Hukumu ya Kumlea Yatima Mkristo kat...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Kumlea Yatima Mkristo katika Familia ya Kikristo

Question

Tunaomba mtujuze kuhusu rai ya dini ya Kiislamu katika kumlea mtoto yatima mkristo katika familia ya kikristo nchini Misri, kwa kuwa kumlea yatima ni ruhusa kwa familia za Kiislamu lakini haliko wazi kwa familia za kikristo.
Jibu.

Answer

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu, rehema na amani zimfikie Mtume Muhammad S.A.W., watu wake, masahaba wake na waliomfuata. Ama baada ya hayo:
Kumlea mtoto yatima ni jambo linalokubalika kisheria na lililopendekezwa na Dini, na ikalijalia ni miongoni mwa sifa za watu wema. Mwenyezi Mungu Mtukufu ameweka huruma duniani ili kwa huruma hiyo wanyama wahurumiane na wanadamu pia. Na katika hadithi tukufu, Mtume S.A.W. amesema: “Mwenyezi Mungu amejalia aina mia za huruma, tisini na tisa akazishika na akashusha duniani aina moja tu, na kwa kupitia aina hii moja ndio viumbe wanahurumiana, mpaka farasi anyanyue kwato zake kwa mtoto wake kwa kuogopa kumdhuru" Imepokelewa na Bukhariy. Na kumuonea huruma yatima inaonesha kwamba mlezi wake ana huruma. Mtume S.A.W. amesema: “Wenye huruma atawarehemu Allah mwingi wa rehma, wahurumieni walio ardhini atakurehemuni aliye mbinguni " Imepokelewa na Abu Daudi.
Na mwenye kumlea yatima: Ni yule anayesimamia jambo lake, anamtunza, anamlea na anamhudumia kimatumizi, ili aje kuwa ni mwananchi mwema anayewanufaisha watu kwa kheri zake na anawaepusha na shari.
Kitendo cha warumi kuwahurumia wanyonge wao na kuwalea mayatima wao kilikuwa ni sababu miongoni mwa sababu zilizomfurahisha sahaba mtukufu Amru ibn Al-As R.A ,pale alipowasifia kwa kusema: “Warumi wana sifa nne: Ni wapole wakati wa fitina, wanazinduka haraka baada ya matatizo, na baada ya watu kukimbia vitani wao hurejea haraka, na mbora wao ni masikini, yatima na myonge. Na sifa yao ya tano nzuri ni wanawazuia wafalme kudhulumu”. Imepokelewa na Muslim.
Ama swali la fatwa hii kuhusu kumlea mtoto mkristo wa familia ya kikristo baada ya kuondokewa na baba yake na mama yake kwa kufa au kupotea au kufungwa jela na mfano wa hayo, basi hakuna kizuizi katika kumlea, bali ni wajibu wa kijamii unaosisitizwa ili asipotee mtoto na akawa bila ya ulezi.
Ama mtoto asiyejulikana nasaba yake au ameokotwa basi haisihi kukulia na kulelewa isipokuwa katika mazingira ya dini ya Kiislamu ikiwa yupo katika nchi ambayo wakazi wake wengi ni waislamu. Katika hali hii waislamu wanawajibika kumlea mtoto wa aina hii na ni bora kumlea kuliko kulelewa na wakristo. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi wa yote.
 

Share this:

Related Fatwas