Kumkataza mke kuzaa kwa sababu ya m...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kumkataza mke kuzaa kwa sababu ya maradhi ya kiurithi

Question

Mimi nimeoa miaka mitano iliyopita, na ninaishi vizuri na mke wangu, na nimezaa naye mtoto mmoja, lakini nimegundua kuwa mtoto ana maradhi ya(Homa ya  Bahari ya kati), na baada ya vipimo imebainika kwamba mke wangu ana maradhi ya kiurithi katika familia yao, Pamoja na kuwa tumefanya vipimo vya lazima kabla ya ndoa, na tumeshauriwa tusizae tena, na mke wangu anag’ang’ania kuzaa, kwa madai kwamba maradhi yanatoka kwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu Anaweza kuwaepusha nayo Watoto, je,  naweza kumzuia kuzaa kutokana na maneno ya madaktari, na kwa yale tunayopitia katika jaribio la mtoto tulienae ambaye ana ugonjwa huu hatari? Muulizaji ameambatanisha na ripoti ya daktari inayothibitisha hilo

Answer

Ikiwa ripoti ya madaktari ikithibitisha au kukidhaniwa kwa kiasi kikubwa kwamba katika mimba kuna hatari kwa mtoto kwa kuthibitisha kuwa mke ana maradhi hatari, basi hakuna kizuizi kisharia kutumia njia za kuzuia mimba katika hali hii, na hilo halizuii kuwa ni haki ya mume; kwa kulinda kupatikana mtoto atakae teseka Maisha yake yote kutokana na maradhi haya ya muda mrefu, na kufanya juhudi za kupatikana utulivu wa Maisha ya ndoa; kutokana na yele yatakayomgharimu miongoni mwa matatizo makubwa ya kifedha, kimwili, na kibinafsi.

Maelezo

Maradhi ya homa ya Bahari ya kati: Ni maradhi ya kuirithi ambayo yanaambukiza kutoka kwa wazazi wawili kwa pamoja, inayosababisha maumivu, dalili zake huanza katika umri wa miaka mitano mapaka kumi na tano kikawaida, inatokana kwa sababu ya mabadiliko ya kijenatiki, na inaathiri katika mfumo wa kinga na viungo vingine vya mwili, jambo ambalo hudhoofisha udhibiti wa homa na kusababisha hali ya afya kuwa duni mara kwa mara.

Na wataalamu wameeleza kwamba hakuna dawa ya kutibu ugonjwa huu mpaka sasa, na kwamba dawa zinazotumika katika kutibu ugonjwa huu ni za kupunguza maumivu na kuchelewesha kuibuka kwa hali hiyo. Maradhi haya yanatokana na kuwepo kwa jenitiki zinazohama kutoka kwa wazazi wawili au mmoja wao Kwenda kwa mtoto, kutokana historia ya familia ya maradhi haya; hivyo basi ikiatwa (Homa ya kifamilia ya Bahari ya kati), na inasababisha madhara makubwa kama ripoti za waganga zinavyoeleza, jambo ambalo linapingana na kusimama vizuri kwa Maisha na kusimama sawa.

Na kuzaa japo kuna ni masilahi ya Dini na dunia, isipokuwa ni kwamba kunachungwa kutosababisha kuzuka madhara makubwa kwa mmoja wa wanandoa wawili au kwa wote, au kwa mtoto wao kwa namna madhara yasiwe makubwa kuliko malengo yake, na kanuni ya kisharia imethibiti kwamba “Kuchunga kuzuia madhara ni bora kuliko kuchunga kupata masilahi”, na kanuni ya “Madhara huondoshwa” na kanuni ya “Yakigongana mambo mawili yenye madhara hukwepa lenye madhara makubwa kwa kufanya lenye madhara madogo”.

Na kushinda dhana ya kupatikana maradhi akizaa mtoto kutokana na historia ya maradhi ya kiurithi kwa mmoja wa wazazi wawili kunawahalalishia kutumia njia za kuzuia mimba ili kuepuka kuendelea kwa maradhi haya kwa Watoto,  kwa kufuata ruhusa ya kuvua katika hadithi inayoruhusu kuvua ikibainika kuwa hilo linapelekea kupatikana madhara kwa mtoto, miongoni mwa hilo ni  hadithi hii “Nilikuwa nataka kukataza kumuingilia mwanamke akiwa ananyonyesha, mapaka nilipojuwa kuwa wafusi na warumi wanafanya hivyo na haliwadhuru Watoto zao”. Imetolewa na Imamu Muslim katika sahihi.

Na Sharia Tukufu japokuwa imeweka sharti ya mume kumzuia mke kuzaa, lakini hilo  kwa idhini yake mke na ridhaa yake kwa kushirikiana Pamoja katika haki hiii, na kwamba mume hana haki ya kuthubutu kuondoa haki yake, isipokuwa ruhusa ya mke hapa inategemea na hali ya kuchagua na kutochagua na kukosekana kuwepo hatari au madhara yanayothibitika kwa mtoto baada ya kumzaa, na hii ni kwa yale waliyoyaeleza mashekhe wa madhehebu ya Hanafy, pia maelezo ya madhehebu ya Hanafy yanaeleza kuwa nyudhuru zinazoondoa ruhusa ya mke zinachunga mabadiliko ya hali na muda, na huu ndio muktadha maelezo ya madhehebu ya Hanbali.

