Mume na Mke kukubaliana kugharamia ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mume na Mke kukubaliana kugharamia watoto baada ya Talaka

Question

Wanandoa wamekuabaliana kuachana na wana Watoto wakike na wakiume, na kwa kuhofia kuzuka migogoro kuhusu kuwagaharamia Watoto baada ya talaka, wameingia mkataba wa makubaliano unahakikisha kupamga kiwango cha gharama na jinsi ya kukitekeleza, je, makubaliano haya yanajuzu kisharia? Na je, kunawezekana kwa mwanamume kuvunja makubaliano hayo? Je, kiwango cha gharama ni thabiti hakibadiliki kwa kubadilika hali za Maisha na kuongezeka bei za bidhaa?

Answer

Makubaliano kati ya wanandoa juu ya matumizi ya Watoto wao baada ya talaka hayakatazwi kisharia, muda wa kuwa yanaleta masilahi kwa Watoto, na linafanyiwa kazi muda wa kuwa hali ya kiuchumi haijabadilika, ikibadilika kunajuzu kuomba kufanyiwa marekebisho kiwango cha gharama zilizoafikiwa, kwa kuongeza na kupunguza pamoja na kuchunga masilahi ya Watoto katika kila hali. Na wanandoa wanashauriwa kupanga vizuri tofauti za ndoa kwa njia ya ustaarabu inayokuwa katika wema, na kulinda mapenzi na fadhila, ili Watoto wapate kheri na baraka

Maelezo

Sheria imepitisha kuwa kuwagharamia Watoto wasio na mali ni wajibu kwa baba; kwa kuwa mtoto ni sehemu ya baba yake na ametokana na yeye, Mwenyezi Mungu Anasema: “Na juu ya baba yake chakula cha kina mama, na nguo zao kwa mujibu wa ada” [Al-Baqarah:233].

Ikiwa gharama za anayelea Watoto ni wajibu, hii ni aina ya gharama ndogo- basi gharama za kukidhi mahitaji ya msingi kama chakula, nguo na mfano wa hilo ni wajibu zaidi na kunasisitizwa zaidi; imepokewa Hadithi kutoka kwa Mama wa Waumini Aisha R.A. kwamba hind bint Utba alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hakika Abu Sufyan ni mtu bahili sana, na hanipi kinachonitosha mimi na Watoto wangu, isipokuwa kile ninachochukua nayeye hajui, Mtume S.A.W. akasema: “Chukua kinachokutosha wewe na Watoto wako kwa wema”. Imepokelewa na Al Bukhary.

Na makubaliano yaliyofikiwa ni wajibu kwa baba, na hili sawasawa Maisha ya ndoa kati ya baba na mama bado yapo au yamekatika, na kuwa Watoto ni wadogo au wakubwa- kwa kundi kubwa la Wanazuoni wa Fiqhi - muda wa kuwa hawana uwezo wa kutafuta kihisia; kama kuwepo kiziwzi kinawazuia kupata kipato, au kimaana, kama kushughulika kwao na elimu, au kuwa wasichana masikini wadogo au wakubwa, wanaweza kuwa na kipato au laa.

Na hili ndilo lilipitishwa katika sheria ya Misri, kimekuja kifungu cha (18) kikikariri mara mbili katika sheria nambari(25) ya mwaka (1929) kilichofanyiwa marekebisho kwa sheria nambari (100) cha mwaka (1985) kwamba: “Gharama za baba zinaendelea kwa Watoto mpaka binti atakapoolewa, au kupata kipato kitakachotosha gharama zake, na mpaka mtoto wa kiume afikishe miaka kumi na tano na kuwa na uwezo wa kupata pato linalotosheleza, akifika miaka hiyo na akawa hawezi kupata kipato kwa matatizo ya kimwili, kiakili au kutafuta elimu inayoendena na umri wake na maandalizi yake, gharama zitaendelea kwa baba yake. Mwisho wa kunukuu.

Asili baba awagaharamie Watoto wake kwa kiasi cha kuwatosheleza kwa kinachoendana na hali yake Tajiri au masikini, kwa maana kwa kuwapa aina ya gharama za vyakula na vinywaji na mavazi na malazi na mengineyo, Ikitokea haiwezekani kuwagharamia kwa njia ya kuwapa fursa ya kutumia tu (Tamkeen)—kwa mfano kutokana na kutokuwepo kwake karibu nao—basi inalazimu kutoa matumizi hayo kwa njia ya kuwamilikisha (Tamlik); yaani: kwa kuwamilikisha thamani ya kifedha inayokidhi aina za mahitaji hayo."

Na mke na mume wakifikia kuachana, wanaposhindwa kuendelea na masha ya ndoa, na wana watoto wanaostahiki kugharamikiwa kwa wajibu, watakubaliana kwa njia nzuri kwa kiwango chake katika yanayohusiana na hilo na wataandikishiana hilo katika njia ya makubaliano kama ilivyo katika suala hili, makubaliano haya yanajuzu kisharia hayana ubaya; kwa kufuata yale waliyoafikiana Wanazuoni katika asili ya mikataba na makubaliano kati ya watu yanayosimama katika maridhianao na kuafikiana,  kusihi, muda wa kuwa haya halalishi haramu au hayaharamishi halali.

