Kuhodhi Bidhaa (Ulanguzi)

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuhodhi Bidhaa (Ulanguzi)

Question

Baadhi ya watu wanasikia kuwa bei ya bidhaa fulani itapanda, basi wanakwenda kuzinunua kwa mwuuzaji ambaye hajui chochote kuhusu ongezeko hilo la bei linalotazamiwa kutokea. Wanunuzi hao hufanya hivyo Kwa kusudio la kuzilundika na kuziuza bidhaa hizo baada ya kupanda bei yake, na wakati mwingine mnunuzi huyo huzinunua zikiwa ghali na akazikusanya na kuzilundika akingojea ongezeko la bei ya juu zaidi. Je, nini hukumu ya tendo hilo? Na je mfanyabiashara akibobea katika kuzalisha au kutengeneza bidhaa fulani na kuiuza kwa bei anayoitaka, je hali hii inazingatiwa ni kuhodhi bidhaa ambako kumekatazwa au la?

Answer

Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na waliomfuata. Ama baada ya hayo:

          Miongoni mwa sifa za miamala ya fedha katika Uislamu ni udhamini wa masilahi ya pande zote husika ambapo hapatokei madhara yenye athari kwa upande wowote. Sifa hiyo ni ya kimaumbile kwa mujibu wa uadilifu kamili uliowekwa na misingi imara ya sheria ya Kiislamu. Na yote hayo yamewekwa hivyo kwa kuwa asili ya kutendeana inajengeka kiuchoyo na siyo kiusamehevu, na kwa ajili ya kufikia lengo hilo, wanasheria wamezuia baadhi ya miamala ambayo inadhuru masilahi ya upande mwingine. Na wanasheria wakaiziba vyema mianya ya utendeanaji huo kwa lengo la kukausha (kuzuia) vyanzo vyake.

          Miongoni mwa utendeanaji huo ni kuhodhi bidhaa (ulanguzi) ambako ni moja ya sababu za msingi za kujitokeza kwa kile kijulikanacho kama Soko la magendo (Soko la Ulanguzi).

          Na kuhodhi bidhaa (ulanguzi) katika lugha kuna maana nyingi na miongoni mwake ni; ubanaji, uhaba, ulundikaji, uzuiaji na udikteta. Na maana zote hizi za matumizi ya kilugha zinabeba maana ya tabia mbaya, na kwa kuwa mwanadamu ni dhalimu katika kutendeana kwake, maana hizo zote huifanya nafsi ichukie utendeanaji huu wenye madhara.

          Na ufafanuzi wa wanavyuoni kuhusu kuhodhi bidhaa unahitilafiana kwa sababu ya masharti na hukumu zilizowekwa na kila mwanachuoni ambapo mwingine inawezekana asizione hivyo. Kwa upande wa wanavyuoni wa Madhehebu ya Shafiy; kuhodhi bidhaa ni mtu kununua chakula asichokihitajia wakati wa ughali na sio wakati wa urahisi, na kukilundika na kisha kukiuza kwa zaidi ya thamani yake kwa lengo la kuwabana watu. [Nehayat Al Muhataaj 3/472, Ch, Dar Al Fikr].

          Na wanavyuoni wa Madhehebu ya Hanafiy wanaona kuwa ulanguzi ni kukilundika chakula ili bei yake ipande. [Al Enaya 10/58. Ch. Dar Al Fikr]

          Na wanavyuoni wa Madhehebu ya Hanbaliy wanasema kuwa: Ulanguzi ni "kununua chakula cha mwanadamu na kukilimbikiza kwa ajili ya kudhuru". [Al Mubdii' 4/47, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiya]

          Na wanavyuoni wa madhehebu ya Malikiy hawakuweka mpaka wa kuhodhi bidhaa, lakini kutokana na maneno yao inachukuliwa kuwa kuhodhi bidhaa ni kulundikia kitu kama chakula n.k katika wakati wa kuhitajika chakula hicho kwa watu na kuwasababishia madhara. [Al Bayan na Al Tahseel kwa Ibn Rushd 17/284, Ch. Dar Al Gharb Al Islamiy].

