Mke kuchukua maamuzi ya kutozaa peke yake kwa sababu mume ni Mraibu wa madawa ya kulevya
Question
Mwanamke amechumbiwa ndani ya muda mfupi, kisha akaolewa, baada ya ndoa kwa muda mchache ikabainika kwamba mume anatumia mihadarati, jambo ambalo linaathiri hali ya Maisha, na ndugu wameingilia, na wakajaribu kumtibu katika kliniki maalum, na hali yake ikawa nzuri baada ya matibabu ya muda mfupi, kisha akarudia tena kutumia mihadarati, na mpaka sasa mkewe hana mimba, na anahofia kubeba mimba kumuogopea mtoto kuwa hatapata malezi mazuri, je, kunajuzu kwake kisharia kuchukua maamuzi ya upande mmoja ya kuzuia kizazi?
Answer
Kuzaa ni haki ya ushirikiano kati ya wanandoa wawili, wala hakujuzu kwa mmoja wao kuchukua maamuzi ya peke yake kuzuia kizazi au kukichelewesha bila ya mwingine kutaka hilo, isipokuwa kukiwa na haja inayopelekea kuchelewesha, kukiwa na haja kama mke kuhofia uraibu wa madawa ya kulevya kwa mume, na hatari yake kwa mtoto wake akiwa tumboni au baada ya kuzaliwa; basi kunajuzu kwake kuchukua maamuzi ya upande mmoja kwa kuchelewesha kuzaa mpaka mume atakapopona uraibu na kuhakikisha kuwa mtoto hatoathirika na matokeo ya Uraibu huo.
Maelezo
Sheria ya Kiislamu katika kuchunga kwake mambo ya msingi ambayo Maisha ya watu hayakai sawa isipokuwa kwayo, na masilahi yao hayafikiwi isipokuwa kwa kuyachunga, kama nafsi, akili, dini, kizazi na mali, ikafanya kuhifadhi mambo hayo ndiyo malengo yake ya juu, na kwayo zinazunguka hukumu zake na sharia zake, mpaka ulazima wa kuhifadhi mambo haya Wanazuoni wakayapa jina la: “Malengo makuu ya Sharia” ambapo hayatoki katika uangalizi wake hukumu yoyote katika hukumu zilizoelezwa, na ndiyo marejeo pia katika matukio na hali mbalimbali. Na kwakuwa kulinda kizazi ni katika makusudio makuu ambapo Sharia imehimiza kuyalinda, Mwenyezi Mungu Ameweka maumbile ya kupenda kizazi kwa mwanadamu, mpaka akafanya kuwa ni katika mapambo ya Maisha ya Dunia, Mwenyezi Mungu Anasema: “Mali na wana ni pambo la maisha ya dunia”[Al-Kahf: 46].
Hivyo imekuwa ni jambo la kukatashauri kwa wazazi kwa hali ya maumbile kufanya juhudi kubwa ili Watoto wakue katika makuzi mema, isipokuwa ni hatari sana kuzembea katika haki ya Watoto, pamoja na kuthibiti kutofautiana katika tabia zawatu na usafi wa maumbile, na kutofautiana kukadiria kwao masalahi na uharibifu, Sharia Tukufu haikuacha jambo la kulea Watoto katika huruma kama hiari ya wazazi, au upole wao, bali imewalazimisha hilo katika amri ya kukatashauri na kuwapa jukumu la kisharia, mpaka ikaeleza kwamba lau kama mwanadamu atakuwa hana dhambi katika Maisha yake isipokuwa amepoteza haki za Watoto wake, ukubwa wa dhambi hiyo unaweza kutosha kuondoa amali zake zilizobaki.
Imepokewa Hadithi kutoka kwa Abdullah bin Amr R.A. kwamba Mtume (S.A.W. amesema: “Inatosha kwa mtu kuwa amefanya dhambi kumpoteza anaemlisha” imetolewa na Abu Dawoud katika Al Sunan, ikiwa dhambi za kupoteza Watoto zinatosha kwa mwanadamu kuangamia na kunapelekea kuadhibiwa, basi hapo ni wajibu kwa wanandoa kuhakikisha uwezo wao wa kuwalea Watoto wao na kusimamia haki zao, kabla ya kuanza kuzaa; hii ni kwa sababu masuala ya malezi, uangalizi wa kiafaya na wa kiasaikolojia na kielimu kwa Watoto ni zaidi ya umuhimu wa gharama za kifedha, hasa katika hatua ya utoto; kwani kukidhi mahitaji ya kifedha kunaweza kuendeshwa na wazazi na wasiokuwa wazazi katika jamaa na ndugu, na hakuna anayeweza kuchukua nafasi yao katika kukidhi mahitaji ya kimalezi na uangalizi.
Ikiwa mwanadamu dhana yake kushindwa kuwalea Watoto itakuwa kubwa, na kwamba hawezi kuwapatia utulivu, amani na malezi, kwa kuwa anasafiri, au maradhi au anahofia hatari kwao, hapo kunaruhusiwa kwake kuzuia kizazi, mpaka dhana yake ya kuwa na uwezo wa kusimamia hilo itakapokuwa kubwa, hivyo basi kwa kufanya hivyo anakuwa amechunga hali yake na uwezo wake, na anakuwa amejiondoshea madhambi ya kujikalifisha mwenyewe kwa lililo juu ya uwezo wake.