Na yanaingia katika jumla ya nyudhuru hizi, yaliyokuja katika swali kwa wazazi wawili au mmoja wao kuhofia kuzaa mtoto mwenye maradhi haya sugu, yataendelea kumsumbua aaisha yake yote pamoja na kubeba mateso na shida, na kuzuia kutoenea kwa maradhi haya kwa vizazi vijavyo, hasa kwamba homa ya kifamilia ya Bahari ya kati ni maradhi ya kiurithi kama tulivyokwisha eleza. Katika hili kumechungwa masilahi ya mtoto asije kuishi maisha ya kutengwa au udhalili, au kupata machungu ya kuwa mbali na wazazi wawili, naka tika kuzingatia hilo au mfano wake kipindi cha maradhi au kuzuka maumivu.

Suala la kuzaa Watoto na kuendeleza kizazi japokuwa ni katika mambo ya yanayoendana na sababu za kimaumbile na lengo la ndoa halali, isipokuwa ni kwamba kunachungwa katika hilo mambo mawili:

Jambo la kwanza: Kuwa linafungamana na usalama wa mke na mume na afya ya kizazi chao, katika yale ambayo yanawafikisha katika maana ya utulivu, hivyo basi Sharia Tukufu imewahimiza wanaotaka kuoana kuchagua mbegu zao, na kufanya hesabu katika kuchagua wanaoendana wenye afya nzuri, imepokewa Hadithi kutoka kwa Mama wa Waumini Aisha R.A. amesema: amesema Mtume S.A.W.: “Chagueni kwa ajili ya mbegu vizuri wake wa kuwaoa, na uoeni mnaoendana nao na waozesheni mnaofanana nao” imetolewa na Ibnu Majah na AL Bayhaqy katika Sunan, na Al Hakim katika mustadrak.

Na kwamba “Muumini mwenye nguvu anapendeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko Muumini dhaifu” kama ilivyokuja katika Hadithi ambayo imepokelewa na Muslim kutoka kwa Abu Hurayra R.A. na kwamba kuepuka madhara na kuchukua tahadhari ni jambo la lazima; Mwenyezi Mungu Anasema: “Enyi mlioamini! Chukueni hadhari yenu! Na mtoke kwa vikosi au tokeni nyote pamoja!” [An-Nisaa: 71].

Na imepokewa Hadithi kutoka kwa Abee Saeed Al Khudry R.A. amesema: amesema Mtume (S.A.W): “Usidhiru wala usijidhuru” imepokewa na Hakim katika Mustadrak. Mwanadamu wakati wote anatakiwa kufanya juhudi katika kila jambo kile ambacho anaweza kuzuia madhara na hatari inayotegemewa, na imekuja katika kanuni kwamba “Kinga ni bora kuliko tiba”.

Jambo la pili: ni kwamba kuzaa ni katika masuala yanayofungamana na hisia tu kwa kulinganisha na masilahi makubwa ya mtoto na kuhakikisha kufikia kubeba majukumu kamili katika kuwalea na kuwalinda, imekuja katika Hadithi: “Ehee nyote ni wachunga na nyote mtaulizwa kwa mlichokichunga” imepokelewa na Bukhary na Muslim. Na miongoni mwa yanayopasa kwa wanandoa: ni kulinda kizazi, na kuwakinga Watoto wao na maangamizi, na muktadha wakulinda nafsi zao pia, Hapana shaka kwamba kulinda nafsi iliyo hai ni mingoni mambo muhimu zaidi ya lazima au mambo Matano makuu ya lazima ambayo Sharia imeagiza kuyahifadhi.

Kupata mtihani na magonjwa sugu kama hayo ni kutokana na kudura na rehema za Mwenyezi Mungu, na hupelekea katika wema na huleta huruma. Majaribu huleta baraka, na kila kitu kinachompata mtu kwa upande wa majaribu na dhiki kwa kweli ni kuinuliwa kwa cheo cha Muumini, ongezeko la thawabu zake, na kuondolewa kwa adhabu yake, hata mwiba unaomchoma. Imepokewa Hadithi kutoka kwa Mama wa Waumini, Aisha, R.A, amesema: Mtume (S.A.W), amesema: "hakupatwa Muumini na kitu kama mwiba na kitu kingine chochote kikubwa kuliko hilo, isipokuwa kwamba Mwenyezi Mungu humpandishia daraja kutokana nao, au kumwondolea dhambi kutokana nao." imetolewa na Imamu Muslim katika "Al-Sahih".

Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:

Ikithibi katika ripoti ya daktari kwamba kupatikana kwa mimba ni hatari kwa mtoto, kwa kuthibitika kuwa mke ana maradhi hatari: basi hakuna kizuizi kisharia kutumia njia za kuzuia mimba katika hali kama hiyo.

Kunatakikana kuwa kuzuia mimba kwa njia za muda si za kudumu; kwani huenda kukapatikana tiba ya maradhi haya ya kiurithi kutokana na maendeleo ya kila siku, au njia ya kuwaepusha Watoto kupatwa na maradhi.

Pamoja na kuzingatia kwamba haya yote ni katika njia kubainisha haki za matokeo yanatokana nayo, lau si kama hiyvo mlango wa fadhila za kushauriana kati ya mke na mume ndio unaochungwa na kutangulizwa muda wote, na kwamba haki hii kunatakikana kwa wanandoa kuifahamu kwa kushirikiana kwa Pamoja kati yao.

Share this:

Related Fatwas