          Na maana iliyoangaliwa katika fafanuzi zote hizo ni kwamba, kuhodhi bidhaa ni kuwabana watu na kuwasababishia madhara, kwa kununua bidhaa maalum wakati wa ughali wake na kuizuia ingawa watu wanaihitajia, ili iuzwe kwa bei ya juu zaidi kuliko thamani yake.

          Na kukatazwa kuhodhi bidhaa kumetajwa katika hadithi kadhaa, kama hadithi ya Muammar: " Hahodhi bidhaa ila mtu mtenda makosa" [Imepokekewa na Musilim]. Na katika mapokezi mengine: "Aliyehodhi bidhaa ni mkosa".

          Na hadithi ya Abi Umamah: "Mtume S.A.W. amekataza kuhodhi chakula" [Imepokelewa na Al Tabaraniy]

          Na miongoni mwazo ni hadithi ya Abu Hurairah: "Atakayehodhi bidhaa kwa lengo la kuwapandishia bei waislamu yumakosani" [Imepokolewa na Ahmad, Al Hakem, na Al Bihaiqiy].

          Na hadithi ya Maaqil Bin Yasaar: "Yoyote aliyeingilia kitu miongoni mwa bei za waislamu kwa ajili ya kuwapandishia, basi ni haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kumkalisha makazi mabaya motoni siku ya Kiyama" [Imepokelewa na Ahmad, Al Hakem, Al Bihaiqiy na Al Tabaraniy].

          Na ilipokelewa kwa Sanadi Dhaifu: "Muuza bidhaa huruzukiwa na anayehodhi bidhaa hulaaniwa" [Imepokolewa na Ibn Majah na Al Bihaiqiy katika Sunnan].

           Na kwa kupitia hadithi hizo, jamhuri ya wanavyuoni wa Fiqhi wameharamisha kuhodhi bidhaa, kwani kukanusha ulanguzi wa bidhaa katika hadithi ya Muammar ni dalili tosha ya kuharamisha kuliko kukataza. Hadithi hiyo inaashiria kuwa hakuna ruhusa kwa mtu yoyote kufanya kitendo hicho.

          Na mtu mwenye kufanya kosa, anapata dhambi na anakuwa ameasi. Al-Shaukaniy anasema baada ya kuzitaja hadithi za kuhodhi bidhaa: " Bila shaka hadithi za mlango huu zinajulisha kutojuzu kuhodhi bidhaa, na kama itasemwa baadhi ya hadihi si sahihi, basi vipi ilhali hadithi ya Muammar imetajwa katika Sahihi ya Muslim? Hadithi ambayo imeweka wazi kuwa mwenye kuhodhi bidhaa amefanya makosa.". [Nail Al Awttaar 5/261, Ch. Dar Al Hadith]

          Na tamko la wazi la chakula katika hadithi ya Abi Umamah haifai kulichukulia kwa maana ya kukataza kiujumla, lakini katazo lililotajwa katika hadithi zote nyingine ni kiujumla sio kuhusu kitu maalum.

          Lakini kuharamisha huko hakuthibiti ila kwa masharti. Wanavyuoni wanakaribia kuafikiana juu ya masharti matatu nayo ni: kununua bidhaa zinazopatikana mjini wakati wa ughali wa bei, kuzilundika bidhaa hizo pamoja na kungojea zipande bei, na kuwasababishia watu madhara kwa sababu ya mlundiko huo wa bidhaa. [Badaai' Al Sanaai' 5/129, Ch. Dar al Kutub Al Elmiya, na Mawaheb Al Jalil 4/227, Ch. Dar Al Fikr, na Asniy Al Mattalib 2/37, Ch. Dar Al Kitaab Al Islamiy, na Al Mughniy 4/154, Ch. Dar Al Fikr, na Al Sharh Al Kabeer kwa Ibn Abi Omar 4/47, Ch. Dar Al Kitaab Al Arabiy]

          Kama sharti moja kati ya masharti hayo matatu litakosekana basi haizingatiwi kuwa huko ni kuhodhi bidhaa. Lakini kama mtu akihodhi bidhaa na watu wakawa hawana haja na bidhaa hizo, au alizilundika pamoja na kuziuza kwa bei ya kawaida, au alizinunua katika hali ya dhiki na ughali ili kupata faida bila ya kuzilundika, basi mambo hayo yote hayazingatiwi kuwa ni kuhodhi bidhaa.

