Uzazi wa Mpango

Egypt's Dar Al-Ifta

Uzazi wa Mpango

Question

Ni ipi hukumu ya Uzazi wa Mpango?

Answer

Uzazi wa Mpango ni jambo linalofaa kisharia kwa sharti wanandoa wawili kukubaliana; kwa kipimo cha kuvua (Kumwaga mbegu nje ya njia ya uzazi) zama za Mtume (S.A.W.) na hili halipingani na Wito wa Uislamu katika kuongezeka.

Maelezo

Makusudio ya Uzazi wa Mpango au kama ijulikanavyo kupanga familia: ni wanandoa kukubaliana kufua njia ambazo wanaziona kuwa zinaweza kurefusha vipindi vya ujauzito, au kusimamisha kutunga ujauzito kwa muda maalum wanaoukubaliana ili kupunguza ukubwa wa familia kwa njia ambayo itakayowafanya wazazi wawili wanaweza kulea Watoto wao malezi kamili pasi na mvurugiko.

Na hii ndiyo maana inayokusudiwa katika Uzazi wa mpango na ni jambo linalojuzu wala halikatazwi na maandiko ya kisharia, muda wakuwa kuna sababu zinzokubalika kisharia zinazopelekea kuchelewesha uzazi kwa muda, kunashartizwa kukubaliana wanandoa wawili katika hilo, na hii kwa kulinganisha na kuvua, ambako ni mwanamume kutoshusha mbegu za uzazi ndani ya mfuko wa mimba wakati wa kukutana na mke wake ili asishike uja uzito, na kwa sharti kwamba huku kuchelewa kusisababishe madhara, mwenye akili ni yule mwenye mipango katika mambo yake yote; kwa sababu mpango ukipatikana katika jambo lolote hulipamba, Mwenyezi Mungu Anasema: “Na hakuna chochote ila asili yake inatokana na Sisi; wala hatukiteremshi ila kwa kipimo maalumu” [Al-Hijr: 21].

Imamu Ghazaly amekusanya sababu zinazopelekea kuvua (Kumwaga mbegu nje ya njia ya uzazi) amezitaja miongoni mwao ni: Kuhofia kuwa na Watoto wengi na kuingia katika dhambi kwa sababu yao[1].

Na kuvua (Kumwaga mbegu nje ya njia ya uzazi) wamelifanya hilo Masahaba katika zama za Mtume (S.A.W) na haikupokewa kuwa Mtume (S.A.W). alikataza, imepokewa kutoka kwa Jabir bin Abdillah R.A. amesema: “Tulikuwa tunavua (Kumwaga mbegu nje ya njia ya uzazi) katia zama za Mtume (S.A.W) likamfia hilo Mtume (S.A.W,) na hakutukataza” Hadithi hii imepokelewa na Bukhary na Muslim. Kama Kuvua (Kumwaga mbegu nje ya njia ya uzazi) ingekuwa haramau Mtume (S.A.W). angetukataza kulifanya.

Na tunachokisisitiza ni kwamba hili halipingani na wito wa Uislamu katika kupanga Uzazi na wito wa kisharia wa kuzaa kwa wingi, bali ni kupanga uzazi ni katika njia za kutoa kizazi kitakachopata haki yake katika malezi kamili na kupata uangalifu wa kutosha, jambo ambalo litamuandaa kubeba majukumu, Kauli ya Mtume (S.A.W).: “Oeni wanawake wazuri wanaozaa sana, kwani mimi nitajifaharisha Siku ya Kiyama kwa kuwa Uma wenye watu wengi” imepokelewa na Abu Dawoud, makusidio ni kuwa na Umma wenye Waumini wengi wema wenye nguvu, uzalishaji na maendeleo, Mtume (S.A.W). hajifaharishi kwa wingi wenye udhaifu katika sehemu kubwa ya Maisha; kwani kujifaharisha kwa uma dhaifu hakuna faida yoyote, na hilo ndilo alilolimaanisha Mtume (S.A.W). katkika Hadithi Mashuhuri ambayo anasema ndani  yake: “kunakaribia uma za makafiri kuungana dhidi yenu kama wanavyoitana ngamia katika chakula, akasema: Tukasema ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hivi ni kwa uchache gani tutakaokuwa nao kipindi hicho? Akasema: Nyinyi mtakuwa wengi lakni mmesambrataika kama yanavyosambaratika maji ya mvua”. Imepokelewa na Imamu Ahmad katika Musnad; kwa maana wingi wenye udhaifu hauna thamani, wala madhara kwa adui wala manufaa kwa rafiki.

Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:

Uzazi wa Mpango ni jambo linalojuzu kwa maandiko ya kisharia, muda wa kuwa kuna sababu inayopelekea hilo kisharia ambazo zinzopelekea kuchalewesha kuzaa kwa muda, na kwa sharti ya kukubaliana wanandoa wawili.

 

([1]) Ihyaa Uluum El Deen cha Al Ghaly 2/52.

Share this:

Related Fatwas