Wanandoa kuchafuana baada ya Talaka
Question
Imekuwa kawaida kwa watu na kwenye mitandao ya kijamii kwa mmoja ya wanandoa kumchafua mwenzake na kutaja kasoro zake baada ya talaka, Tunaomba maoni ya kisharia kuhusu jambo hili.
Answer
Ni haramu kisharia na ni kosa la jinai kumchafua mmoja ya wanandoa wawili, sawasawa kipindi cha ndoa au baada ya kuachana, na kutaja mabaya katika yale anayoyachukia, au yanayohusiana na siri binafsi za mmoja wao, bila ya dharura au muktadha wa kisharia au sababu inayozingatiwa, na wajibu kwao wao kustiriana, na kuchunga tofauti kwa wema na fadhila.
Maelezo
Sharia Tukufu imehimiza kustiriana na kufumbia macho makosa ya watu na kasoro zao, na kutochunguza kasoro zao, na kutowachafua kabisa; ili kusiwe na sababu ya kueneza ubaya kwa upande mmoja, na kuwa stara na kusaidiana katika kurekebisha nafsi, na kusimama katika toba kwa upande mwingine.
Imepokewa Hadithi kutoka kwa Abu Hurayra kwamba Mtume (S.A.W) amesema: “Mwenye kumstiri Muislamu, Mwenyezi Mungu Atamstiri duniani na Akhera, na Mwenyezi Mungu yupo katika kumsaidia mja muda wa kuwa mja yupo katika kumsaidia ndugu yake” Imetolewa na Muslim katika sahihi yake.
Na katika riwaya nyingine: “Mwenye kustiri aibu ya ndugu yake Muislamu, Mwenyezi Mungu Atamstiri Siku ya Kiyama, na mwenye kufichua aibu za ndugu yake Muislamu, Mwenyezi Mungu Atafichua aibu zake mpaka amfedheheshe nyumbani kwake”. Imetolewa na Ibnu Majah katika Sunanih.
Katika Hadithi hii tunajifunza kwamba: Mwenye kumstiri Muislamu kwa kutomtangazia mambo ambayo hayatakikani kuyadhihirisha miongoni mwa makosa madogomadogo, basi atalipwa duniani na Akhera.
Na mmoja ya wanandoa kumchafua mwenzake kwa kasoro zake, na kumzungumzia kwa ubaya baada ya talaka bila ya ulazima wa kisharia unaohitaji hilo, ni jambo linalopingana na yote yaliyotangulia, na linahesabiwa kuwa ni katika kuvunja stara ya mwingine pasi na sababu halali, na hilo ni katika kusengenya kuliko haramu kisharia.
Kusengenya: Ni kumtaja ndugu yako Muislamu kwa analolichukia katika dini yake au dunia yake au familia yake au mengineyo katika yanayohusiana naye, iwe kwa maneno, kuashiria au kwa alama, ama kumtaja kwa kile asichokuwa nacho kunakuwa ni uzushi.
Na kusengenya ni katika madhambi yaliyoharamishwa ambayo kuna dalili nyingi za kisharia katika Qurani Tukufu na Hadithi na makubaliano ya Wanazuoni juu ya uharamu wake na kujiweka mbali nalo. Miongoni mwazo ni kauli ya Mwenyezi Mungu: “Enyi mlio amini! Jiepusheni na dhana nyingi, kwani baadhi ya dhana ni dhambi. Wala msipelelezane, wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je! Yupo katika nyinyi anaye penda kuila nyama ya nduguye aliye kufa? Mnalichukia hilo! Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba, Mwenye kurehemu”[Al-Hujrat:12].
Na imepokewa Hadithi kutoka kwa Abu Hurayra kwamba Mtume (S.A.W). amesema: “Mnajua maana ya kusengenya” wakasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ni Mjuzi zaidi, akasema: “Kumtaja ndugu yako kwa analolichukia”, wakasema: Waonaje kama kinachosemwa kina ukweli, akasema: “Ikiwa anacho kinachosemwa umemsengenya, na akiwa hana basi umemzushia” Imetolewa na Muslim. Na Hadithi zinazotahadharisha usengenyi ni nyingi na uharamu wake ni nyingi sana, na uma umekubaliana juu ya uharamu wa kusengenya.
Ikiwa kusengenya ni mtu kumtaja ndugu yake kwa analolichukia ni jambo la haramu kwa ilivyotangulia, basi uharamu hapa unakuwa mkubwa mno; kwa kuwa hili linajumuisha kufichua siri za Maisha ya ndoa baada ya talaka, na hili limeelezwa na Mtume (S.A.W.): “Hakika mtu mwenye nafasi mbaya kwa Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama, ni mtu anakaa faragha na mke wake, kisha anatangaza siri zake”. Imetolewa na Muslim katika sahihi yake.
Hadithi hii inatufundisha juu ya uharamu wa mtu kutangaza yale yanayofanyika kati yake na mke wake katika mambo ya strehe, na kusimulia undani wake na yale anayoyafanya mwanamke katika kauli au vitendo au mfano wake, ni haramu kwa wote wawili kutoleana siri, na kutaja kasoro binfsi za mmoja wao pasi na sababu ya inayokubalika, sawasawa katika hali ya kuwepo kwa mahusiano ya ndoa au baada ya kukatika.
Pia hili linapingana na suala la kuishi vizuri, na kupinga wema uliokuja katika kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na mtakapo wapa wanawake t'alaka, nao wakafikia kumaliza eda yao, basi warejeeni kwa wema au waachilieni kwa wema..”[Al-Baqarah: 231]. Neno wema ni kila jema katika kusimamisha haki katika kuwa Pamoja na kuachana.
Na kauli ya Mwenyezi Mungu: “T'alaka ni mara mbili. Kisha ni kukaa kwa wema au kuachana kwa vizuri” neno vizuri ni kutekeleza haki yake, asimuudhi, asimtukane wala asimdhuru kwa maneno au kumchafua.
Hapanashaka kwamba mmoja wa wanandoa kumchafua mwenzake kwa kutaja kasoro zake na kumzungumzia kwa ubaya kunapingana na kuachana kwa wema na uzuri, na ni jambo lisilokubalika na akili salama na tabia nzuri.
Halkadhalika sheria ya Misri imelifanya kosa la jinai kitendo cha kumchufua mtu au kumtukana na kutangaza siri zake, na ikalifanya kuwa ni kosa ambalo lina adhabu ya kifungo na faini au kimoja wapo, likikamilika nguzo zake, hii kwa mujibu wa ufafanuzi uliopo katika mlango wa saba “Matusi na kutoa siri”. Katika vifungu (301,310) katika sheria ya adhabu nambari 58 ya mwaka 1937.
Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:
Sharia Tukufu imehimiza stara na kutochunguza makosa ya watu na kasoro zao, na kutowachafua hata kidogo.
Kusengenya ni katika madhambi yaliyoharamishwa ambayo kuna dalili nyingi juu ya uharamu wake na ubaya wake.
Mmoja wa wanandoa wawili kumchafua mwenzake kwa kutaja aibu zake na kumzungumzia kwa ubaya kunapingana na kuachana kwa Uzuri na kwa Wema.
Ni haramu kisharia na ni kosa kisharia mmoja wa wanandoa kumchafua mwenzake, iwe wakati wa ndoa au baada ya kuachana, na kumtaja kwa analolichukia.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