          Na kama akilundika mazao ya shamba lake au bidhaa ya kiwanda chake au akanunua bidhaa kutoka nje ya mji na akazilundika, basi vitendo hivyo havizingatiwi kuwa ni kuhodhi bidhaa, na hata kama bei ya bidhaa hizo itakuwa juu. Lakini tu kwa sharti la watu kutokuwa na dharura ya kuhitajia bidhaa hizo, ambapo wangepata madhara kwa sababu ya ulundikaji huo. Kwani lengo la kuzuia kuhodhi bidhaa ni kuondosha madhara kwa watu wanaotumia bidhaa hizo, kwa sababu ya wengine kuhodhi bidhaa wakati wa dhiki na ughali. Na wanavyuoni wa Shafiy walizitaja aina hizo.

          Imamu Al Mawardiy anasema katika kitabu cha [Al Haawiy 5/411, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiya]: "Na ama kuhodhi bidhaa na kungojea mizigo (bidhaa) haichukizi kwa vitu visivyokuwa vyakula. Na vyakula haichukizi kuvilundika kama kuna vyakula vya kutosha na bei zake ni rahisi. Na ama kuhodhi bidhaa katika kipindi cha dhiki na watu wanazihitajia kwa lengo la kuja kupandishia bei ni Makruhu na Haramu. Na kama mtu atazinunua wakati wa bei ghali na shida, kwa lengo la kuja kupata faida kubwa zaidi, basi hili halizingatiwi kuwa ni kuhodhi bidhaa".

          Imamu Al Juweniy anasema katika kitabu cha [Al Nehayah 6/64, Ch. Dar Al Minhaaj]: "Anayenunua chakula wakati wa bei rahisi na kuzorota kwa masoko, na akalundika ili akiuze baada ya kupanda bei yake, basi halaumiki na hana kosa lolote. Kwani asili ya kulundika na kungojea kwake ilikuwa katika wakati wa urahisi wa bei ambapo hakuna madhara, na pengine bidhaa zilizolundikwa ni kama akiba, zitawafaa watu baadaye, na kama hazikulundikwa zitaharibika na kupotea. Na pia mtu yoyote mwenye mazao kutoka shambani kwake, na akaamua kuyalundika kwa lengo lolote, basi ana ruhusa ya kufanya hivyo na wala haingii katika watu wenye makosa. Na kauli hiyo katika jambo hili inahusika na janga kubwa, nayo ni kuwa watu wakikumbwa na janga kubwa nalo ni kifo na kuangamia- na kila mmoja akafikia kuhalalisha mzoga na chakula cha mwingine, basi hakuna ubaya kwa mtu kulundika chakula kwa ajili ya nafsi yakemwenyewe na familia yake kwa mwaka mzima.Basi anapaswa kuuza kwa kilichozidi. Na kama hakufanya hivyo basi kiongozi mhusika atamlazimisha kuuza; kwani katika kuuza huko ni faida kwa watu wengine bila ya yeye kujidhuru”.

          Ndani ya kitabu cha [Nail Al Awtaar 5/262], Al-shaukaniy amemnukuu Al Subkiy, anasema,: "Yanayopasa kusemwa katika jambo hilo ni kwamba kama mtu atamzuia mtu mwingine kununua bidhaa na akawa katika hali ngumu basi kuzuia huko ni haramu. Na kama bei zitakuwa rahisi na kiasi cha bidhaa anazozinunua watu hawazihitaji sana, basi hakuna haja ya kumzuia kuzinunua na kuzilundika mpaka pale watu watakapokuwa na haja nazo.

          Al Qadhi Husain na Al-rabaniy wanasema: "Na pengine kulundika ni jambo zuri lenye thawabu, kwani watu watanufaika baadaye ... Na iwapo itakuwa wakati wa ukame, na watu wakawa wanakusanya na kulundika asali, samli, mafuta, na mafuta ya ufuta, n.k., na kufanya hivyo ikawa kuna madhara, basi lazima wanasheria waamue kuharimisha. Na kama hakuna madhara yoyote basi kulundika vyakula kunachukiza.

          Na Al Qadhi Husain anasema: "Kama watu walikuwa wanahitajia nguo n.k. kwa ajili ya baridi kali au kwa kuficha viungo maalum, basi ulundikaji wake ni Makruhu.