Na hii ni muktadha wa mapokezi ya maandiko ya kisharia, ambapo yameeleza kuwa wanandoa wawili au mmoja wao akihofia mateso au madhara au kutoweza kusimamia wajibu wao wa kisharia kwa Watoto, kunajuzu kuzuia kizazi, mpaka kitapoondoka kinachohofiwa, na kufikia uwezo wa kukidhi mahitaji ya malezi yao, Mwenyezi Mungu Anasema: “Wala halazimishwi mtu ila kwa kadiri ya uwezo wake. Mama asitiwe taabuni kwa ajili ya mwanawe, wala baba kwa ajili ya mwanawe”[Al-Baqarah: 233] Aya hii tukufu inaeleza kwamba kuwadhuru Watoto kumekatazwa kwa njia zote, ikawa njia ya kufikia katika hilo imekatazwa kwa kile kilichofikiwa kuwa “Kinachopelekea katika uharamu nacho ni haramu”.
Pia zimepokewa Hadithi tukufu juu ya uhalali wa kutumia njia za kuzuia mimba, ikithibitika kuwa inaweza kuleta madhara kwa mtoto, katika hadithi hizo ni ile ambayo Mtume (S.A.W.) alipotaka kukataza kumuingilia mwanamke akiwa ananyonyesha, ili asipate mimba na kumdhuru mtoto anayenyonya-alipojua kuwa hilo halimdhuru mtoto hakukataza, imepokewa Hadithi kutoka kwa Judhama bint Wahab Al Asadiyya R.A. kwamba yeye alimsikia Mtume (S.A.W.) akisema: “Nilikuwa nataka kukataza kumuingilia mwanamke akiwa ananyonyesha, mapaka nilipojuwa kuwa wafusi na warumi wanafanya hivyo na haliwadhuru Watoto zao”. Imetolewa na Imamu Muslim katika sahihi.
Pia kama Masahaba walivyowahi kutumia njia za kuzuia mimba, kwa kuhurumia wake zao wasibebe mimba wakiwa ananyonyesha, na Mtume (S.A.W.) hakukataza hilo pamoja na kujua, pamoja na kuweka wazi kwamba ikiwa hayathibitika madhara hakukua na haja ya kuzuia mimba, imepokewa Hadithi kutoka kwa Saad bin Abi Wiqaas R.A. kwamba mtu mmoja alikuja kwa Mtume (S.A.W). akasema: Mimi ninavua kwa mke wangu (Anamwaga mbegu nje ya njia ya Uzazi) Mtume (S.A.W.) akasema: kwanini unafanya hivyo? Yule mtu akasema: Ninamuhurumia mtoto wake au Watoto wake, Mtume (S.A.W.) akasema: Lau kama lingekuwa linadhuru basi lingedhuru wafusi na warumi”, Al Zuhayr amesema katika mapokezi yake: “Ikiwa ni hivyo usifanye, wafursi na warumi haliwadhuru hilo”. Imetolewa na Muslim katika sahihi yake. Na katika Hadithi hii kuna hoja ya kuhalalisha kuvua.
Asili ni mmoja wa wanandoa wawili asichukue maamuzi ya upande mmoja ya kuzuia mimba; kwa kuwa ni haki shirikishi kati yao, kwa Hadithi iliyokuja kutoka kwa Ibnu Khatab R.A. Mtume (S.A.W.) amesema: “Mtume (S.A.W.) amekataza kuvua isipokuwa kwa idhini ya mwanamke”. Imetolewa na Ibnu Majah katika Sunan na Al tabarany katika Muujam Al Awsat. Isipokuwa inatolewa katika hilo baadhi ya hali ambazo zinahofiwa wanandoa wawili kupata madhara, ambapo wahakiki wa madhehebu ya Hanafy wameeleza kwamba kutumia njia za kuzuia mimba ni halali kwa haki ya wanandoa wawili kwa Pamoja.
Muktadha wa hilo ni kwamba kunajuzu kwa mke ikiwa atahofia kumdhuru mtoto wake wa tumboni au mtoto wake, kuchukua maamuzi ya upande mmoja ya kuchekewesha kubeba mimba, na kutumia njia husika katika hilo, hasa ikithibitika kitaalamu kuwepo hatari kadhaa za kiafya kwa mtoto akiwa tumboni itakapotunga mimba ikiwa mmoja ya wazazi wawili anatumia madawa ya kulevya, kama kupungua uzito wa mtoto tumboni, au kupata maradhi ya kimaumbile, au kuchelewa kiwango cha kukuwa kiakili, au kuwa katika hatari ya kifo, pia ikiwa atahofia mtoto kukosa malezi na uangalizi wa kiafya na matumizi ya lazima.
Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:
Kulinda kizazi ni katika malengi makuu ya Sharia ambapo sharia imehimiza kuyachunga.
Asili ni kutochukua maamuzi ya upende mmoja kwa mmoja ya wanandoa wawili kwa kuzuia mimba kwa kuwa ni haki ya Pamoja kati yao.
Kunajuzu kwa mke kuchukua maamuzi ya upande mmoja ikiwa atahofia mtoto wake wa tumboni kuwa atapata madhara, na kutumia njia rasmi za kuzuia mimba.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