Mkataba wowote ni wakisharia ukiwa katika muktadha wa Sharia ili watu wafikie katika malengo yao ya Maisha, ikiwa watu watakusudia katika mikataba yao maana ambayo imieiweka sheria katika kila mikataba, na mkataba ukatekeleza sharti zote zinazotakiwa ili kuufikia, na wote wakaridhia walioafikiana, basi ni sahihi.

Na mktaba huu unakuwa unawalazimu pande zote mbili, kwa upande wa asili, na hakuna kwa mmoja wao kuuvunja au kuurekebisha au kuubadilisha kwa mapenzi yake; kwa kauli ya Mwenyezi Mungu: “Enyi mlio amini! Timizeni ahadi” [Al-Maidah:1]. Miongoni mwa utekelezaji wa mikataba: kutekeleza makubaliano ya pande mbili, na kanuni inasema: “Maagizo yakija moja kwa moja hajafungwa huchukuliwa kama yalivyo”.

Kwamba lau kungesihi kuvunja moja ya pande mbili kwa waliyokubaliana: makubaliano yasingekuwa na faida wala athari, na hili linapingana na makusudio ya masharti na makubaliano.

Isipokuwa tunaposema mke na mume washikamane na makubaliano yao, kunachungwa hali ya maisha pia kutokana na kupanda kwa bei na kushuka, au kubadilika hali ya mtoaji kuwa nzuri au mbaya, hali ikibadilika: kunajuzu kurekebisha kipengele cha makubaliano ili kufikia masilahi ya watoto, na kuwa kwa maridhiano na makubaliano kwa pande mbili, kukiwa hakuna maridhiano, basi watakwenda mahakamani. Kwani makubaliano asili yake yanarejea kufikia kuwatosheleza wanaogharamikiwa kwa mujibu wa hali ya anayepasa kugharamia, pia hukumu zilizotoka katika gharama zina hoja za muda.

Kinachozingatiwa katika kiwango cha gharama katika kila hali ni masilahi ya Watoto wadogo, kwa namna mume na mke wakikubaliana gharama za watoto wao kabla ya talaka, na waliyokubaliana yakawa ni zaidi ya gharama zao; halidhuru hilo, ikiwa waliyokubaliana ni kidogo kuliko gharama zao na hakitoshelezi mahitaji yao; basi kiwango cha gharama kitaongezwa mpaka kiwatosheleze, kwa sababu wajibu wa baba ni kiwango kitakachowatosha na kutosha mahitaji yao katika hali ya umasiki na utajiri.

Wala hakuathiri kusaini makubaliano haya kwa kuzingatia kwake kufuata au kutengeneza haki; kwa sababu baba katika hali zote anatakiwa kugharamia kwa kiasi cha kuwatosheleza watoto wake, iwe mkataba huu ni wapande mbili, au baba kwa upande wake mwenyewe na mama kwa upande wa watoto wake wadogo. akiuzingatia mkataba huu ni lazima: inarudi kwake kukubali uwezekano wa kubadilika kwa mujibu wa hali, na ukiwa ni kufuata haki basi haki hii inajiboresha pia inapotakiwa kwa mujibu wa waliyofikiana Wanazuoni wa Fiqhi wa Madhehebu ya Hanafy.

Paia kifungu cha sheria namba 8 katika sheria nambari 10 ya mwaka 2002, kuhusu kuanzishwa mahkama ya familia kuzingatia wanayokubaliana mke na mume, na wanapatana katika mambo ya gharama, malezi na mfano wao, na kuyaandika katika karatasi kwa kutambua ofisi ya utatuzi na kutiwa Saini na wote na wawakilishi wao, ili makubaliano haya ya kirafiki yawe wajibu kuyatekeleza katika mipaka ya usuluhishi, kwa kile kinachohifadhi haki za mwanamke na haki za wototo wake katika waliyokubaliana na kufikai suluhu kati yao.

Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:

Matumizi ni wajibu kwa baba kwa Watoto wake wadogo ambao hawana mali, kwa kuzingatia kwamba Watoto wenyewe  hawana uwezo wa kipato.

Asili katika mikataba na makubaliano kati ya watu inasimama kwa maridhiano na makubaliano: ni kusihi, muda wa kuwa haiharamishi halali au kuhalalisha haramu.

Hakuna kizuizi kisharia kuingia makubaliano kati ya wazazi wawili juu ya gharama za Watoto zao baada ya talaka, muda wa kuwa hilo linafikia masilahi ya watoto, na kunachungwa katika hilo hali za kiuchumi na mabadiliko yake.

Share this:

Related Fatwas