          Kwa hakika sababu ya kuzuia kuhodhi bidhaa sio ulundikaji wenyewe kama ulivyo, bali ni kudhuru watu. Kwa hivyo Imamu Al Baihaiqiy anasema katika kitabu cha [Al Maarifah 8/206, Ch. Dar Al Wahiy mjini Halab] baada ya kutaja hadithi ya Muammar: "Amekusudia - na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi wa yote - kama kuhodhi chakula kunaleta madhara kwa watu basi haifai”. Na kudhuru huku ni katika hali mbili, dharura na kuhitajika kwake. Kama watu watahodhi kwa kisingizio cha dharura au haja basi ni haramu, na kuhodhi huku ni katika kitu chochote na sio chakula tu. Katika kuhodhi bidhaa, wanachuoni wanahitalafiana kuhusu namna – hitilafu ya lafdhi -, madhehebu ya Malikiy yanazingatia kuhodhi bidhaa ni katika vitu vyote, vyakula au vitu vingine, hata kama itakuwa dhahabu au fedha. Kauli hiyo imetolewa pia na Abi Yusuf wa madhehebu ya Hanafiy.

          Madhehebu ya Shaafiy na Hanbaliy yanasema kuwa kuhodhi bidhaa ni katika vyakula tu, na kauli hiyo ni fatwa katika madhehebu ya Hanafiy. Na chakula wanachokusudia wanachuoni wa Hanbaliy katika kuhodhi bidhaa ni chakula cha mwanadamu tu, na sio chakula cha wanyama. Lakini wanaosema kwa kuhusisha vyakula waliweka sharti la kutohitaji watu vitu vinavyohodhiwa -yaani vitu vingine mbali ya vyakula- na maana yake ni kutojuzu ulundikaji kama watu wana shida na wanahitaji vitu hivyo vinavyolundikwa. Na hali ya dharura au haja ndio inayopelekea maana ya kuhodhi bidhaa kama tulivyoeleza hapo juu.

          Na kama watu hawana haja na bidhaa hizo, na hawakulazimika kuzinunua, basi haziingii katika maana ya kuhodhi bidhaa, hata kama muuzaji akizilundika na bei yake ikapanda.

          Na katika kitabu cha [Al Dur Al Mukhtaar cha Imamu Al Haskafiy Al Hanafiy 6/399, Ch. Dar Al Fikr]: "(Na kulundika mavuno katika ghala la mkulima si kuhodhi bidhaa) bila ya hitilafu".

          Ibn Abdeen anasema katika (Hashiyah): "Na kilichowazi hapa ni kwamba mtu hapati dhambi ya kulundika bidhaa (kwa maana ya kuhodhi), lakini kama akingojea kupanda bei au ukame kwa nia mbaya ya kuwadhuru waislamu basi atapata dhambi. Na je, analazimishwa kuuza bidhaa hiyo? Ni dhahiri kuwa ndiyo, iwapo watu watakuwa na dharura ya kuhitaji chakula hicho kilichohifadhiwa".

          Na mazao ya shamba ni sawa na bidhaa za viwandani, kama mtu atalundika basi hapati dhambi kwa kufanya hivyo. Hata hivyo, mtawala ana haki ya kuziuza bidhaa zilizolundikwa kama watu watakuwa na mahitaji ya dharura juu ya bidhaa hizo.

          Na katika kitabu cha [Hashiyat Al Jamal Ala Sharh Al Manhaj 3/93, Ch. Dar Al Fikr]: "Vyakula kama bidhaa (mizigo) haiharimishwa kuilundika, isipokuwa pale inapohitajika kwa dharura."

          Al Bahutiy anasema katika kitabu cha [Kashaaf Al Qinaa'i 3/87, Ch. Alam Al Kutub]: "(Na haiharimishwi) kuhodhi bidhaa (katika vimiminika kama vile asali na mafuta) n.k. (wala) kuhodhi (nyasi kavu za wanyama); kwani haja kwa vitu hivyo haienei kama ilivyo katika nguo na wanyama."

