mali kwa batili, hata kama muuzaji ataiongeza thamani kwenye bei ya bidhaa, mradi tu hakutokei udanganyifu mkubwa kwa mnunuzi katika bei ya bidhaa hiyo kwa mujibu wa desturi. Baadhi ya wanazuioni wamesema kwamba ujira wa dalali ni miongoni mwa mambo yanayoongezwa kwenye bei kwa desturi ya wafanyabiashara. Isipokuwa haifai katika kuuza kutumia ibara inayoweza kueleweka kana kwamba amenunua bidhaa kwa bei hiyo, bali atumie maneno kama: “amenigharimu kiasi kadha,” ili kujumuisha gharama zote, na hivyo kuonesha kuwa hailazimu kumweleza mnunuzi maelezo ya kina ya jambo hilo.
Ni jambo lililoamuliwa kisheria kuwa “desturi -huwa kama marejeleo- ya hukumu,” na desturi ni hoja kisharia, kama walivyosema wanasheria katika kanuni zinazotumika katika sheria ya Kiislamu.
Kwa hivyo, kupokea malipo kutoka kwa pande zote mbili, muuzaji na mnunuzi, huku mnunuzi asijue kwamba dalali anapokea malipo kutoka kwa muuzaji au kinyume chake — ni jambo halali kisheria.
Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:
Udalali ni makubaliano halali mradi tu yawe yametakasika kutokana na vizuizi vya kisheria kama vile uharamu ya kile kilichokubaliwa, udanganyifu, khiyana, na kisiwe chenye gharama zisizo wazi, na lisitokee udanganyifu mkubwa kama unavyofahamika kikawaida.
Inafaa kwa dalali kuafikiana na muuzaji au mnunuzi kwa pamoja, au kwa mmoja wapo, mradi tu si wakala wa mmoja wao, na ridhaa imepatikana kuhusu udalali huyo na malipo yake kati ya dalali na anayemlipa.
Haiwi sharti katika hali hiyo kujua upande mwingine katika uuzaji kuhusu udalali huo au malipo yake.
[1] Ni uuzaji unaofanywa kwa kubainisha kitu kinachouzwa kwa kurembea kijiwe – kokoto au kitu kinachofanana na hicho.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