          Na kutoa sababu ya kutoenea haja, ina maana kwamba kama haja itaenea basi hakuna shaka ya uharamu wake. Na hivi ndivyo inavyoeleweka katika matini za wanachuoni wa Hanbaliy inapotafutwa sababu ya kuharimisha kuhodhi bidhaa ya vyakula. Na katika kitabu cha [Sharh Al Muntaha kwa Al Bahutiy 2/27, Ch. Alam Al Kutub]: "(Na mlundikaji bidhaa) analazimishwa kuziuza kama wauzavyo watu wengine. Yaani vitu alivyovihodhi katika vyakula vya binadamu, kwa sababu ya kueneza masilahi na kuhitajika bidhaa husika kwa watu".

          Na mambo yanayopaswa kuashiria ni kwamba wanachuoni wametahadharisha pia namna inayofanana na kuhodhi bidhaa, kama wanavyofanya baadhi ya wafanyabiashara katika kuliporomosha soko kwa bidhaa maalum na kupunguza bei yake ili kuwalazimisha baadhi ya wafanyabiashara kutoka sokoni, na hii inamaanisha kile kinachoitwa katika Elimu ya Uchumi “kuhodhi bidhaa iliyopo sokoni”, na umbo lake ni mtu mmoja au kundi la watu kuhodhi kitengo miongoni mwa vitengo vya uzalishaji kisha mtu huyo au watu hao wakawa wanahodhi bei za bidhaa hizo ili kukabiliana na wanunuzi kadhaa.

          Na lengo la kuzuia aina hii si kwa kuwa ndani yake kuna maana ya kuhodhi bidhaa bali ni kwa sababu ya madhara kwa watu kiujumla, na huenda ikatolewa sababu ya kuzuia umbo la kwanza kutokana na yaliyopokelewa na Malik, Al Bihaiqiy na Abdulrazaaq katika Hadithi ya Ibn Al Musaeib kwamba Omar Bin Al Khataab alipita kwa Haatib Bin Abi Bala'ah, aliyekuwa anauza zabibu sokoni, Omar akamwambia: "Ima upandishe bei, au uondoke katika soko letu".

          Na maana ya hayo ni khofu ya Omar inayotokana na jaribio la kutaka kuhodhi soko kwa njia ya kuwatoa baadhi ya wafanyabiashara sokoni kwa sababu ya kupunguza bei.

          Ama kwa umbo la pili; Ibn Abdeen amelielezea vyema. Katika kitabu cha [Tanweer Al Absaar kwa Al Timirtashiy: "(Na wala hazuiwi mtu aliyehuru na aliyebaleghe (Mukalaf) isipokuwa mufti mbaya, mganga mjinga na mjanja aliyefilisika)".

          Na Ibn Abdeen anasema: "na mambo haya matatu yanaambatana na mengine matatu: mwenye kuhodhi bidhaa, wenye vyakula iwapo bei zao zitapindukia kiwango cha kawaida wakati wa kuuza, na kama mtumwa wa mwenye dhima atasilimu na bwana wake akakataa kumwuza, basi jaji ana haki kumwuza. Nilisema: na mlango wa kuamrishana mambo mema ni mpana kuliko hivi ilivyo.

          Tanbihi: inaeleweka kutokana na hayo, haijuzu kwa wamiliki wa viwanda au wataalamu wa kazi za mkononi kumzuia mtu anayetaka kufanya kazi katika ujuzi wao hali ya kuwa anaelewa vyema au anataka kujifunza ujuzi, basi haifai kumnyima mtu huyo ujuzi, kama ilivyotolewa fatwa katika Alhamidiya. [Rad Al Mukhtaar, 6/148]

     Kutokana na yaliyotangulia hapo juu; kununua bidhaa zinazotarajiwa kupanda bei kwa ajili ya faida, kama zitauzwa kwa bei inayokubalika bila ya kuhodhi bidhaa basi hilo linajuzu. Na kama mtu atazinunua wakati wa ughali wa bei zake na akazilundika akingojea kupanda kwa bei huku watu wanazihitaji na yeye amezilundika, basi hiyo ni kuhodhi bidhaa na ni haramu. Na si vibaya iwapo mfanyabiashara atalundika bidhaa alizozizalisha mwenyewe na kuziuza kwa bei anayoitaka, endapo watu hawahitajii bidhaa hizo zilizolundikwa.

          Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mjuzi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas